Elimu, utaifa na uzalendo

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kwa kipindi sasa nimekuwa sionekani humu jamvini. Kimya changu kingi hakikuwa cha bure. Bali nimeendelea kujielimisha katika mazingira Magumu na kame.

Kwa mti au mmea wowote ili ukue unahitaji ardhi yenye rutuba, unahitaji kupaliliwa na kuwekewa mbolea. Tunapalilia mimea ili kuondoa magugu, Tunamwagilia maji mmea ili ukue vizuri. Wote sisi ni kama mmea ukuaji wetu unategemea sana mazingira tuliyokulia na elimu tunayopewa pamoja na makuzi yetu. Dira ya kila mmoja wetu inategemea vitu hivyo. Maendeleo ya taifa lolote lile hutegemea tabia za watu wake zimeumbwaje na kuelekezwa katika mkondo gani wa fikra na matendo. Sisi ni zao la matendo yetu kama mtu mmoja mmoja na kwa pamoja kama taifa. Taifa tulilonalo ni zao la fikra zetu na matendo yetu. Tukibadili matendo yetu na fikrza zetu tutabadili moja kwa moja taswira ya taifa letu.

Nini maana ya elimu? Na ni mtu gani aliyeemika?

Dhana ya kwanza ambayo wengi tunayo ni kwamba elimu ni kupata maarifa. eg kujua kuandika na kusoma, kuweza kuwa na fani fulani labda kuwa daktari, muuguzi au pengine mwanasheria. Watu wanaosema hivyo wanaweza kuwa wanapatia kwa kiasi fulani. Lakini elimu haswa ni zaidi ya hivyo. Mtu kuwa na hivyo peke yake pasipo kuwa na hivi vingine ninatakavyojadili ni sawa sawa na mtu kutembea uchi. Nitafafanua kwa kadiri ya uwezo wangu katika ligha nyepesi.

Mtu aliyeemika lazima awe na uwezo pasipo kupapasa kutofautisha kati ya sahihi na potofu na kufuata kilicho sahihi. Lazima awe na nidhamu ya kuzuia mihemko na hisia na mawazo yake na kuyaoongoza katika kutenda mema. Elimu lazima imuongoze mtu kutofanya mambo mabaya. Lazima imjenge na kusafisha tabia yake ili kumfanya kuwa raia mwenye faida na mzalishaji kwa taifa lake. Bila ya haya elimu yetu haijakamilika elimu bila nidhamu ni sawa sawa na mto bila kingo. Kama elimu haimfanyi mtu kuwa mwema na binadamu bora faida yake nini? Kama elimu hamuondoi unyama uliomo ndani ya mtu na kumfanya kuwa binadamu mwenye kutenda mema haina faida na haina faida kwa jamii na kwa taifa. Hautuwezi kuwapa watu wetu skills za kazi na kuacha kujenga tabia tukadhani tutaendelea. We will going to have many educated fools. Watu ambao ambao wanaelimu ya darasani lakini kwa kukosa nidhamu wnafanya maamuzi ya kijinga.

Elimu lazima ilete order katika maisha ya mtu na katika jamii. Kwa njia hii pekee kwa kuleta na kuwafanya watu kuwa na nidhamu elimu itakuwa na mantiki. Elimu lazima ilete ustaarabu. Na ustaarabu ni kutenda katika misingi ya haki taratibu na sheria.

Hatuwezi kamwe kujisifia kama elimu yetu itazalisha waongo, walaghai na wafitini. Elimu ya namna hii haiwezi kupeleka taifa letu mbele kama watu wetu wanaogopa kusema ukweli kwasababu ya maslahi yao binafsi. Hatuwezi kusema tumeelimika kama tunaishi katika upotofu. Elimu ya namna hii haijatuweka huru. Na jukumu la elimu ni kuwaweka huru watu dhidi ya ujinga na upumbavu. Kama tunaendelea kufanya upumbavu na ujinga katika taifa hili tusijidanganye tumeelimika kisa tuna digrii mbili au tatu. Tukiutupa ukweli badala ya kuusimamia kwasababu ya maslahi yetu binafsi au kwasababu ya starehe tusahau kuhusu kuelimika. Nasema tena elimu haijakamilika pasipo maadili. Ili elimu iwe na tija lazima watu wajengwe kuwa na nidhamu na maadili. They Must know what is right for their country and what is wrong. Bila kujua taifa hili matendo yetu wenyewe yataanganiza taifa hili.

Elimu ni kukuza na kumuelimisha mtu, kujenga tabia ya mtu, mkondo wa mawazo ambao utamfanya kuwa na matendo yenye faida sio kwake mwenyewe peke yake bali pia kwa taifa. Kwahiyo taasisi zetu za elimu kama hazijengi tabia za watu ili wawe na matendo na fikra za namna fulani wamefeli. Hatuwezi kujenga tabia za nchi kama mkondo wa mawazo wa wananchi wetu haujajengwa na kuelekezwa mahala ambapo taifa linataka kwenda. Ni sawa sawa na shamba ambalo magugu na mahindi yanaota pamoja. kwakufanya hivi raia hawatajua nafasi yao ni ipi kwa taifa lao na watahusikaje katika kulijenga. Hili ni kwasababu watu wameingia kwenye uroho wa mali na kusahau ujenzi wa nchi. Kwasababu nchi haijengwi kwa kuwa tu na mabara mabara mengi au hospitali nyingi. Kama tunataka maendeleo ya haraka zaidi ni lazima watu wapangwe na wawe wamoja na wenye dira ya namna moja hili haliwezi kufanikiwa katika mazingira ya ubinafsi ambapo kila mtu anajivutia kwake. people must serve each other.

Hatuwezi kuwa taifa kubwa kwa fikra tulizonazo na tabia ninazoziona sasa hivi ambazo zimemea miongoni mwetu. Tabia hizi zinaonyesha kutokuwepo kwa fikra za utaifa, nidhamu na maadili na kukokosekana kwa order na dira. Mtu yoyote anayefikiri taifa lolote linaweza kuendelea bila uwepo wa maadili hafikirii sawa sawa. Taifa haliwezi kuendelea bila watu wake kuwa wakweli, waaminifi na wazalendo.
 
Back
Top Bottom