Elimu Please: Mid term Elections ni nini in US political structure/administration system?

Elimu Please: Mid term Elections ni nini in US political structure/administration system?

Hiyo manake ni uchaguzi mdogo wa marekani. Kwetu hapa ni uchaguzi wa serikali za mitaani ambapo ccm wakitumia walimu na mpolisi huiba kura
Kwa usa uchaguzi huu ni muhimu kwakuwa unatoa taswira ya uchaguzi mkuu utakavyo kuwa. Kwa hali ya mambo ilivyo chama Cha donld trump kinakwenda kuchapika kwenye uchaguzi huu. Sababu ni nyingi lakini vita ya kipumbavu dhidi ya Iran na Ukraine havita muacha salama
 
asante nimepata mwanga. kwahiyo uchaguzi wa "wabunge" unapishana na wa rais kama wa kwetu wa serikali zamitaa na Rais na wabunge..
 
asante nimepata mwanga. kwahiyo uchaguzi wa "wabunge" unapishana na wa rais kama wa kwetu wa serikali zamitaa na Rais na wabunge..
Wenzetu Wana mabunge mawilo so wabunge wa bunge Moja siyo sent wanapatikana katika uchaguzi huu. Endelea Kusoma utapata kujua zaidi
Asante
 
Hiyo manake ni uchaguzi mdogo wa marekani. Kwetu hapa ni uchaguzi wa serikali za mitaani ambapo ccm wakitumia walimu na mpolisi huiba kura
Kwa usa uchaguzi huu ni muhimu kwakuwa unatoa taswira ya uchaguzi mkuu utakavyo kuwa. Kwa hali ya mambo ilivyo chama Cha donld trump kinakwenda kuchapika kwenye uchaguzi huu. Sababu ni nyingi lakini vita ya kipumbavu dhidi ya Iran na Ukraine havita muacha salama
Pole

GOP watapoteza House lakini sio Senete, ni kama mwaka 2024, GOP walitamba na red Tsunami lakini bado Biden aliweza ku-control Senete.

2014 pamoja na Obama kupendwa ila Democrats walipigwa kipigo kitakatifu
 
Siielewi nime google inaleta vitu vingi. Kwa ufupi ni nini?
Wacha nikusaidie kidogo.
Wamarekani wana chaguzi kubwa tatu. Uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Maseneta na Uchaguzi wa wabunge.
Uchaguzi wa Rais ni kila baada ya miaka minne. Uchaguzi wa Maseneta term ni miaka 6. Uchaguzi wa wabunge term miaka miwili.

Kwahiyo uchaguzi ambao huhusisha chaguzi hizi zote tatu tatu ni uchaguzi Mkuu. Hufanyi ka kila baada ya miaka minne. Miaka miwili baada ya uchaguzi Mkuu kuna mid term elections. Hii ni kuchagua wabunge na Maseneta. Wabunge ni wote 436. Maseneta ni one third Yaani seneta Karibu 33 huchaguliwa kila baada ya miaka miwili.

Kwahiyo uchaguzi huu wa November wanaenda kuchagua one third ya senators na wanaenda kuchagua wabunge wote.

Ni uchaguzi Muhimu sana tu. tofauti tu na uchaguzi Mkuu ni hawachagui Rais.

Pia kuna uchaguzi wa Magavana kuongoza states. Kila state hufanya ratiba yake. Mwaka 2026 Magavana wengi wana uchaguzi. Kwahiyo November hii kazi ipo.
 
Ipo hivi: Mid term ni neno la kiingereza linaloamanisha katikati ya muhula au nusu muhula. Kwa hiyo midterm elections mana yake ni uchaguzi unaofanyika katikati ya muhula au uchaguzi unaofanyika baada ya muhula wa Rais unapofika nusu ya muda wake.
Huo muhula wenyewe ndiyo upi sasa? Ni kipindi kati ya uchaguzi mmoja wa Rais na uchaguzi unaofuata. Kwa Marekani muhula wa Rais ni miaka 4 hivyo Rais akitimiza miaka 2 madarakani (Midterm/Nusu muhula) uchaguzi unaoitwa midterm election hufanyika.

Uchaguzi huu huwahusu:
1. Wawakilishi
2. Seneti
3. Governors
4. Viongozi wote wanastahili kuchaguliwa ktk ngazi ya majimbo.
Ukilinganisha na uchaguzi wetu, uchaguzi huu unafanana na uchaguzi wetu wa serikali za mitaa ambao hufanyika mwaka 1 kabla ya uchaguzi mkuu.

Kwa kuwa Rais wa sasa wa USA, Donald Trump, alichaguliwa mwaka 2024 maana yake huu mwaka 2026 kipindi chake Cha uongozi kimetimiza nusu muhula kwani kitaisha mwaka 2028. Ndiyo maana uchaguzi wa Novemba mwaka huu unaitwa uchaguzi wa nusu Muhula.

Uchaguzi huu hauhusu Rais Bali viongozi niliowataja hapo juu. Uchaguzi wa Rais utafanyika mwaka 2028 na rai mteule ataapishwa na kuanza kazi January 2029.
 
Back
Top Bottom