RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 3,590
- 8,479
Haijalishi mnaoenda vyuoni mnaenda kusoma nini, kama ni engineering field, au Health field, au business field, au kada yeyote, jamii inahitaji output ya ulichoenda kusomea na sio umesomea nini.
Kwahiyo mzingatie elimu ngumu au course ngumu sio kwamba ndio elimu sahihi, msiende kuchagua course fulani kisa ajira zinapatikana kiurahisi kwa wakati huu, bali angalieni output mtakazotokanazo vyuoni baada ya kumaliza.
Utakuta mtu kasoma Mechanical engineering mwaka wa tano yuko mtaani, mwingine kasoma ualimu au accountant miezi kadhaa yuko ofisini au kinyume chake ikawa sahihi, muhitimu alienda kusoma ualimu ili apate ajira haraka, miaka kadhaa ikiisha yuko mtaani lazima achanganyikiwe. Suala kubwa nikutambua elimu ngumu inaweza kuwa sio elimu sahihi Kama output haitaonekana baada ya kuingia mtaani.
Kwahiyo wahitimu mchague kada kwa kuangalia baada yakumaliza mtatoa output chanya?. Vinginevyo utasoma Medical doctor halafu utakuja dharaulika na aliesoma takwimu.
Au unaweza soma Mechanical,civil, electrical,Biomedical, ukaja dharaulika nawale wakada ambazo uliziona za hovyo. Au ukasoma ualimu,uhasibu,sanaa,survey,diplomasia,Kama hutokuwa na output nzuri basi utaendelea kudharaulika.
Kipindi unasoma zingatia output unayo/utakayoenda kuitoa katika jamii.