nkumbison
JF-Expert Member
- Sep 22, 2013
- 2,219
- 2,971
Bado nakusoma na nazidi kukuelewa na kuyaelewa mengi zaidi. Maswali na comment zangu zitafuata kila ninapomaliza somo moja maana nimejipa muda wakuzielewa hizi nadharia kabla yakupractice!Melody ya Muziki- Melodic Contour and Melodic Motion
Mkong’osio au melody ndiyo sehemu kubwa ya muziki ambayo hukumbukwa sana na wasikilizaji kwani ndiyo inayoingia sana ubongoni mwa msikilazji; ni muungano wa sauti inayobadilika badilika kwa vipindi mbalimbali kadri muda unavyokwenda. Melody nzuri ni zile zinazofananana na mazungumzo yanayohusisha maswali na majibu; yaani zina vipindi vyenye msukumo au maswali (tension) sana na vipindi vyenye kuondoa msukumo huo au majibu ya maswali (tension release).
Post hii isome kwa makini sana kwa sababu ndiyo inajenga msingi wa kutunga nyimbo zinazoweza kuingia sana kwenye ubongo wa msikilizaji na hivyo zikawa za kukumbukwa kwa muda mrefu sana. Nadhani sehemu hii ndiyo ambayo wanamuziki wetu wengi sana hawaijui, kwani nimechambua nyimbo zao nyingi na kuona kama zinatungwa kwa uvumbuzi (intuition) tu na mara nyingi hazinagalii ukweli huu. Jikumbushe tena maana ya phrase na measure kwenye wimbo lama tulivyozijadili huko nyuma.
Kumbuka tena kuwa katika sauti zote 12 za kwenye Octave moja ni sauti saba tu zinashabihiana, ambazo mwanzoni tulizionyesha kwa namna za kirumi I-II-III-IV-V-VI-VII, tukimalizia na sauti ya nane VIII ambayo ni sauti ya kwanza kwenye kwenye Octave inayofuata. Zile sauti 12 za octave hujulikana pia kama chromatic scale, wakati sauti hizo saba zinazoshabihiana hujulikana kama diatonic scale. Sauti hizi za diatonic scale kuanzia ya chini hadi ya juu ndizo zina majina kama ifuatavyo kwenye jedwali hili:
Sauti Jina Matumizi I Tonic
Sauti za kupumzikia; hutumika mwanzo na mwisho wa phrase mojaII Supertonic III Meadiant
Sauti za kuhama kutoka na kuingia kwenye tonicIV Subdominant V Dominant
Sauti za Kuchangamsha, yaani zenye msukumo sanaVI Submediant VII Leading tone VIII Next tonic Sauti ya kupitia kuingia na kutoka kwenye octave inayofuata.
Kwenye utunzi wa melody sauti hizi zimegwawanya katika mafungu mawilii; yaaini stable tones na unstable tones. Sauti za Tonic, Mediant na Dominant ndiyo ndiyo stable tones, halafu zile Supertonic, Subdominant, Submediant, na Leading tones ni unstable tones. Tonic (I) ni stable zaid ya ikifuatiwa na Dominant (V) na kuishia na Mediant (III) kwa stability. Sauti ya Leading note (VII) ndiyo ambayo ni unstable zaidi ikifuatiwa na Sebmediant (IV) halafu Supertonic(II) na kushia na Subdominant (VI). Picha hii inaonyesha mlingano wa stability katika sauti hizo.
View attachment 1183739
Kwa waliofanya physics ya pendulum ukihusisha na potential energy, mnajua kuwa pendulum bob ikiwa inaning’ia freely chini ya kamba yake inakuwa stable kwa sababu potential energy ni ndogo sana; ukiiacha katika position hiyo, itabaki imepumzika pale pale, ila ukiihamisha kutoka hiyo stable position, basi itaanza kuswing kujaribu kurudi kwenye stable position yake. Ina maana unapoihamisha kutoka kwenye stable position yake basi unaiweka kwenye unstable position ambayo siyo comfort zone yake.
View attachment 1183740
Sauti za diatonic scale pia zina tabia hiyo hiyo, hizo unstable tones zinakuwa zinamfanya msikilizaji atake zirudi kwenye kweye stable tones. Siku zote Leading tone itapenda kuingia kwende Dominant siku zote, na Submediant nayo itapenda kuingia kwenye Dominant siku zote. Sauti za Subdominant nazo zitapendwa kwenye kwenye Dominat kwa vile ni stable zaidi ya Mediant; hata hivyo inaweza kwenda kwenye Mediant na kukubalika. Supertonic nazo zitapenda zaidi kwende kwenye tonic kwa vile hiyo ni stable zaidi ya median, lakini pia zinaweza kuingia kwenye mediant na kukubaliwa bila matatizo yoyote.
View attachment 1183741
Kama tulivyosema huko nyuma wimbo mzuri huanza kwa sauti za Tonic au Supertonic lakini pia unaweza kuanza na Dominant kwa vilanayo ni stable tonic, lakini ni lazima kushia na sauti za Tonic kwa vile hiyo ndiyo sauti stable kuliko zote. Kutoka kwenye sauti stable na kelekea kwenye sauti unstable kunaweka msukumo mkubwa yaani tension ambayo humfanya msikilizaji atake iondolewe kurudi kwenye stable tena ambayo ndiyo comfort zone ya ubongo; kipindi hicho cha sauti unstable kinajulikana kama Continuation, kwamba ukishaiingia kwenye unsatable tone, basi msikilizaji anategemea uendelee ili urudi kwenye stable tone tena. Continutiation hutokea sehemu yotote katikati ya phrase, kabla phrase haijaisha lazima tension iondolewe kwa kiasi fulani. Wakati tension inaondolewa, inaweza kurudi kwenye stable kabisa yaani Tonic au kwenye less stable za Dominant au Median. Mapumuziko katika stability tone ya tonic inaitwa Finality, yaani hali inayomuashiria msikilizaji kuwa mambo yamekwisha. Mapumizko katika satuti za Dominant au Submediant yanajulikana kam Temporary repose, yaani mapumziko mafupi yanayompa msikilizaji nafasi ya kupumua akijua kuwa safari bado inaendelea.
Kwa kawaida melody nzuri hairudi kwende Tonic kabla shairi lote halijaisha, kwa hiyo wakati wa kumaliza phrase ndani ya shairi unaweza kuingia kwenye Mediant au Dominant, yaani temprora repose lakini usiashiririe finality. Kuondoa tension kabisa, yaani finality, hutokea mwisho kabisa wa shairi ambapo ndipo unarudi kwenye Tonic. Melody inatakiwa iwe inamjaza msikilzaji tension yaani upepo, na kuuondoa kidogo na kujaza tena na kuondoa kidogo hadi kufikia mwisho ndipo unaaondoa upepo wote na kufanya ubongo upumzike tena. Mambo haya ya kumjaza msikilizaji upepo na kuuonda hufanyika pia kwenye Vibwagizo Tangulizi, Vibwagizo na Vivuko; Utangulizi ni sauti unstable tu, Tamatisho ni sautu stable tu lakini Mapumuziko piayanachanganya suti satble na unstable tu. Hata hivyo, kwa vile Vibwagizo tangulizi vinamtayarisha msikilizaji kuskia kibwagizo, huwa haviishii na Tonic, vinaweza kuishia na Mediant au Dominant.
Melodic Motion na Melodic Contour
Mtungaji wa wimbo, iIangalie melodi kama safari ya kupanda mlima wenye maumbile (contour) mbalimbali zenye vilima na mabonde yanayoruhusu mapumziko kidogo ndani na kisha mwishoni ni kushuka chini kabisa; safarihiyo hujulikana kama melodic contour. Upandaji, mapumziko na kushuka huo mlima hujulikana kama melodic motion. Kila utunzi una contour yake; safari inaweza kuanza kwa kuingia bondeni kabla ya kupanda tena, na vile vile inaweza kuanza kwa kurukia juu klabisa ya mlimna na baadaye kuanza kutua. Contours zenye tension (contiuation) nyingi na mapumziko ya kati (temporary repose) mengi kabla ya kufikia mwisho (finality) hufanya ubongo wa msikilizaji kuwa busy sana na iwapo unapanda kwa spidi sana, yaani kama BPM yake ni kubwa sana basi unaweza kumchosha kuzikiliza haraka sana. Kukiwa na uwiano mzuri kati ya BPM na wingi wa vilima na mabonde kwenye controur hiyo, basi msikilzaji ataburudika sana na ataupenda sana wimbo huo.
Melodic contour nzuri ni ile yenye mlingano mzuri kati kupanda na kushuka na ina kilele (peak au sauti ya juu kabisa) moja tu, ambacho kinatakiwa kwenye sehemu ya pigo moja kubwa kwenye rhythm yako. Tofauti kati ya sauti yza chini kabisa sauti ya juu kabisa hitwa range. Melodic contrours zenye range kubwa ndizo zenye tension sana na vile vile ndizo zinazosisimua sana kuliko zile zenye range ndogo. Mifano ya michache ya melodic Contours ni kama hizi zifiatayo; kila sehemu tambarare (palateau) ni sehemu ya kuondolea tension na kwenye slope ni sehemu yenye kujaza tension.
View attachment 1183750View attachment 1183751
Mahairi ya wimbo wa Kwangaru wa Harmonize yanatumia melodic contour rahisi kama hii lakini yana peak moja kwa kila shairi, na range ya wimbo ni kubwa sana, ndiyo maana wimbo huo umekubalika sana, hauchoshi kirahisi.
View attachment 1183753
Ingawa kibwagizo chake kina contour tofauti.
Kwenye mwendo huo wa melodic motion, kutoka point moja hadi nyingine, sauti zitakuwa zinabadilika kwa kutumia mojawapo ya style nne: (a) sauti zinazojirudia (repeats) kwa mfano kutoka sauti C hadi sauti C tena; (b) sauti zinazoruka kwa noti moja moja kwenda juu au chini (steps) kwa mfano kutoka sauti C mpaka sauti D kwenye C-major; (c) sauti zinazoruka noti mbili kwenda juu au chini (skips) kwa mfano kutoka sauti C mpaka sauti E kwenye C-major, na (d) sauti zinazoruka zaidi ya noti mbili kwenda juu au chini (leaps) kwa mfano kutoka sauti C mpaka sauti G kwenye C-major. Picha hii inaonyeshaa style hizo.
View attachment 1183756
Ili kupata uwiano mzuri kati kati ya kupanda na kushuka kwenye contror yako, ukianza na steps kadhaa za kwenda upande mmoja, basi jaribu kuweka skips au leaps za kurudi upande ulikotoka kidogo kabla ya kurudi kwenye upande wa kwanza tena kama bado unaendelea, ila bila kuingia kwenye sauti stable tones. katika kufanya hivyo, punguza sana matumizi ya repeats kadri iwezekanavyo, na vile vile usiwe na steps nying sana.
Kati ya mapungufu makuu ya wimbo wa Diamond wa My Number one original ni kuwa una steps na repeats nyingi sana na vile vile hauna peak inayojulikana wazi wazi kwenye kila phrase, yaani range yake ilikuwa ndogo sana; hivyo ilikuwa ni rahisi kwa wimbo huo kuchosha msikilizaji wake haraka sana. Remix waliyofanya Davido ilirekebisha sana makosa hayo wakabadilisha steps nyingine kuwa skips na hivyo kuweza kuwa na peak kubwa kidogo kuliko mwanzo. Kupendwa wa My Number One remix hakutokani na davido tu bali vile vile ile balance ya tension na tension release iliyokuwapo kwenye wimbo huo tofauti na ule original ambao haukuwa na tension kabisa.
Katika Makala ijayo, nitaongelea dhana tatu kubwa kabla ya kuanza kutunga melodies zetu wenyewe na kuchambua melodies za waimbaji wengine; dhana hizo zitakuwa ni articulation, melodic motiffs na melodic phrases.
Tuendelea kutumia sauti za diatonic major na minor scales tu japokuwa kuna scales nyingine nyingi ambazo siyo diatonic (non diatonics scales), na ambazo siyo diatonic ambazo siyo major au major au minor (zinaitwa diatonic scale modes), lakini kama nilivyotambulisha huko nyuma, mambo hayo tatawaachia maveterani tu. Sisis tutatumia diatonic major na diatonic minor tu.
Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz , Frega Bao,MRI; nadhani mjadala huu hili kuhusu melodic motion na melodic contours za nyimbo umeeleweka. Nimegundua kuwa kabla ya kuanza mjdala juu ya utungaji wa mkong'osio wa wimbo bado kuna mambo ya msingi kujadilia.katika mada ijayo tutajadili articulation, melodic motiffs na melodic phrases
Tupo pamoja maan naupenda sana muziki kuanzia kuuimba mpaka kuuandaa ila natumia kipaji zaidi so hapa pananitamanisha ku deal na hii elimu kiundani zaidi.