Elimu na nadharia ya muziki

MIZANI KUU ZA MUZIKI (Major Scales- cont'd)-TOLEO LA PILI

Katika toleo hili tutaangalia major scales zenye flats; zote pia huundwa kwa sauti zinazoruka hatua kwa mfumo KKN-K-KKN. Note za asili kwenye Octave zinakuwa ni C- D♭-D- E♭-E-F- G♭-G - A♭- A- B♭-B-C wakati zile sharp zimebadilishwa na flat zenye sauti sawa. Vile vile tunaanza na mizani ya kwanza ambayo ni C-major, halafu mizani inayofuata inatumia sauti ya nne ya sauti iliyopita ikiwa na flat kwenye mizani hiyo;

C-Major
Hii mizani ya C-major tumeiona katika toleo lililopita. Haina sharp wala flat yoyote ikiwa na sauti za C-D-E-F-G-A-B-(C ). Mizani inayofuatia ikiwa na flat itakuwa ni F-major kwa vile sauti ya nne katika C-Major ni F

1152986


Labda niongezee kwenye maelezo yangu ya awali kuwa wimbo wa
It's All Coming Back To Me Now wa Céline Dion umo katika C-major, lakini unatumia sauti zinazojaza Octave mbili na nusu.

F-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya F utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti F- G♭-G - A♭- A- B♭-B- C- D♭-D- E♭-E-F. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za F – G – A – B♭ – C – D – E – F ambamo sauti B ni flat; hii inaonyeshwa kwa kuwekwa alama ya flat kwenye mstali wa kwanza kutoka juu kwenye note B. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni B♭-major kwa vile sauti ya nne kwenye F-major ni B♭.
1152987

Nyimbo za
Blank Space wa Taylor Swift na Locked Out of Heaven wa Bruno Mars zimeimbwa katika mizani hii ya F-Major. Labda niongezee pia kuwa wimbo wa Taifa wa Tanzania nao pia umeibwa katika F-major:
1153056




B♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya B♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti B♭-B- C- D♭-D- E♭-E- F- G♭-G - A♭- A- B♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za B♭ – C – D – E♭ – F – G – A – B♭ ambamo sauti za B na E ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni E♭-major kwa vile sauti ya nne kwenye B♭-major ni E♭.
1152990


Nyimbo za
Irreplaceable wa Beyoncé na Rocket Man wa Elton John zimeimbwa katika mizani hii ya B♭-Major.


E♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya E♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti sauti E♭-E- F- G♭-G - A♭- A- B♭- B- C- D♭-D- E♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za E♭ – F – G – A♭ – B♭ – C – D – E♭ ambamo sauti za A, B na E ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni A♭-major kwa vile sauti ya nne kwenye E♭-major ni A♭.

1152997


Nyimbo za In
My Head wa Jason Derulo na Valerie wa marahemu Amy Winehouse zimeimbwa katika mizani hii ya E♭-Major.

A♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya A♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti A♭- A- B♭- B- C- D♭-D- E♭-E- F- G♭-G-A♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za : A♭ – B♭ – C – D♭ – E♭ – F – G – A♭ ambamo sauti za A, B,D, na E ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni D♭-major kwa vile sauti ya tano kwenye scale hii A♭-major ni D♭.

1153002

Nyimbo za
Happy wa Pharrell Williams na The Power of Love wa Céline Dion zimeimbwa katika mizani hii ya A♭-Major.

Mizani zinazofuata nimeziweka kwenye rangi tofauti pia kama kwenye toleo lililopita kwa vile tutaziangalia tena huko baadaye, kuona kuwa zinafanana na mizani nyingine; zinajulikana kama Enharmonic Major Scales

D♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya D♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti D♭-D- E♭-E- F- G♭-G-A♭- A- B♭- B- C- D♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za D♭ – E♭ – F – G♭ – A♭ – B♭ – C – D♭ ambamo sauti za A, B, D, E, na G ni flat. Scale yenye flat inayofuatia hii itakuwa ni G♭-major kwa vile sauti ya tano kwenye D♭-major ni G♭.
1153003

Kwa vile scale hii ya D♭ ni sawa kabisa na scale ya ya C# kama tutakavyoona kwenye post inyofuata, basi nyimbo za Nyimbo za Sacrifice wa Elton John, na Umbrella wa Rihanna zilizoimbwa katika mizani ya C-Sharp zimo pia katika mizani hii ya D♭-Major.

G♭-Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya G♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti G♭-G-A♭- A- B♭- B- C- D♭-D- E♭-E- F-G♭. Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za G♭ – A♭ – B♭ –(B) C♭ – D♭ – E♭ – F – G♭ ambamo sauti za A, B, C, D, E, na G ni flat. Angalia kuwa sauti ya nne (B) imegeuzwa kuwa C-flat kusudi kusiwe na B mbili zenye mkazo tofauti- C flat ni sawa na B. Scale yenye flat inayofuatia hii sasa itakuwa ni C♭ -major kwa vile sauti ya tano kwenye G♭ -major ni hiyo ya C♭.
1153005

Kwa vile scale hii ya G♭ ni sawa kabisa na scale ya ya F# kama tutakavyoona huko mbele pia, basi nyimbo za Nyimbo za Beat it wa Michael Jackson, Rude Boy wa Rihanna na Born this way wa Lady gaga zilizoimbwa katika mizani ya F-Sharp Major zimo pia kwenye mizani hii ya hii ya G♭-major.

C♭ -Major
Ukichukua sauti za asili zinazoanza na sauti ya C♭ utakamilisha mizani kwa kutumia OCTAVE mbili zenye sauti (B)C♭ C- D♭-D- E♭-E- F-G♭-G♭-G-A♭- A- B♭-(B)C♭ . Kwa hiyo ukichagua sauti za kufuata mtindo huo huo wa KKN-K-KKN utapata mzani wenye sauti za C♭ – D♭ – E♭ – F♭ – G♭ – A♭ – B♭ – C♭ ambamo sauti zote ni flat.

1153006


Scale hii haitumiwi sana na wanamuziki.Katika nyimbo maarufu zinazojulikan, sijawahi kusikia wimbo uliotolewa kuwa ni C♭ -Major, ila kunakuwa na nyimbo za B-major, kwa vile hizi ni scale zinazofanana kama nitakavyoeleza huko baadaye basi nyimbo zote za B-major pia ni za C♭ -Major.


Baada ya hapo, mizani ya F♭ haiwezekaniki kwa sababu kama tulivyoongea kutokuwezekana mizani ya G♯- huko nyuma.
 

Attachments

  • 1563053816268.png
    1563053816268.png
    3 KB · Views: 58
  • 1563072914293.png
    1563072914293.png
    37.8 KB · Views: 66
MIZANI KUU (Major Scales): Enharmonic Major Scales- Toleo la tatu

Toleo la kwanza lilionyesha mizani kuu nane za C-Major, G-Major, D-Major, A-Major, E-Major, B-Major, F♯-Major, C♯ -Major. Katika toleo hilo mizani tatu za B-Major, F♯-Major, C♯ -Major ni Enharmonic Major Scales

Toleo la pili lilionyesha mizani nane pia za C-Major, F-Major, B♭-Major, E♭-Major, A♭ -Major, D♭-Major, G♭-Major, C♭-Major. Katika toleo hilo mizani tatu za D♭-Major, G♭-Major, C♭-Major ni Enharmonic

Kwa jumla tunakuta mizani 16, ila kwa vile C-major imeonekana katika toleo la kwanza na la pili, tunabaki na mizani 15 tu.

Sasa nataka tuziangalie hizo mizani za Enharmonic katika matoleo yote mawili.

  • Sauti za kwenye B-Major ambazo ni B – C♯ – D♯ – E – F♯ – G♯ – A♯ – B ziko sawa kabisa na zile za kwenye C♭-Major ambazo ni C♭ – D♭ – E♭ – F♭ – G♭ – A♭ – B♭ – C♭, kwani ukiondoa flats kwenye sauti za C♭-Major na kuziwekea sharp zinazofanana unapata B – C♯ – D♯ – E – F♯ – G♯ – A♯ – B. Kwa hiyo C♭-Major siyo maarufu sana kwa vile hakuna kibonyezo cheusi cha C♭ kwenye piano. Badala ya C♭-Major ni B-Major ndiyo hutumika.

  • Tukiangalia sauti za F♯-Major ambazo ni F♯ – G♯ – A♯ – B – C♯ – D♯ – E♯ – F♯ na kuzilinganisha na zile za G♭-Major ambazo ni G♭ – A♭ – B♭ –(B) C♭ – D♭ – E♭ – F – G♭, tunaona kuwa hizi nazo ni zile zile Kwa vile hakuna kibonyezo cheusi cha E# kwenye piano, ni scale ya F#-Major haitumiki sana, badala yake G♭-Major major ndiyo hutumia.

  • Vile vile tukiangalia sauti za C♯-Major ambazo ni C♯ – D♯ – E♯ – F♯ – G♯ – A♯ – B♯ – C♯ na kuzilinganisha na zile za D♭-Major ambazo ni D♭ – E♭ – F – G♭ – A♭ – B♭ – C – D♭, tunaona kuwa hizi nazo ni zile zile. Sasa kwa vile kibonyezo cheusi cha B# kwenye piano hakipo, mizani ya C♯-Major nayo haitumiki sana, badala yake D♭-Major ndiyo hutumika.

Kwa pamoja tunabaki ni mizani kuu 12 tu kama ifurtavyo: C-Major, G-Major, D-Major, A-Major, E-Major, B-major, F-Major, B♭-Major, E♭-Major, A♭ -Major, D♭-Major, G♭-Major.


Watu wanaoanza kufanya sanaa ya muziki wanashauriwa kuwa wachague kama mizani tatu au nne tu za kutumia mara kwa mara mpaka wazizowee na kujiua undani wake ndipo waanze kuingia kwenye mizani nyingine.


Katika maelezo haya ya ujenzi wa ya mizani kuu nilikwenda ndani sana ili kuonyesha misingi yake. Baada ya kujua misingi hiyo, nitatoa malezo mafupi sana kwenye ujenzi wa mizani ndogo kwa vile ujenzi huo unafuata mising hii hii. Katika post ijayo nitazungumzia mizani ndogo (Minor scale) ambazo hutumiwa zaidi kwenye nyimbo za huzuni.

Ngoja niwaache kwa burudisho hili la watoto wa undergraduate wa kimarekani miaka hiyo ya themanini wakiwa kwenye fraternity house wakicheza mduara wao baada ya kumaliza mitihani; muziki huu uliimbwa katika D-major.




nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles
 
Mwalimu Kichuguu bora umeamua kuhamia darasa la muziki. Siasa mwachie dakta John.
Hapana, sijaacha mijadala ya kisiasa au ya aina yoyote ile. Nimeona kuwa kwa vile mimi ni mwanamuziki niliyobobea kiutaalamu na sijawahi kushea na wanachama hapa huo utaalamu wangu, nikaona ngoja nitumie siku chache kuuanika utaalamu wangu hapa kwa lugha rahisi kadri nitakavyoweza.

Huwezi kujua ni nani atafaidika nao kwani najua elimu ya muziki haifundishwi vizuri Tanzania; ndiyo maana tuna wanamuziki mastaa wanatoa miziki isiyokidhi viwango, yaani wanakuwa na vipaji lakini hawana misingi. Nadhani mchango wangu huu utawasidia baadhi yao kuwajenga misingi ya muziki kusudi wakichanganya na vipaji vyao basi watoe muziki mzuri. Mimi ni mwanamuziki mzuri sana nilifundishwa utaalamu wa muziki mapema sana lakini sikuutumia kujipatia mkate wangu wa kila siku ingawa nina bendi kamili nyumbani kwangu pamoja na familia yangu kwa ajili ya burudani yetu sisi wanafamilia tu.
 
MIZANI NDOGO (Minor Scales)

Kabla ya kuanza kutambulisha minor scales, nataka tuelewe sauti zake. Scale yenyewe ina sauti nane kama tulivyoona kwenye major scale

I-II-III-IV-V-VI-VII-VIII

Ambapo sauti hizi zina majukumu kwenye wimbo kama ifuatavyo:

  • Sauti I na sauti II zinaitwa Tonic na Supertonic kama ilivyo kwenye major scale. Hizi ni sauti za kuanzaia na kumalizai shairi.
  • Sauti III an sauti IV zinaitwa Mediant na Submendiant kama ilivyo kwenye major scale: hizi ni sauti za kuingilia au kutokea kwenye Tonic na Supertonic kama ilivyo kwenye major scale.
  • Sauti V na sauti VI ndizo sauti za kuchangamsha. Hizi ni pungufu kuliko kwenye major scale, ndiyo maana miziki ya namna hii inajulikana kama ya maombolezo. Sauti hizi zinaitwa Dominant na Submediant.
  • Sauti VII na sauti ni Subtonic na Tonic zinazotumika kuhamia kwenye octave nyingine iwapo wimbo unatumia Octave Zaidi ya moja.

Kitu cha kuona wazi hapa ni kuwa minor scale ina sauti sita tu kwenye kila Octave wakati major scale ina sauti saba.

Nilitambulisha huko nyuma kuwa kuna natural minor, harmonic minor, na melodic minor. Scale kuu ya minor ni hiyo ya natural minor ambayo ndiyo tutakayojadili hapa. Harmonic minor hupandisha juu kwa nusu hatua sauti ya saba, yaani Subtonic, wakati melodic minor hupandisha juu kwa nusu hatua sauti ya sita na ya saba, yaani submediant na subtonic.



A-Minor

Wakati major scale zinaundwa kwa kuanza na sauti C, minor scale zinaundwa kwa kuanza na sauti A. Sauti zinazofuata zinachaguliwa kwenye OCTAVE kwa kuruka nyingine kulingana na utaratibu wa KNK-KNK+K kama nilivyoeleza huko nyuma. Kuanzia na A sauti 12 za zilizopo ni

A-A#-B- C-C#-D-D#-E-F-F#-G-G#- A

au

A-Bb-B- C-Db-D-Eb-E-F-Gb-G-Ab- A



Kwa hiyo tukifuata utaratibu wa KNK-KNK+K tunapata scale ya kwanza ambazo ni A –Minor kama ifuatavyo A-B-C-D-E-F-G-A. Ni scale ambayo haina sharp au flat yoyotre. Hii ndiyo minor scale rahisi kuliko zote.

Baada ya mizani ndogo ya ya A, mizani inayofuata huchaguliwa ama kwa kuchukua sauti ya tano na kutumia sharp, au kuchukua sauti ya nnne kutumia flat kama tulivyoona kwenye maelezo ya mizani kuu toleo la kwanza na la pili huko nyuma.

E-Minor

Scale ya minor yenye sharp inayofuata A-Minor itaanza na sauti E kwa vile hiyo ndiyo sauti ya tano kwenye A-Minor; itatokana na sauti za E-F-F#-G-G#- A-A#-B- C-C#-D-D#-E na kwa kufuata utaratibu wa KNK-KNK+K itakuwa na sauti zifuatazo E – F♯ – G – A – B – C – D – E



D-Minor

Scale ya minor yenye flat inayofuata A-Minor itaanza na sauti D kwa vile hiyo ndiyo sauti ya nne kwenye A-Minor; itatokana na sauti za D- E♭- E-F- G♭-G- A♭- A- B♭-B- C- D♭-D na kwa kufuata utaratibu wa KNK-KNK+K itakuwa na sauti zifuatazo D – E – F – G – A – B♭ – C – D.

Kwa utaratibu huo huo unaweza kujenga lis nzima ya mizani ndogo. List hii nimeionyesha kwenya jedwali hapa chini; zile mizani zilzozungushiwa box jekundu ni Enharmonic Minor scales. Kwa kutumia uchambuzi kama tulivyofanya kwenye major scale, tunaona kuwa A♭ ni na G#-minor. Ila kwa vile A♭-Minor inatumia sauti ya C♭ ambayo haina kibonyezo cheusi kwenye piano, basi huwa haitumiki, badala yake Scale yote inakuwa ni G#-minor tu. Vile vile scale za B♭-minor A#-minor zina sauti zile zile, ila kwa vile A#-minor inahitaji kibonyezo cheusi cha cha E#, basi scale zote mbili hujulikana kama B♭-minor.
1153049


Tatizo linalowakoroga watunzi wengi ni pale wanapotaka E♭-minor au D#-minor. Scale hizi zote zina sauti zile zile, kwa hiyo ni scale ile ile moja. Tatizo ni kuwa E♭-minor inahitaji kibonyezo cheusi cha C♭ ambacho hakipo, na vile vile D#-minor inahitaji kibonyezo cheusi cha E# ambacho pia hakipo. Kwa hiyo utunzi na upigaji wa muziki katika scale hizi huwa ni kazi ngumu sana inayofanywa na maveterani wa muziki tu.

Kwa hiyo kuna scale 12 za minor kama ifutavyo: A- Minor, B-Minor, F#-minor, C#-minor, G#-Minor, G-Minor, C,Minor, F-Minor, B♭-Minor, na ama E♭-minor au D#-minor.

Baada ya kutambulisha namna ya kuchagua sauti zinazokubalina kwenye muziki kama Major Scale au Minor scale. Nitapumzika kidogo kabla sijaaza kujadili namna ya kutumia sauti hizo katika kutunga muziki wenye mshiko.
 
PHRASES AND MEASURES:

Muziki wowote, hata ule unaopigwa na chombo kimoja tu una sifa kuu kuwa ni sauti inayobadilika badilika. Katika post zilizopita tuliongelea sauti tu yaani pitch au note, tukaelezea kuwa kuna sauti kumi na mbili zinajulikana kwa pamoja kama Octave moja, na kuna jumla ya Octave 9 kamili kuanzia sauti ya chini hadi sauti ya juu ingawa nilionyesha Octave saba tu kwenye mifano mmoja huko nyuma.

Vile vile tukaeleza kuwa kati ya sauti hizo kumi na mbili ni saba tu zinazoshabihiana kwenye wimbo, ambazo zinaiwa music scales au mizani. Kuna mizani kuu 12 za muziki wa kuchangamasha (Major scales), na mizani nyingine ndogo 12 za muzikia wa kupoza (Natural Minor scales). Katika hizo mizani ndogo, kila moja inaweza kubadilishwa kuwa ama melodic minor au harmonic minor na tukaeleza namna ya kufanya mabadiliko hayo.

Jambo ambalo hatukuliongea katika hizo mizani ni kitu kinachoitwa music modes. Kwa sasa jambo hilo ama tutawaachia maveterani wa muziki au tutaliongelea huko mbeleni. Tutaendelea maelezo yetu kwa kutumia hizo major scales na minor scales tulizokwishatambulisha.

Ubadilikaji wa sauti ndani ya muziki umegawanyika katika vina (phrases) ambavyo vina urefu usiozidi na muda ambao binadamu anaweza kuimba bila kupumua, takribani sekunde 30 hivi. Mwisho phrase ndio hutoao nafasi ya mwimbaji kupumua; kwa hiyo phrase huwa inaishia na sauti za Tonic na Supertonic.

Kwenye kila phrase kuna vipimo (measures) kadhaa, na kila kipimo kina mapigo (beats) kadhaa. Kwa kawaida phrase moja yaweza kuwa na measures kati ya mbili hadi 8 kwani siyo kawaida phrase moja kuwa maeasure zaidi ya nane. Vile vile measure moja yanaweza kuwa mapigo mawili hadi 12, siyo kawaida kuwa na mapigo zaidi ya kumi na mbili. Miziki mingi hutungwa kuwa na measures nne kwa phrase, na mapigo mawili hadi nane kwa measure.

Muziki mmoja unaweza kuwa na phrases moja au zaidi, lakini phrases zote ziko katika mpangilio huo. Miziki ambayo ina mashari na vibwagizo, phrases za vibwagizo zaweza kuwa tofauti na phrases za mashairi makuu.

Katika post hii nitapenda kuelezea dhana ya phrases na measures kwanza, halafu baadaye huko mbeleni ndipo nitazungumzia beats kwa kina, kwani hizo ndizo zinatawala katika kuuelezea muziki wenyewe . Kwenye staff ya sauti, measure moja huishia na mstali wa wima (bar line) mmoja kama ionekanavyo kwenye picha hii hapa chini. Kwa bahati mbaya, hakuna alama ya kuonesha mwisho wa phrase, ila wanamuziki wanaijua kwa kuangalia measures zinazoishia na sauti za Tonic au Supertonic
1155390



Ili kuelewa measures, tuangalie haya mashairi ya wimbo wa taifa. Kila mstali kwenye mashairi haya ni phrase moja na kila phrase measures mbili. Kwa hiyo mwimbaji anapumzika kidogo na kuvuta pumzi kila baada ya mstali mmoja wa wimbo huu. Kibwagizo chake pia kina phrases zenye measures mbili mbili, ila phrase ya mwisho ina measure moja tu, ebu uuangalie kwanza mashari yake hapa chini.

1. Mungu ibariki- Afrika
Wabariki Viongo-zi wake
Hekima Umoja na- Amani
Hizi- ni ngao zetu
Afrika- na watu wake.

Kibwagizo:
Ibari-kiii Afrika,
Ibari-kiii Afrika
Tubari-kii watoto wa
Afrika.

2. Mungu ibariki- Tanzania
Dumisha uhuru- na Umoja
Wake kwa Waume na- Watoto
Mungu -Ibariki
Tanzania na-watu wake.

Kibwagizo:
Ibari-kii Tanzania,
Ibari-kii Tanzania
Tubari-kii watoto wa
Tanzania.

Mpangilio wa sauti zake ni huu hapa chini: achilia mbali makossa ya Kiswahili yaliyofanywa na mwandikaji wake, lakini sauti zimepangiliwa kama ilivyo kwenye wimbo wenyewe.
1155391

1155392

1155393



Maneno au herufi zilizoko chini ya alama ya sauti fulani kweye staff huimbwa kwa kutumia sauti inayowakilishwa na alama iliyo kwenye nafasi hiyo. Kwa mfano kwenye phrase ya kwanza, measure ya kwanza ina herufi Mun,gu,i,ba,na ri, wakati measure ya pili ina herufi za ri,A,ri, na ka. Herufi hizi zinawakikilishwa na sauti kama ifuatavyo kwenye jedwali hili hapa chini.
HerufiMunguibarikiAfrika
SautiFEFGAAGGF
Kwa vile wimbo huu uko kwenye mizani F-major, tunaona pia phrase yake inaanza na sauti F na kuishia sauti F.

Vifimbo na vibendera vilivyoko kwenye alama za notes hizo zinaonyesha urefu wa muda unaotumiwa na sauti hiyo; hilo tutalijadili baada ya kuzungumzia dhana ya beat kwenye post ijayo. Pigo moja linaweza kudumu kwa muda wowote, kwa hiyo ni lazima kueleza kwa uwazi kuwa udumu wa pigo moja la muziki husika ni muda gani ili kusudi mwimbaji mmoja asiimbe wimbo huo huo kwa saa moja wakati mwingine anauimba kwa nusu saa. Kwa mfano waimbaji hawa wa wimbo wa taifa wametumia mapigo tofauti kwa wimbo ule ule, ingawa waimbaji hao wa t-Shirt and Jeans hawakuuimba katika B-flat major bali wameimba katika B-flat minor na kubadilisha kabisa kibwagizo chake.







Nadhani video hizo tatu za wimbo mmoja zimeonyesha kiuwazi maana ya pigo na jinsi gani pigo linavoathiri mwendokasi wa wimbo wote. Katika post ijayo nitaongelea kwa kina mapigo (beats) ya muziki na matumizi yake katika tungo.

Kwa bahati mbaya sana watu wengi wanaposema neno beat huongelea rhythm na melody badala ya beat yenyewe; hili ni kosa linalofanywa na watu wote duniani hasa katika hii miziki inayotungwa electronically. Utawasikia watu wekisema kwa mfano biti za nyimbo za WCB zinatungwa na Laizer, lakini siyo kweli kwani Laizer anatunga melody na rhythms tu. Ni kama ambavyo melody na rhythms zilizotumiwa kwenye nyimbo nyingi za Michael Jackson zilivyotungwa na Quincy Jones na bado anamiliki tungo hizo hadi leo.
 
BEATS, TIME SIGNATURE AND TEMPO

BEATS


Beat ni kipimo cha muda kinachotumiwa kwenye muziki. Mojawapo ya matokeo ya muziki unapoingia ubongoni ni kusababisha viongo fulani vya mwili vitake kuchezacheza kwa kujirudia rudia. Kwa mfano, muziki unaweza kumfanya mtu awe anapiga mguu wake chini kwa mtindo fulani wa kujirudiarudia katika kila baada ya muda fulani: muda huo wa kukamilsha mwondoko mmoja ndiyo beat (pigo). Inawezekana pia mtu akwa anachezesha chezesha kichwa chake kwa mtindo fulani unaojirudia rudia,- muda anatumia kukamilisha kichwa kutoka sehemu moja hadi kurudi pale ndiyo beat.

Angalia miondoko ya miguu na vichwa vya wanamuziki wa wimbo huu hapa chini; miondoko hiyo ndiyo beat yenyewe.



Kama muziki unapigwa na watu wengi, ni kawaida pia kuwa na conductor anayesimama mbele ya wote na kuwa anachezeshachezesha mikono yake kuasihiria beat inayotumika. Kwenye miziki ya marching akama vile kwenye gwaride la kijeshi, beat huamuliwa na ngoma kubwa. Lakini pia huweza kuwa na conductor anayekuwa na kifimbo kinachochezeshwa kuashiria beats. Angalia miondoko ya mikono ya conductor (huyo aliyesimama mwenye jacket jeupe) wa nwimbo huu; miondoko hiyo ndiyo inashiria beat yenyewe.




Beat hutambulishwa kwa kutumia urefu wa muda unaotumiwa noti kamili au mojawapo ya vipande vyake ambavyo huonyeshwa kwa kuunganisha mlingoti na vibendera kwenye note za sauti hizo kama ifuatavyo.


1155556
Yai jeupe lenye mistali miwili kila upande huwakilisha noti mbili kamili; unajulikana kama unajulikana kimuziki kama Breve.

1155557
Yai jeupe huwakilisha noti kamili; unajulikana kimuziki kama Semibreve.

1155558
Yai jeupe lenye mlingoti wa juu au wa chini huwakilisha nusu noti; unajulikana kimuziki kama Minim.

1155559
Yai jeusi lenye mlingoti wa juu au wa chini huwakilisha robo noti; unajulikana kimuziki kama Crotchet.

1155560
Yai jeusi lenye mlingoti wa juu au wa chini na bendera moja huwakilisha sehemu 1 ya 8 ya noti kamili; unajulikana kimuziki kama Quaver. Bendera za quaver mbili au zaidi zinazofuatana huunganishwa kama inavyookenana hapo.

1155562
Yai jeusi lenye mlingoti wa juu au wa chini na bendera mbili linadumu huwakilisha sehemu 1 ya 16 ya noti kamili; unajulikana kimuziki kama Semiquaver. Bendera za semiquaver mbili zinazofuatana huunganishwa kama inavyookenana.

1155564
Yai jeusi lenye mlingoti wa juu au wa chini na bendera tatu huwakilisha sehemu 1 ya 32 ya noti kamili; unajulikana kimuziki kama Demisemiquaver. Bendera za demisemiquaver mbili zinazofuatana huunganishwa kama inavyookenana.

1155566
Yai jeusi lenye mlingoti wa juu au wa chini na bendera nne huwakilisha sehemu 1 ya 64 ya noti kamili; unajulikana kimuziki kama Hemidemisemiquaver. Bendera za hemidemisemiquaver mbili zinazofuatana huunganishwa kama inavyookenana.


Urefu wa kila noti (sauti) unaweza kuongezwa kwa nusu kipimo chake iwapo sauti imefuatiwa na nukta (dot) moja au zaidi. Kila nukta inayofuata huongeza nusu nyingine ya noti iliyotangulia kama inavyoweza kuelezwa kwa kusoma picha hii hapa.

1155567




TIME SIGNATURE

Time signature
hutambulisha kuwa beat moja ni sehemu ipi ya noti kamili, na kuna beat ngapi katika kila measure moja kwa kutumia namba mbili mwazoni mwa muziki wenyewe. Namba moja inakuwa juu ya nyingine kama ifuatavyo.

1155568


Namba iliyoko chini, inaonyesha sehemu ya noti kamili inayotumiwa kama beat moja, halafu ile ya juu inaonyesha kuwa kuna beat ngapi kwenye measure moja. Kwa mfano, time signature hii
1155569
inaonyesha kuwa beat moja ni nusu noti, yaani
1155570
, halafu zimo beats 3 kwenye kila measure. Kwenye huu hapa, beat moja ni nusu noti, na kuna beat nne kwenye kila measure kama inavyoonekana wazi
1155571



Time signatures ambazo mi maaurufu zaaidi ni hizi mbili,
1155572
hivyo zimepewa utambulisho mwningine maalum kama ifuatavyo hapa chini
1155574


Hiyo herufi
1155576
inaonyesha kuwa ni "Common" time signature halafu hiyo
1155575
inaonyesha kuwa ni Cut time.



TEMPO

Muda unaotumiwa na beat moja ya muziki unatambulisha kwa kuelezea mwendokasi wa muziki huo yaani tempo ambayo ni idadi ya beats zilizo katika dakika moja (Beats Per Minute au BPM). Nyimbo nyingi za pop hupigwa katika tempo kati ya 100 BPM hadi 140BPM, wakati nyimbo za reggae zina tempo kati ya 80BPM hadi 110 BPM. Miziki yenye tempo za chini sana ni jazz na blues ambazo tempo zake zinaanzia 40BPM na hazizidi 100BPM.

Iwapo wimbo una tempo ya juu sana zaidi ya 145BPM huwa hauchezeki kirahisi. Nyimbo nyingi za rock ndizo zinazongoza kwa kuwa na temp kubwa sana na ndiyo maana uchezaji wake huonekana kama ni wa fujofujo. Kwa mfano wimbo huu wa Lazaretto ulioimbwa na Jack White na tempo ya 181BPM ambayo ni juu sana.



Vile vile wimbo wa Jailhouse Rock wa Elvis Presely unapigwa na tempo ya 176 BPM ambayo pia ni ya juu sana.



Tempo inayotumiwa na muziki hufafanuliwa ama kwa kwa kutumia maneno kitaliano au kwa kutumia namba. Maneno ya kiitaliono yanayotumiwa kwenye muziki hasa ule wa kizamani ni kama Larghissimo – chini ya 24 BPM, Adagio – kati ya 66 BPM mpaka 76BPM, na kadhalika. Unaweza kupata list kamili ya maneno hayo hapa Wikipedia.

Muziki wa kisasa hautumii maneno hayo ya kitaliano tena, badala yake hutamka wazi kuwa kuna BPM ngapi kwa kuonyesa alama kama hii
1155587
mwanzoni mwa muziki huo. Alama hii hapa inaonyesha kuwa kuna robo noti 80 katika kila dakika. Kwa hiyo iwapo beat ni robo noti basi muziki utakuwa na tempo ya 80BPM, lakini iwapo beat ya muziki huo ni nusu noti, basi kutakuwa na 40BPM na kadhalika.


TAMATI

Baada ya maelezo hayo hapo juu, ni wazi kuwa iwapo beat moja ni robo noti, na wimbo una tempo ya 120BPM, yaani kila dakika kuna robo noti 120, basi kila robo noti itakuwa inaimbwa kwa nusu sekunde, ambapo nusu noti itaimbwa kwa sekunde moja, na noti kamili itaimbwa kwa sekunde mbili na kadhalika.

Hebu tuunganishe maarifa haya kwa kuangalia tena wimbo wetu wa taifa
1155577


Kwanza tunaona kuwa time signature yake ni Common
1155578
, yaani beat moja ni robo noti, na kuna beat nne kwenye kila measure (ukizihesabu utaona hivyo). Halafu pia tunaona kuwa kuna robo noti 80 katika kila dakika, kwa hiyo kwa vile beat moja ni robot noti pia, basi tempo ya wimbo ni 80BPM. Sasa tunaweza kupima muda unaotakiwa kuimba muziki kwa kuangalia kuwa kila measure itakuwa inachukua inachukua daika 4/80 au sekunde tatu, na kwa vile wimbo wote una measures 17x2=34, basi unatakiwa uimbwe kwa kutumia sekunde 102, yaani dakika 1.7. Kwenye zile video tatu za wimbo wa taifa nilizoonyesha katika post iliyopita, ni wazi kuwa zote hazukuuimba vizuri wimbo huo ingawa ile video ya kwanza ndio iliyojitahidi zaidi.


Ngoja nifunge post kwa kuwaachia burudani hili la uchezaji halisi wa muziki wa rock 'n roll

 
Respect.... huu uxi nsupitia in slow motion way coz ni darasa na ili kulielewa muds na utulivu ni muhim... nskosa mafunxo kwa vitendo tuu... vp una darasa la Muziki?
 
Respect.... huu uxi nsupitia in slow motion way coz ni darasa na ili kulielewa muds na utulivu ni muhim... nskosa mafunxo kwa vitendo tuu... vp una darasa la Muziki?
Respect sana mkuu;

Ila lugha yako imenipiga chenga kidogo mkuu wangu. Je, unauliza iwapo kuna sehemu ninafundisha muziki kwa vitendo?
 
Ingawaje tunajua kuwa mziki ni mtiririko wa sauti zilizopangiliwa kwa mfumo fulani. Ukweli ni kuwa siyo lazima mtililiko huo uendelee bila kuwa na mapengo ndani yake. Ukisikiliza wimbo kama huu wa hayati Bob Marley, utagundua kuwa kila anapoimba, anapumizika kidogo, vile vile hata upigaji wa gitaa una sehemu ambazo hupumzika kwa muda Fulani



Sehemu ya maandiko ya muziki huo nimeyaweka hapa chini, na kuonyesha sahemu zenye mapumziko kwa kuyazungushia kwa kalamu ya rangi nyekundu.
1564125145985.png




Mapuziko au mapengo hayo yanaitwa rests; urefu wake unategemea pia beat ya muziki wenyewe na unashabahiana na urefu wa noti kama nilivyozitambulisha huko nyuma kama ifuatavyo hapa chini

1564125217660.png
Mapumziko ya urefu wa noti mbili, yaani Breve rest

1564125245029.png
Mapumziko ya urefu wa noti moja, yaani Semibreve rest

1564125277864.png
Mapumziko ya urefu wa nusu noti moja, yaani Minim rest

1564125305230.png
Mapumziko ya urefu wa robo noti moja, yaani Chrotchet rest

1564125348998.png
Mapumziko ya urefu wa sehemu 1 ya 8 ya noti moja, yaani Quaver rest

1564125398371.png
Mapumziko ya urefu wa sehemu 1 ya 16 ya noti moja, yaani Semiquaver rest

1564125425767.png
Mapumziko ya urefu wa sehemu 1 ya 32 ya noti moja, yaani Demisemiquave rest

1564125455659.png
Mapumziko ya urefu wa sehemu 1 ya 64 ya noti moja, yaani Hemidemisemiquave rest
 
Hapana, sijaacha mijadala ya kisiasa au ya aina yoyote ile. Nimeona kuwa kwa vile mimi ni mwanamuziki niliyobobea kiutaalamu na sijawahi kushea na wanachama hapa huo utaalamu wangu, nikaona ngoja nitumie siku chache kuuanika utaalamu wangu hapa kwa lugha rahisi kadri nitakavyoweza. Huwezi kujua ni nani atafaidika nao kwani najua elimu ya muziki haifundishwi vizuri Tanzania; ndiyo maana tuna wanamuziki mastaa wanatoa miziki isiyokidhi viwango, yaani wanakuwa na vipaji lakini hawana misingi. Nadhani mchango wangu huu utawasidia baadhi yao kuwajenga misingi ya muziki kusudi wakichanganya na vipaji vyao basi watoe muziki mzuri. Mimi ni mwanamuziki mzuri sana nilifundishwa utaalamu wa muziki mapema sana lakini sikuutumia kujipatia mkate wangu wa kila siku ingawa nina bendi kamili nyumbani kwangu pamoja na familia yangu kwa ajili ya burudani yetu sisi wanafamilia tu.
Hongera, wengi tutafaidika mkuu
 
Respect sana mkuu;

Ila lugha yako imenipiga chenga kidogo mkuu wangu. Je, unauliza iwapo kuna sehemu ninafundisha muziki kwa vitendo?
Typing error tuu mkuu sikukumbuka kuedit.. ila namaanisha hivyo kama una darasa la music... pia kama utanisaidia kupata huu uzi ukiwa wote kwa pdf au doc... unapatikana vp
 
Typing error tuu mkuu sikukumbuka kuedit.. ila namaanisha hivyo kama una darasa la music... pia kama utanisaidia kupata huu uzi ukiwa wote kwa pdf au doc... unapatikana vp
Nimebakiza kama makala tatu za nadharia, halafu nitakuja na makala kama nane hivi za vitendo. Wakati wa vitendo nitazungumzia utangaji wa nyimbo za kuimba mtu mmoja mmoja, na baadaye nyimbo za kwaya, nyimbo za vyombo vingi kama Brass band, Orchestra na Jazz, na baadaye nitamalizia na electronic music unaotumiwa na wanamuziki wengi majukwaani kama vile Bongo Flava- Nitatumia Abbleton Live na FL Studio ambazo ndiyo popular zaidi. Ukijua kutumia hizo mbili ni rahisi kuhamia packages nyingine kama Dr.Drum, Turbo Dub 2 na nyinginezo. Nikishamaliza yote nitakutengenezea PDF yake. Kwa sasa sina document lolote kwa vile mambo yote nitayoandika hapa yako kwenye hand draft tu kama uonavyo hapa chini.

Kuhusu darasa la muziki, ni kweli huwa nafundisha Muziki watoto wadogo kwa kujitolea kwenye jumuia ya kanisa; tupo waalimu wengi wa kujitolea.

1564209271790.png
 
Asante nimekuelewa vizuri, tupo pamoja darasani, tena siti ya mbele kabisa.
Nimebakiza kama makala tatu za nadharia, halafu nitakuja na makala kama nane hivi za vitendo. Wakati wa vitendo nitazungumzia utangaji wa nyimbo za kuimba mtu mmoja mmoja, na baadaye nyimbo za kwaya, nyimbo za vyombo vingi kama Brass band, Orchestra na Jazz, na baadaye nitamalizia na electronic music unaotumiwa na wanamuziki wengi majukwaani kama vile Bongo Flava- Nitatumia Abbleton Live na FL Studio ambazo ndiyo popular zaidi. Ukijua kutumia hizo mbili ni rahisi kuhamia packages nyingine kama Dr.Drum, Turbo Dub 2 na nyinginezo. Nikishamaliza yote nitakutengenezea PDF yake. Kwa sasa sina document lolote kwa vile mambo yote nitayoandika hapa yako kwenye hand draft tu kama uonavyo hapa chini.

Kuhusu darasa la muziki, ni kweli huwa nafundisha Muziki watoto wadogo kwa kujitolea kwenye jumuia ya kanisa; tupo waalimu wengi wa kujitolea.

View attachment 1164046
 
Utunzi wa Muziki Toleo la 1-(Rhythm: Timing and Meters)

Kutunga muziki kuna mambo mawili ya kufanya: (a) kutunga mashairi (lyrics) ya muziki wenyewe, halafu (b) kutunga mpangilio wa sauti (arrangement) za muziki huo. Watu wenginge hutunga mashairi kwanza halafu wakaishia na kuweka sauti, na wengine hufanya kinyume kwa kuanza na sauti, halafu wakajaza mashairi. Nilishwahi kufanya kazi na watu waliokuwa wakitunga mashairi na sauti moja kwamoja. Kila mtu ana njia yake ya kukamilisha muziki wake ingawa wataaalamu wa muziki hushauri kuwa usianze na mashairi kwani utaweza kulazimisha muziki kufuata sauti za maneno yaliyo kwenye mashairi hayo badala ya mashari yako kufuata muziki. Kwa jumla kuanza na mashairi hurahisisha sana utungaji kuliko kuanza na sauti, lakini kila mtunzi ana mbinu zake. Mziki wa instrumental huhusisha kutunga mpangilio wa sauti tu.

Katika thread hii, hatutaongelea kuhusu utungaji wa mashairi, tutajikita kwenye sauti tu. Utunzi wa sauti huhusiha mpangilio wa mkong’osio (melody) na kuupa mpangilio huo mdundo (rhythm). Mkong’osio ni upanganji wa sauti (pitch) zenyewe kwenye phrases na measures, halafu mdundo ni upangaji wa urefu wa muda kwa kila sauti: yaani beat, time signature na tempo. Iwapo muziki huo unahusisha vyombo vingi basi utunzi huhusisha pia upangaji wa vyombo kuleta mwafaka (harmony), ubadilishaji wa sauti za vyombo mbalimbali ili visikike vizuri katika position mbalimbali (timbre) na mchanganyiko wa mabadiliko ya nguvu za sauti za vyombo mbalimbali (dynamics) ili kuongeza madoido ya mziki wenyewe.

Katika makala haya ninataka kuelezea kuhusu utungaji wa rhythmn ya muziki wa chombo kimoja na vile vile ya vyombo vingi kama kwenye bendi. Maelezo yangu yanachukulia kuwa angalau shairi moja na kibwagizo chake vimeshaandikwa. Kwenye mifano yote itakaofuatia baada ya post hii nitatumia shairi lilioandikwa na mtaalamu Amiri Sudi Andanenga (Sauti ya Kiza) lijulikanano kama KUKU; nimechukua beti mbili tu kati ya tano na nitaliwekea mdundo wa reggae.

LEO nitahadithia, kwa vile nina uchungu
Ama mtanibishia, nawajua walimwengu,
Bali leo yangu nia, kuyapasua matungu,
Kibwagizo: Kuku mwala nyama yangu, kinyesi mwakichukia. x2
Mavi mnayachukia, mwaipenda nyama yangu,
Sana mwaona udhia, ninyi na wale wa tangu,
Kama chombo nimenyia,mwakivunja kwa marungu,
Kibwagizo: Kuku mwala nyama yangu, kinyesi mwakichukia. x2


Mifano ya tungo zangu kwenye makala hizi itatumia programs za Ableton Live 10 Lite na Finale Note pad Utunzi unahitaji maandalizi kwanza kabla ya kuanza kuweka utaalamu wa muziki.

Maandalizi

Kabla ya kuanza kuamua mdundo au rhythm yako, weka plani ya awali kwa kufikiria mambo yafuatayo:
Hisia unazotaka wimbo wako uzifikishe kwa msikilizaji: hofu, matumaini, simanzi, furaha, hasira, mapenzi, chuki, upendo, mshangao, n.k. Kulingana na hisia hizo, chagua tempo au mwendokasi (BPM) wa sauti ya wimbo wako inayoendana na hisisa hizo. Unaweza kutumia metronome hii inayotolewa bure na Google kujaribu BPM yako, au kutumia App hii ya Metronome Beats inayopatikana kwa ajili ya Android. Metronome ni kifaa kinachosaidia mtunguaji kujua beat na BPM anayotumiea wakati wa hatua za zawali za utunzi; siyo kila mwana musziki natumia metronoe, lakini ni nzuri sana kwenye katika kuthibit consistency ya muziki. Kama utakumbuka zile nyimbo tatu za taifa huko nyuma zilitofautiana urefu kwa sababu hazikuwa na BPM ambayo ni consistent.

Pima urefu wa kila msitali (yaani idadi ya sauti- syllables- au noti zake) na idadi ya mistali katika kila shairi, halafu pia kadiria idadi ya mashairi katika wimbo. Endapo kila shairi linategemewa kuwa na kibwagizo, basi fikiria vile vile idadi ya mistali katika kila kibwagizo. Amua aina ya mapumuziko (rests) unayotaka yawemo kwenye mashairi hayo. Habari hiyo itakusaidia kuamua idadi ya measures katika kila phrase.


Meter

Kutokana na habari ulizokusanya hapo juu kamilisha vipimo vya rhythm yako kwanza kwa kuamua beat ya wimbo na hivyo urefu wa measure (time signature). Baada ya kufanya hivyo, tengeneza kitu kinaitwa meter, yaani mpangilio wa sauti zinazojirudia rudia katika kila baada ya measure moja. Mpangilio huo ndio ambao hutambulishwa kama beat ya muziki na ndiyo rhythm yenyewe. Kwa kawaida Meter itakuwa na sauti moja kubwa inayojipambanua katika kila mzunguko, mara nyingi inatokea mwanzoni mwa mzunguko; meter inakuwa na pigo moja kubwa ikifuatiwa na mapigo mengine madogo kwenye kila mazunguko huo.

Kinadharia kuna aina mbili za meter kimsingi: simple meter na compound meter. Mzunguko wa Simple meter una nafasi mbili, ambapo mojawapo inatumiwa na pigo kubwa lakini zote mbili zinaweza kutumia na mapigo madogo pia, wakati compound meter ina nafasi tatu ambamo mojawapo ni ya pigo kubwa lakini zote tatu zinaweza kutumiwa na mapigo madogo pia. Picha hizi mbili zinaonyesha maana za hizo za simple meter na compound meter; picha inayoonesha simple meter ina meter nne, wakati picha inayoonyesha compound meter in meter tatu kulingana na mapigo makubwa. Simple meter ina beats mbili kwa measure wakati compound meter in beats tatu kwa kila measure. Hizo beats ndogo za blue zinaweza kuondolewa na sehemu zake zikabaki tupu, na bado kukawa na rhythm inayoelewaka.
1564576574777.png
1564576590698.png







Iwapo dunia yote tangu mwanzo hadi leo ingekuwa inatumia meter hizo mbili tu, basi kuna miziki mingi leo ingekuwa inatumia rhythm inyofanana. Kutofautisha rhythm tofauti tofuati, kuna kitu kinaitwa grouping, yaani kuunganisha hizo meter za msingi katika magroup kwa kuondoa pigo moja au zaidi na muungano huo kutumika kama meter moja . Magrupu makubwa ni matatu, na yanajulikana kama Duple, Triple na Quadruple Meter. Duble meter zinatokana na kuunganisha meter mbili, tripple meter zinatokana na kuunganisha meter tatu na vile vile Quadruple zinatokana na kuunganisha meter nne. Katika muunganisho huo, mapigo fulani yanaweza kuondolewa ili kuwe na pigo moja kubwa kwenye measure moja kama nilivyoonyesha kwenye picha hizi mbili hapa chini ambapo simple meter mbili zimeunganishwa; kwa hiyo badala ya kuwa na beats mbili kwa measure, sasa tutakuwa ne beats nne kwa measure wakati pigo kubwa ni moja tu.
1564577154521.png
1564577191950.png







Unaweza kufanya hivyo pia kwa kuunganisha compound meter mbili, tatu au nne na kuondoa mapigo fulani kadri utakavyotaka rhythm yako iwe, mradi tu uhakikishe unaacha pigo kubwa kwenye sehemu ya kwanza ya measure yako. Kama maelezo haya hayakueleweka vizuri, uko huru kuni PM kwa maelezo zaidi. Katika mifano ifuatayo nitakuwa natumia Simple compound meter ambayo ni maarufu kwa miziki mingi inayofuata common time signature, yaan i
1564577393819.png
, nitazgroup mbilimbili.


Rythym ya Muziki wa Chombo Kimoja

Kwa muziki wa kuimbwa na mwimbaji mmoja au kupigwa kwa chombo kimoja tu (kisichotoa sauiti nyingi kwa mpigo kama aambavyo piano hufanya), meter inaweza kuwa ni makofi, au namna ambavyo mimbaji au mpigaji atakavyokuwa anachezesha chezesha kichwa au miguu yake kama nilivyoanisha huko nyuma nilipofafanua maana ya beat. Meter inaweza pia kuwa ni kuhesabu mapigo kwenye measure moja: kwa mfano MOJA-na-mbili-na-tatu-na- nne, MOJA-na-mbili-na-tatu-na-nne. Beat au pigo la muziki linakuwa ni kwenye nafasi ya namba MOJA.
1564577864932.png


Rhythm yangu ya ya reggae kwa sasa itaanza meter hiyo hapo juu kwa tempo ya 110 BPM ambayo ni ya kawaida kwenye miziki ya regae. Nimeitengeneza kutumia free version software ya Finale Note pad kama ifuatavyo
1564578117368.png
1564578136149.png

1564578163158.png
1564578192071.png



Rhythm au beat hiyo itasikika hivi.



Rhythm ya Muziki wa Vyombo Vingi.

Rhythm ya muziki wa vyombo vingi hutengezwa kwa kutumia ngoma (drums), vichekecheke vya pembeni (percussions) na vyombo vya bass (bass instruments). Katika aina zote za muziki, kiini kikubwa cha rhythm ni ngoma; piano nyingi za kisasa huweza pia kupiga sauti za ngoma kama sehemu rhythm.

Kuna aina tau kuu za ngoma: (a) Bass au kick drums- Hizi ndizo hutumika kutoa mapigo makubwa, (b) Tom tom, yaani ngoma ndogo, na (c) Snare Drums, yaani ngoma zenye kamba chini yake ili kutoa sauati za chaka-chaka-chaka-chaka-chaka (angalia picha). Hizi ngom za Tom Tom na Snare ni kwa ajili ya mapigo madogo kwenye meter. Ngoma hizi zinapatikana katika miundo mbalimbali kulingana na matumzi, kwa mfano muziki unoapigwa na watu walioketi kama kwenye Orchestral, jazz, Rock, reggae, pop, basi hutumia ngoma mfano wa picha niliyoweka hapa katikati. Iwapo mzuki unapigwa na watu wanaotembea kama kwenye brass bend za kijeshi, basi ngoma hizi hutengezwa katika muundo unaoruhusu mpigaji kuzivaa mabegani. Zote zinatoa sauti za aina ile ile.
1564578603398.png
1564578621275.png
1564578646133.png


Vichekecheke vya pembeni (percussions) ni vyombo vinavyotoa sauti ndogo lakini kali zikiwa ama zinadumu muda mfupi au muda mrefu. Vyombo hivi vyote hutumika katika mapigo madogo kwenye meter. Vichekecheke vya pembeni ni pamoja na kengere ya pembetatu (triangle), matoazi (Cymbals – yenye kofia na yasio na kofia), marimba, vipenga (whistles), ngoma za mkononi za kihindi, njuga, vibuyu vyenye kete, na kadhalika. Vyote hivyo huchangia kutoa mapigo madogo.

Mapigo makubwa ya meter hayategemei bass drum tu huweza pia kusaidiwa na vyombo vya bass, kama bass guitar, Sousaphone, tuba na kadhalika, mradi tu ile sauti (noti) inayotumika kwenye pigo kubwa iwe ni ile ile. Hii ni process inayoweza kuwa ya kujaribu na kukosea (trial and error) au inaweza kufanyika kwa kutumia uzoefu mpaka mtungaji apate ile rhythm anayotaka almradi tu mapigo yanatoseheleza nadharia kama nilvyokiwsha andika huko nyuma.
Katika project hii, tunataka kutengeza rhythm ya ngoma zilzioonyeshwa hapo juu (drum set) kwa kufuata meter hii
1564578909175.png


Katika mfano huu sitatumia Finale note pad kwa sababu tunahitaji kujadili nadharia ya chords na chord progression ambayo nategemea kuifanya katika post ijayo kabla ya kuanza kuadika rhthm ya vyombo vingi katika Finale Note pad. Badala yake nitatumia . Abletone live ambayo itaniletea ngoma moja kwa moja; ukiifungua mara ya kwanza huonekena kama picha inayofuta invyoonyesha; mwonekano huo hujulikana kama session view. Set time signature yako kuwa 4/4, na temp yako kuwa 110BPM kama ilivyoonyeshwa kwenye kibox chekundu. Kwenye Ableton Live huna haja ya kuchagua scale kwa sababu ni wewe mwenyewe utakayechagua sauti kulingana na scale unayotaka kutumia.

1564579077852.png


Kwa lengo la mjadala huu, hatukusudii kuandika kila kitu kuhusu kutumia Ableton Live Lite; kutokana na umaarufu wake kuna video nyingi sana Youtube zinazoonyesha jinsi ya kuitumia. Ni program nzuri sana kuliko program zote za muziki ninazojua; ninazo kadhaa ikiwa ni pamoja Dr Drum, Dark Wave Studio, FL Studio na Dub Turbo.

Ili kuendelea na mjadala wetu wa rhythms, weka mouse kwenye 2 Mid, right click na kuchagua delete ili kuifuta. Fanya hivyo pia kwa 3 Audio, 4 Audio A reverb, na B Delay. Fungua Drums kwenye column ya kushoto kabisa yaani Collection, chagua Drum rack uivute kwa mouse yako na kuiweka kwenye 1 Mid utapata kitu kifuatacho.

1564579233744.png


Sasa angalia ile Drum rack uliyopata ambayo nimezungushia rangi nyekundu hapo chini. Inakuruhusu kuweka ngoma za kutosha Octave zote nane za muziki; tutatumia Octave ya kwanza tu kwa ngoma hizo tunazotaka. Kwa sasa hivi hakuna ngoma yoyote iliyokwishawekwa ni lazim wewe mwenyewe uchague ngoma unazotaka kutumia. Kumbuka ngoma zinazotakiwa ni Bass au Kick drum, Tom Tom, Snare, na vile vile unaweza kuweka matoazi yaani Cymbals.

Ukiwa umechagua Drums, type neno "Kick" kwenye search bar hapo nilipozungushia kwa kalamu nyekundu. Itakufungulia aina mbalimbali za Kick drums zilizoko kwenye Library ya Ableton; chagua mlio wa kick drum unayotaka wewe halafu uuvute na kuuweka kwenye note ya C1 kwenye drum rack yako. Unaweza kuweka kwenye noti yoyote lakini mara nyingi watu huiweka kwenye C1 kama sauti ya chini kabisa kwenye C-Major.

1564624448750.png



Kwa vile nimefikia limit ya attachement, nitaendelea na maelezo haya kwenye post ifuatayo baada ya kufunga post hii.
........ Continues to next post
 

Attachments

  • 1564577221200.png
    1564577221200.png
    3.7 KB · Views: 36
  • Meter1.mp3
    174.7 KB · Views: 24
..... Timing and Meters cont'd

Fanya vivyo hivyo tena kwa sauti za Tom1, Tom2, Tom3, Snare, Hi-Hat(closed), Hi-Hat(open) ili kukamilisha sauti za ngoma zote ambazo nimeweka picha zake hapo juu. Nimezipanga na kuzipa majina kama ionekanavyo hapa chini.

1564579855410.png


Kwa vile Ableton ina benki ya sauti za ngoma nyingi, kila mmoja anaweza kuchagua sauti zake lakini hakikisha kweli zinaendana na ngoma kweli kusudi yasitokee matatizo iwapo muziki unapigwa live badala ya playbak.

Baada ya kupanga ngoma zangu, sasa ni hatua za mwisho mwisho za kutengeneza rhythm niitakayo; kwanza hakikisha kuwa hizo alama za M na S kwenye kila chombo ulichochagua zote ziko OFF kabla ya kuendelea mbele. Ukigonga sehemu iliyoonheswa “Gonga hapa” kwenye picha ifuatayo, utafunguliwa boksi la njano hapo chini.
1564579984189.png


Kwenye boksi hilo kuna vitu vitano ambavyo nataka uviangalie tena kwa makini ukilinganisha na yale ambayo tumeshayaongea huko nyuma. Kitu cha kwanza ni signature 4/4- nadhani sasa inaeleweka, kitu cha pili ni tempo ambapo jamaa hawa wametumia yale maneno ya kitaliano Legato- hata hivyo nadhani pia inaeleweka, halafu kitu cha tatu ni list ya ngoma ambazo tumechagua kutumia kwenye rhythm yetu, nne tunaonyeshwa kuwa sauti fupi sana tunayoweza kutumia kwenye rhythm yetu ni 1/16 ya noti yaani semiquaver, na mwisho kabisa mbele yetu tuna measure moja ambamo ndimo tutakapoweka meter ya rhythm yetu. Rhythm hiyo itakuwa kama ionekanavyo kwenye picha ya mwisho kabisa hapa chini.

1564580116698.png


Ukishafika hapo, unaweza kujaribu maungano (combinations) mbalimbali za mapigo madogo kutafuta radha unayotaka mwenyewe. Pigo kubwa ni hiyo Kick drum halafu yale mapigo madogo nimeyagawanya kati vya ngoma nyingine zilizobaki. Kumbuka kuwa Hit-hat closed hat pamoja na Bass- kick drum zinapigwa kwa miguu, kwa hiyo vinaweza kupigwa pamoja,lakini ngoma nyingie zilziobaki ambazo zinapigwa kwa mikono, ni mbili tu ndioz zinazweza kupigwa poamoja, yaani mkono wa kushoto na mkono wa kulia.

Huu ni mfano tu lakini unafanya kazi ingawa ile closed hit-hat niliyochagua haiskiki sana; hata hivyo tutaendelea nayo tu. Rhythm itokanayo na ngoma hizi ni hii hapa



Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz ; ingawa post hii ni ndefu, nadhani somo hili kuhusu matumizi ya time signatures, tempo, beat, meter na utunganji wa mdundo au rhythm ya muziki limeeleweka. Somo lijalo nitajadili chords, na chord progression katika kutunga melody (mkong'osio) ya Muziki. Stay tuned. Nitakuwa natumia program hizi hizi mbili; zote zinauzwa tena kwa bei mbaya lakini uzuri ni kuwa zina free versions zake ambazo zinatosheleza kabisa kwa matumzi ya thread hii.
 

Attachments

  • Meter2.mp3
    158 KB · Views: 24
Ili muziki uwe wa kusisimua kwa msikilizaji, ni lazima muundo wa meter kuwa inabadilika badilika. Muziki ukitumia meter moja tu muda wote utamchosha msikilizaji wake, yaani unakuwa monotone. Time signature inaweza kubaki ile ile lakini ama meter ikawa inabadilika badilika au hata tempo pia ikawa inabdilika badilika; inawezekana vile vile kubadili time signature ndani ya muziki. Miziki mingi ya Beetles ilikuwa inabadili time signature katikati, na muziki mmoja wa kikongo ambao ulibadili tempo, meter na time signature mara nyingi (sijui kama watunzi walikuwa wanajua hilo) ni huu wa hapa. Miziki mingi yenye kusisimua imetungwa kwa mfumo huo wa kuwa na meter tofauti tofauati ndani ya muzki, na mara nyongine kubadilisha badilisha tempo.
 
Back
Top Bottom