Chords and Chord Progression
Kumbuka kuwa huko nyuma tulieleza kuwa katika sauti zote 12 za kwenye Octave moja ni sauti saba tu zinazoshabihiana, ambazo mwanzoni tulizionyesha kwa namba za kirumi I-II-III-IV-V-VI-VII, tukimalizia na sauti ya nane VIII ambayo ni sauti ya kwanza kwenye kwenye Octave inayofuata. Zile sauti 12 za octave hujulikana pia kama chromatic scale, wakati sauti hizo saba zinazoshabihiana hujulikana kama diatonic scale. Sauti hizi za diatonic scale kuanzia ya chini hadi ya juu ndizo zina majina kama ifuatavyo kwenye jedwali hili:
| Sauti | Jina | Matumizi |
| I | Tonic | Sauti za kupumzikia; hutumika mwanzo na mwisho wa phrase moja |
| II | Supertonic | |
| III | Meadiant | Sauti za kuhama kutoka na kuingia kwenye tonic |
| IV | Subdominat | |
| V | Dominant | Sauti za Kuchangamsha, yaani zenye msukumo sana |
| VI | Submediant | |
| VII | Leading | |
| VIII | Next tonic | Sauti ya kupitia kuingia na kutoka kwenye octave inayofuata. |
Jedwali hili tutalirudia tena huko mbele, lakini kwa leo nataka tuzichambue tena sauti hizo kwa kuchanganya sauti tatu tatu zijulikanao kwa pmaoja kama diatonic triad, kwa mfano wakati wa kupiga piano. Kuna chords za kutumia sauti nne nne pia lakini hizo sitazijadili ili kupunguza urefu wa post.
Chords hutumiwa sana kwenye miziki ya piano kwa kila mkono kubonyeza vibonyezo vitatu au vinne kwa kwa mpigo, na kwenye miziki ya magitaa ambapo mpigaji anapiga nyuzi tatu au nne kwa mpigo.
Wapigaji wa magitaa maeneo yetu haya ya Africa ya mashariki na ya kati hasa wapiga magitaa ya solo wa Kongo hawatumii sana hizi chords, wao hupiga ile Diatonic scale moja kwa moja, ndiyo maana utaona mikono yao inakwenda kwa haraka sana katika kubonyeza na kukwapua nyuzi za gitaa kwenye mkono wa gitaa, na vile vile wanachambua uzi mmoja mmoja. Watu wanaopiga gitaa kwa kutumia chord huwa hawatembezi mikono mikono yao haraka haraka kwenye mkono wa gitaa, na hupiga nyuzi tatu au nne kwa mpigo. Angalie utofautishe mifano hii miwili ya upigaji magitaa ya solo
Wapiga gitaa wengi wanaotumia chords hupiga kwa kutumia chord za sauti nne nne ambazo nimesema kuwa hatutazijadili kwenye mfululizo huu.
Major and Minor Chords
Katika sauti hizo saba michangayiko ya sauti tatu tatu zinazoshabihiana inaitwa
triads na huundwa kwa kuruka sauti moja baina yao, kwa mfano
C+E+G, na zinajulikana kama
diatonic triad chords. Sauti au noti ya chini kabisa katika mchanganyiko huo huitwa
ROOT, halafu noti ya pili huitwa
THIRD MAJOR (ni ya tatu kutoka kwenye ROOT) na ile sauti ya tatu huitwa
PERFECT FIFTTH (ni ya tano kutoka kwenye ROOT).
Kuna aina mbili za michanganyiko hiyo: major chord na minor chord. Maneno
major chord na
minor chord hapa yasichangwane na
major diatonic scale na
minor diatonic scale ambazo tumekwishajadili. Major diatonic chords na minor diatonic chords zinapatina kwenye diatonic scale zote yaani kwenye major diatonic scales na kwenye minor diatonic minor scales. Kwa hiyo unaweza kuwa major chord kwenye scale ya C-major na vile vile kwenye scale ya A-minor ingawa chords hizo hazitahusisha noti zinazofanana. Inawezekana kuwa na mchanganyiko wa sauti nne ujulikanao kama
seventh ambao huongeza noti moja ijulikanayo pia kama the seventh juu ya perfect fifth; hatuzazingumzia hizo diatonic
seventh chords.
Sauti tatu za Major Cord zinatengana kwa urefu wa
2K-3N halafu sauti tatu za Minor chord zinatengana kwa urefu wa
3N-2K. Kwenye mtengano huu
2K inaonyesha kuwa zimeachana kwa hatua kamili mbili, na
3N inaonyesha kuwa zimetengana kwa nusu hatua tatu kwenye chromatic scale.
Nitaongelea diatonic chords za C-major diatonic scale na A-minor diatonic scale tu nikitegemea kuwa maelezo haya yataweza kutumika kwa diatonic scale nyingine zote tulizoongea huko nyuma
Kumbuka tena kuwa sauti za C-major ni
C-D-E-F-G-A-B-C, kwa hiyo chord zake zitokanazo na kuruka sauti moja moja zitakuwa ni
CEG, DFA, EGB, FAC,GBD, ACE, BDF, CEG
Sasa kwa vile note za chromatic scale zinatengana kwa nusu hatua na ni hizi hapa
C C#-D-D#-E-F-F#-G-G#- A-A#-B
Utaona kuwa kutoka
C hadi
E kuna nusu hatua nne, sawa na hatua kamili 2, halafu kutoka
E hadi
G kuna nusu hatua tatu, kwa hiyo Chord
CEG ni major chord. Kwenye chord
DFA tunaona kuwa kutoka sauti
D hadi
F kuna nusu hatua tatu, halafu kutoka
F hadi
A kuna nusu hatua nne sawa na hatua kamili mbili, kwa hiyo
DFA ni minor chord. Tukiendelea na chord
EGB tunakuta nusu hatua tatu kati ya
E na
G, na vile vile nusu hatua nne kati ya
G na
B, kwa hiyo hiyo nayo ni minor chord. Chord
FAC ina nusu hatua nne kati ya
F na
A, na vile vile nusu hatua tatu kati ya
A na
C, kwa hiyo
EGB ni major chord.
Kwa utaratibu huo huo tunaweza kumalizia kwa kuonyesha kuwa
GBD ni Major chord na
ACE ni minor chord. Mambo ni tofauti kidogo kwenye chord na
BDF kwa sababu kuna nusu hatua 3 kati ya
B na
D, na vile vile nusu hatua 3 kati ya
D na
F, kwa hiyo chord hii siyo major wala siyo minor bali inajulikana kama diminished chord. Wanamuziki wengi huwa hawaitumii chord hii kwenye tungo zao kwa vile haijichanganyi vizuri na hizo chord nyingine.
Chord hizi hutambulishwa kwa root notes zake
C, Dm, Em, F,G, Am, Bo na
C; katika notation hii
C ina maana ya major chord
CEG, na
Dm ina maana ya minor chord
DFA. Itaonekana kuwa kwenye major scales zote, major cords ni zile za kwanza, nne na tano; kwa hiyo chord za kwenye major scale zimepewa namba za kirumi
I-ii,ii,IV,V,vi,viio
Yaani zile namba zilizoandikwa kwa herufi kubwa ni major chords, na zile za herufi ndogo ni minor chords na ile inayoishia na o ni
diminished chord.
Ukitumia utaratibu huo huo pia kwenye natural minor scales, utagundua uwa major chords ziko kwenye nafasi ya 3, 6 na 7, wakati minor chords ziko kwenye nafasi za 1,4, na 5, na ile diminished chord iko kwenye nafasi ya 2. Kwa kutumia mfano wa scale ya A-minor, Diatonic chords zake ni
ACE, BDF, CEG, DFA, EGB, FAC,GBD, ACE,
Kama ionekanavyo kwenye picha hii
Chords hizi zinafanana kabisa na chords za kwenye C-major key kwa vile A-Naural minor na C-major zinatumia sauti zile zile ila katika mipangilio tofauti. Tatizo liko kwenye chord
EGB, kwani iwapo utakuwa kwenye A-natural minor amabayo sauti zake ni
A-B-C-D-E-F-G-A basi chord hiyo inakuwa ni minor chord, hata hivyo ukiwa kwenye A-harmonic minor ambayo sauti zake ni
A-B-C-D-E-F-G#-A yaani noti ya
G imepandishwa juu kwa nusu hatua basi chord hiyo ya
EGB itakuwa ni major chord. Vile vile ukiwa kwenye A-medolic minor ambayo sauti zake ni
A-B-C-D-E-F#-G#-A, chord hiyo ya
EGB itakuwa na maana tofauti. Kwa hiyo uwe makini iwapo unatumia scale ya natural minor au harmonic minor au au melodic minor.
Chord za minor scale zimepewa namba za kirumi pia kama
i,iio,III,iv,v*,VI,VII
na pia zinatumia majina ya root notes zake na kuonyesha kama ni minor kama ilivyo kwenye cleff hii
Ni vizuri kuelewa kuwa matumizi ya meneno Major chord na minor chord hayana maana ya kufifisha umuhimu wa minor chord na kukuzu ule wa majopr chord, ni kama ambavyo tuliona kwenye major scale na minor scale kuwa zote zina umuhimu sawa lakini Major scale ina sauti za "furaha", walaki minor key ina "sauti" za huzuni kwani katika muziki kuna miziki inayotungwa kwa ajili ya huzuni na nyingine kwa ajili ya furaha. Ni vivyo hivyo pia kwenye michanganyiko ya chords; major cord ni mchanganyiko wa sauti za furaha, wakati minor chord ni mchanganyiko wa sauti za huzuni, yaani sauti zisizo na msisimko sana. Kwenye wimbo wowote ule, aina zote za chord yaani major cords na minor chords hutumika kwenye sehemu mbalimbali za wimbo. Iwapo lengo ni kumfanya msikilizajajisikie "kuchangamka" kwenye sehemu fulani ya wimbo, basi sehemu hiyo inaandikwa kwa kutumia major chords; vile vile iwapo lengo ni kumfanya msikilizaji ajisikie "kuhuzunika" basi sehemu hiyo ya wimbo inaandikwa kwa minor chords.
Chord Inversions
Hizo diatonic chords tulizojadili hapo juu zinajulikana kuwa ziko kwenye root positions zao, yaani sauti ya chini kabisa (bass) ni ya root note ya chord, ambayo ndiyo iko chini sana. Inversion ni kitendo cha kuhamisha noti moja au mbili kwa Octave nzima, mradi noti mojawapo ibaki kwenye nafasi yake. Kwa vile noti yoyote moja au mbili zinaweza kuhamishiwa chini au juu kwa OCTAVE moja basi katika noti tatu za triad moja kuna iversions nyingi kidogo. Hizo chord tulizoona hapo, juu ndio zinazoitwa
root chords. Inversion maarufu zaidi ni First inversion na Second inversion kama ionekanavyo kwenye picha hii.
First inversion kuhamisha noti ya chini na kuipekea Octave moja juu ikiacha zile noti nyingine mbili mahala pake, na Second inversion huhamisha noti mbili za chini OCTAVE moja na kuacha noti ya tatu mahala pake. Kama chord ilikuwa kwa mfano CEG kama hiyo kwenye picha hiyo hapo juu, First inverstion yake inakuwa ni EGC* wakati C* ikiwa kweye Octave inayofuatia juu; kwa vile sauti yake ya chini sasa itakuwa ni E, basi hujulikana C/E, yaani chord ya C lakini ambayo bass note ni E. Second Inversion yake itakuwa ni GC*E* ambapo noti C* na E* ziko kwenye Octave inayofuatia juu, chord hii pia hujulikana C/G kwa maana kama nilivyoeleza hapo juu. Jambo la ajabu ni kuwa inversions hizi huwa hazibadilishi sana sauti ya mziki ila zinaongeza madoido ya muziki wenyewe na vile vile kufanya upigaji wake uwe rahisi hasa katika uimbaji na upigaji wa nyuzi za gitaa au vibonyezo vya piano.
Kwa mfano kwenye guitar badala ya kubonyeza nyunzi za C-chord kwenye root position ambazo ni ngumu kwa mpiga guitar kwa vile kidole kimoja kinatakiwa kiruke uzi mmoja na kubonyeza nyuzi mbili zinazofuata, mpigaji anaweza kupiga first inversion yake ya C/E akitumia kidole kimoja kubonyeza nyuzi zote na kile che pili kuruka nyuzi mbili na kubonyesa uzi mmoja wa tatu, au kwa kutumia second inversion ya C/G ambamo kidole cha kwanza kinabonyeza nyuzi zote, halafu kile cha pili kinaruka uzi mmoja na kubonyeza uzi mmoja tu wa pili.
Kuna jamaa waliotayaraisha poster linaloonyesha ubonyezaji wa nyuzi za guitar katika chord mbalimbali pamoja inversions zake;
lipatikana Amazon. Linaoneka hivi
CHORD Progression
Huu ni mtililiko wa chords zinazotumiwa kwenye wimbo. Kwa leo sitaujadili sana mpaka nikishaanza kujadili mada ya mwafaka (harmony) kwenye wimbo. Kwa kawaida wimbo wowote hutumia chords mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa zijajirudia rudia kwa mfumo unaotabilika au usiotabilika. Tutukatane tena kwenye topic hii huko mbeleni.
Leo nitawaacha na wimbo huu maarufu sana wa
Imagine ulioimbwa na John Lennon. Wimbo huo umo katika diatonic key ya C-major kwa kutumia triad chords hizi
C, Dm,Em F, G, Am,
Chord ya C kwenye mashairi inapigwa katika root position kama C ikifuatiwa na first inversion yake kama C/E; halafu pia chord ya Em kwenye kibwagizo inapigwa katika root position kama Em ikfuatiwa na first inversion yake kama Em/G. Wimbo wenyewe ni huu
[Mwanzo- Yyombo vitupu]
C - C/E - F
C - C/E - F
[Shairi la kwanza]
C - C/E - F
Imagine there's no Heaven
C - C/E - F
It's easy if you try
C - C/E - F
No hell below us
C - C/E - F
Above us only sky
[Kibwagizo Tangulizi]
F - Am - Dm - F
Imagine all the people
G - C - G - C
Living for today
[Shairi la pili]
C - C/E - F
Imagine there's no countries
C - C/E - F
It isn't hard to do
C - C/E - F
Nothing to kill or die for
C - C/E - F
And no religion too
[Kibwagizo Tangulizi]
F - Am - Dm - F
Imagine all the people
G - C - G - C
Living life in peace
[Kibwagizo]
F - G - C - Em - Em/G
You may say I'm a dreamer
F - G - C - Em - Em/G
But I'm not the only one
F - G - C - Em - Em/G
I hope someday you'll join us
F - G - C
And the world will be as one
[Shairi la tatu]
C - C/E - F
Imagine no possessions
C - C/E - F
I wonder if you can
C - C/E - F
No need for greed or hunger
C - C/E - F
A brotherhood of man
[Kibwagizo Tangulizi]
F - Am - Dm - F
Imagine all the people
G - C - G - C
Sharing all the world
[Kibwagizo]
F - G - C - Em - Em/G
You may say I'm a dreamer
F - G - C - Em - Em/G
But I'm not the only one
F - G - C - Em - Em/G
I hope someday you'll join us
F - G - C
And the world will be as one
Herman Cain alipokuwa CEO wa Godfather’s Pizza aliubadilisha akaimba Imagine there is no pizza kama ifuatavyo hivi
Lyrics za Cain ni hizi hapa chini; sikuzichambua muundo wake bali nime copy-n-paste
Imagine there’s no pizza
I couldn’t if I tried
Eating only tacos
Or Kentucky Fried
Imagine only burgers
It’s frightening and sad
You’re lucky you have pizza
To feed your kids for you
Only frosting or cookies
And no dishes you must do
I magine eating pizza
Each and every day
You may say it’s junk food
But to me it’s so much more
It gives my life its meaning
And it makes a lot of dough
Imagine mozzarella
Anchovies on the side
And maybe, pepperoni
Rounds out your pizza pie
Imagine getting pizza
Delivered to your door
You don’t have to give up now
On my skateboard I will go
I’ll be back in 30 minutes
I just bought Dominoes
All I am saying
Give pizza a chance
All I am saying
Give pizza a chance!
All I am saying
Give pizza a chance!
You got to, you got to, you got to
Give pizza a chance!
Wasomaji wangu wakuu nkumbison, Madaga, Gyole, Extra miles, MzaramoTz ; ingawa post hii ni ndefu, nadhani somo hili kuhusu mpangilio wa chords kwenye major scale na kwenye minor scale, maana ya major and minor chords, na chord inversion na matumizi yake katika kupiga muziki limeeleweka. Makala ijayo nitajadili miundo mbali mbali ya nyimbo na sehemu zake kabla ya kuanza utunzi wa melody.