kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Inasemekana kuwa Shabiki ni mchezaji 12 wa timu wakati wa mechi, hivyo Ally Kamwe na Ahmed Ally wasemaji wa Yanga na Simba wanafanya kila jitihada ya kuwataka wanachama na mashabiki wa timu hizo washangilie mwanzo mwisho wa mechi zao muhimu. Hata hivyo sayansi ya akili na tabia ya mtu inamtaka mtu mwenye afya timamu ya mwili na akili afurahi, kushangilia, kucheka, kupiga makofi na vigelegele na kutabasamu pale tu anapokutana, sikia au kuona tukio zuri linalompendeza.
Nipunguani tu anaeweza kucheka na kushangilia wakati wa huzuni. Kwa maana hiyo hakuna mwanachama wala shabiki wa Simba au yanga anaeweza kushangilia, kucheka na kupiga vigelegele mfululizo hata kama timu yake iko nyuma kwa magoli 3 dhidi ya mpinzani wake. Watu wanaoweza kushangilia timu muda wote hata kama timu imefungwa ni ama punguani au mtu mwenye maslahi na mechi husika zaidi ya furaha tu ya kushinda mechi.
Hivyo, basi ili watu ambao wanaweza kushangilia timu mwanzo mwisho bila kujali chenga za wachezaji wala matokeo ni watu wenye maslahi ya moja kwa moja (palpable) na mechi zaidi ya timu kushinda. Hawa watu wenye masilahi ya moja kwa moja (wanaolipwa) ndio wanaowatia hamasa ya kushangilia muda wote mashabiki ambao malipo yao ni furaha tu kwa timu kushinda mechi, Kifupi Yanga na simba lazima wawe na kikundi ambacho kitalipwa kwa kazi ya kushangilia bila kujali mwenendo na matokeo ya mechi. Timu zote kubwa kwenye nchi zote wanafanya hivyo.
Nitoe mfano kule US ambako basket ball inachezwa sana kwa hamasa. Vikundi vya hamasa vya kulipwa vina uwezo mkubwa mpaka wa kupita angani kwa ndege ndogo siku na muda mchache kabla ya mechi kuhamasisha watu kwenda uwanjani kwa kupeperusha mabango (banners) na moshi wenye rangi za timu husika. Ndege zinapita mitaa yote ya mji kualika watu waende kushangalia timu husika.
Kule kiwanjani kuna kuna kundi linashangilia sana na kuanzisha nyimbo ambazo zinafahamika na washabiki wote wa timu hiyo, hivyo uwanja wote wanaimba wimbo mmoja kutoka kona zote waliko mashabiki wao, na kama ni kelele ni za aina moja tu uwanja mzima. Hawa wanawaambukiza wengine kushangilia hata wale wenye njaa na kuwa kitu kimoja pale uwanjani. Hiki kikundi kitaimba na kushangilia kwa nguvu sana hata kama timu iko nyuma, maana wao wana maslahi mengine kabisa ambayo yana vigezo vyake vya ufanisi na ulipaji.
Huwezi kutegemea mtu mwenye njaa, asiekuwa na usafiri wa kurudia kwake na asiyelipwa chochote ashangilie timu yake hata kama imefungwa, huo utakuwa upunguani kama watafanya hivyo.