Kiasi cha pesa utakayoingiza youtube kinategemea sana video zako zinatizamwa wap pia.
Ngoja nikupe soma
Youtube ina sources mbili za kuingiza pesa.
1. Matangazo
Nitaiongelea sana hii kwa sababu hii ndo inaingiza pesa nyingi sana
2. Youtube Red
Hii ni youtube ya kulipia. Haina matangazo. Unapata pesa kama mtu akiangalia video yako
Pesa kwa njia ya matangazo
Hapa zipo aina kuu mbili za matangazo
1. Matangazo ya Video
Matangazo haya huonekana kabla ya kuanza kuangalia video ya muhusika. Muhusika ataingiza pesa yake kama mtazamaji ataangila video hiyo zaida ya sekunde..... (nimesahau idadi) kabla ya kuruka tangazo hilo. Matangazo hayo huonekana kwenye youtube ya simu, pc na tv. Hvyo huingiza pesa nyingi.
2. Matangazo ya picha na maandishi
Haya hutokea pembeni ya video au juu ya video. Mwenye video huingiza pesa endapo tu mtu ataclick tangazo hilo. Haya hayaingizi hela nyingi kwa kuwa hayaonekani kwenye simu, ni kwenye pc tu.
Unaweza ukawa na viewers wengi kwenye video lakin ukaingiza pesa chache kuliko yule mwenye viwers wachache. Hii inatokana na sababu zifuatazo.
1. Nchi ambayo video zako zinatazamwa
Nchi zilizoendelea kuna biashara nying na kila biashara hutangaza online. Kwa hyo gharama ya matangazo ni kubwa sana due to high demand. Kwahyo kama video yako itatazamwa marekani na watu 10,000 unaweza ukapata USD 5 lakini ikitazamwa na watu 10,000 Tanzania unaweza ukapata USD 0.5
Na vilevile wingi wa views ndio wingi wa matangazo, Tanzania kuna biashara chache, matangazo machache. Malizia hesabu hiyo....
2. Aina ya video na description ya video
Matangazo ya youtube huendana na aina ya video, mfano ukiruhusu autoplay halafu ukaanza kuangalia nyimbo za diamond utaona lazima matangazo ya nyimbo zingine yaje katikat ya nyimbo zake.
Ukiangalia video za review za products unaweza ukakutana na tangazo la product inayofanana na unayoangalia.
Kwahyo kama video yako haieleweki inaweza isipate tangazo, au itapata tangazo linaloendana na mambo ambayo mtazamaji anayapenda kwa sababu google (youtube) wanajua almost kila kitu unachofanya. (hili nalo ni somo jingine)
Hiyo ndo basic understanding ya matangazo
Jinsi ya kupata pesa zako
1. Kwanza kabsa lazma ufikishe idadi kadhaa ya jumla ya views za video zako zote (sijui 100,000? nimesahau, google)
2. Baada ya hapo omba partnership na youtube ili wawe wanaweka matangazo kwenye video zako.
3. By default video haiingizi pesa mpaka uiruhusu, so kuna sehemu utaruhusu kila video utakayoupload iingize pesa.
4. Tengeneza google Adsense Account. Hii ndio account itakayokuwa inatumiwa na youtube au google kuingiza pesa ya youtube.
5. Verify Adsense account yako. Google watakutumia post card yenye PIN ya kuverify account yako.
6. Baada ya kuverify then ingiza bank details zako ambazo google watatumia kukuingizia pesa zako
7. Ukifkisha zaidi ya USD 100 kila mwezi, google watakuwa wanakutumia kiasi hcho kila tarehe 20 ya mwezi.
Goodluck!