Elimu inaondoa akili ya asili, aliyozaliwa nayo binadamu

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,482
40,497
Elimu ni kitu kizuri, ila changamoto yake inaondoa ule uelewa wa asili ulio zaliwa nao (geniusism) na kupandikiza mawazo ya watu wengine.

Na hii inapelekea kupunguza idadi ya wavumbuzi kama enzi za kina Isack Newton.

Tunaamini akili ulio zaliwa nayo, ndiyo yenye mapinduzi ya kweli kifikra na kitafiti; ila hii ya kwenda shule na kumezeshwa mawazo au historia ya mafanikio ya watu fulani, ina futa ule uwezo wa akili wa binadamu alio zaliwa nao.

Kwa mangiki hiyo, aliyesoma sana hajavumbua kitu kipya zaidi ya kumezeshwa mawazo ya watu wengine na kutaka kuyaishi mawazo hayo. Hii ni sawa na kusema, matumizi mabaya ya ubongo.

Na kama tutaweza kutumia akili tulizo zaliwa nazo na si mawazo tuliyoyapata shuleni; matatizo ya ajira hayata kuwepo.

Karibuni kwa mjadala

NB: Wengi walio ajiriwa wanatumia akili za mashuleni; na wengi walio jiajiri wanatumia akili za kuzaliwa nazo.​
 
Back
Top Bottom