Elimu bure ni usanii mtupu

Hivi watu wengine wanajibu tu bila kufikiri. Tunalisemea hili tupo kwenye field na tunazijua changamoto zilizopo. Mnajua bei ya box moja la chaki? Na kwa watoto 1200 unatumia box ngapi kwa siku. Na walimu watakabaki kufundisha remedial kwa slow learners watalipwa na hizi shs 309? Fikirini kwa mapana. Hakuna elimu bure hapo wazazi ni lazima kuchangia ili kuisadia serikali. Vinginevyo ni siasa tu katika masuala ya kitaalam. Hamuamini subirini watakavyofeli watoto kwa kurudi makwao saa nane ndio mtajua hasara za elimu Burr.
 
Well said mkuu. Kihonda ina zaidi ya wanafunzi 1000 inapewa 580k jaribu kufikiri unaendeshaje shule kwa hali hiyo?? Mifano ipo mingi waalimu watusaidie fedha hizi sio siri jamani .

Duc in Altum
 
Elimu ya nchi hii itakuwa bora pale itakapotenganishwa na siasa.
 
Reactions: J33
HII si kweli nilimsikia MAGUFULI mm mwenyewe akisema pesa wamepelekewa kila shule zaid ya 1b kwa 3months

akatoa na onyo "ole wake yeye ataetumia vibaya"

wametoa Sh. 18bilion kwa Halmashauri zote.
Shule za Msingi zipo kama 13,000 hivi... na sekondari zinaweza kufika 3000 hiyo pesa kama ni kwa mwaka mzima haitoshi kabisa.
 
wametoa Sh. 18bilion kwa Halmashauri zote.
Shule za Msingi zipo kama 13,000 hivi... na sekondari zinaweza kufika 3000 hiyo pesa kama ni kwa mwaka mzima haitoshi kabisa.
Mkuu Secondary zipo zaidi ya 4000 to date.

Duc in Altum
 
Niambie ukweli ni upi. Acha ushabik hakuna swala la chama hapa.

Duc in Altum
 
Wee ni mkurupukaji! Nina uhakika kuna vitu huvijui. Kwa akili zako unaona hiyo pesa uloweka hapo juu inawezekana?? NI LAZIMA UMEKURUPUKA.
 
Billion 18 ni sawa na milion 18,000.
kama shule za msingi zipo 10,000 tu, na za Sekondari 3000 tu hiyo pesa unaigawaje? mayb wawe wanaitoa kila mwezi.
 
Taja jina la shule ili tumuulize simba chawene maana mwalimu wa mabibo hukoalipo anahaha
 
Billion 18 ni sawa na milion 18,000.
kama shule za msingi zipo 10,000 tu, na za Sekondari 3000 tu hiyo pesa unaigawaje? mayb wawe wanaitoa kila mwezi.
Watu mnakurupuka kweli, yaani mmekaa kitako Magu anakosea wapi muanze kuchonga, HIZO PESA NI ZA MWEZI, angalieni kitimoto usiku wa leo, Simbachawene ataongelea kuhusu hii wlimu bure, kaongea ITV habari na kusema hiyo ni pesa ya mwezi.
 
Basi shule zitakuwa na UKATA sana, mkuu acha povu, maendeleo ya elimu hayaji kama unavyofikiria...
 
...vipi kuhusu bei elekezi kwa shule za watu binafsi?...
 
Wamesahau pesa za kuwatunuku wanafunzi wanaofanya vyema, walimu wanaofaulisha sana n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…