A
Anonymous
Guest
Ofisi ya Mkuu wa Shule hiyi imekuwa kikwazo kwa kuongeza michango ya shule pasipo utaratibu. Ukishatoa michango hiyo kama kiingilio unapaswa tena kuchangia gharama za kuishi hosteli hiyo kwa Mwaka 860,000 michango ambayo haina uhalisia.
Uchanganuzi wa michango hiyo upo hivi:
1. Tsh 250,000 kitanda
2. Tsh 65,000 Dawati
3. Tsh 50,000 ukarabati
4. Tsh 25,000 walimu wa muda
5. Tsh 645,000 chakula
Tunaomba JF itusaidie kufichua uovu huu ni kero iliyoshindikana.
Tumechukua hatua kadhaa kutoa taarifa kwa viongozi ngazi mbalimbali lakini hakuna hatua sitahiki zilizochukuliwa.
Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanatozwa fedha ambazo hawakustahili kutozwa, ndio maana Walimu wengi wakiwemo wanaoshirikiana na Mkuu wa Shule na Idara ya Uhasibu wanatamani kubaki hapo kwa kuwa kuna maslahi mengi.
Taratibu za kuongeza malipo hazizingatiwi kwa kuwa Shule ya Serikali Mwalimu Mkuu au Uongozi hauwezi kujiamulia bila kushirikisha Wazazi na Walezi kisha kwenda hatua nyingine ngazi ya Wilaya na Mkoa, yote hayo hayafanyiki.
Serikali ya sasa mifumo yake mingi malipo yanafanyika kwa Control Number lakini huku Wazazi na Walezi wao wanalipia kupitia Akaunti ya Shule ambayo wanajua wanaimudu kutoa fedha.
WAKAGUZI WALIANDIKA RIPOTI IMEPOTEZEWA
Wakaguzi wa Kanda walikuja na kufanya ukaguzi kuhusu mambo mbalimbali, wakaandika ripoti lakini waliyoandika hayakutekelezwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Sengerema kwa sababu ambazo wanazijua wao wenyewe.
TAKUKURU SENGEREMA NAO WALIINGIA MITINI
Taarifa ya kinachoendelea ilifikishwa hadi TAKUKURU Taifa, wao wakaishusha ngazi ya Mkoa kisha ikashushwa TAKUKURU Sengerema, ikaanza kufanyiwa kazi vizuri hadi ikafikia hatua Mkuu wa Shule na Mhasibu Mkuu wakatakiwa kutotoka nje ya Mkoa.
Muda mfupi baadaye kimya kikatawala, TAKUKURU waliokuwa wakisimamia jambo hilo hawakutoa ushirikiano tena, tukajua tu KAZI TAYARI.
Wahusika wakaanza kutamba mtaani kuwa hawawezi kufanywa chochote na TAKUKURU kwa kuwa tayari wameshamalizana nao.
Tunakoelekea itafika hatua watu tutaacha kuripoti changamoto kama hizi kwa kuwa hakuna uwajibikaji, kama mamlaka tunazozitegemea na Viongozi tunaowategemea ambao ni wasaidizi wa Rais wananunulika kirahisi hivyo, basi ni ngumu kutoboa.
Video inayoonesha Shule ya Sekondari Nyampulukano.