Elimu bure: Bomu kwa taifa

Elimu bure: Bomu kwa taifa

Hatupaswi kufurahia kushindwa utekelezaji wa mikakati yenye tija kwa taifa leo na siku zijazo..twapaswa kushiriki kwa karibu ktk kuisaidia serikari kutatua changamoto zilizopo kwa kila mmoja wetu hasa wenye uwezo kuchangia kwa namna moja uboreshaji wa baadhi ya miundombinu,vifaa ktk mashule yanayotuzunguka huku tunakoishi,tunakofanyia kazi,fanyia starehe n.k

Haya ndiyo mawazo yanayotakiwa ili kuwasaidia watunga sera na watekelezaji wa sera hizo.

Basically, hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuupinga mpango huu kwa sababu lengo na dhamira yake ni njema, kuifanya elimu kuwa huduma ambayo accessible kwa kila mtu mwenye uwezo na asiye na uwezo.

Problem ina raise ktk utekelezaji wake, kuwa hakukuwa na maandalizi ya kutosha.

Mfano, serikali ya awamu ya nne ilikuja na sera ya ujenzi wa shule za sekondari ktk kila kata

Walifanikiwa kwa kiasi kikubwa japo ni sera ambayo iliibua changamoto nyingi ambazo mpaka leo hazijatatuliwa ikiwemo;

1. Upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi

2. Uhaba au kutokuwepo kabisa kwa nyumba za walimu hasa maeneo ya vijijini

3. Nyingi ya shule hizi za sekondari za Lowassa (about 95%) kutokuwa maabara kwa ajili ya kufundishia masomo ya sayansi kwa vitendo.

4. Shule hizi kutokuwa na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vinavyokidhi mahitaji ya wanafunzi k.v vitabu, vifaa vya maabara nk

5. Mengi ya majengo ya shule hizi yalijengwa chini ya viwango kiasi ambacho lifespan yake si zaidi ya miaka 20 ijayo yatakuwa yamechakaa kwa kubomoka kabisa!

6. Malalamiko ya walimu hawa hawa wachache waliopo kutopatiwa ufumbuzi wa kudumu. Mfano; uboreshwaji wa maslahi yao, kutolipwa kwa madeni na stahiki zao mbalimbali za miaka mingi, walimu kutokuwa na nyumba za kuishi ktk maeneo ya kazi nk

Sasa leo kabla serikali haijayapatia suluhisho la kudumu haya imekuja na sera nyingine inayotumia mabilioni ya shilingi ktk utekelezaji wake na wakati huohuo matatizo hayohayo yaliyopo miaka mingi nayo yanahitaji uwekezaji wa mabilioni ya fedha huku eti wazazi/walezi woote bila kujali uwezo wao wakivuliwa jukumu lao la kuchangia elimu ya watoto wao. Yaani tumesahau kabisa sera ya "cost sharing!!"

Sina hakika kama hii kitu itakuwa sustainable. Naamini kabisa, mzigo huu in the end serikali itashindwa kuubeba na ni kwa sababu ya hali ya uchumi wetu kutokuwa na uwezo huu.

Na kwa maana hiyo, kama ambavyo wazo au sera hii chanzo chake ikiwa ni mihemko ya kisiasa "ili tushinde uchaguzi", vivyo hivyo mzigo huu in the end utakavyorejeshwa kwa wazazi/walezi kwa njia ileile ya kisiasa!!

Tusubiri bajeti ya kwanza ya JPM 2016/2017 utapata uhalisia wa hili!!
 
Haya ndiyo mawazo yanayotakiwa ili kuwasaidia watunga sera na watekelezaji wa sera hizo.

Basically, hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuupinga mpango huu kwa sababu lengo na dhamira yake ni njema, kuifanya elimu kuwa huduma ambayo accessible kwa kila mtu mwenye uwezo na asiye na uwezo.

Problem ina raise ktk utekelezaji wake, kuwa hakukuwa na maandalizi ya kutosha.

Mfano, serikali ya awamu ya nne ilikuja na sera ya ujenzi wa shule za sekondari ktk kila kata

Walifanikiwa kwa kiasi kikubwa japo ni sera ambayo iliibua changamoto nyingi ambazo mpaka leo hazijatatuliwa ikiwemo;

1. Upungufu wa walimu hasa wa masomo ya sayansi

2. Uhaba au kutokuwepo kabisa kwa nyumba za walimu hasa maeneo ya vijijini

3. Nyingi ya shule hizi za sekondari za Lowassa (about 95%) kutokuwa maabara kwa ajili ya kufundishia masomo ya sayansi kwa vitendo.

4. Shule hizi kutokuwa na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vinavyokidhi mahitaji ya wanafunzi k.v vitabu, vifaa vya maabara nk

5. Mengi ya majengo ya shule hizi yalijengwa chini ya viwango kiasi ambacho lifespan yake si zaidi ya miaka 20 ijayo yatakuwa yamechakaa kwa kubomoka kabisa!

6. Malalamiko ya walimu hawa hawa wachache waliopo kutopatiwa ufumbuzi wa kudumu. Mfano; uboreshwaji wa maslahi yao, kutolipwa kwa madeni na stahiki zao mbalimbali za miaka mingi, walimu kutokuwa na nyumba za kuishi ktk maeneo ya kazi nk

Sasa leo kabla serikali haijayapatia suluhisho la kudumu haya imekuja na sera nyingine inayotumia mabilioni ya shilingi ktk utekelezaji wake na wakati huohuo matatizo hayohayo yaliyopo miaka mingi nayo yanahitaji uwekezaji wa mabilioni ya fedha!

Sina hakika kama hii kitu itakuwa sustainable. Naamini kabisa, mzigo huu in the end itashindwa kuubeba hii ni kwa sababu ya hali ya uchumi wetu kutokuwa na uwezo huu.

Na kwa maana hiyo, kama ambavyo wazo au sera hii chanzo chake ikiwa ni mihemko ya kisiasa "ili tushinde uchaguzi", vivyo hivyo mzigo huu in the end utakavyorejeshwa kwa wazazi/walezi kwa njia ileile ya kisiasa!!

Tusubiri bajeti ya kwanza ya JPM 2016/2017 utapata uhalisia wa hili!!
bravo mkuu, umesema kweli
 
Mitanzania ikoje . Magu asingeanzisha elimu bure sasa hivi ingekuwa inalalamika tena...

Mitanzania inasema ukisema "elimu bure" peleka ndururu za kutosha mashuleni. Hilo tu basi!. Kwa nini ni vigumu kuelewa? Mitanzania mingine bwana!
 
Tutarajie maumivu zaidi fikiria sasa mwaka huu Form 2 na Form 4 hawatafanya Mock wala Pre-National Exam, wao wanajiandaa kwa NATIONAL EXAM tu. Tutarajia vitimbi matokeo ya mtihani wa Taifa.
NB: kama unafikiri elimu ghali jaribu ujinga.
 
Mbona ninyi wakuu wa shule mnalialia sana??.
Kwani hamna mishahara?.
Mlizoea kupiga dili mwaka huu mmekoma.
Mkaanzisha makundi na kuwachukia walimu walokuwa wanahoji mapato na matumizi ya shule.
Magufuri kawaweza maana walimu wengi walikuwa wamekata tamaa kwa kuwaona ninyi mkineemeka na hali hamfundishi na wale wanaofundisha mnawakanyagia chini.
Kuondolewa kwa michango mashuleni naunga mkono 100%,maana kulikuwa na mgongano wa maslahi ulio sababisha walimu wengi kutofanya kazi kwa moyo.
MAGUFULI,HAPA UMEWEZA MAANA WALIMU KWA SASA TWAFANYA KAZI KWA MOYO NA SIYO KUKUOGOPA.
We MWL wa wapi? Huku kwetu hata walimu makada wa ccm hawaafiki juu ya Elimu bure. Ni hasira kubwa kwa watoto waliopo shuleni kwa sasa. TAIFA hakuna dira ya Elimu kila Rais na waziri wa Elimu wanaamua juu ya mwelekeo wa Elimu.
Kwa sasa shule zimekuwa sehemu ya kujumuika badala ya kujifunza.
 
tufike wakati tufanye masikhara kwingine kama ATCL, TTCL, VIWANDA sijui, BIBI BOMBA, Mashindano ya CHIPSI-YAI, NYAMA CHOMA FESTIVAL lakini si kwenye ELIMU wandugu.
 
Mitanzania ikoje . Magu asingeanzisha elimu bure sasa hivi ingekuwa inalalamika tena...
Bora kulalamika kukosa kuliko kupewa kitu kibovu! Shule hata uwezo wa kuchapa mitihani hazina achiliambali kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia
 
Wataalamu hawalioni hili sijui kwa nini?Shetani siasa kaingilia kati anafanya atakavyo eeh!mungu tusaidie.
Hivi unadhani Tanzania tuna wataalamu? Katika umasikini kama huu wetu usitegemee kuna mtaalamu yeyote serikalini ayasimama na kusema hili wazo au lile Ni batili au halitekelezeki.wanakubali chochote wakati wowote ili mradi wapate riziki.

Waliambiwa wafute michezo shuleni, wakafuta! Wakaambiwa wafute baadhi ya masomo kama kilimo, biashara, Ufundi, home economics, wakafuta hata bila kuhoji wakafuta.
Leo hii shule inatumiwa shs laki tatu kwa mwezi, zitafanya nini? Stupid! Katika Wizara ina watu vilaza ni Wizara ya Elimu.Kila wazo wanalipokea kama lilivyo!
 
Duh. Ukianglia hali ya uchumi, Ubabe kwenye siasa, deni la taifa, elimu mbovu unaweza kutoa machizi kama ni nzalebdo na unamachungu na nch yako.
 
Wangejaribu kuchota uzoefu toka Kenya waliokuwa na bajeti kubwa kuliko sisi lakini walikutana na changamoto kibao
 
Mzee wa kukurupuka kuhamia Dodoma utakua disaster kuliko elimu
Mwambieni kila uamuzi mkubwa unataka utafiti kwanza sio mwendokasi kuelekea kusikojulikana
 
Shule za umma nchini (msingi na sekondari) zimeelekezwa kwa waraka na. 5 wa mwaka 2015 kutoa elimu BUREEE pamoja na nia thabiti jambo hili limefanywa kwa mhemko wa kisiasa.

Maana ruzuku toka serikali kwa shule husika ni kichekesho cha karne. Wazazi wameelekezwa kutotoa mcahngo wa aina yoyote, mfano shule ya Msingi kihagara, kijiji anachotoka Naibu Waziri wa ELIMU (wilaya ya Nyasa, mkoa wa Ruvuma) imepewa 150,000/=TUTAFIKA?
😀😀 150,000 ni hela nayo lakini duuuuuuuuuuuu.
 
tufike wakati tufanye masikhara kwingine kama ATCL, TTCL, VIWANDA sijui, BIBI BOMBA, Mashindano ya CHIPSI-YAI, NYAMA CHOMA FESTIVAL lakini si kwenye ELIMU wandugu.
Eti Nyama Choma Festival
 
Back
Top Bottom