ni kweli michango ya wazazi ilikua mingi na isiyoeleweka, wakuu wa shule walikua wakipiga sana hizi fedha, lakini pia zilikua zinasaidia, wanafunzi wanaenda shule wanakula wanasoma vizuri, ila sasa hivi wanafunzi inabidi watoke saa 8 badala ya saa 11 kwa sababu ya njaa,
pia ukarabati mdogo wa vitu kama madawati, ujenzi wa vyoo, kuleta maji shuleni n.k hivi vitakua vinasubiria hela serikali kuu ambayo itakua haitoki kwa wakati na ikitoka haitoshi
kwa ufupi tumezidi kuharibu elimu
labda serikali ingejaribu ku regulate michango na kusaidia wale wasiojiweza kabisa ila sio kufuta michango yote