Elimu bure: Bomu kwa taifa

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
8,281
10,795
Shule za umma nchini (msingi na sekondari) zimeelekezwa kwa waraka na. 5 wa mwaka 2015 kutoa elimu BUREEE pamoja na nia thabiti jambo hili limefanywa kwa mhemko wa kisiasa.

Maana ruzuku toka serikali kwa shule husika ni kichekesho cha karne. Wazazi wameelekezwa kutotoa mcahngo wa aina yoyote, mfano shule ya Msingi kihagara, kijiji anachotoka Naibu Waziri wa ELIMU (wilaya ya Nyasa, mkoa wa Ruvuma) imepewa 150,000/=TUTAFIKA?
 
Niliwahi kuandika humu jamvini jinsi ccm na elimu bure wanavyoishadadia. Huu ni mkakati wa makusudi wa kuwatengeneza failures wengi kwa maslahi ya ushindi wa kishindo Siku za mbeleni kwani hawa waliosoma shule za kata waliwanyima kura mwaka jana. Hivi katika bajeti ya 2015-16 kulitengwa fedha za elimu bure? Kama hazikuandaliwa ufanisi wa elimu bure utatoka wapi? Waalim wanadai had I nauli zao za likizo za desemba 2015 hawajalipwa. Kasma ilifika ikazuiwa kusubiri mwongozo hadi februari jambo lilosababisha walimu kujinunulia makaratasi ya maazimio na maandalio. Unaipa shule yenye wanafunzi 1800 shs. 53000/- za ukarabati na shs 23000/- za uendeshaji wa ofisi ikiwa no pamoja na bill za umeme na maji na mlinzi. Huu ni utani hebu watuombe radhi tuendelee na utaratibu wa zamani wao wajipange. Huko sekondari walimu wa sayansi wamekimbia kwani wengi walikuwa wanalipwa na wazazi kwa michango yao ambayo wameizuia. Kwangu Mimi hawana nia njema na watoto wetu kwani watafeli Sana miaka hii mitano.
 
Tunafanya mchezo na ELIMU na hilo ndo anguko letu kama taifa. Sasa hivyo viwanda vitaendeshwaje ikiwa hakuna wasomi mahiri?
 
CCM wangesitisha hili swala la elimu bure , wajipange kwanza hawakufanya maandalizi.... Siyo dhambi wala siyo aibu kukubali kuwa walikurupuka kusema watatoa elimu bure ili washinde uchaguzi.... fedha zinazopelekwa mashuleni ni aibu kwa kweli..
 
Mitanzania ikoje . Magu asingeanzisha elimu bure sasa hivi ingekuwa inalalamika tena...
 
Shule za umma nchini (msingi na sekondari) zimeelekezwa kwa waraka na. 5 wa mwaka 2015 kutoa elimu BUREEE pamoja na nia thabiti jambo hili limefanywa kwa mhemko wa kisiasa.

Maana ruzuku toka serikali kwa shule husika ni kichekesho cha karne. Wazazi wameelekezwa kutotoa mcahngo wa aina yoyote, mfano shule ya Msingi kihagara, kijiji anachotoka Naibu Waziri wa ELIMU (wilaya ya Nyasa, mkoa wa Ruvuma) imepewa 150,000/=TUTAFIKA?
acha tu.wataanza kuwaomba wananchi jamani tuchangie elimu.japo kidogo.maana me niliwaza kuzaa na wife kama watoto 9 hivi shule bure.lkn nikipiga hesabu.atakae kuja baadae.
 
sie tunaangalia tuuu elimu ikizidi kuzikwa....

mungu nibariki watoto wangu waliepuke hili janga....
 
Kwa mtazamo wangu, hiki kidogo kinachopelekwa shuleni kisingekewa kigezo cha kuondoa uwajibikaji wa wazazi/walezi nao kuchangia kidogo kwa maendeleo ya watoto na shule zao!!

Kwa kifupi sana ni kwamba, hili neno sijui sera ya ELIMU BURE tayari ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya elimu yetu.

Wasitegemee kuwa wazazi au walezi watashiriki ktk uchangiaji wa maeneo mengine kama ujenzi wa miundo mbinu kama madarasa, maabara au nyumba za walimu nk.........yes, elimu si ni bure bwana?

Hili linaweza kufanyika kwa mitulinga na kwa kuwalazimisha wananchi kuchangia. Lakini ukweli ni kuwa mgogoro ndo utaanzia hapo kati ya serikali na wananchi kama contradiction No. 1 ya sera ya ELIMU BURE na ni kaburi la kuizika rasmi CCM!!
 
Mbona ninyi wakuu wa shule mnalialia sana??.
Kwani hamna mishahara?.
Mlizoea kupiga dili mwaka huu mmekoma.
Mkaanzisha makundi na kuwachukia walimu walokuwa wanahoji mapato na matumizi ya shule.
Magufuri kawaweza maana walimu wengi walikuwa wamekata tamaa kwa kuwaona ninyi mkineemeka na hali hamfundishi na wale wanaofundisha mnawakanyagia chini.
Kuondolewa kwa michango mashuleni naunga mkono 100%,maana kulikuwa na mgongano wa maslahi ulio sababisha walimu wengi kutofanya kazi kwa moyo.
MAGUFULI,HAPA UMEWEZA MAANA WALIMU KWA SASA TWAFANYA KAZI KWA MOYO NA SIYO KUKUOGOPA.
 
Back
Top Bottom