Elias Mpedi Magosi, mrithi wa Dkt. Stergomena Tax kiti cha Ukatibu Mkuu wa SADC

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
ELIAS-MAGOSI.jpg

Elias Mpedi Magosi

Elias Mpedi Magosi ameidhinishwa kukalia kiti cha Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), akimrithi Dkt. Stergomena Lawrence Tax, Mtanzania aliyehudumu nafasi hiyo tangu mwaka 2013. Dkt. Tax ni mwanamke wa kwanza kabisa kuiongoza SADC katika nafasi ya Ukatibu Mkuu na uongozi wake unafikia kikomo tarehe 31 mwezi huu (Agosti) 2021.

Magosi amembwaga Faustin Luanga Mukela wa DRC ambaye kwa sasa ni Afisa Mwandamizi wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) huko Geneva, lakini pia amewahi kuwa Mshauri wa Uchumi na Maendeleo wa Rais Kabila

DRC na Botswana ndizo nchi mbili pekee zenye haki ya kisheria ya kuteua wagombea wa wadhifa huo kwa mwaka huu

Elias Magosi ni nani?
Bwana Elias Mpedi Magosi ni Katibu Mkuu wa Rais (Permanent Secretary to the President – PSP) na Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Botswana, na pia Katibu wa Baraza la Mawaziri la Botswana. Tangu Aprili 2021 amekuwa akihudumu kama Kaimu Balozi chini ya Wizara ya Mambo ya Kimataifa na Ushirikiano.

Ana utajiri wa uzoefu wa uongozi unaohitajika katika usimamizi wa sekta zote za umma na za kibinafsi, na pia ndani ya mashirika ya kimataifa. Kabla ya kuteuliwa PSP, Bwana Magosi aliwahi kuwa Naibu wa Kudumu kwa Rais, kuanzia Mei 2018 hadi Februari 2020.

Bwana Magosi pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, (Desemba 2016 hadi Februari 2017); na Wizara ya Mazingira, Uhifadhi wa Maliasili, na Utalii, (Machi 2015 hadi Novemba 2016). Pia aliwahi kuwa Mratibu wa Mageuzi ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, kuanzia Januari 2004 hadi Februari 2007.

Bwana Magosi ana uelewa na maarifa juu ya utendaji kazi wa SADC, akiwa aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Sekretarieti ya SADC, kuanzia Machi 2017 hadi Aprili 2018.

Katika ngazi ya sekta binafsi, Bwana Magosi aliwahi kuwa Mkuu wa Rasilimali Watu, Kusini mwa Afrika, katika Benki ya Standard Chartered Botswana, kuanzia Januari 2013 hadi Oktoba 2014; na, Mkuu wa Rasilimali Watu, Botswana Insurance Holdings Limited, kuanzia Julai 2010 hadi Desemba 2012.

Kwa mujibu wa gazeti la Botswana Guardian, Magosi ndiye mtumishi wa umma anayelipwa pesa nyingi zaidi nchini Botswana, akiwa amemzidi hata Rais Mokgweetsi Masisi.

Elimu
Bwana Magosi ana Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Shirika (Master of Organisation Development Degree) kutoka Chuo Kikuu cha Bowling Green State huko Marekani

Stashahada ya Uzamili katika Huduma za Usimamizi (Graduate Diploma in Management Services) kutoka Chuo Kikuu cha Bolton nchini Uingereza

Shahada ya Sanaa katika Uchumi / Takwimu (Bachelor of Arts Degree in Economics/Statistics) kutoka Chuo Kikuu cha Botswana.

PIA, SOMA:
-
Dkt. Stergomena Tax amaliza muda wake SADC
 
Back
Top Bottom