Eid Vs Pasaka na X-mass

Inategemea na wewe upo sehem gani...Kama ni Pwani yani (Dar, Zenji, Tanga, Mtwara na Pwani) utaona Eid, Xmas, then pasaka ya mwisho.. lakini ukiwa mikoa iliyobaki Tz ni Xmas, pasaka the Eid ya mwisho.
Pengine maana mimi nipo dar na experience yangu ni ya dar. wewe upo mkoa gani mkuu??
 
Inategemea na wewe upo sehem gani...Kama ni Pwani yani (Dar, Zenji, Tanga, Mtwara na Pwani) utaona Eid, Xmas, then pasaka ya mwisho.. lakini ukiwa mikoa iliyobaki Tz ni Xmas, pasaka the Eid ya mwisho.
Eid ni mwisho kabisa mkuu, huku nilipo hata hawajui kama kuna sikukuu ya eid na vile iko jumamosi ndo kabisaa, watoto hawaendi shule kisa ni weekend.

Yaani hawajui kitu kuhusu uislam, hizi sikukuu ni eneo na eneo. Huku nanenane na sabasaba zinabamba kuliko eid aisee.
 
Eid Mubarak ya Amani na Furaha ndugu! Mengine ni mbwembwe tu.
 
Kufananisha sikukuu ambazo ni ibada na sikukuu zisizofahamika mwanzo wake isipokuwa kutoka kwenye ushirikina huweza kukupelekea ukakufuru kabisa,kuwa makini mara nyingine unapouzungumzia uislamu mkuu, hakuna mtu aliyewahi kupata hasara kwa kunyamaza, kama huna cha kuandika unanyamaza tu.

abdulqadirj
 
Eid ni kubwa DSM, Pwani, Zenji, Tanga, Lindi na Mtwara.

Mikoani huko, wengi hawajui kuhusu Eid.
Christmas inafahamika kote na inabaki kuwa sherehe kubwa zaidi ya kidini hapa kwetu Tanzania.
Inawezekana, wewe upo mkoa gani mkuu?? na hali ipoje huko??
 
Kafanye utafiti wako vizuri.... katika mwaka kuna kitu kinaitwa "msimu wa sikukuu" hii hua desemba mwishoni kwenda januari,hii hubebwa sana na sikukuu ya noeli....tuache itikadi za kidini.to be honest Christmas ndo sikukuu kubwaaaa kuliko zote duniani..... angalia hata maofisi ya umma na makampuni makubwa binafsi,hua yanapambwa na mapambo rasmi ya siku hiyo.ubaya wa eid ni kwamba haina uhakika....yaan ili kuamua km ubaki nyumbani au uende kazini inabid upige simu kwa jamaa zako waislamu,au uwashe data kuvizia clip za mufti....ila kwa wakristo tarehe zote za sikukuu ziko wazi.nawasilisha
 
Mmesahau ile misafara inayoelekea kaskazini kwaajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka hii skukuu ya idi sawa ni kubwa ila ukiongelea amsha amsha amsha asee achana kabisa na xmass hao waislamu wenyewe wanasubiri maana kila kona ni nyimbo kuanzia tarehe 15 mpka mwaka unaisha😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…