Naamini kabisa pesa nyingi kama hii mpaka bank itoe kuna idhini ya bank kuu BOT, nafikiri ndani ya BOT kuna uozo wa hali ya juu, hii Stanbic hata mwaka mmoja haujapita imetoka kupiga dili la Escrow, je hawa na bank ya mkombozi wako juu ya sheria za bank kuu?
Gavana mkuu ana nini mpaka sasa anatazamwa tu?
Pale BOT ajira nyingi za watoto wa vigogo wasio na ujuzi kabisa,
Wizi huu umefanywa na Kamishna Mkuu wa Zamani TRA Kitilya ka ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Stanbic Bank ambae pia alikuwa Mratibu wa Kampeni wa Ndugu Lowassa anaitwa Bashiru Awale alietimuliwa hivi karibuni hapa nchini walizidisha deni kwa dolla million sitta sawa na 15 Billion tsh. Iligundulika baada ya Maofisa wa BOT kuhisi huo mchezo
Mkuu BOT hawajui kitu maana hawa jamaa kabla hawajaanza uchunguzi wanahojiwa kwa kitu wanachotaka kufanya katika kipindi bbc kama si outsorce ni hardtalk harafu inaweza pita hata mwaka wanakuja na mrejesho wa kazi yao sasa wanadai kuna Rushwa kubwa ingine ni vile umeme ndio tatizo kama unawafatilia utajua mengi kuriko hao BOT unaowasema maana wanasubiri kama sisi tu kupata taharifa za uwizi wa fedha..
ni EGMA, sio EFGM. na ni Harry, sio HenryAISEE OMBENI SEFUE KATUMBUA JIPU ZITO ITV JAMANI
KUMBE ILE KAMPUNI ILIOTUPIGA IKISHIRIKIANA NA STANBIC BANK WAHUSIKA.N HENRY KITILYA XTRA ....NA MBOYA ...SASA UKITAKA KUJUA DUNIA HARAMU +NA YULE.MISS UTAELEWA SASA NA YEYE ALIiNGIZWAJE
MH MAGUFULI KURUDISHIWA HELA AISAIDII TUNAKA WALIOOHONGWA WAFUNGWE WAENDE NDANI..SFO WAMETAJA WALIOHUSIKA N MZEE WETU H KITILYA NA JAMAA MMOJA SOMEBODY MBOYA..KUWEKA NCHI IWE NA ADABUWAPELEKWE MAHAKAMANI NA KESI iSIKAE MIZEZI 3..
NAKAMA WAO WANA AMA WALITUMIKA KAMA MIDDLEMAN WASEMA TOP NANI..
Maafisa wa BOT ndio waliohisi huu mchezo baada ya kufanya reconciliation kati ya deni lililo ripotiwa na Stanbic Tz na Stanbic UK wakaona tofauti kufuatilia hiyo tofauti wakakuta ni Agent fee ambayi haikuwa kwny mkataba na ilipitia kweny kampuni ya Kitilya ndipo ikaomba Msaada wa SFO
Dah inasikitisha kuona uingereza inatusaidia kuibua madudu yetu, hivi hao mabalozi wanakazi gani huko abroad, nikweli hawajui maofisa wetu wanapokuja huko wanafanya madudu gani, ofisi zao huwa wapo waambata kibao mpaka maofisa usalama, ila nasikia wanalipwa mishahara duni, (but where is loyalty) hata hvyo nyie maofisa waandamizi, nyie wasomi wetu kwenye positions muhimu ni mbwembwe tu, majivuno, suti, magari na nyumba zakifahari, lakini ni aibu tu. Huwa mnajidai tu lakini hamna lolote. Yani mmeitia aibu nchi na raia wake. Hamna hata aibu, nasasa mnaumbuka.
Standard Bank to Pay $32 Million Over Tanzania Bribery Case - WSJNingeomba THE BOSS aje alisemehe ili maana anamkubal sana uyo KITILYA
Stanbic Tanzania In Financial Scandal Scandal - Bing NewsSefue ametumia lugha laini mno! Anasema kama kuna watu walihongwa! Kah!!! Waingereza wamesema wazi kuwa zile pesa zilitumika kuwahonga maafisa wa serikali Tanzania!
Sefue anataka kuweka credit kwa benki kuu Tanzania kitu ambacho Nina mashaka nacho, benki nao in watuhumiwa katika hili! Ningewaelewa kama wangekuwa wa kwanza kukamata hawa wezi na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola bila kusubiri hisani ya waingereza kutukamatia!
Kama waingereza wasingefuatilia sidhani kama hii pesa ingerudi! Inaonekana kabisa hapa kuna ubia wa uovu kati ya benki kuu na stanbic bank! Haiwezekani hii benki ikawa inatoa Fedha cash kwa mabilioni katika muda mfupi bila kuwa na hofu na benki kuu kama hawana ubia! Wakati wa sakata la escrow ni hawa hawa waliruhusu pesa zichukuliwe kwenye viroba kwa mabilioni na mpaka Leo "wamegoma" kutoa orodha ya wahusika na wanaendelea na biashara kama kawaida pamoja na bunge kupiga makelele! Namwomba Magufuli awatembelee kwa kushtukiza na awaombe hiyo orodha ya escrow tuone kama naye watamgomea! Hilo jipu linamsubiri Magufuli maana watanzania wanalijua japo nasikia inasemekana limekaa pabaya!! Tukubali tuna matatizo makubwa ya uadilifu benki kuu, wanakubali kutumiwa na mafisadi!