EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

EFD: Wafanyabiashara Kariakoo wagoma!

Peter jaluo

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2013
Posts
1,750
Reaction score
253
Mgomo tena Leo.

wafanyabiashara wa kariakoo.wamefunga maduka yao kwa muda usiojulikana kutokana mgomo wa mashine.

Wafanyabiashara katika viunga vya Kariakoo, Wilaya ya Ilala wamegoma kufungua maduka leo ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Sababu za mgomo huo ni kupinga amri ya Seriakali kuhusu matumizi ya mashine za kielectronic (EFD). Migomo ya namna hiyo imeripotiwa katika miji ya Musoma, Mwanza, Iringa, Mbeya nk. Migomo ya namna hii inahatarisha uchumi wa nchi ambao uko katika kipindi kigumu kuliko muda wowote katika mwongo huu.

Je, si wakati muafaka kwa Serikali kukaa chini na kutafakari maamuzi yake?

Kariakoo ni eneo ambalo ni muhimu sana katika kuingizia serikali mapato pengine kuliko eneo lolote nchini. Zaidi ya hayo ni eneo ambalo hutegemei mfanyabiashara atengeneze faida kubwa kulingana na makato yanayotakiwa kufanywa kwa kila mauzo...

Tujadili mada hii kwa hoja za msingi ili kunusuru uchumi wetu!
 
na wanachi kuhusu kupanda kwa gharama za umeme wangefanya kama wafanya biashara.
 
Mgomo tena Leo.wafanyabiashara wa kariakoo.wamefunga maduka yao kwa muda usiojulikana.kutokana mgomo wa machine jk upo mpaka hapo

Jk anahusikaje hapo?
Waache ujinga kulipa kodi ni lazima tatizo wameshazoea kukwepa kodi.
 
na wanachi kuhusu kupanda kwa gharama za umeme wangefanya kama wafanya biashara.

Mpaka uchaguzi mkuu ufike tutajikuta hata tukiongea au tukipumua tunatozwa kodi za kifisadi ili chama cha baba kipate pesa za kushinda.Bora punda afe mzigo wa baba ufike.
 
Leo wafanyabiashara wamegoma nchi nzima
kuhusu hizo mashinde za EFD

Chanzo:Radio One Stereo.
 
Leo tar.10/02/2014 wafanyabiashara
Songea mjini leo kwa pamoja
wamegoma kufungua biashara zao
ikiwa ni njia ya kuonyesha
kutokubaliana na mashine za kutolea
risiti za TRA (EFD).Wafanya biashara
hao wamedai kuwa mashine hizo ni
UTAPELI mtupu.Wengine wameenda
mbali kwa kusema mashine hizo ni
UKIMWI wa BIASHARA.my
take:Serikali ikae na
wafanyabiashara kutatua tatizo
hili,vinginevyo hata kama
watawalazimisha kununua mashine
hizo, wanaweza kufanya hujuma ktk
mashine hizo na hivyo kufanya lengo
la TRA kutokufikiwa.
 
Tunataka barabara nzuri, tunataka hospitali zenye huduma nzuri, tunataka huduma nzuri za maji bila kusahau tunataka Elimu bora na ya bure.HII INAWEZEKANA TU KAMA TUTALIPA KODI MBONA WAFANYAKAZI WANALIPA KODI BILA TATIZO.LIPA KODI KWA MANUFAA YA NCHI YAKO
 
Hawataki kulipa kodi? Wao si maajenti tu wa kukusanya kodi? Hapa serikali inabidi ikae kimya, wakipitisha siku tatu iwanyanganye leseni zao za biashara kuonyesha kuwa 'the system works..'
 
Hapa jk anaingiaje kwani yeye ni waziri wa viwanda na biashara?
 
Hawa watu hawataki kulipa kodi halafu wanajifanya kugoma wapolwe leseni basi hakuna kuwabembeleza.
 
Nimesikia kua mgomo upo Tanzania nzima!

Nchi nzima si balaa hili.
Hapa serikali inatakiwa iwasikilize wafanyabiashara lakini hizo mashine zitumike ili ukwepaji kodi usiwepo..
 
Hawa watu hawataki kulipa kodi halafu wanajifanya kugoma wapolwe leseni basi hakuna kuwabembeleza.

Kuwapokonya leseni sio suluhisho, hao TRA ndio wanaharibu katika hizo mashine. Suala ni kukaa na kusikiliza madai yao.
 
Tunataka barabara nzuri, tunataka hospitali zenye huduma nzuri, tunataka huduma nzuri za maji bila kusahau tunataka Elimu bora na ya bure.HII INAWEZEKANA TU KAMA TUTALIPA KODI MBONA WAFANYAKAZI WANALIPA KODI BILA TATIZO.LIPA KODI KWA MANUFAA YA NCHI YAKO

We unajua kodi tunayolipa inakwenda wapi? Au na wewe ni walewale? Watu wanazunguka dunia nzima kuomba omba tu huku wanajiongezea kiinua mgongo bungeni alafu vijijini hamna kitu. We unashabikia uzuzu?
 
Anyways..mashine zinaweza kua ni tatizo kwamba bei yake iko juu..ila tukiangalia kinachowapa hasira wafanyabiashara wengi ni ile 18% ya VAT ambayo inasababisha bei ya bidhaa zao kuwa juu na wengi wanahofia kupoteza wateja na pia wengi wao sio wakweli mana walikua wanapeleka hesabu za uongo TRA ili walipe kodi kidogo, sasa mashine zinakuja kuweka ukweli waz na watu hawako tayari kupoteza pato lao!
 
Back
Top Bottom