ni kweli dear. Vitu vingine ukikaa ukafikiria unavyofanya kila siku unapata moyo wewe ni super woman. Uamke asubuhi mzee umpe cha asubuhi, mtoto aandaliwe shule, mzee anyooshewe nguo za kazini na zako, wakati huo chai ipo jikoni, na hakuna muda jina mama linaitwa mara nyingi kama asubuhi(kwangu mimi), uangalie kila kitu kipo sawa, na uweke utaratibu wa mchana vizuri hadi jioni, upo kazini unawaza jioni itakuwaje, upige simu mara nanenane kukumbushia vitu. Bado ukirudi jioni u do it all over again. Sio rahisi hata kidogo ila ina heshima na baraka zake.