Edward Ngoyai Lowassa anataka kuharibu kanuni za maisha (principals of life)

Omuchimati

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
427
202
SALAMU,
Salamu kwa wanablog wote ulimwenguni hizi ni salamu zangu nazitoa kwa unyenykevu wa hali ya juu, na kwa mapenzi mema kabisa kwenu ninyi wana blog wenzangu wenye mtizamo chanya wa maisha ya sasa na yajayo.

Awali ya yote namshukuru MUNGU muumba nchi na ulimwengu pamoja na miiisho yote ya dunia yeye ndiye tumaini letu katika kila jambo , tuiwapo na raha au shinda sifa huwa zinamwendea yeye kwani yeye ndiye mwanzo na mwisho yaani ALFA NA OMEGA, na pasipo yeye pasingalikuwapo kitu.

Ndugu zangu Watanzania nadhani wote tunamfahamu vizuri ndugu yetu NGOYAYI LOWASSA,sipendi sana kuongelea historia yake maana kila mmoja wetu anayo historia iliojaa mema na mabaya, inategemea tu kiwango cha mema au mabaya ambayo historia yako imebeba kwa hiyo sipo hapa kuelezea mema aua mabaya ya MHE EDWARD NGOYAI LOWASSA,

Mada yangu itajikita zaidi kwenye kichwa cha habari hapoa juu, ni nini kanuni za maisha (principals of life) The laws of nature, Ukisoma Biblia yako au quran tukufu inaonesha kuwa mwanadamu alipoumbwa aliwekwa Eden MUNGU akamwambia mwanandamu ailime na kuitunza bustani hiyo,wakati huo mwanandamu alikuwa hajamwasi MUNGU,kwahiyo naamini kabisa kama mwanandamu angeendelea kuishi maisha yale ya kumhemshimu MWENYEZI MUNGU,asingekula kwa taabu wala kuzaa kwa uchungu,

Baada ya mwanandamu kumuasi MUNGU kwa kisingizio kuwa mwanamke aliyepewa ndie kasababisha anguko lake MUNGU aliweka Principals(kanuni) za mmwanandamu za namna ya kuishi zinazoendanadana na kanuni ya asili (THE LAW OF NATURE)kutokana na lile anguko la mwanadamu pale EDEN,kwamba itabidi ufanye kazi kwa bidii ili upate kipato chako haijalishi umezaliwa katika mzingira gani,usipofanya kazi kwa bidii huwezi kufanikiwa hata ukiwekewa mamilioni ya pesa mlangoni kwako,utaugua na itafika wakati utakufa,utazaa kwa uchungu.

MHE EDWARD NGOYAI LOWASSA anakiuka misingi asili alioweka MUNGU kwa kuwarubuni wanandamu wa Tanzania kuwa yeye anao uwezo wa kuwafanya wawe matajiri pasipo kufanya kazi wala kujituma,

Amekuja kuharibu kanuni za maisha kama vile shetani alivyomshukia Hawa pale EDEN na kumwambia kuwa kama angekula lile tunda angefanana na MUNGU,LOWASSA anawaambia Watanzania kuwa yeye anao uwezo wa kuondoa umaskini na kumfanya kila mmoja wa watanzania awe kama Bakheresa hyo ni nchi ya namna gani?

Ushauri wangu kwa Watanzania tumieni hekima na akili kuamua mambo yenu.
 
Wewe mbona hujaweka wazi unachoumwa?

Kwanza hili ni jukwaa la siasa sio dini
 
Usimuhukumu mwenzako nawe usijeukahukumiwa

Magamba yanatia huruma sana. Na hii dhambi itayatafuna.

Embu wajiulize akina JK na MAGUFULI walifuata nini Samunge kunywa kikombe kama ni wazima??

Umaskini unaweza kutoka ndio, kama hili jini nyonyanyonya linalopeleka mali zetu ulaya kila siku, dhahabu yetu, tanzanite yetu na fedha zetu, litaondolewa!
 
Watanzania ataowarubuni ni wale wale wajinga ndiyo waliwao.

Lowasa kafanya nini alipokuwa Waziri Mkuu? Miaka miwili tu kajilimbikizia mabilioni mpaka CCM wakamtema.

Huyo ni shtani aliyepelewa umalaika na DJ.

Hivi Mbowe na yeye si mchapaji tu? Mmesahau Mafuso chakavu aliwauzia shilllingi ngapi chadomo?
 
Magamba yanatia huruma sana. Na hii dhambi itayatafuna.

Embu wajiulize akina JK na MAGUFULI walifuata nini Samunge kunywa kikombe kama ni wazima??

Umaskini unaweza kutoka ndio, kama hili jini nyonyanyonya linalopeleka mali zetu ulaya kila siku, dhahabu yetu, tanzanite yetu na fedha zetu, litaondolewa!

Toka misingi ya dunia kuumbwa sijawahi ona nchi ambayo wakazi wake wote ni matajiri hata wewe umeshindwa kuumaliza umaskini ulio kwenu jifunze kufikiri.
 
Wewe unauelewaje umaskini?

kama unavyofikiri wewe ndivyo ulivyo umaskini hatuwezi kufanana wote kama vilivyo vidole vya mikononi mwako,hyo ndiyo principal ya maisha,na mabadiliko yanatokana na wewe mwenyewe uimtegemee Bwana kama wewewe ili akufanyie mabadiliko.
 
Kati ya ccm na Lowassa nani wakala wa shetani? Ni ccm ambayo kwa miaka 54 huku kukiwa na easilimali za kutosha pamoja na kuwahamasisha watanzania kufanya kazi usiku na mchana kwa kauli mbiu zao za kilimo cha kufa na kupona watu wakalima bado wanazidi kua masikini,huku ccm hiyo hiyo ikiwaibia wakulima na wafanyakazi.

Ni ccm ambayo Mungu kawapatia watanzania utajir wa kutosha wao wameiharibu kwa kuuza wanyama,kuua tembo tena nk, ccm ni wakala wa shetani, kazi ya shetani ni kuiba,kuharibu na kuua, hayo yote yamefanywa na ccm.

Ccm haihitajiki tena na haitakiwi, imeshindwa kuleta maendeleo kwa miaka 54 sasa utawezaje kwa miaka 5 ijayo wakati washakula rasilimali zote wakamaliza.

Nusu karne ya mateso na uonevu imefika mwisho, ccm angalieni ustaarabu mwingine.
 
acha unafiki ni lini amewai kusema ataleta utajiri bila kujituma wala kufanya kazi???alichosema yy ni kuwa na mbinu za kuondokana na umaskini km vile kufufua viwanda ili kuongeza soko la ajira kwa vijana...msome vizuri utamwelewa usikurupuke
 
acha unafiki ni lini amewai kusema ataleta utajiri bila kujituma wala kufanya kazi???alichosema yy ni kuwa na mbinu za kuondokana na umaskini km vile kufufua viwanda ili kuongeza soko la ajira kwa vijana...msome vizuri utamwelewa usikurupuke

Kwanini alishindwa kuyafanya hayo akiwa waziri mwenye afya yake nzuri?
 
Nyie vijana mnao ishi kwa shemeji zenu hata hamjui nini maana ya umasikini..mnakula bure..mnalala bure...Ccm inagawa gas bure kwa wachina nyie mnashangilia tu Ccm hoye...toka usingizini amka msaidie shemeji yako kutafuta kwa kumtoa mkoloni mweusi Ccm ambaye kauza Mali asili zetu zote
 
SALAMU,


MHE EDWARD NGOYAI LOWASSA anakiuka misingi asili alioweka MUNGU kwa kuwarubuni wanandamu wa Tanzania kuwa yeye anao uwezo wa kuwafanya wawe matajiri pasipo kufanya kazi wala kujituma,LOWASSA NI MJUMBE WA SHETANI


MHE EDWARD NGOYAYI LOWASSA NI MGONJWA,yeye analijua fika hilo kutoka moyoni mwake kama anabisha aiweke wazi ripoti ya daktari wake,.

Ukichanganya siasa na dini unaishia kuwa mwehu....

1- Ni lini na wapi Edward alisema atawafanya watu matajiri from air bila kufanya kazi?
2- Kama wewe unajua ugonjwa wake kwa nini usiuweke wazi? Ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari.... kwa post yako inaonekana wewe ni mgonjwa zaidi ya Lowasa.

NB....Sitampigia Lowasa au Magufuli kura si kwa sababu ninawachukia wao na vyama vyao, bali kwa sababu nafurahia sera za Mtikila za miaka ya 90's.
 
Mtamaliza malimao na ndimu, tumetembea na Lowassa jana siku nzima. Watanzania tunampenda, tunamkubali, tumemuamini na tutampa kura zetu kwa kishindo aende Ikulu
 
Wewe sio bure umetumwa,na hapa sio mahali pake nenda huko CCM na maneno yako ya kipumbavu,na wapumbavu wenzako wana CCM,hapa hupati kitu
 
Back
Top Bottom