Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Namshauri lowasa akate rufaa haraka sana. Kwani walishamkata tangu jana. Na wameondoka na jina la augustino ramadhan kuwa ndio rais. Na hiyo hivyo vikao ni danganya toto tu kwan mgombea wanae. Lowasa lijue hilo mapema. Lakin sisi tunamtaka lowasa kama wao wana mtu wao basi wabaki na chama chao na mtu wao na sisi na mtu wetu lowasa tutajua la kufanya.

chukueni lowasa wenu na pelekeni mnapotaka kwenda nae,

lakini jua kuwa Ramadhani wala hawezi pitishwa na ccm maana majina matatu ndo yanapitishwa na kwenda kupigiwa kura kama haujui kitu bora ukae kimia,maana mnaboa juzi mumemzushia makongoro kuwa kakamatwa na rushwa kumbe uongo nyie vipi?
 
Sisi tujadili anakatwa au akatwi...kenya wameleta reli za mwendo kasi huko...

Ndio maana tunataka akatwe huyu fisadi ili tuluweke rais wakutuletea hizo treni za mwendo kasi maana huyo hata barabara zitaota nyasi
 
Katika pitapita yangu mitaa ya mjini jana wakat msanii anasindikizwa uwanja wa ndege kuelekea dodoma yupo jamaa ni mfanyabiashara wa madini alituelezea kuwa jina la LOWASA limeshakatwa na wameamua kumpa AUGUSTINE RAMADHANI.

Haikuniingia akilini kama ccm na utashi wao wakamuacha mtu anayependwa na wananchi, nikawaza neno moja tu kumuomba Mungu afanye muujiza wake pale kikwete atakaposimama na kutaka kutangaza ataje jina la LOWASA kama atatamka vinginevyo namuomba sana LOWASA ajiunge na chama chochote wananchi tumpe nchi.

Nayasema haya kwa sababu ukiangalia sehemu zote ccm ilipopigwa,iwe kwa mwenyekiti wa mtaa, diwani au mbunge ni pale walipomkataa anayetakiwa na wananchi na kumuingiza asiyetakiwa, na katka hili wakikata jina la LOWASA, LOWASA aingie chama chochote achukue nchi.

Ikulu sio genge la wezi, kama mnampenda mkanywe nae chai, mwe need serious people sio wasanii, tumechoka na mbwembwe!Agustino Ramadhani au Makongoro Nyerere full stop!Hawa hawajui style za serikali na hawajawahi kuwa mawaziri wa serikali zote lakini wana sifa za uongozi wa kiutumishi na that is what we need this year!Kwa nini mlalie upande mmoja tu, mmepewa nn!? Haiwezekani mtu atumie nguvu kubwa hivi kuingia ikulu kunanini pale!?
 
Nani sio fisadi nchi hii....labda tubadilishe sheria za nchi hii na nani atazibadilisha kama wananchi wenyewe ndo hawa watz
 
maybe awe rais wa waendesha bodaboda jamani jamani hivi kama kweli watanzania wanampenda namna hii kwa nini atumie nguvu kubwa namna hii kuingia magogoni
 
Mtakanyagana sana, sisi yetu masikio na macho. Mradi tu msimalizaneni na kulogana.

Sisi tunawasubiri atakayekuwa na misuli na aje atutawale. Ndio dalili za mwisho wa dunia, mauovu ndio yanazidi kuwa na mamlaka zaidi ila yana mwisho wake.


Wengine tutateseka kimwili ila roho zi hai. Huu ndio muda wenu wa mavuno toka kwa wagombea uongozi.
 
Namshauri lowasa akate rufaa haraka sana. Kwani walishamkata tangu jana. Na wameondoka na jina la augustino ramadhan kuwa ndio rais. Na hiyo hivyo vikao ni danganya toto tu kwan mgombea wanae. Lowasa lijue hilo mapema. Lakin sisi tunamtaka lowasa kama wao wana mtu wao basi wabaki na chama chao na mtu wao na sisi na mtu wetu lowasa tutajua la kufanya.

Tatizo ni ajira yenu itakuwa imeishia hapo. Next time plz......
 
Hakika jina la Lowassa kupitishwa au kutopitishwa ni faid murua kwa UKAWA.Lowassa ni rahisi sana kushindwa na upinzani na hana cha kusema chukwani zaidi ya kudai ushahidi kwa raia wasio na uwezo wa kumpatia.

Asipopitishwa huyu bwana ni Nailotic,anaweza kususia vyote.Hii itakuwa faida murua kwa upinzani.

Hivyo maandiko yanaelekea kutimia yale aliyoyanena baba wa Taifa.Watz wanaweza kutafuta mabadiliko nje ya CCM.

Heri ccm wampitishe kuliko kutokumpitisha maana hadhari ya kutokumpitisha ni kubwa kwa chama na wanachama kuliko kumpitisha ambako atapambana na kuweza kushinda Urais.

CCM wajue hali ya hewa ni hatari kwa chama hicho kuliko wakati wowote ule.Na wakicheza hakika wanakwenda kupoteza uchaguzi huu na ccm kusambaratika kama KANU
 
maybe awe rais wa waendesha bodaboda jamani jamani hivi kama kweli watanzania wanampenda namna hii kwa nini atumie nguvu kubwa namna hii kuingia magogoni


Hiyo nguvu unayoiongelea ni ipi? ndio ujue kuwa nguvu uliyoiona ni nguvu ya umma..umma unamuhitaji ndio maana hamuishiwi la kusema.
 
Lowassa ndiye Rais mtarajiwa, hakuna sababu yeyote itakayopelekea jina lake likatwe.
 
peleke mwizi wenu sisi rais wetu atakuwa kati ya hawa,

1,magufuli
2,mwandosya
3,ramadhani

hawa ni watu makini na wachapa kazi,
 
Namshauri lowasa akate rufaa haraka sana. Kwani walishamkata tangu jana. Na wameondoka na jina la augustino ramadhan kuwa ndio rais. Na hiyo hivyo vikao ni danganya toto tu kwan mgombea wanae. Lowasa lijue hilo mapema. Lakin sisi tunamtaka lowasa kama wao wana mtu wao basi wabaki na chama chao na mtu wao na sisi na mtu wetu lowasa tutajua la kufanya.

Tatizo ajira zenu zitakuwa zimeishia hapo. Next time please hatumuhitaji sasa.
 
Lowassa ndiye Rais mtarajiwa, hakuna sababu yeyote itakayopelekea jina lake likatwe.

sababu hizi hapa
1,makundi
2,rushwa
3,visasi
4,kashifa
5,afya
6,zarau zidi ya viongozi wake
7,kampaini kabla ya ilani ya chama,
 
Hiyo nguvu unayoiongelea ni ipi? ndio ujue kuwa nguvu uliyoiona ni nguvu ya umma..umma unamuhitaji ndio maana hamuishiwi la kusema.

wanaccm ni milion 7 yeye wakati anakusanya watu wake hata milion 1 hawakufika je unazani waliobaki wako nyuma ya nani?mnachekesha nyie.
 
Tuambie ufisadi wa Lowasa uko wapi..tupe vielelezo sio unaropoka tu hapa.


1 Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowassa na wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya wakati, na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowassa ameanza kampeni ya urais Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu na kumwaga rushwa ya kutisha!

2 Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake, katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowassa amefanya mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi katika kila mkutano wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa kura zao awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.

3 Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi, kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini, upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu sana ya kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa nchini na fisadi Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani, kumehusika ‘’Money laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo yote ni halali, na kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa ajili ya Taifa. Ni marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa kugombea urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa nchi yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Utawala wa Sheria

4
Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya mmwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza nchi nzima makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano makali ya mara kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu Lowasa ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa asilimia 95 ya wananchi! Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea kiasi cha kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!

5
Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na kujipatia maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.

6
Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli wote aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu mengi na kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua mvua Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi.

Ni mlemavu wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa, anayeweza kumruhusu fisadi Edward Lowassa agombee urais. Sifa za mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama “Baba” yao, kuwa hafai kabisa kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, kama alivyomtangaza hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!

Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.

Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake wa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi kama China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa kupigwa risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!

7.
Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais! Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima mwombaji awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:

a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.

b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa utendaji wa akili zake.

c.
Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote yanayowatokea wananchi wote kila walipo, na kusimamia utekelezaji wa majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa, hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na afya bora yenye kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote

d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo kiongozi mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa mambo yake na ya familia na jamii yake atatumikia maslahi yake zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!

e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje ya nchi, kukosekana na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya dhamana kubwa aliyopewa n.k. Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa macho tu, kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya afya bora, ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa dhamana kubwa sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais kwenyewe anatafuta kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya anagombea asichokiweza kabisa.

Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli tunalithamini na kuliheshimu Taifa. Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA.

Ni dhana potofu sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’. LOWASA NI MOJAWAPO WA WAGONJWA WA MAGONJWA SUGU WA;IOKUWA WANATIBIWA NA BABU WA LOLIONDO NA TANGIA PALE HAJAPONA NA ZAIDI SANA ANAANZA KUTETEMEKA




HILI NI FISADI TU!!! KASHFA ZOTE HIZO!!!
 
TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.

Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.

Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.

Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni

Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO

Hivii kweli Mwakumbuka shuka ingali kumeisha pambazuka kweli ???? Does this click in ur head ???
Muda woote mlihaswa acheni hizoooo ni kukiuka taratibu za chama lakini mliendelea fanya upuuzi huo mikoani kisa njaaa zenu kumbe mlikuwa sijui mmetumwa kumharibia Ndg Edwadi Lowassa.

My Take
Ulie andika huo ujumbe we ni msaliti na mvurugaji wa kwanza wa kampeni za Lowassa kwani ulipaswa jua taratibu zote za mchakato huu mzima mwanzo hadi mwisho na kupanga strategies zote za kuhakikisha Lowassa anafanikiwa na kupitishwa na CCM kuwa M/Kiti na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ila leo Unakurupuka mda wa kiti moto kimeisha anza kufuka.


 
Back
Top Bottom