Kuna mizee lazima imwangushe Lowassa, yenyewe ipo kuchuma tu haijali watoa jasho.Wote hao wasubiri kupigwa za uso tu pamoja na mtu wao Lowassa.
Mm na jamaa zangu 3 tuko 4u movement, pesa tunakula vzr tu, lkn Kura zetu ni kwa Dk SLAA,
NA MAPAMBANO YA CHINI KWA CHINI YANAENDELEA,
TANZANIA KWANZA MAFISADI MKAFIE MBALI
fiks tupu hata kama simtaki Lowasa lakini si kwa andiko jepesi kama hili
Muungano wa mafisadi special thread
Mkuu, hata team Lowassa, Friends of Lowassa na 4U Movement kinachowapeleka kwake ni mshiko tu , ukweli wanaujua sana tu.Sipendi Lowasa awe raisi wa taifa hili....
comrade Tata habari imekaa kiwepesi sana kwa wepesi huo hakuwezi kuaminika.......Tata kupambana na ufisadi hasa wa akina EL na ma cccm kunabidi hoja nzito nzito sio nyepesi kama hii........hata kabla hajamaliza ziara zake palitoe maneno hyohayo pale Iringa na mimi nilishuhudia wazee baadhi na vijana haohao wa 4u wakidai nauli haitoshi ili warudi kijijini boma la ng'ombe na kidabaga.....lakini still hao ho wakaonekana tena songea wakimsapoti........hija yangu iko hapa inabidi kuwe na hoja nzito ili kupambana nao hapo ndipo tutawashinda lakini kwa hizi nyepesinyepes kwa hawa waliozoea kupewa kanga,ubwabwa t shirt na kofia ni vigumu kuwaeleweshaMbona habari imekamilika kabisa mkuu au ndo moja ya wale Team Lowassa nini? Ila ni furaha kwa wachukia mafisadi, endeleeni kusigishana.
Ndo maana Watanzania applications zenu za kazi zikitua kwenye desks za Wasomi Mambo Leo lazima applications hizo wazipige chini na mwishowe mnaishia kulalamika! Hicho ulichoandika hapo juu kinapaswa kuandikwa na kusomwa kama risala ya wakati wa mazishi yake na sio kama mtu anayetafuta the top most leadership position! Unakuta mtu ana MSc. Economics anashusha CV eti mwaka fulani hadi mwaka fulani I worked as Planning Officer in so and so institution; mwaka fulani hadi fulani I worked as a researcher! Mwaka fulani hadi fulani I worked as Senior Economist ministry of so and so... mwaka huu hadi ule nilifanya huku na kule.... SO WHAT? Does it mean anything for someone looking for results? Tell us what you did and not the chair you sat. We all know kwamba kuna watu kwenye viti vyao vizito kazi yao ni kupiga mihuri na signatures tu wakati hawana hata ubavu wa kuvielezea hivyo wanavyovihidhinisha achilia mbali kuvifanya! Ikiwa nitalazimika kumchagua Lowassa kwavile amekuwa Mbunge tangu 1990 basi ni bora tungemshawishi Anna Makinda agombee ambae amekuwa mbunge tangu kabla wengi wetu hatujazaliwa! Ikiwa nitalazimika kutaka kumchagua kutokana na kuhudumu nafasi mbali mbali za uwaziri, ni kwanini basi nisimchague Mwandosya ambae ana additional credit ya u-profesa huku nae akiwa pia amepata kuhudumu nafasi mbalimbali za uwaziri?! Au kwanini nisimchague Pinda au Sumaye ambao wamehudumu muda mrefu zaidi kwenye nafasi ya u-PM huku wakiwa pia wamepata kushika nafasi mbalimbali kuliko huyo Lowassa! Kwanini nisimchague Dr. Asha Rose Migiro ambae si tu kwamba ni msomi kuliko Lowassa lakini amewahi kushika nafasi kubwa duniani ambayo there's no way Lowassa atakuja kuishika! Ikiwa viti ambavyo mtu amepata kukaa ni muhimu ni kwanini basi tusimchague Mahiga ambae pamoja na kwamba ni msomi wa hali ya juu kuliko Lowassa lakini amepata pia kushika nafasi mbalimbali zenye ushawishi wa kimataifa! Kwanini nisishawishike kwamba Muhongo ndie the best candidate kutokana na usomi wake usio shaka uliomfanya atambulike sehemu mbalimbali duniani kupitia taaluma yake?
Endelea kufahamu kidogo kidogo kuhusu Lowassa
Lowassa alizaliwa tarehe 26 August 1953 mkoani Arusha. Ni waziri wa 8 wa JMT akipokea kijiti kutoka kwa Mh Fredrick Sumaye kutoka 30 Desemba 2005 hadi 7 Februari 2008 na kumuachia Mh Mizengo Pinda ambaye hadi tunavyooandika hapa ndie waziri mkuu wa JMT nae ametangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya ccm mwaka 2015!
Kabla ya kuwa waziri mkuu, Lowassa alikuwa waziri wa Maji na Maendeleo ya mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 akiwa chini ya rais Mkapa. Wizara hii alimuachia Mh Stephen Wassira baada ya yeye kuteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka 2005. Aliingia bungeni kama mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM mnamo Novemba, 1995.
Lowassa aliwahi kuwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu kipindi cha pili cha urais wa Mh Ali Hassan Mwinyi. Mwaka 1995 alianza harakati zake za kuwania urais wa JMT ndani ya CCM. Hakufanikiwa kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM mwaka huo wa 1995 hivyo aliamua kugombea ubunge wa jimbo la monduli na kushinda kwa zaidi ya 90%.
Mnamo mwaka 1997 aliteuliwa kuwa waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais - mazingira na umaskini. Lowassa alidhihirisha uwezo wake wa kiongozi zaidi akiwa waziri wa Maji na Mifugo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005.
Mwaka 2005 Lowassa aliacha harakati zake za kuusaka urais badala yake akaanza harakati za kumuunga mkono Mh Jakaya Kiwete kwenye mbio zake za urais. J Kikwete alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu sana, naye Lowassa alikubali kuwa campain manager kwenye mbio zake urais, ambapo Mh Jakaya Kikwete alishinda urais wa JMT kwa zaidi ya 80% chini ya menejimenti ya Lowassa
Yaani Lowasa angekuwa mcheza mpira hata kwenye reserve hayumoMkuu hata kama ningekuwa mimi nisingeendelea kuwapa mgawo, sasa ataendeleaje kuwalipa wakati kazi aliyokabidhi wameshindwa kuifanikisha??!! aaah hata 10 bora kashindwa kuingia
Ndo maana Watanzania applications zenu za kazi zikitua kwenye desks za Wasomi Mambo Leo lazima applications hizo wazipige chini na mwishowe mnaishia kulalamika!
DUH! Aisee we unashangaza! Yaani hoja ya msingi hapo umeona kuandika CV?Sisi Waafrika bhana! Tukishafika Ulaya tunasahau tulikotoka na kuanza kuponda na kukebehi Watu na maisha ambayo tulikuwa tunaishi hapo mwanzo!
Nimekutana na Wazungu, Wajapani na watu wa nchi nyingine tajiri ingawaje waliona mapungufu yangu kwenye utendaji lkn kamwe hawakunibeza na kunikebehi kwamba ndio maana hujui hiki au sijui wewe ni Mwafrika, bali walielewa mazingira niliyokuliwa na kwamba kuna tofauti na mazingira waliokulia wao hivyo wakanivumilia wakanifundisha kazi na sasa niko vizuri, lkn Mwafrika mwenzangu siku akifika tu Ulaya anaona wale wote walioko nyumbani ambako ndiko amekulia ni takataka na hawajui kitu bila kutambua kwamba kama yeye asingepata nafasi ya kufika huko Ulaya angekuwa hivyo hivyo!
Sasa kwa nini liwe jambo la ajabu kwa Mtz kutokujua kuandika CV? Ni wapi Mtz anafundishwa kuandika CV ktk maisha yake?
Na wewe kama unajua kuandika CV vizuri basi ni kwa nini usichukue hilo jukumu kama msaada wako kwa nchi yako na watu wako kumfundisha?
Ndivyo wenzetu Wazungu, Wajapani wanavyofanya hawachekani bali wanapogundua tatizo wanasaidiana na kuelekezana lkn siyo kukebehiana kama sisi!