Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Wala usishangae Fisadi lazima awe adui wa kila mzalendo wa nchi hii mkuu
 
Mkombozi atakayetunusuru na madhila ya maisha ni MUNGU. Tutadanganywa mpaka basi na wagombea wanaojifanya miungu watu
 
Wakuu
Mi si mpenzi wa siasa,
Lakini naomba niseme japo kidogo,lakini kiukweli lowassa anatishaa,Nimekuwa nafuatilia siasa hapa na pale lakini nimeona kila anayegombea adui yake namba moja ni lowassa!Najiuliza kwanni bila kupata jibu,imefika mahali hata vikao vya ccm vimekuwa vikiaahirishwa mara kwa mara kuepuka mafuriko ya huyu mh ikumbukwe kuwa si kawaida ya chama cha mapinduzi mpaka muda na mwezi kama huu hawajapata mgombea,lakini ukichunguza siyo kana kwamba wamekusudia lakini kiukweli nikwamba wanajaribu kukwepa jina lowassa.Lowassa ameonekana kuwa tishio kwa wagombea wengine,na kibaya zaidi kinachowauma ni pale wanapomtukana lowassa lakini lowassa amekuwa mstaarabu kwa kuchaguwa kuwa kimya huku yeye binafsi akijikita kutafuta ushawishi kwa wananchi,ni hivi tu karibuni kutafanyika vikao vya maamuzi ndani ya ccm lakini kuna kila dalili za kutofanyika kikao hicho vinavyotegemewa kuanza wiki ijayo.Ushauri wangu kwa ccm kwa muda mmeshalewa lowassa yuko mbali sna nawashauri tafuteni njia ya kidiplomasia mzungumze naye,mi siyo mwanasiasa lakini nimeliona hili je nyie mlioko huko juu??Yangu macho nione

Wewe ni hatari katika Taifa na mpumbavu utauziwa hata nyumba yako. Achana na lowasa.
 
unaenda mbali sana ww c unasubiri jina lake likatwe na cc,wenyewe wanajua kumchinja kobe inatakiwa timing .wao hawamtaki sisi tulio wengi tunamtaka....tupeni lowassa wetuuuuu.....
 
hauwezi kulala wakati shetani ameingilia familia yako ,ndo maana hata kanisani wakishajua kuwa kuna mawakala wa shetani lazima wachungaji wakeshe kwa maombi ili shetani asiangushe kanisa la mungu ndo wanachokifanya watu makini wanaolitakia mema taifa hili

Sasa wewe ukimtoa lowassa unadhani nani anastahili kijiti, kama sio yeye?????? Yani ni bora mgombea binafsi kuliko unayemhisi wewe anafaa
 
Yaani siamini macho yangu

Huyu madabida ameisha ua ndugu zetu kibao kwa kuwauzia vidonge feki huku akifurahia mihela wao wakifa. Leo anajua Lowasa akiwa Rais kesi yake itafutwa hivyo anamfananisha na mtume wetu kipindi hiki cha mfungo?

Kweli hela ina nguvu, yaani na sisi waislamu tunaamini kabisa kuwa Lowasa ndio Mtume wetu?

TAKBIIIIR!
 
CCM nawaambia tena kwa herufi kubwa Lowassa aliposimama siyo kwa ajili unafiki wenu ni kwa ajili ya Mungu!

Lazima tuyakubali matokea. Wanafiki na wasaliti wa Chama wenye hisa na CCJ walipokuwa wanatokwa na hofu walitafuta hifadhi ya kisiasa nje ya CCM kwa maslahi yao wenyewe wakagota kwamba.

Hawa pia walifikiria kwa kutumia jina la Lowassa kama mtaji wa kisiasa watafanikiwa lakini hsikuweza kuwa hivyo.

Haya yamedhiirika wakati wa kusaka wagombea. Watu wengi Sana wameshajua hila za CCM. Kikubwa zaidi tayari watu wanamamuzi sahihi iwapokosa litafanyika.

Pia sikio la kufanya halisikii dawa. Hiyo ndiyo CCM inayokufa taratibu! Tusubiri tuone pamoja na hii miswaada ya dharura ya kinyonyaji hakitapona.

Mgonjwa anapokaribia kufanya ubishi Wa kinywa dawa na kutii masharti ya daktari unaongezeka. Haya ndiyo yanayotokea Leo
 
Wadau, hongereni kwa mapumziko ya mwisho wa wiki baada pilika pilika za wiki nzima.

Wiki hii pamoja na wiki ijayo macho na Masikio ya Watanzania ni Makao Makuu ya Nchi yetu, Dodoma.Ni katika mji huu na ndani ya kipindi hicho, moja kati ya watangazania wapatao 38 waliorudisha fomu wakiomba kupata ridhaa ya Chama chao kupeperusha bendera katika nafasi ya urais hapo oktoba 2015 atakapopatikana.

Wakati hayo yakiendelea, nahabarika nikiwa mitaa ya mikocheni karibu kabisa na moja ya eneo ambalo mmoja wa watangaza nia ni maarufu sana na aliyejizolea wadhamini wengi kuliko wenzake, Edward Ngoyayi Lowassa kuwa kambi yake siyo shwari.

Itakumbukwa kwamba Kambi ya Lowassa inaundwa na makundi matatu ambayo ni Team Lowassa, Friends of Lowassa na 4u Movement, Team Lowassa likiundwa na watu wa aina zote yaani wazee, vijana na hata wanasiasa, Friends of Lowassa likiundwa na Marafiki zake wa siku nyingi.

Wafanyabiashara huku 4u Movement likiundwa na vijana pekee na hawa ndiyo waliotawala kwenye mitandao ya kijamii ukilinganisha na makundi mengine.
Mmoja wa vijana wanaounda kundi la 4U Movement amedokeza kuwa kuwa wamekuwa hawapati mgawo unaotolewa na Lowassa ( wao wanatumia jina Mzee ili kuonesha kwamba kundi lao ni la vijana) kama ambavyo kundi la Team Lowassa(Hawawalaumu sana Friends of Lowassa kwa sababu wao pia wanahusika kwa upatikanaji wa mlungula) limekuwa likipata.
Hali hii imezua tafrani hasa kwa Mzee siyo kwa sababu tu ya kazi kubwa wanayoifanya hawa vijana kwenye mitandao ya kijamii na kuzunguka nchi nzima kueneza injili ya Mzee kwa vijana wenzao bali pia Mzee anajua hiyo ndiyo rasilimali kubwa hapo Oktoba kwani wakiamua kubadilika (Mzee anasema these youths are flexible and mobile) hali inaweza kuwa mbaya hapo Oktoba.

4U Movement wanaona kama umri wao unawaponza na kupelekea kudharauliwa.
 
Huu ni uwongo uliopitiliza,jf tumevamiwa na wahuni,Lowassa anawanyima wengi usingizi kumbe,hata wake zenu sasa mtasema lowassa katembea nao.Kuna kiongoz mmoja alisema mmeshachelewa lowassa yuko mbali
 
Mkuu hata kama ningekuwa mimi nisingeendelea kuwapa mgawo, sasa ataendeleaje kuwalipa wakati kazi aliyokabidhi wameshindwa kuifanikisha??!! aaah hata 10 bora kashindwa kuingia
 
Huu ni uwongo uliopitiliza,jf tumevamiwa na wahuni,Lowassa anawanyima wengi usingizi kumbe,hata wake zenu sasa mtasema lowassa katembea nao.Kuna kiongoz mmoja alisema mmeshachelewa lowassa yuko mbali
Mkuu kanusha kwa kuweka ukweli kwamba hilo fungu limepotelea wapi?au weka mchanganuo wa mgawo.
 
Simpendi LOWASSA awe Raisi wa nchi hii ila kwa hilo uliloandika ni kama unafanya dua ili hilo litokee na wakati halijatokea na huna hakika kama limetokea. Sasa kama Lowassa hatakuwa Raisi nani mwingine anafaa kuwa raisi ndani ya ccm?
 
Mm na jamaa zangu 3 tuko 4u movement, pesa tunakula vzr tu, lkn Kura zetu ni kwa Dk SLAA,
NA MAPAMBANO YA CHINI KWA CHINI YANAENDELEA,
TANZANIA KWANZA MAFISADI MKAFIE MBALI
 
Back
Top Bottom