Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Ha ha ha makonda alitaka kuzuia mafuriko kwa mikono akazidiwa kisha akasepa. Kamuacha mamvi kafanya mambo..
 
Umaarufu wa vyama vya upinzani hasa ukawa unaenda sambamba na umaarufu wa Lowassa licha ya kuandamwa na kashifa ya rushwa!

Kwa maono yangu Tanzania imekerwa na awamu ya nne ya uongozi baada ya kutoa ahadi ya maisha bora na kupotea nayo Ikulu. Sasa Watanzania hawana matumaini wanaona Kama Lowassa alionewa maana yeye alifanya mambo lukuki kwa muda mfupi sana. Wengine wamekatatamaa kabisa wanaona bora na wao waingie kwenye siasa ili wapatepo ulaji. Wengine wachoka na utawala wa CCM wanaona bora ukawa!

Lakini hii yote ni awamu ya nne kusindwa kutekeleza jukumu la maanaendeleo na kuamua kuendesha nchi kwenye vyombo vya habari na si kutekeleza maisha bora kwa kila Mtanzania Kama walivyoahidi mwazoni 2005. Tukio likiasemwa sana kwenye vyombo vya habari basi kesho yake utamuona mtu kutoka serikalini! Iwe ni msiba mafuriko ujambazi nakadharika. Nataka niwambie viongozi waliyopo madarakani kuwa kuna mengi sana hambayo hayaandikwi. Mfano unajua mwalimu akicheleweshewa mshahara ama madai yake unajua matukio yanafanyika ndani ya hiyo familia?. Police anaemugopa Mungu alichukua rushwa unajua kinachofuata?

Watanzania tumechoka kabisa ndio maana kama ulikuwa ndani ya serikalini alafu unaomba wadhamini ukifika tunakuomba rushwa na Lowassa anadhaminiwa buree tena kila mtu anasikia raha kumdhamini timewachoka nendeni mkapumzike

Natabiri Lowassa asipoteuliwa nchi unaenda UKAWA maana Watanzania wanataka maendeleo na si selfie tu!

Watanzania si wapumbavu kabisa ingawa wengi wao wanaongea hovyo hovyo lakini kuna Watanzania hawana nafasi kwenye media na ndio wengi na ndio wanaoijua nchi ndani na nje na ndio wenye maamuzi watawaliwe vipi!
 
Nimemfahamu Lowasa kama kiongozi mwenye msimamo na Kiongozi anayesimamia mambo bila kuyumbishwa.

Kinachonipa wasiwasi kwake ni Watu waliomzunguka ambao ndio wanaoisapoti safari yake ya matumaini.

Watu hao ni Rostam Aziz, Ibrahim Msabaha, Nazir Karamagi na wengine wengi ambao wamewahi kutuhumiwa kwa ufisadi.

Mashaka yangu kwa Watu hawa. Ni je baada ya ushindi wa El kama Rais hawa watu si watagawana Nchi vipande vipande kwa manufaa yao na ili kurudisha gharama zao walizotumia kwenye safari ya Matumaini?.

Watanzania tutafakarini sana kwa maslahi ya wote na sio kwa ajili ya wachache.
 
Mmmh ukisikia kuruka mavi na kukanyaga mkojo ndo huku yangu macho..
 
Magari ya matangazo hapa Morogoro yanapita mitaani kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Lowasa atakapokuja kutafuta wadhamini, hivi kwenye kutafuta wadhamini wanachi wanahamasishwa kujitokeza kufanya nini?
 
Magari ya matangazo hapa Morogoro yanapita mitaani kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Lowasa atakapokuja kutafuta wadhamini, hivi kwenye kutafuta wadhamini wanachi wanahamasishwa kujitokeza kufanya nini?

Mwache aharibu tu !....anategemea aki cross over atakubalika
 
Nauliza swali hii maana ninapenda sana midahalo na uwa nawapima vizuri uwezo na weredi wa viongozi, lakini zaidi nilifurahishwa sana na midahalo niliyoona marekani kipindi cha obama na israel uchaguzi uliopita maana hoja za maana na uwezo wa kujenga hoja kwa wale wagombe kiliwasaidia sana wananchi kufanya maamuzi ya kupata rais.

Pia Naamini ukawa watampitisha slaa na nimefatilia speech za lowasa alipokuwa anatafuta wazamini,niliyoyaona yananifanya kuuliza kama wakimpitisha lowasa je midahalo itakuwepo na kama itakuwepo nani atawavutia wengi?
 
Edward Ngoyai Lowassa namfananisha na John F Kennedy maana hakuna Rais wa Marekani aliekuwa anapendwa na Wamarekani kama John Kennedy, hata Obama haoni ndani. Lowassa anapendwa na Watanzania mwenyewe anapenda kusema mahaba
 
Edward Ngoyai Lowassa namfananisha na John F Kennedy maana hakuna Rais wa Marekani aliekuwa anapendwa na Wamarekani kama John Kennedy, hata Obama haoni ndani. Lowassa anapendwa na Watanzania mwenyewe anapenda kusema mahaba

Acha fujo za kudanganya watanzania, mwache john apumzike kwa amani. Ulimwengu wa kwanza huwezi kuhonga alafu uwe rais. Au uliwai kuwa na scandal halafu uombe kura,hayo hayapo. Pia useme 'mimi nampenda' sio 'sisi ' watanzania wote hawatumii tumbo kama wewe.
 
Rais akitoka tena ccm basi Tanzania si sehemu salama ya kuishi,mbali ya tuhuma chache sana kwa mzee EL ila hilo genge la ccm ndio linanipa mashaka makubwa
 
Mwenye ushahidi wa kuwa Lowassa ni Fisadi auweke hapa, tumalize mjadala huu, maana sasa kila siku Fisadi, ushahidi uwekwe hapa mtushawishi na sisi.
 
Back
Top Bottom