Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

acha apitishwe tu hakuna namna



EL yuko well ahead ya huu mchezo... the guy is political tactician and technician... he knows exactly anafanya nn, 100%... habahatishi aiseee... yuko makini sana sana.. i can't imagine...!!! Huyu jamaa kichwa kwa kweli, huu mchezo anaujua haswa...!!!
 
Heshima sana wanajamvi.

Katika harakati za kusaka wadhamini team Lowassa Ndossy iliandaa maandamano ya Piki piki kutoka uwanja wa ndege wa KIA hadi Arusha mjini.Duru za kiusalama zililazimika kuzuia piki piki zote maeneo ya KIA hadi King'ori ili kuepusha msongamano wa magari usiokuwa wa lazima.

Taarifa zaidi zinadai kila Boda boda ililipwa Tsh 60,000/=@ na mafuta lita 10 kwaajili ya kufanikisha zoezi hilo.

Waendesha boda boda tayari walishalipwa fedha zao ili kuepusha madai ambayo wakati mwingine yanasababisha kuichafua kambi ya Edward Lowassa Ndossy.

Tayari kambi hiyo wanajindaa kudai kiasi cha fedha kwakuwa kazi iliyokusudiwa haikufanyika hata kwa 5%.

Zoezi la utoaji taarifa lilifanyika katika uwanja wa Msikiti Mkuu wa Bondeni ambao pia ulitumika kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba za msikiti.

Waislam wengi walisikika wakilalamika kwasababu shughuli hiyo ilisababisha usumbufu wakati wa swala ya adhuhuri kwakuwa wahudhuriaji walikuwa wakipiga makelele na waandaaji wa shughuli walitumia vyombo vyenye sauti kubwa.

Nawasilisha.

Wewe ni mzushi na muongo mkubwa. Binafsi nilikuwa kwenye viwanja huko ambao watu walijaakupitiliza. Watu walikwepo wengi wengine wakipiga kelele za furaha na shangwe. Walitamani sSana wazungumzaji wengine wasipewe nafasi ili Lowassa apate muda wakutosha.

Lowassa aliwashukuru Sana huku watu wakasikika wakipaza sauti zao za furaha na shangwe wakisema RaisrRais.....pia Lowassa alimpa pole ndugu Manga aliyevamiwa na wahunu.
 
Kwa wadhamini hao mbona Lema angepigwa chini asubuhi mapema.



Yaani wee Acha tu, kasomba Arusha yotee... Arusha town itahamia CCM bila shaka kabisa, kama mwendo ni huu, CDM watakiona cha mtema kuni..!!!

Lowassa ni Mwamba, na juu ya Mwamba huo Mungu kaamua kujenga nyumba yake...Hakika EL ni chaguo la watanzania wengi, chaguo la Mungu wa mbinguni...!!
 
Ni wazi kabisa yanayofanywa na Lowassa hayawezi kumsaidi na bila shaka hata mwenyewi hili analijua.Kinachofanywa na Lowassa na watu wake sasa kinastahili kuitwa fujo za kisiasa na si vinginevyo.

Huyu bwana Kwa sasa ameshaka tamaa ila alichoamua ni kuandika tu historia ya kuwa mtangaza nia aliewahi kudhaminiwa na idadi kubwa ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuliko mtu mwingine yeyote tangu Uhuru.

Pia,hata kama kuna madai kuwa wanaomdhamini wananunuliwa,kumbukumbu itakayoingia katika historia ni hiyo bila kujali wananunuliwa au laa na pia bila kujali chama hakihitaji wadhamini zaidi ya 450.

Jamaa amegundua kuwa, "something is better than nothing and also "the end justifies the means".

Mhurumieni tu huyu mtu.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mkuu nyie kama wanaccm mnamtaka nani awe rais??


Huyo emma ni CDM... anahangaika sana kumchafua EL, CDM kakosa wanaume, anakuja tafuta wanaume CCM, bahati mbaya CCM hatuli makombo...!!
 
Yaani wee Acha tu, kasomba Arusha yotee... Arusha town itahamia CCM bila shaka kabisa, kama mwendo ni huu, CDM watakiona cha mtema kuni..!!!

Lowassa ni Mwamba, na juu ya Mwamba huo Mungu kaamua kujenga nyumba yake...Hakika EL ni chaguo la watanzania wengi, chaguo la Mungu wa mbinguni...!!

Pesa ina nguvu za ajabu
 
Wana CCM wengi wamerudi kwa Lowassa, baada ya kuwa na matumaini nae... so CC Arusha ingawa ni ngome ya CDM, ila wameapa, Urais ni EL tu... hawasikii, hawaoni, hawaelewi..hawaangalii chama, wanaangalia mtu...!!!

Arusha, siasa zimewaaingia haswa... wenyewe waangalia mtu, sio chama..!!!
Alafu wewe!! hivi kwa nini ni MJINGA sana??
Umelaaniwa kiasi hicho??? pyewwwwww!!!
 
Pesa ina nguvu za ajabu



Sio pesa bana....unaweza kuwa na pesa, watu wakala na wasikupe udhamini au kura...!!!

So lazima upendwe na wananchi kama EL, then fedha ktk uchaguzi ni lazima... so bila fedha huwezi gombea...!!! ndio ukweli...!!! Hakuna asiyetumia fedha ktk kugombea Ubunge au Urais...hakuna, sema viwango vinatofautiana, VYAMA VYOTE HUTUMIA MABILIONI KTK UCHAGUZI... eg CCM, CHADEMA..

Dr. Slaa juzi kaenda wiki nzima Ulaya kuomba fedha za uchaguzi kwa wafadhili, na kaahidiwa mabilioni...!! So fedha ndio injini ya Uchaguzi...
 
Ndio maana yake wenyeviti wamepewa pesa wanaangaika nyumba kwa nyumba ili wapate wazamini bahati mbaya wanaenda kwa watu wasio jua kusoma kazi kuweka gumba tu
 
Back
Top Bottom