EDWARD LOWASSA:Pamoja na Kashfa za Ufisadi bado anaota Urais.

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
549
Edward Lowassa huenda ndio mwanasiasa anayeonekana mchafu zaidi hapa Tanzania kutokana na kashfa za Ufisadi zilizomfanya kujiuzuru bafasi ya uwaziri mkuu 2008.

Mbali na hapo inaonekana ndio mtu mwenye nia, mipango na mikakati mingi zaidi kuhakikisha anakuwa rais wa Tanzania 2015 kwa gharama yoyote!!

Ukiondoa wafuasi wake, watu wengi wakisikia jina la Lowassa fikra na mawazo yao yote huhamia kwenye kashfa za Ufisadi alizonazo kuliko kitu kingine chochote kinachomuhusu Lowassa.

Lowassa ameonekana akifanya juhudi kadhaa kuhakikisha nyota yake ya kutaka urais inang'aa kupitia mikakati kadhaa;

1/Kuhakikisha wapambe wake wanapata nafasi muhimu za kisiasa ndani ya serikali, bungeni na ndani CCM.(Kwa sehemu kubwa sana amefanikiwa hususani ndani ya CCM)

2/Kufifisha nguvu ya kambi zingine pinzani za urais ndani ya CCM.

3/Kujitakasa kisiasa kwa kutumia taasisi za kidini hususani makanisa(Kila mara ameonekana makanisani kama mgeni wa heshima na kutakaswa kwa maneno ya mibaraka kama ''Lowassa ni mnyonge hodari aliyeonewa''!!)

4/Kumwaga pesa nyingi za kumsafisha kwenye taasisi, vyombo vya habari, jamii na baadhi ya watu hususani viongozi wa dini na wanasiasa.

*Ni vipi Lowassa anaweza kuvuka kisiasa katika hali hii ya kashfa za kifisadi zinazomwandama ambazo hazifutiki?
 
Kama lowassa ni jembe mbona kugombea nec alienda wilayani badala ya taifa kuonyesha ujembe wake?
 
Kiburi kinamfanya asijitambue. Anafikiri watu hawajui kuwa yeye ni fisadi mkubwa.
 
Lowasa ni jembe...ma presdent 2015 is lowasa japo me si mwanachama wa ccm namchagua kam yeye...huyu lumumba ni wale vijana wa elfu 7000per diem wanaolipwa kuja kutoa mapofu tunajua kundi lako na unamhofia lowasa sana magufuli kashawakana bado mitume wenzenu wa ufsad
 
wew Lumumba unajifanya Chadema ila wew ni kasuku wa Membe, unaongoza kuleta thread za kumponda Lowassa humu, yeye na Sitta aliyekuwa mwenyekit wa TIC nani mchafu? mikataba yote mibovu ya ubinafishaji ilipitia kwake.

Alafu hiyo kauli anaongoza kwa "Makashfa" zingine ni zipi?? mana si tunajua Richmond ambayo kila mwenye akili anajua aliyekula nani, ila kwa sababu ya UNAFIKI KAMA WAKO TUMEACHA KUFIKIRI NA KUPIGA PROPAGANDA, sema wazi anayeongoza kwa kashfa Mzee wa Kaya na Mwanae, wew mnafki tu na uwezo mdogo wa kufikiri, mwepesi kutumia vidole kuandika huu ujinga bila kushirikisha akili, i mean ur hands are fast in motion while ur brain is not in gear,, Ndo watuleta pumba hizi????
 
Anatembea na magunia ya pesa kichwani anasambaza makanisani na misikitini nchi nzima.hizi pesa anazipata wapi?watanzania muwe waangalifu sana.akiwa rais hizi pesa zitatutokea puani.alipokuwa waziri mkuu alitoka na single ya richmond ambayo inatutesa mpaka leo akiwa rais atatoka na nini?
 
Kwangu mimi ni bora Fisadi aliyeiba na kuwekeza nchini mwake na Watanzania wanaona kuliko Mafisadi waliotuibia na hela zao hatujui wameficha wapi!
 
Huwa ninajiuliza 'vision' ya Lowasa kuutaka uraisi ni ipi lakini? au anataka tu cheo?
 
Kama anaweza kugawa pesa kwa kila mwenye shida, kuna haja gani ya wewe kuutaka urais, si awe anaamka asubuhi anakaa kama posta watu wana mueleza shida yeye anagawa pesa, mpaka watu waishiwe shida...Hapa jamaa anawekeza, anajua anachokiwinda, na akikipata mtamsoma jina
 
Mi nashindwa kuwaelewa baadhi ya watu kila mtanzania ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kwa hyo watanzania wenyewe ndo wataamua kama unaona lowassa hafai mwache agombee watu hawatompa kama watampa maana yake hafai!!
 
Lakini pia usisahau kuwa mtu yoyote anayetaka urais lazima tumpime na kumjadili kuhusu uwezo wake wa kutuongoza na sio nyota ya umaarufu anayosafiria.
 
wew Lumumba unajifanya Chadema ila wew ni kasuku wa Membe, unaongoza kuleta thread za kumponda Lowassa humu, yeye na Sitta aliyekuwa mwenyekit wa TIC nani mchafu? mikataba yote mibovu ya ubinafishaji ilipitia kwake.

Alafu hiyo kauli anaongoza kwa "Makashfa" zingine ni zipi?? mana si tunajua Richmond ambayo kila mwenye akili anajua aliyekula nani, ila kwa sababu ya UNAFIKI KAMA WAKO TUMEACHA KUFIKIRI NA KUPIGA PROPAGANDA, sema wazi anayeongoza kwa kashfa Mzee wa Kaya na Mwanae, wew mnafki tu na uwezo mdogo wa kufikiri, mwepesi kutumia vidole kuandika huu ujinga bila kushirikisha akili, i mean ur hands are fast in motion while ur brain is not in gear,, Ndo watuleta pumba hizi????
Msiumbuane nyie wote ni Lumumba project tatizo hamuaminiani, nawasubiri wa nchimbi aje!
 
Msiumbuane nyie wote ni Lumumba project tatizo hamuaminiani, nawasubiri wa nchimbi aje!
Hah hah hah!!!
JF ina vituko sana. Leo mimi naitwa wa Lumumba posho buku saba!!!

Na kweli vijana wa Nchimbi wafakuja humu soon kwa fujo.
Kesho utasikia wa Wassira wakija hapa tena kwa hoja nzito nzito!!!
 
Hizo pesa ni sehem ya marejesho ya matumizi yake(jamaa tangu nyerere yupo hai anamfaham mpunga mchafu) na kwenye vyama kuna ilan za chama kama ilan inamuongoza mwachen aingie kweny jumba la kijeruman ikulu,mzee ruksa alisema kwenye masuala ya mpira ni kichwa cha wendaazim uwenda azim umeingia mpaka kwny siasa.
 
Jamani mzee wa MVI alishakana kupitia ndani ya kikao cha NEC-CCM kilichoongozwa na mwenyekiti wke taifa kwamba: ' Ninashangaa mimi kuitwa fisadi, nini msichokijua. Kama ni Richmond niliamua kuwafukuzilia mbali na wewe mwenyekiti ukashauri tuwaache kwanza, sasa iweje mniite mimi ni fisadi ilhali kila kitu mnakijua?' Vile vile kumbuka, wakati wa kujiuzulu kwa alitamka haya; "Ili kuweka historia vizuri, Watu wamekwenda mpaka Marekani kutafuta ushahidi, hawakuniuliza chochote wala kunishirikisha, hawakuniita nikakataa, Kama ni uwaziri mkuu ndiyo shida basi naachia ngazi. Sasa tunamhukumu EL kwa sababu zipi? Acheni laigwanani apumzike jamani.
 
kwa mtazamo wangu mimi katika viongozi wote wa ccm Mh lowassa anafa kugombe urais kuliko kiongozi mwingine yeyote yule kwasababu hanamamuzi magumu kuliko magamba yoyote yule kwa sasa
 
Lowasa ni jembe...ma presdent 2015 is lowasa japo me si mwanachama wa ccm namchagua kam yeye...huyu lumumba ni wale vijana wa elfu 7000per diem wanaolipwa kuja kutoa mapofu tunajua kundi lako na unamhofia lowasa sana magufuli kashawakana bado mitume wenzenu wa ufsad
hii topic inawafaa na akina ze marcopolo na wenzao wa lumumba.
waendelee kuchafulianachafuliana,
Fisadi lowasa juu lumumba!!
 
Back
Top Bottom