Gazeti la Leo Jumatatu Julai 17, 2017 la Mwananchi ukurasa wa mbele limepambwa na kichwa cha habari kikubwa kinachosomeka LOWASSA: NITAGOMBEA URAIS TENA MWAKA 2020. Lowassa ni mjumbe wa kamati kuu Chadema.
Binafsi huwa siwaelewi kabisa chama kinachojipambanua kuwa Chama Cha demokrasia lakini ukitazama matendo yake utagundua hiyo demokrasia wanayoisema ipo kwenye makaratasi na si kivitendo.
Mathalani kuna nafasi zina wenyewe ndani ya Chadema na hazigusiki endapo mtu akihoji huitwa msaliti, hufukuzwa uanachama ama kupatwa na mabalaa zaidi makubwa.
Hata kwenye nafasi za teuzi nazo pia zina lalamikiwa demokrasia kupindishwa kwa watu kupatikana kutoka mifukoni mwa wakubwa.
Leo hii mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema atagombea tena urais 2020. Ina maana vikao vimesha kaa na kumpitisha tena Mhe. Lowassa kuwa mgombea urais 2020? Demokrasia wameitupia wapi mpaka kuruhusu udikteta huu?
Kauli ya Lowassa inadhihirisha kutangaza nia na kuanza maandalizi ya kampeni za Urais. Huu uhaini wa kuanza kutangaza nia ya kugombea urais kabla ya wakati wakati kuna Rais halali Dk. Magufuli, nani ameubariki? Ina maana hawajui kuanza kutangaza nia ya kugombea kabla ya wakati ni kosa kisheria?
Chadema mpaka sasa hawajakanusha uhaini huo. Chadema wajitathmini kwa matendo yao, kauli zao, nia zao huku wakiheshimu sheria, taratibu na kanuni za nchi.
Shilatu E.J
Sent from my TECNO-L8Plus using
JamiiForums mobile app