Najua wanajamvi wengine hawatanielewa,ila nachokisema ni kwamba,lowassa ajiandae kisaikolojia maana mpaka sasa hivi ccm wamekaa kimya wakipanga first eleven,CCM ni bingwa mzoefu,CCM ni watu wa offside,CCM ni watu wa fitina,najaribu kutafakari kwa kina kwamba,Lowassa akitangazwa ameshindwa,je atakubali kushindwa au ndio vurugu zitaanzia hapo?
Je, vurugu hizo zitakuwa na tija kwetu?
Ndio maana nasema Lowassa jiandae kisaikolojia kwani utafungwa kwa gori la offside kwasababu marefarii wasaidizi ni wa kwao na refa wa kati ni wa kwao.siongei kiushabiki maana ushindi hauanzii ndani bali na nje!
Kwa upande wa pili CCM na nyie mjiandae kisaikolojia maana ukawa wanacheza sana na akili za watu na kutafuta majority hivyo endapo wananchi watajitokeza kwa wingi kupiga kura kama walivyojitokeza kujiandikisha basi kuna uwezekano mkubwa UKAWA kushinda.
Jambo jingine nawaasa wanasiasa kwamba tuache siasa za kupakana matope kwani wananchi bado tunahoji?
Tumeupenda upinzani kwa kuikosoa serkali na kuwaumbua wala rushwa wakubwa nchini akiwemo mh. Lowassa.
kwa pamoja bunge liliadhimia kumuondoa waziri mkuu kwa kuitumia vibaya ofisi....je nyie wapinzani mtatueleza nini watanzania ili tuwaelewe?
Leo Lowassa msafi,kesho Chenge msafi,kesho kutwa akina Muhongo na akina Kalamagi watakuwa wasafi endapo watapata fursa kuhamia CHADEMA.
Je, mnapozunguka mtaani kutueleza kwamba Magufuli ameuza nyumba mna ushahidi? Na kama mna ushahidi si mpeleke mahakamani?
Acheni siasa taka wananchi tunaelewa!