Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

hivi wabongo bado hamuamini tu kwamba nguvu za lowassa zimekwisha sasa kama za samson wa delila..bado mnadhani ni yule lowassa wa zamani.Sasa hivi lowassa ni sawasawa na nyoka wa kibisa,anatisha tu kwa kuwa ni nyoka jina lakini hana madhara tena
Kura za maoni AruMeru Mashariki zinarudiwa kwa sababu gani? Wanahangaika kumuengua mgombea wa Lowasa, Sioi. Asikudanganye mtu, nguvu ya Lowasa bado ipo sana tu katika kila kikao, taasisi zinazoongozwa na CCM ukiwemo Urais wa nchi hii.
 
Askofu anayezungumziwa kukamatwa si wa kanisani ni askofu mfanya biashara wa mawe kwa hiyo askofu ni jina tu,hata Mathias ni mfanyabiashara wa mawe pia.

You are right. Askofu ni yule mfanyabiashara wa mawe wa Mbuguni sijui Mererani. Ila kuna kitu nataka kuwatahadharisha. Hapa mnashindwa kuelewa huyu EL si mjinga wala negligent kiasi hichi tunachofikiria. Tunakaa kushangilia kusema ameumbuka lakini hamjui huyu jamaa ana mtandao wake vile vile ambao wako kwenye payroll yake meaning chochote kinachotokea anakuwa informed.

Watumishi wengi sio waadilifu halafu wana tamaa sana na walafi. EL hawezi kwa kutumia simu yake kutuma sms inayohusu kutoa hongo au rushwa kwa watu ukizingatia tayari ameshaundiwa zengwe la huyu mkwe wake kuhusu uchaguzi wa Arumeru. Jamaa ni smart na anajua mbinu nyingi hawezi kutumia mbinu rahisi na ya kitoto kiasi hiki. Labda useme huyu aliyekamatwa amemhusisha EL. Lazima ujue huyu EL anacheza mchezo wa kuviziana na maadaui zake.

Yetu macho. Ila kwa kifupi wameamua kumuengua Sioi kwa namna yoyote ile na ndio haya tunayoyaona. Sioi ndio kaenda na maji akajipange upya.
 
Huwezi kutenganisha RUSHWA NA CCM. Kama kweli wamekamatwa hiyo ni kiini macho tu. kwa hali ilivyo sasa ndani ya chama hicho hitokuja kutokea uchaguzi/uteuzi wowote kufanyika bila ya RUSHWA kutembea.
 
Wangekuwa wanafanya haya kwa chaguzi zote ingekuwa shega!
 
Magamba and their goose chase!!!!!!!! Aibu tupu! Halafu bado kuna watu wanawashabikia!
 
Habari za kufikirika na movie za kihindi. Mtu kama Lowassa hawezi kutumia mbinu hizo za kutuma sms. Mleta uzi ni mzushi tu mwenye chuki binafsi ndio mana hata chanzo hakiweki.
 
Kura za maoni AruMeru Mashariki zinarudiwa kwa sababu gani? Wanahangaika kumuengua mgombea wa Lowasa, Sioi. Asikudanganye mtu, nguvu ya Lowasa bado ipo sana tu katika kila kikao, taasisi zinazoongozwa na CCM ukiwemo Urais wa nchi hii.
Yani we mwenyewe unajichanganya mtu mwenye nguvu mgombea wake anaenguliwaje tena..!angekua lowassa yule tunaemjua huyo mgombea wake kuna mtu angethubutu hata kufikiria kumjadili tu?!we mnajua lowassa au unatania kamuulize mzee philip mangula akueleze alichomfanya ili mgombea "wake" kwenye uenyekiti wa ccm mkoa wa iringa JAH PIPO apitishwe,mangula na jah pipo ni kifo na usingizi,lakini kwa kuwa jah pipo alikua mtu wa lowassa yule wa zamani "alimshinda" mangula
 
Mimi naona hii ni thread ya promo tu kwa maggamba... ili badae ionekani aliyebaki ni msafi!!!

ukiona wezi wanaliana timing, funga milango, weka makufuli kaa macho na panga, wakipatana utakoma!!!
Right on man!!!

Wezi wanaliana timing!!!!
 
Tunaomba kama ni kweli mambo hayo yasiishie hewani yaende mahakamani ili ukweli ujulikane na EL apate aibu na aukose urais kirahisi maana atajulikana kuwa ni mtu wa kuhonga honga 2.
 

hata hapa jf kikiongelewa mpaka ndani ya cc acha sekretariet tunakipata mapema sana mzee ina maana na sisi tuna nguvu ndani ya ccm?kumbuka huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia hakuna siri kama north korea hapa,watu wanaingia kwenye hivyo vikao na ccm kwa taarifa yako na watu media kwa mfano huwa wanasikilizishwa kikao chote live kupitia simu za mikononi hizi mabzo wajumbe wa vikao wanapiga kwa mtu wanaetaka kumsikilizisha kikao then wanaiacha on mwanzo mwisho hiyo ni kawaida sana,lakini tunachozungumza ni kwamba lowasa au rostam zamani walikua na uwezo wa kupata taarifa mapema lakini walikua na uwezo wa kudhiti kila ambacho hawakitaki kwenye taarifa hizo,uwezo huo wano tena leo???Haya mabadiliko ya katiba ya ccm mbona taarifa zake walizipata mapema na hawakuyapenda haya mabadiliko kwa kuwa yanawaumiza zaidi wao lakini mbona nec ambako huwa mnadai lowassa ana nguvu yamepita licha ya kingunge na peter serukamba kupigana kiume kwa ajili ya mwanaume wenu wa shoka lakini haikufaa kitu?badala yake alilolitaka nape na wenzake kwenye sekretariet ndio limekua?

Na kuhusu mwigulu naona tu humfahamu ndio mana.
 
Sioi hajaenguliwa na hataenguliwa. CCM wanajua gharama za kumuengua mgombea wa MunguMtu wao Lowasa! Unalinganisha zama zile na za sasa? Mazingira ya sasa ni tofauti. Yanataka mbinu na "approach" tofauti. Wakati ule wa Mangula na JAH PEOPLE Lowasa alikuwemo kwenye vikao hivi vya juu kabisa. Sasa hivi anahudhuria kwa "remote".
 
Tatizo lipo kwa hao wapiga kura wanaokubali kununuliwa!
 
kwa hiyo kwa mtazamo wako wewe ukihudhuria kwa remote ndio unakua na nguvu nyingi zaidi kuliko ukiwa mmoja wa wajumbe wanaoshiriki kufanya maamuzi sio?hapo ndio unapozidi auchanganya mambo mzee,leo naona ungepumzika tu hauko sawa kabisa aise sijui ulilala wapi usiku wa kuamkia leo
 
Nashukuru kwa kuifafanua vizuri hoja yangu mwalimu KK. Sekretariet ina watu wachache zaidi kuliko CC. Nadhani kwa muundo wa sasa hawafiki 10. Iweje mazungumzo yavuje kirahisi hivo na wasimjue msaliti wao! KK, kwa nini kura za maoni CCM zinarudiwa? Ni kweli Mwigulu simfahamu. Ni mtu mpya sana ndani ya CCM na sio kada.
 

Huyu mzee wetu mwenye kichwa cheupe kama vile amejipaka chokaa anatia aibu kweli. Kila mwaka yeye kujipaka vinyesi vya rushwa tu. Ina maana mambo yake yeye hayaendi kabisa bila kutoa rushwa. Kweli Mungu wake amsamehe bure, maana anateseka sana mpaka anatia huruma sana!!!
 
1. Ukweli kuhusu hii habari unanipa shaka. Kifupi ni kuwa siiamini hii habari.
2. Hata kama ni ya kweli, bado ninaamini hakuna mwenye ubavu wa kumgusa Lowassa achilia mbali kumshtaki
3. Lowassa nae anataka kupandikiza chuki za UDINI, tutampiga vita hadi dakika ya mwisho, HATUFAI hata kuwa katibu kata. Akagombee urais VATCAN au IRELAND.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…