Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Weka hicho kifungu cha Katiba kinachomnyima Raisi huwo uwezo, ili tuone ni kama Raisi kavunja Katiba au la, uweke kweli hicho kifungu kinyume na hapo utakuwa ni kilaza tu kama vile fisadi Lowasa, hivyo nasubiri uweke kifungu kilichovunjwa !
Mimi pia niliamini Lowassa ni fisadi. Ila leo nimejua kuwa Lowassa sio fisadi ni propaganda tu. Fisadi ni hawa, Masamaki, Mramba, Ridhiwani, kina said lugumi, Dau, Yona, Kitilya na Barbarosa.
 
Lowassa anajaribu kuwarudisha CHADEMA kundini... Anaongea pumba tupu... Yeye kama ataki watu wa Mwanza wajengewe barabara aseme tunajua ana chuki na wasukuma sababu walimwonyesha misimamo yao,,, alitaka hizo hela zikanunulie kofia na kukodisha ngoma hiyo ndio vision au kwake kupunguza msongamano kwenye barabara kwa kuzipanua sio vision?

Hiyo pesa zilishaidhinishwa na bunge alichofanya Magufuli ni kubadili tu matumizi tena kwa mema sio kwa ubaya vision imekosekana wapi hapo.. Fisadi mwizi mkubwa ebu atupishe tujenge nchi yeye alijua kuiba tu.
Unaweza soma ila ukabaki mjinga tu.
Mkurugenzi anapopewa fedha za miradi akitaka kubadili matumizi huomba kibali TAMISEMI na HAZINA,ndipo azitumie

Pesa zinapotengwa kwa ajili ya jambo Fulani kisha ukabadili matumizi ndio chanzo cha hati chafu.

Rais katika Katiba na sheria za Binge ,hakuna ibara au kifungu chochote cha kisheria kinachomruhusu kubadili matumizi,hulazimika aende kwenye muhimili mwingine akaombe kibali.

Suala LA Utawala bora ndio hili ambalo wazungu wamekuwa wakituwekea masharti ya mikopo,lakini cha ajabu nashindwa kukuelewa kinachomuogopesha Rais kutumia waziri aende kuomba kubadili matumizi ni nini?
 
Ujue Lowasa mimi huwa namuona kama hajitambui vile sijui nani kamroga anaongea pumba tupu yani hajui hata pesa ipi inatakiwa kuidhinishwa na bunge na pesa gani ipo kwenye mamlaka ya Rais,mtu mzima hovyo kabisa.
Una akili wewe

Aliyekaa bungeni tangu 1985, aliyekuja kuwa mjumbe Wa Baraza LA Mawaziri kisha waziri mkuu
Unasema hajui anajisemea tu???

Hivi simiyu katika nchivn hii,we we na Lowassa nani ni Pumba?
 
Jinga kweli wew. Mlimpaje uwaziri mkuu, uwaziri wa maji, uwaziri wa ardhi?
Alivyogundulika mwizi...wabunge wa CCM walilazimika kumtosa.......akaanza kulialia....baaadae kakatwa ndio akawanunua ninyi kwa amri ya mbowe.
 
Mfikisheni mahakamani kama kina Mramba na Yona tujue kweli ni mwizi. Mnapata wapi authority ya kuthibitisha kuwa ni mwizi? Wezi na wala rushwa wanafikishwa mahakamani kama kina Lugola wanaojidai kupiga kelele sana kumbe wala rushwa
 
Natamani na mimi kumjibu lakini nitaambiwa "mwanakijiji uchaguzi umeisha"
Utaandika chuki bure badala ya hoja maana ulikataa kuzungusha mikono juu kuunga mabadiliko feki. Kwa Magufuli huwezi toka tena maana ulishamuunga mkono. Kwa hiyo maamuzi yoyote hata yakiwa ya hovyo hutasema. Mzee naongopa?
 
- Amlalamikia Rais Magufuli kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo chenye mamlaka kugawa fedha kipo ambacho ni bunge.(Pesa za uhuru na Pesa za Muungano)

- Asikitishwa na uachishwaji wa kazi kwa wafanyakazi, asema hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo ndio usababisha utendaji hafifu.

- Asononeshwa na hali ngumu ya maisha mtaani.

- Asikitishwa na ushukaji wa huduma ya Bandari kushuka kwa asilimia 50 na kusababisha vijana wengi kusota mtaani.

- Kitendo cha wahisani kujitoa kuisaidia nchi asema n i pigo kubwa kwetu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.

- Asema si kweli kwamba uongozi wa Rais mstaafu Kikwete kila mtu alikuwa mla rushwa, ni kweli mfumo ule ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

==================

Dar es Salaam: Siku 155 baada ya Dk John Magufuli kuapishwa kuwa Rais, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi huo, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomfanya autilie shaka mustakabali wa Taifa chini ya uongozi wa Rais huyo wa Awamu ya Tano.

Akizungumza na wanazuoni wa ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala nyumbani kwake Masaki Dar es Salaam, Lowassa alisema: “Hali ya siasa nchini ni ya hamasa lakini isiyo na msingi endelevu.”

Lowassa, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo baada ya kupata kura milioni 6.07 sawa na asilimia 39.97 aliyataja mambo hayo kuwa ni Rais kugawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo, watumishi kuachishwa kazi, upitishaji mizigo Bandari ya Dar es Salaam kushuka, nchi kunyimwa misaada na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi hivi sasa.

Katika uchaguzi huo, Rais Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47 na kumshinda Lowassa ambaye alikuwa amejiunga Chadema Julai mwaka jana akitokea CCM ambako jina lake lilikatwa katika mchakato wa chama hicho kupata mgombea urais.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kutengua uteuzi au kuwasimamisha kazi watendaji mbalimbali wa Serikali, kufuta maadhimisho ya sherehe mbalimbali na kuagiza fedha zitumike kutekeleza miradi mingine huku akiwabana wafanyabiashara kulipa kodi.

Uamuzi wake huo unaofanywa pia na mawaziri wake umekuwa ukipongezwa na kukosolewa na watu wa kada mbalimbali na jana Lowassa alikuwa miongoni mwa wakosoaji hao ikiwa ni mara yake ya pili tangu Dk Magufuli aingie madarakani.

Mara ya kwanza, Lowassa alikosoa sera ya elimu bure, alipoitofautisha na ile aliyokuwa ameahidi ya kuanzia awali hadi chuo kikuu na kuhoji iwapo Rais Magufuli mbali na ada angefuta pia michango mingine, jambo ambalo lilifanyiwa kazi.

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo hayo, Profesa Mukandala alisema: “Tunafanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi, utawala bora na ushindani wa siasa na tunazungumza na watu kutoka vyama mbalimbali na viongozi wa Serikali.”

Waziri wa Habari, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lowassa alisema waziri mkuu huyo wa zamani anapingana na viongozi wa Chadema wanaokiri wazi kuwa Rais Magufuli anatekeleza sera na mikakati ya upinzani.

Kauli ya Lowassa

Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Lowassa ilisema mwanasiasa huyo aliwaeleza wanazuoni hao kuwa; “hali ya siasa hivi sasa ni ya hamasa kutokana na Serikali mpya na ‘style’ mpya. Kwa kipindi kifupi atakuwa lakini hakuna mafanikio ya kiuchumi mbele ya safari.”

Alisema Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni Bunge.

Rais Magufuli amekuwa na utaratibu kuidhinisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe mbalimbali kutumika katika shughuli nyingine. Juzi, aliagiza Sh2 bilioni zilizokuwa zitumike katika Siku ya Muungano zitumike kupanua barabara inayokwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Pia, amewahi kuamuru Sh4 bilioni za Siku ya Uhuru kupanua Barabara ya Morocco – Mwenge, Dar es Salaam. Aliagiza pia fedha za maadhimisho ya siku ya Ukimwi kutumika kununua vifaatiba na Sh225 milioni zilizotengwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge zilinunulia vitanda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Lowassa pia alieleza kusononeshwa na hali ngumu ya maisha na idadi kubwa ya watu kuachishwa kazi.

“Nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.

“Bandarini sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale kulikuwa na vijana wetu wengi wana ajira, sasa hivi wako mitaani, hali inatisha maisha ya mwananchi yanazidi kuwa magumu,” alisema.

Lowassa aligusia uamuzi wa Marekani kupitia bodi yake ya Changamoto za Milenia (MCC) kusitisha msaada wa zaidi ya Sh1 trilioni. “Ni pigo kwa mustakabali wa uchumi. Halafu tunasema tunataka nchi ya viwanda, hela tutatoa wapi kama si hawa wafadhili wa ndani na nje kusaidia katika hilo?” alihoji.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema: “Hawa wafadhili siyo watu wa kuwabeza wataturudisha nyuma. Jakaya (Kikwete- Rais mstaafu wa Awamu ya Nne) kwa kiasi kidogo alijitahidi kuvutia wawekezaji, japo kulikuwa na uzembe na ufisadi katika kuwasimamia.

“Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu,” alisema.

Alisema si kweli kuwa kila mtu katika Serikali ya Awamu ya Nne alikuwa mla rushwa huku akikiri kuwa mfumo wa Serikali hiyo ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

Aliwaeleza wanazuoni hao kuwa: “Uchaguzi ule tulishinda (upinzani) na kila mtu anajua hivyo. Hata Magufuli anajua hilo...,” alisema.

Akizungumzia mikakati ya upinzani, Lowassa alisema wamejipanga kuhakikisha hawaporwi tena ushindi na kusisitiza kuwa joto la kutaka mabadiliko bado ni kubwa na Watanzania wameichoka CCM.

Kauli na Nape

Akijibu hoja zilizotolewa na Lowassa, Nape alisema, “Anajichanganya tu, maana Mbowe (Freeman – Mwenyekiti wa Chadema) amenukuliwa akisema Rais Magufuli anaiga kila kitu cha Chadema, sasa yeye (Lowassa) anaposema hayo maana yake haelewani na Mbowe.”

Alisema litakuwa jambo la ajabu kama Lowassa atakubali kila jambo linalofanywa na Serikali iliyopo madarakani kwa kuwa ndivyo alivyo.

“Katika Uchaguzi Mkuu Lowassa hakuchaguliwa na wananchi ila Magufuli alichaguliwa kwa sababu wananchi walifurahishwa na sera zake, hivyo amuache mwenzake atekeleze ahadi zake kwa wananchi,” alisema Nape.

“Kwanza Lowassa amekuwa mtetezi wa wezi, mafisadi na wala rushwa. Unawateteaje watu wa aina hii wanapofukuzwa kazi. Amebanwa tu na kwake kazi inayofanywa na Magufuli inampa maumivu.”

Chanzo: Mwananchi

Kumbe Mhe. Lowassa kichwa chake kinafanya kazi sana, huyu jamaa ana akili sana yaani haya aliyoongea yupo juu ya mstari na mimi siku zote nilikuwa nahoji huu ubora wa JMP uko wapi hadi sasa siku 120 alizokaa madarakani??

Anashika madagaa na vipapa hela inaingia serikalini lakini kuhusu mustakbali wa maisha ya watu maisha yanaelekea kuwa magumu zaidi, ajira sasa ndio imekuwa ni ndoto mana walio makazini wanapunguzwa wanawkwa nje, matajiri ndio hao nao wameanza kukwepa bandari ya Dar es salaam ivi baada ya miaka 5 tutakuwa wapi?? Iyo nchi ya viwanda itaanzia wapi kama wafadhili wameingia mitini?

Hongera baba Lowassa Mungu akuweke 2020, watanzania waliandikia mate sasa wanaona wino unavyofanya kazi tunasubiri hiyo nchi ya Viwanda hadi leo hakuna dalili ni porojo tu.

Kumbe Lowassa kubaki kimya anasoma mwenendo tu wa JMP., tayari CCM imekwisha habari yake ata mwaka 1 bado. Hongera baba Lowassa.
 
Mimi pia niliamini Lowassa ni fisadi. Ila leo nimejua kuwa Lowassa sio fisadi ni propaganda tu. Fisadi ni hawa, Masamaki, Mramba, Ridhiwani, kina said lugumi, Dau, Yona, Kitilya na Barbarosa.

Unaweza kuamini unavyotaka kuamini, hata kama ukiamini kwamba fisadi Lowasa ni baba yako na yule uliyeambiwa ulisingiziwa huwo ni uamuzi wako lkn haibadilishi Ukweli kwamba na Dunia nzima inajua kwamba Lowasa ni fisadi!
 
Kumbe Mhe. Lowassa kichwa chake kinafanya kazi sana, huyu jamaa ana akili sana yaani haya aliyoongea yupo juu ya mstari na mimi siku zote nilikuwa nahoji huu ubora wa JMP uko wapi hadi sasa siku 120 alizokaa madarakani??

Anashika madagaa na vipapa hela inaingia serikalini lakini kuhusu mustakbali wa maisha ya watu maisha yanaelekea kuwa magumu zaidi, ajira sasa ndio imekuwa ni ndoto mana walio makazini wanapunguzwa wanawkwa nje, matajiri ndio hao nao wameanza kukwepa bandari ya Dar es salaam ivi baada ya miaka 5 tutakuwa wapi?? Iyo nchi ya viwanda itaanzia wapi kama wafadhili wameingia mitini?

Hongera baba Lowassa Mungu akuweke 2020, watanzania waliandikia mate sasa wanaona wino unavyofanya kazi tunasubiri hiyo nchi ya Viwanda hadi leo hakuna dalili ni porojo tu.

Kumbe Lowassa kubaki kimya anasoma mwenendo tu wa JMP., tayari CCM imekwisha habari yake ata mwaka 1 bado. Hongera baba Lowassa.
yaani huyu mzee namuheshimu sana,japo wanambeza lakin kiakili yupo vizur sana
 
- Amlalamikia Rais Magufuli kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo chenye mamlaka kugawa fedha kipo ambacho ni bunge.(Pesa za uhuru na Pesa za Muungano)

- Asikitishwa na uachishwaji wa kazi kwa wafanyakazi, asema hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo ndio usababisha utendaji hafifu.

- Asononeshwa na hali ngumu ya maisha mtaani.

- Asikitishwa na ushukaji wa huduma ya Bandari kushuka kwa asilimia 50 na kusababisha vijana wengi kusota mtaani.

- Kitendo cha wahisani kujitoa kuisaidia nchi asema n i pigo kubwa kwetu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.

- Asema si kweli kwamba uongozi wa Rais mstaafu Kikwete kila mtu alikuwa mla rushwa, ni kweli mfumo ule ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

==================

Dar es Salaam: Siku 155 baada ya Dk John Magufuli kuapishwa kuwa Rais, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi huo, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomfanya autilie shaka mustakabali wa Taifa chini ya uongozi wa Rais huyo wa Awamu ya Tano.

Akizungumza na wanazuoni wa ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala nyumbani kwake Masaki Dar es Salaam, Lowassa alisema: “Hali ya siasa nchini ni ya hamasa lakini isiyo na msingi endelevu.”

Lowassa, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo baada ya kupata kura milioni 6.07 sawa na asilimia 39.97 aliyataja mambo hayo kuwa ni Rais kugawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo, watumishi kuachishwa kazi, upitishaji mizigo Bandari ya Dar es Salaam kushuka, nchi kunyimwa misaada na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi hivi sasa.

Katika uchaguzi huo, Rais Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47 na kumshinda Lowassa ambaye alikuwa amejiunga Chadema Julai mwaka jana akitokea CCM ambako jina lake lilikatwa katika mchakato wa chama hicho kupata mgombea urais.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kutengua uteuzi au kuwasimamisha kazi watendaji mbalimbali wa Serikali, kufuta maadhimisho ya sherehe mbalimbali na kuagiza fedha zitumike kutekeleza miradi mingine huku akiwabana wafanyabiashara kulipa kodi.

Uamuzi wake huo unaofanywa pia na mawaziri wake umekuwa ukipongezwa na kukosolewa na watu wa kada mbalimbali na jana Lowassa alikuwa miongoni mwa wakosoaji hao ikiwa ni mara yake ya pili tangu Dk Magufuli aingie madarakani.

Mara ya kwanza, Lowassa alikosoa sera ya elimu bure, alipoitofautisha na ile aliyokuwa ameahidi ya kuanzia awali hadi chuo kikuu na kuhoji iwapo Rais Magufuli mbali na ada angefuta pia michango mingine, jambo ambalo lilifanyiwa kazi.

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo hayo, Profesa Mukandala alisema: “Tunafanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi, utawala bora na ushindani wa siasa na tunazungumza na watu kutoka vyama mbalimbali na viongozi wa Serikali.”

Waziri wa Habari, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lowassa alisema waziri mkuu huyo wa zamani anapingana na viongozi wa Chadema wanaokiri wazi kuwa Rais Magufuli anatekeleza sera na mikakati ya upinzani.

Kauli ya Lowassa

Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Lowassa ilisema mwanasiasa huyo aliwaeleza wanazuoni hao kuwa; “hali ya siasa hivi sasa ni ya hamasa kutokana na Serikali mpya na ‘style’ mpya. Kwa kipindi kifupi atakuwa lakini hakuna mafanikio ya kiuchumi mbele ya safari.”

Alisema Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni Bunge.

Rais Magufuli amekuwa na utaratibu kuidhinisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe mbalimbali kutumika katika shughuli nyingine. Juzi, aliagiza Sh2 bilioni zilizokuwa zitumike katika Siku ya Muungano zitumike kupanua barabara inayokwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Pia, amewahi kuamuru Sh4 bilioni za Siku ya Uhuru kupanua Barabara ya Morocco – Mwenge, Dar es Salaam. Aliagiza pia fedha za maadhimisho ya siku ya Ukimwi kutumika kununua vifaatiba na Sh225 milioni zilizotengwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge zilinunulia vitanda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Lowassa pia alieleza kusononeshwa na hali ngumu ya maisha na idadi kubwa ya watu kuachishwa kazi.

“Nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.

“Bandarini sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale kulikuwa na vijana wetu wengi wana ajira, sasa hivi wako mitaani, hali inatisha maisha ya mwananchi yanazidi kuwa magumu,” alisema.

Lowassa aligusia uamuzi wa Marekani kupitia bodi yake ya Changamoto za Milenia (MCC) kusitisha msaada wa zaidi ya Sh1 trilioni. “Ni pigo kwa mustakabali wa uchumi. Halafu tunasema tunataka nchi ya viwanda, hela tutatoa wapi kama si hawa wafadhili wa ndani na nje kusaidia katika hilo?” alihoji.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema: “Hawa wafadhili siyo watu wa kuwabeza wataturudisha nyuma. Jakaya (Kikwete- Rais mstaafu wa Awamu ya Nne) kwa kiasi kidogo alijitahidi kuvutia wawekezaji, japo kulikuwa na uzembe na ufisadi katika kuwasimamia.

“Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu,” alisema.

Alisema si kweli kuwa kila mtu katika Serikali ya Awamu ya Nne alikuwa mla rushwa huku akikiri kuwa mfumo wa Serikali hiyo ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

Aliwaeleza wanazuoni hao kuwa: “Uchaguzi ule tulishinda (upinzani) na kila mtu anajua hivyo. Hata Magufuli anajua hilo...,” alisema.

Akizungumzia mikakati ya upinzani, Lowassa alisema wamejipanga kuhakikisha hawaporwi tena ushindi na kusisitiza kuwa joto la kutaka mabadiliko bado ni kubwa na Watanzania wameichoka CCM.

Kauli na Nape

Akijibu hoja zilizotolewa na Lowassa, Nape alisema, “Anajichanganya tu, maana Mbowe (Freeman – Mwenyekiti wa Chadema) amenukuliwa akisema Rais Magufuli anaiga kila kitu cha Chadema, sasa yeye (Lowassa) anaposema hayo maana yake haelewani na Mbowe.”

Alisema litakuwa jambo la ajabu kama Lowassa atakubali kila jambo linalofanywa na Serikali iliyopo madarakani kwa kuwa ndivyo alivyo.

“Katika Uchaguzi Mkuu Lowassa hakuchaguliwa na wananchi ila Magufuli alichaguliwa kwa sababu wananchi walifurahishwa na sera zake, hivyo amuache mwenzake atekeleze ahadi zake kwa wananchi,” alisema Nape.

“Kwanza Lowassa amekuwa mtetezi wa wezi, mafisadi na wala rushwa. Unawateteaje watu wa aina hii wanapofukuzwa kazi. Amebanwa tu na kwake kazi inayofanywa na Magufuli inampa maumivu.”

Chanzo: Mwananchi
Hizo ni kelele za mwana siasa aliyepoteza kuchaguliwa. Rais ni mmoja wa mihimili mikuu mitatu ya utawala. Anayo mamlaka kupinga kabisa matumizi mabaya yaliyopitishwa na Bunge. Kama Lowassa na timu yake wanaona kuwa ni kosa kufuta matumizi ya sherehe na kuzipeleka kwa wananchi moja kwa moja, basi WASIMAME BUNGENI NA KUSEMA HAYO WATU WAWASIKIE. Halafu Rais alifute Bunge kwa mamlaka yake, na awatake wote warudi kwa wananchi kuchaguliwa upya, ili wajulikane ni wanapiganiua masilahi ya wanaonufaika na sherehe, au wanapigania masilahi ya wananchi. Waone cha mtema kuni, kama hata mtu mmoja, atayesme utumbo huo wa Luwassa, atachaguliwa kurudi kama mbunge! Tuache porojo za kisiasa na kelele za walioshindwa, na kukosa hoja. Tujenge nchi. Lowassa na genge lake asuburi uchaguzi mwengine kisha aseme hayo katika kampeni zake.
 
Unaweza kuamini unavyotaka kuamini, hata kama ukiamini kwamba fisadi Lowasa ni baba yako na yule uliyeambiwa ulisingiziwa huwo ni uamuzi wako lkn haibadilishi Ukweli kwamba na Dunia nzima inajua kwamba Lowasa ni fisadi!
Mfikisheni mahakamani sasa kama ushahidi huo unao. Kusema sema tu fisadi inatusaidieje?
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Mfikisheni mahakamani kama kina Mramba na Yona tujue kweli ni mwizi. Mnapata wapi authority ya kuthibitisha kuwa ni mwizi? Wezi na wala rushwa wanafikishwa mahakamani kama kina Lugola wanaojidai kupiga kelele sana kumbe wala rushwa
Kijana wacha hasira!
 
Mfikisheni mahakamani sasa kama ushahidi huo unao. Kusema sema tu fisadi inatusaidieje?

Usiwe na mchecheto Mahakamani ni lazima atapelekwa TAKUKURU ni lazima watamfikia muda siyo mrefu, kuwa na subira!
 
Unaweza kuamini unavyotaka kuamini, hata kama ukiamini kwamba fisadi Lowasa ni baba yako na yule uliyeambiwa ulisingiziwa huwo ni uamuzi wako lkn haibadilishi Ukweli kwamba na Dunia nzima inajua kwamba Lowasa ni fisadi!
Si Una ushahidi kafungue shitaka mahakamani.
 
Lowassa anajaribu kuwarudisha CHADEMA kundini... Anaongea pumba tupu... Yeye kama ataki watu wa Mwanza wajengewe barabara aseme tunajua ana chuki na wasukuma sababu walimwonyesha misimamo yao,,, alitaka hizo hela zikanunulie kofia na kukodisha ngoma hiyo ndio vision au kwake kupunguza msongamano kwenye barabara kwa kuzipanua sio vision?

Hiyo pesa zilishaidhinishwa na bunge alichofanya Magufuli ni kubadili tu matumizi tena kwa mema sio kwa ubaya vision imekosekana wapi hapo.. Fisadi mwizi mkubwa ebu atupishe tujenge nchi yeye alijua kuiba tu.
Lowasa amekosoa kuwa raisi hafuati utaratibu!
Itakuwaje akiamua kusema bajeti ya uchaguzi 2020 ihamishiwe ktk ujenzi wa daraja la kwenda Zanzibar maana ni muhimu kuwepo na mawasiliano baina ya hizi nchi mbili zilizoungana!
Ok! Kwanini bajeti nyingi zilizopindishwa zinaelekea barabarani?
Kwanini isingeenda shuleni?
Je kama na yeyye ana cover viporo vyake?
Takukuru inapaswa wachunguze hili suala ili tujiridhishe kuwa anayafanya haya kwa nia njema na sio kufunika viraka vyake!
Huu ndio utawala wa sheria!
Semeni yoote kuhusu Lowasa! Mimi pia namshutumu kwa kuwa na kashfa nyingi ingawa sina uthibitisho! Ila hilo halimnyimi haki ya kutoa maoni, kukosoa na kuunga mkono mambo yanayotokea nchini! Ukishindwa uraisi hakukufanyi usitoe maoni, by the way anaweza akawa bado muwakilishi wa Watanzania 6milion! Kama Magufuli anapata haki just kwa kuwa amechaguliwa na watu mil 8, then mtanzania wa pili kutoa maoni anapaswa awe Lowasa mwenye watu mil 6! Kwa maana nyingine kila alifanyalo Magufuli tulipaswa kwanza tumuulize Lowasa maoni yake kabla wengine hatujazungumza!
 
Back
Top Bottom