Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

- Amlalamikia Rais Magufuli kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo chenye mamlaka kugawa fedha kipo ambacho ni bunge.(Pesa za uhuru na Pesa za Muungano)

- Asikitishwa na uachishwaji wa kazi kwa wafanyakazi, asema hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo ndio usababisha utendaji hafifu.

- Asononeshwa na hali ngumu ya maisha mtaani.

- Asikitishwa na ushukaji wa huduma ya Bandari kushuka kwa asilimia 50 na kusababisha vijana wengi kusota mtaani.

- Kitendo cha wahisani kujitoa kuisaidia nchi asema n i pigo kubwa kwetu kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.

- Asema si kweli kwamba uongozi wa Rais mstaafu Kikwete kila mtu alikuwa mla rushwa, ni kweli mfumo ule ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

==================

Dar es Salaam: Siku 155 baada ya Dk John Magufuli kuapishwa kuwa Rais, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi huo, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomfanya autilie shaka mustakabali wa Taifa chini ya uongozi wa Rais huyo wa Awamu ya Tano.

Akizungumza na wanazuoni wa ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala nyumbani kwake Masaki Dar es Salaam, Lowassa alisema: “Hali ya siasa nchini ni ya hamasa lakini isiyo na msingi endelevu.”

Lowassa, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo baada ya kupata kura milioni 6.07 sawa na asilimia 39.97 aliyataja mambo hayo kuwa ni Rais kugawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo, watumishi kuachishwa kazi, upitishaji mizigo Bandari ya Dar es Salaam kushuka, nchi kunyimwa misaada na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi hivi sasa.

Katika uchaguzi huo, Rais Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47 na kumshinda Lowassa ambaye alikuwa amejiunga Chadema Julai mwaka jana akitokea CCM ambako jina lake lilikatwa katika mchakato wa chama hicho kupata mgombea urais.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kutengua uteuzi au kuwasimamisha kazi watendaji mbalimbali wa Serikali, kufuta maadhimisho ya sherehe mbalimbali na kuagiza fedha zitumike kutekeleza miradi mingine huku akiwabana wafanyabiashara kulipa kodi.

Uamuzi wake huo unaofanywa pia na mawaziri wake umekuwa ukipongezwa na kukosolewa na watu wa kada mbalimbali na jana Lowassa alikuwa miongoni mwa wakosoaji hao ikiwa ni mara yake ya pili tangu Dk Magufuli aingie madarakani.

Mara ya kwanza, Lowassa alikosoa sera ya elimu bure, alipoitofautisha na ile aliyokuwa ameahidi ya kuanzia awali hadi chuo kikuu na kuhoji iwapo Rais Magufuli mbali na ada angefuta pia michango mingine, jambo ambalo lilifanyiwa kazi.

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo hayo, Profesa Mukandala alisema: “Tunafanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi, utawala bora na ushindani wa siasa na tunazungumza na watu kutoka vyama mbalimbali na viongozi wa Serikali.”

Waziri wa Habari, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lowassa alisema waziri mkuu huyo wa zamani anapingana na viongozi wa Chadema wanaokiri wazi kuwa Rais Magufuli anatekeleza sera na mikakati ya upinzani.


Kauli ya Lowassa


Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Lowassa ilisema mwanasiasa huyo aliwaeleza wanazuoni hao kuwa; “hali ya siasa hivi sasa ni ya hamasa kutokana na Serikali mpya na ‘style’ mpya. Kwa kipindi kifupi atakuwa lakini hakuna mafanikio ya kiuchumi mbele ya safari.”

Alisema Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni Bunge.

Rais Magufuli amekuwa na utaratibu kuidhinisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe mbalimbali kutumika katika shughuli nyingine. Juzi, aliagiza Sh2 bilioni zilizokuwa zitumike katika Siku ya Muungano zitumike kupanua barabara inayokwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Pia, amewahi kuamuru Sh4 bilioni za Siku ya Uhuru kupanua Barabara ya Morocco – Mwenge, Dar es Salaam. Aliagiza pia fedha za maadhimisho ya siku ya Ukimwi kutumika kununua vifaatiba na Sh225 milioni zilizotengwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge zilinunulia vitanda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Lowassa pia alieleza kusononeshwa na hali ngumu ya maisha na idadi kubwa ya watu kuachishwa kazi.

“Nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.

“Bandarini sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale kulikuwa na vijana wetu wengi wana ajira, sasa hivi wako mitaani, hali inatisha maisha ya mwananchi yanazidi kuwa magumu,” alisema.

Lowassa aligusia uamuzi wa Marekani kupitia bodi yake ya Changamoto za Milenia (MCC) kusitisha msaada wa zaidi ya Sh1 trilioni. “Ni pigo kwa mustakabali wa uchumi. Halafu tunasema tunataka nchi ya viwanda, hela tutatoa wapi kama si hawa wafadhili wa ndani na nje kusaidia katika hilo?” alihoji.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema: “Hawa wafadhili siyo watu wa kuwabeza wataturudisha nyuma. Jakaya (Kikwete- Rais mstaafu wa Awamu ya Nne) kwa kiasi kidogo alijitahidi kuvutia wawekezaji, japo kulikuwa na uzembe na ufisadi katika kuwasimamia.

“Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu,” alisema.

Alisema si kweli kuwa kila mtu katika Serikali ya Awamu ya Nne alikuwa mla rushwa huku akikiri kuwa mfumo wa Serikali hiyo ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

Aliwaeleza wanazuoni hao kuwa: “Uchaguzi ule tulishinda (upinzani) na kila mtu anajua hivyo. Hata Magufuli anajua hilo...,” alisema.

Akizungumzia mikakati ya upinzani, Lowassa alisema wamejipanga kuhakikisha hawaporwi tena ushindi na kusisitiza kuwa joto la kutaka mabadiliko bado ni kubwa na Watanzania wameichoka CCM.

Kauli na Nape

Akijibu hoja zilizotolewa na Lowassa, Nape alisema, “Anajichanganya tu, maana Mbowe (Freeman – Mwenyekiti wa Chadema) amenukuliwa akisema Rais Magufuli anaiga kila kitu cha Chadema, sasa yeye (Lowassa) anaposema hayo maana yake haelewani na Mbowe.”

Alisema litakuwa jambo la ajabu kama Lowassa atakubali kila jambo linalofanywa na Serikali iliyopo madarakani kwa kuwa ndivyo alivyo.

“Katika Uchaguzi Mkuu Lowassa hakuchaguliwa na wananchi ila Magufuli alichaguliwa kwa sababu wananchi walifurahishwa na sera zake, hivyo amuache mwenzake atekeleze ahadi zake kwa wananchi,” alisema Nape.

“Kwanza Lowassa amekuwa mtetezi wa wezi, mafisadi na wala rushwa. Unawateteaje watu wa aina hii wanapofukuzwa kazi. Amebanwa tu na kwake kazi inayofanywa na Magufuli inampa maumivu.”

Chanzo: Mwananchi
Huyo Edward Lowassa ni nani hasa si bora anyamaze kuliko kutupigia kelele!
 
Watanzania wengi tu kama nyumbu! Warahisi kusifia bila kudadisi yaani sisi hadi tuje kuwa na akili ya kujiuliza maswali kabla ya kusifia ni karne moja ijayo! Ngoja siku atasema fungu fulani likajenge hekalu chato ndio tutajua kuwa tulikuwa tunasifia ujinga

kila siku endeleeni kusema ipo siku, mara ipo siku..... ishu hapa ni zinazookolewa zinafanya nini, sio bunge, kwahyo ulitaka aitishe bunge saizi? tambua kuwa hiyo bajeti kaikuta na mpango wake ni kubana matumizi ili hela ziende kwenye miladi inayo saidia wananchi. bajeti yake inakuja mwenyewe utakubali.
 
Sijamuelewa EL anaposikitika watu kuachishwa kazi, waliyofanya wale mafisadi wa TRA na Bandari bado unasikitika watu kuachishwa kazi? Subiri tu na kwako inakusogelea, kipenzi chako Monaban wa Arusha washambipu!
 
Lowassa anajaribu kuwarudisha CHADEMA kundini... Anaongea pumba tupu... Yeye kama ataki watu wa Mwanza wajengewe barabara aseme tunajua ana chuki na wasukuma sababu walimwonyesha misimamo yao,,, alitaka hizo hela zikanunulie kofia na kukodisha ngoma hiyo ndio vision au kwake kupunguza msongamano kwenye barabara kwa kuzipanua sio vision?

Hiyo pesa zilishaidhinishwa na bunge alichofanya Magufuli ni kubadili tu matumizi tena kwa mema sio kwa ubaya vision imekosekana wapi hapo.. Fisadi mwizi mkubwa ebu atupishe tujenge nchi yeye alijua kuiba tu.
Kwenye kubadilisha matumizi na kuona kuwa yana tija unakosea sana. Hata sisi huku serikalini tunapobadili matumizi ya hela tunakaripiwa sana. Tunatakiwa kuomba kibali juu ya ubadilishaji huo. Mfano ukitengewa fedha ya kununulia kompyuta na wew ukaona unayo badala yake ukaamua kununua printer ujue hilo ni kosa. Kufanya hivyo ni kuingilia mamlaka zingine. Kabla hujafanya hivyo unapaswa kuwajulisha wahusika. Hivyo kusema hata Magufuli anakosea kufanya hivyo. Pesa za muungano zinajumuisha na wazanzibar. Je walishafanya makubaliano ya pamoja na Zanzibar? Kama ndiyo, kwanini zikajenge barabara ambayo sio suala la muungano? Angesema zikanunue sare za Jeshi tungemwelewa
 
kila siku endeleeni kusema ipo siku, mara ipo siku..... ishu hapa ni zinazookolewa zinafanya nini, sio bunge, kwahyo ulitaka aitishe bunge saizi? tambua kuwa hiyo bajeti kaikuta na mpango wake ni kubana matumizi ili hela ziende kwenye miladi inayo saidia wananchi. bajeti yake inakuja mwenyewe utakubali.
Miladi=miradi
 
CCM kufanya cha maana tena ktk nchi ni ndoto. Imebaki kutegemea umaarufu wa mtu mmojammoja kukata soo.

Adui mkubwa wa nchi ni chama
 
Lowassa anajaribu kuwarudisha CHADEMA kundini... Anaongea pumba tupu... Yeye kama ataki watu wa Mwanza wajengewe barabara aseme tunajua ana chuki na wasukuma sababu walimwonyesha misimamo yao,,, alitaka hizo hela zikanunulie kofia na kukodisha ngoma hiyo ndio vision au kwake kupunguza msongamano kwenye barabara kwa kuzipanua sio vision?

Hiyo pesa zilishaidhinishwa na bunge alichofanya Magufuli ni kubadili tu matumizi tena kwa mema sio kwa ubaya vision imekosekana wapi hapo.. Fisadi mwizi mkubwa ebu atupishe tujenge nchi yeye alijua kuiba tu.
Wakarti mwingine jielimisheni kwanza kabla ya kujibu. Matumizi ya serikali yanaidhinishwa kwa kiasi na eneo la matumizi. Kubadilisha lolote kunahitaji idhini ya mamlaka husika na idhinisho. Ingekuwa hivyo unavyosema basi kusingekuwa na haja ya kusema hizo fedha unazoomba idhininyake utazitumiaje.
 
Luwasa ni mwizi....na hazi hela zote wangezipiga kwa kuuza fulana za maadhimisho,mbona haendelei na kutoa harambee makanisanu na misikitini...yale yalikuwa ni maono?..naona kesi ya Sioi inamchanganya!
Lowassa ni mwizi kumzidi mkapa na Ridhiwani kikwete? Au Pinda? Au Masamaki?
 
Hivi huyu bado tu hajaenda huko monduli alikoahidi kua ataenda chunga ng'ombe akishindwa uchaguzi..chezea jiji wewe , mjini patamu asikwambie mtu...tulia babu umeshasahaulika ...
 
Kwenye kubadilisha matumizi na kuona kuwa yana tija unakosea sana. Hata sisi huku serikalini tunapobadili matumizi ya hela tunakaripiwa sana. Tunatakiwa kuomba kibali juu ya ubadilishaji huo. Mfano ukitengewa fedha ya kununulia kompyuta na wew ukaona unayo badala yake ukaamua kununua printer ujue hilo ni kosa. Kufanya hivyo ni kuingilia mamlaka zingine. Kabla hujafanya hivyo unapaswa kuwajulisha wahusika. Hivyo kusema hata Magufuli anakosea kufanya hivyo. Pesa za muungano zinajumuisha na wazanzibar. Je walishafanya makubaliano ya pamoja na Zanzibar? Kama ndiyo, kwanini zikajenge barabara ambayo sio suala la muungano? Angesema zikanunue sare za Jeshi tungemwelewa

angenunua sare za jeshi, ungesema anatumia jeshi kutawala, hamnaga jema ninyi, ww ni msemaji wa wanzanzibari?
 
Watanzania wengi tu kama nyumbu! Warahisi kusifia bila kudadisi yaani sisi hadi tuje kuwa na akili ya kujiuliza maswali kabla ya kusifia ni karne moja ijayo! Ngoja siku atasema fungu fulani likajenge hekalu chato ndio tutajua kuwa tulikuwa tunasifia ujinga
Chato nyumba imejengwa ndani ya miezi mitatu. Huko kamaliza kazi
 
Magu mpeni miaka miwili tu atakuwa kama wenzake tu maana baada hapo uchaguzi utakuwa umekaribia hivyo lazima aende ki CCM maana yeye ndo atakuwa ni Rais na wakati huo huo ni Mwenyekiti wa chama.
Nape angetakiwa kujibu hoja kama ni sahihi Rais kuelekeza matumizi badala ya bunge. na je, kila rais ajaye akifanya hivo haiathiri utaratibu wa nchi. Pia aseme kama ni kweli au si kwel mizigo haijapungua bandarini na kama kukosa huo ufadhili ni kawaida tu.. Kujibu hoja kwa hoja n vizuri kwa viongozi wakubwa kama hawa.
Suala si kupongeza au kushutumu bali kueleza hali halisi ya mambao.
 
Wewe na fisadi Lowasa wote ni vilaza, haujui kama raisi Kikatiba ndiyo mwenye uwezo wa kuamua siku gani iwe sikukuu na nipi isiwe? Kwa taarifa yako tu wacha kubadilisha matumzi ya fedha bali Raisi wa JMTZ ana uwezo wa kuzifuta kabisa hizo siku na zisiwepo na hii ni Kikatiba kabisa!
Leta vifungu vinavyompa authority hiyo hadi akafuta kabisa. Kama ni hivyo ana uwezo pia kufuta hata bunge
 
Poor argument ever seen. Ukisema hivyo hakuna mtu anatoa pesa mfukoni. Hata hazina hupewa pesa kutoka BOT. hivyo ni argument isiyo na mashiko!
Nimeshakuelewa uko upande gani na ndo maana umejibu kwa jazba, tulia usiende hivyo, na hapo kama kuna cha kurekebisha, jazba yako imefanya hujaeleweka kabisaaa. Elewa hivi; bunge linakaa na kujadili bajeti zilizopelekwa pale na Wizara na maidara mbali mbali. Wanapozijadili wanaweza kubadili vitu au wasibadili na ikapita kama ilivyokuja. Baada ya hapo mtekelezaji wa ile bajeti ni Hazina, na hutekeleza kwa kutuma pesa kama zilivyopitishwa na Bunge. Na ni hivyo hivyo pia kwa Sheria na Mahakama. Bunge linatunga sheria mahakama inatekeleza kwa kuzifanyia kazi.
 
Ni wewe usiyepima maoni ya Lowasa....yule ni mwizi tu na alitumia hizi hafla kuuza fulana na anasa...ndio maana kwa sasa hata CHADEMA wanatumbuwa ruzuku hoteli za kitalii..! Hana sifa hata za kugombea serikali ya kijiji.
Jinga kweli wew. Mlimpaje uwaziri mkuu, uwaziri wa maji, uwaziri wa ardhi?
 
Mwaka 1970 hadi 1980 nimiaka ambayo haisahauliki katika akili za watoto Wa Kitanzania.

Ndio kipindi wafadhili walikata miguu kuisaidia Afrika has a nchivn zilizoukanda Wa kusini mwa jangwa LA Sahara,Sababu kubwa ilikuwa mfumo mbovu Wa utawala( utawala bora)

Ccm tens kupitia kwa Magufuli wanarudia kosa lilelile.
 
Ujue Lowasa mimi huwa namuona kama hajitambui vile sijui nani kamroga anaongea pumba tupu yani hajui hata pesa ipi inatakiwa kuidhinishwa na bunge na pesa gani ipo kwenye mamlaka ya Rais,mtu mzima hovyo kabisa.
Leta sasa ufafanuzi wew unayejua? Tupe na kifungu kinachosema bunge likiidhinisha bajet Rais anaweza kubadili matumizi yake
 
Back
Top Bottom