Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Edward Lowassa akosoa uongozi wa Rais Magufuli

Kumbe jamaa ana kampuni ya kuprint t-shirt, mhmhhhhhh sasa naanza kuelewa,ndio maana analalamika. Magu kufunga mirija yote ya jamaa kupata tenda. Hakuna sherehe kwa miaka kama mitano. Tuone kama mtapata tenda ya kuprint tshirt. Magufuli ni noma. Sherehe zote za kumuingizia kipato jamaa zinakatwa.
 
babu lifisadi angepata nchi tungekuwa kama SOMALIA Kiuchumi
 
lowasa lowasa lowasa..........................rais wa wawapigaji
 
nadhani kuna haja cdm kumkanya huu mzee maana hoja zake zinareflect aina ya mtu walionaye
 
Fisadi huyo achaneni naye. Nayeye dawa yake inachemka, ache kijishaua. Hapa kazi tu.
 
Tumuweke Chenge Kuwa Mwenyekiti wa Bunge Nae Ni Kama Lowasa Hamna Ushaidi kama Ni Fisadi Jamani Imepita Ndiyooooooo
 
images
 
JPM Uuzwaji wa Nyumba za Serikali,2, Kivuko kivovu Aka Chakavu, 3,200 Za Kuboresha Vivuko Kigamboni Lakini Ukweli wa Mambo Wakazi wa Kigamboni Wanasubiri MV, Magogoni Au MV, Kigamboni kimoja Kizame Ndio Vinunuliwe Vipya
 
Lowassa anajaribu kuwarudisha CHADEMA kundini... Anaongea pumba tupu... Yeye kama ataki watu wa Mwanza wajengewe barabara aseme tunajua ana chuki na wasukuma sababu walimwonyesha misimamo yao,,, alitaka hizo hela zikanunulie kofia na kukodisha ngoma hiyo ndio vision au kwake kupunguza msongamano kwenye barabara kwa kuzipanua sio vision?

Hiyo pesa zilishaidhinishwa na bunge alichofanya Magufuli ni kubadili tu matumizi tena kwa mema sio kwa ubaya vision imekosekana wapi hapo.. Fisadi mwizi mkubwa ebu atupishe tujenge nchi yeye alijua kuiba tu.
alichoongea lowasa technically kina mantiki
 
Kiongozi wa upinzani ambaye hajaonekana au kusikika kwa muda mrefu anaibuka na kuongea pumba tupu. No substance, no point ya hamasa. Kwani haoni wenzake kama akina Odinga wanavyo ongea na kuyafanya? Tunataka upinzani kwa sababu unachochea moto wa maendeleo. Lakini siyo wa design hii, ilimradi tu mtu kaonekana kwenye media. A loser at best.
 
Unaweza soma ila ukabaki mjinga tu.
Mkurugenzi anapopewa fedha za miradi akitaka kubadili matumizi huomba kibali TAMISEMI na HAZINA,ndipo azitumie


Pesa zinapotengwa kwa ajili ya jambo Fulani kisha ukabadili matumizi ndio chanzo cha hati chafu.

Rais katika Katiba na sheria za Binge ,hakuna ibara au kifungu chochote cha kisheria kinachomruhusu kubadili matumizi,hulazimika aende kwenye muhimili mwingine akaombe kibali.

Suala LA Utawala bora ndio hili ambalo wazungu wamekuwa wakituwekea masharti ya mikopo,lakini cha ajabu nashindwa kukuelewa kinachomuogopesha Rais kutumia waziri aende kuomba kubadili matumizi ni nini?
Kimsingi hata mimi naona ipo shida. Wapo watu wamewahi kuingia matatani japo walikua na nia njema na jambo fulani, lakini ukishabadili matumiz ya fedha kwenda kifungu ambacho sicho kilichoombewa pesa, kwa mtumishi mwingine lazima ile kwako, bila kujali ulikua na nia njema ama la. Huo ndiyo hasa utumishi wa umma. Lazima pesa ulizoomba kununua madawati zifanye kazi hiyo, usibadili matumizi. Sasa kwa level ya mkuu wa nchi inawezekana hakuna shida. Lakini mtumishi wa umma mwingine akithubutu CAG atampa hati chafu na kiukweli lazima ataburuzwa kortini kwa matumizi mabaya ya madaraka. Pesa za kifungu X kuhamishia kifungu Y ni ngumu sana. Labda kama sheria zimebadilika, sina hakika!
 
Lowassa amejaliwa akili sana kitu kinachomtofautisha na wengine wengi....

Akili ya Kupiga na michongo cyo?
Kwa akili hizo kweli anazo na anazitumia kweli kutuumiza as a Nation .... Umeme wa dharura alitumia akili akapiga mzigo Mnene tu..... Na Taifa linazidi kuteketea kwa michongo ya aina hiyo..... Stop it nyie Mafisadi

Ni kweli Magufuli hana vision ndio maana ameanza kufifia!!!
 
“Anajichanganya tu, maana Mbowe (Freeman – Mwenyekiti wa Chadema) amenukuliwa akisema Rais Magufuli anaiga kila kitu cha Chadema, sasa yeye (Lowassa) anaposema hayo maana yake haelewani na Mbowe.”

Alisema litakuwa jambo la ajabu kama Lowassa atakubali kila jambo linalofanywa na Serikali iliyopo madarakani kwa kuwa ndivyo alivyo.

“Katika Uchaguzi Mkuu Lowassa hakuchaguliwa na wananchi ila Magufuli alichaguliwa kwa sababu wananchi walifurahishwa na sera zake, hivyo amuache mwenzake atekeleze ahadi zake kwa wananchi,” alisema Nape.

“Kwanza Lowassa amekuwa mtetezi wa wezi, mafisadi na wala rushwa. Unawateteaje watu wa aina hii wanapofukuzwa kazi. Amebanwa tu na kwake kazi inayofanywa na Magufuli inampa maumivu.”

NIMEIRUDIA
 
...eti maanayake nini..? hata Obama anakosolewa ijekuwa Magufuli...?? alichosema Lowassa matumizi lazima yaidhinishwe na bunge na sio kupanga na kujitekelezea mwenyewe. kesho akisema anataka bilioni mbili zikakarabati nyumba yake pia usijekuhoji...
Miaka yote yamekuwa yanapitishwa na bunge LAKINI matokeo yake tumeona. Na hiyo mifano aliyoitoa ndiyo haina mantiki kabisa. Zile pesa zilishakuwa appropriated na bunge kwamba sherehe iwe 4B. Magufuli alichofanya ni kushangaa jinsi zilivyo too much na kuzipangia matumizi mengine ya maendeleo na watu wamefurahi.
Kwa hiyo Lowassa angeshinda asingeona hatari kutumia Bilioni 4 kwa hiyo sherehe ya uhuru kisa Bunge lilipitisha au ana maanisha nini?
 
image.jpg
image.jpg

Wadau, amani iwe kwenu.

Nimewasikia mara kadhaa wabunge na wanasiasa wa upinzani wakisema kuwa kazi yao ni kukosoa Serikali na si kuisifu. Wabunge wamekuwa wakifanya hivyo ndani ya Bunge. Na viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakifanya hivyo kwenye mikutano yao ya kisiasa.

Ila alichofanya Lowasa hakika amegeuka kuwa kituko. Kuwaita Waandishi wa Habari na kuongea utumbo ule eti analalamika serikali inapowatimuwa watendaji wazembe, mafisadi na majizi hakika amegeuka kuwa kituko. Si kila kiongozi wa serikali unaweza kumpinga. Watanzania tumemkubali Magufuli. Hata ufanyeje Lowasa sana sana utakuwa unampigia mbuzi gitaa ama unatwanga maji kwenye kinu kwa kutaraji upate unga.

Siasa za upinzani zimekushinda bwana Lowasa. Bora ungerudi Monduli kuchunga ng'ombe kama ulivyoahidi kuliko hivi unavyofanya sasa. Unachekesha na unahuzunisha. Sidhani kama unapata ushauri mzuri kutoka kwa chama chako. Mtu pekee ambaye angekushauri kwa karibu ni Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ila kutokana na Mbowe kuchagua galasa, nafasi hiyo ni kama haina mtu kwa sasa. Ndo maana kila mtu ndani ya CHADEMA anaweza kuitisha kikao na media akazungumza anachopaswa kuzungumza hata kama hakina baraka ya vikao halali. Matokeo yake mnaanza kupingana wenyewe kwa wenyewe.
 
Back
Top Bottom