Educated TZ Immigrants in US in tough Situation



Yesu WANGU!!!!!!!!!!!!!
 

FMES

This is a Masterpiece.
 
Simpo facts za maisha, Tanzania ama Marekani;

1) Usiusemee moyo - JD, utamkuta club ukadhani ame-frustrate kumbe ndio raha yake! kama wewe wafurahia kuwa na nyumba wengine wafurahia kuwa na gari, au kuvaa vizuri! Mimi feeeling ya kuwa niko marekani tu, hata kama choka kiasi gani inanifanya nijisikie "high"
2) Money can buy a house not a home, waweza kuwa na jumba lako masaki na waishia kuogopa kwenda, wakati mie na XXL wangu twakaa kwenye sweet "home' $700/mo! Wengine wanasema money won't buy happiness
3) Katika long term impacts, kuna uwezekano mkubwa wa offsprings wa watu walioko marekani kufanya vizuri/kufanikiwa kuliko wa wale walio Tanzania
...
 
Hapa kila mtu na mtazamo wake, kama ww unaona bongo kunafaa ishi bongo, kama USA kunafaau au ulaya ishi huko. Masiha ni popote pale.
 
FMES

This is a Masterpiece.

- Naomba kuongeza hivi miaka mitano ya kwanza majuu, hasa US lazima uwe umepiga hatua kubwa sana kutoka ulikotoka, kama hakuna hatua huenda ni vyema ukaanza kufikiria kurudi nyumbani kwa sababu ulaya sio ya kila mtu.

- Lakini pia naomba kuwashauri vijana wa sasa wanaokwenda au wenye mpango wa kwenda huko hasa US, jaribu kuuliza, jaribu kutafuta ushauri kabla hujaondoka bongo kwa watu positive waliowahi kuishi huko, usijifanye unajua wakati kumbe kwa standards za US, ukweli ni kwamba hujui kitu kabisaa, usirukie tu mambo kwa pupa.

- US bado ni nchi nzuri pamoja na matatizo yake yote ya kichumi kwa sasa, vijana wengi wa sasa wanajaribu kutafuta njia za mkato, wengine mapak wamejiingiza kuolewa na kina mama wenye uwezo, jamani hatari sana hiyo halafu wengine wamejiingiza kuoa kina mama wa kimarekani, hao ninawapa pole sana, kwa sababu I do not care what unakuwa ume-lost tena bigtime, wengine wamejiingiza kwenye mambo ya ajabu sana hata ni aibu kusema.

- Nenda huko ufanye kazi, kubali kufa kwa sababu ya kufanya kazi, kule hakuna mambo ya kibongo bongo kumbuka ni dunia ya kwanza kule, work hard achana na starehe ambazo huziwezi, wewe bongo kwenyewe starehe hukuziweza sasa utaziweza vipi mwanzoni tu wa kufika US? Achana na kujifanya mnyamwezi kwa sababu haitakuja kutokea mnyamwezi akajifanya mbongo. Nyinyi wabongo hata mjibadili vipi kuwa kama wanyamwezi mbele ya wanyamwezi wenyewe nyinyi ni wabongo tu, hamna mpango.

Twende huko majuu kufanya kazi, sio kutegemea njia za mkato kwa sababu hazipo.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Achana na kujifanya mnyamwezi kwa sababu haitakuja kutokea mnyamwezi akajifanya mbongo. Nyinyi wabongo hata mjibadili vipi kuwa kama wanyamwezi mbele ya wanyamwezi wenyewe nyinyi ni wabongo tu, hamna mpango.

Tuko pamoja hapo, na ninaamini unamaanisha uzito wa hoja hiyo.

Na majuzi nikatoa mifano hai ya watu wanaojitahidi kwa udi na uvumba kujigeuza wazawa, kutopea, kuvaa utamaduni wa taswira ya Umarekani. Ukitoka sehemu masikini, sehemu inayodharaulika, ukawa bado kijana, mgeni mgeni ugenini, ukaonekana umeshuka kwenye boti juzi huna mitindo, umetokea kwa wenye unyuma, basi kama hujui vizuri sifa, thamani, historia ya unakotoka, mara nyingi ni lazima ujikatae. Mpaka jina lako utakataa.

Mimi nakataa kuchukua ubini mpya, napenda kuishi nje ya kasri ya Mwinyi mmiliki, kwenye kibanda cha mtwana.



​
Hasheem Thabeet gets caught in his girlfriend's sunglasses
By Eamonn Brennan, Yahoo! Sports​
 
Mkuu naifahamu bongo saana.......hio 50k ina maana kwa mwezi ni more than 4000USD huu ni mshahara wa watu wachache saana tena naweza kusema wale top executive ambapo kuzipata chances kama hizo ama ujulikane undugunization au ulale kwa waganga wa kienyeji......


point tupu.....kwa vitu ulivyoviorodhesha hapo nakubaliana na wewe 1000% yaani hivyo ndio hasa vinaniboa kila siku nawaza kukimbia.......bongo unaweaa kuwa na hela kama za MTM sababu ya mfumo hovyoo ukajikuta unakufa bila mungu kupenda kwa kugongwa na mataahira kama chenge....
.......sina cha kuongeza umemaliza kabisa........
 
Last edited:
I can understand hapa kila mmoja anayatazama maisha kinamna yake lakini kuwa na maisha yenye mwelekeo marekani sio lazima uwe educated.Kuna kazi nyingi tu Marekani ambazo hazihitaji hiyo elimu mnayoizungumzia nyinyi zinahitaji maarifa na uhard work wako.Kuna watu wanaingiza six figure na ukiwaona wala huwazanii sema maisha yashawafit kwa kile kipato chao hivyo hiyo six figure inaingia kwenye account leo na week ijayo account nyeupe lakini yote ni maisha.Na overall ni bora ya huku mlio bongo msijidanganye kama kuna mipango yoyote ya kuja huku mnapokuita unyamwezini njooni wala msisite hata kidogo.Hebu niwaulize nyie mlioko hapa America kwani mtu awe na kipato cha kiasi gani kwa mwaka hata mkubali kwamba mambo yake safi ?

SAHIBA.
 
Maskini vijana wetu na mbio za kujihalalishia kuishi nchi za wengine!! Taabu tupu mwajitakia bure!!! Nilikuwa Marekani juzi kwenye mkutano mkubwa tu huko Monterey CA, maprofessa wengi tu wamarekani walikuwepo, na sisi tulikuwa wachache tu kutoka Africa. Nilipata nafasi kutembea tembea kuona hali halisi ya akademia nchini marekani. Sasa kwenye ule mkutano sikuona mswahili ingawaje najua wapo wasomi watz wanaofudnisha nchini Marekani ( ingawaje naambiwa kwenye masomo ya lugha kama kiswahili, wabongo hamwoni ndani ni wakenya!). Nikiri kabisa watz mlio nje, mmekaa kimya mno, hatuwasikii kwenye hata radio mbao za wenzetu, hatuoni chochote mnacholeta huku, zaidi ya malalmiko. Lawama kwamba kuna viongozi mafisadi hapa bongo ni sahihi, lakini sio sababu ya kukufanya usije ukashiriki katika kulisukumu gurudumu. Ingawaje hata wale tuliowaopoa huko tukawapa madaraka hapa nyumbani wamekuwa mstari wa mbele wa kutufisadi, ni hao Balali, Masha na wengine wengi. Inasikitisha kweli!

Kwanza ni muhimu kuelewa kwamba maisha ni jinsi unavyotaka wewe yawe! Huwezi ukatamani tu yakawa mazuri, lazima uyasotee. Kusema sisi tulio hapa TZ ni wazembe, tunalala, sijui tunachukua muda mwingi kupiga gumzo, kula lunch ni kutuonea. Watu tunafanya kazi hadi jumapili, na muda wa kutoka ofisini sio saa 9 ni saa mbili usiku. Labda kwenye section za makarani ambao hawana la maana zaidi ya kuhudumia wateja wa siku. Hatujui holiday, hatujui hata leave za mwaka huwa tunabembelezwa. Sijui mnapata wapi mawazo hayo. Kweli mishahara yetu ni midogo, lakini sis sio wezi au mafisadi. Tunahangaika na hapa nazungumza wale ambao ni wa level yenu, mmesema 'educated TZ' ambao tunachanganya kazi za mwajiri na kazi za public service yaani consultancy. Kwa ajili hio tunaweza kutumia simu za mkono (kwenu ni rahisi lakini hapa walau $100 kwa mwezi kwa matumizi ya kawaida), gari na mafuta yake, kusomesha watoto.

kwa nini ukatafuta vikaratasi tena kupitia vibabu na vibibi, mnajidhalilisha. Njooni nyumbani lakini sio mkakae beach au Rose Garden, you have to be here ready to work 18 hours a day! Kwa nini mnyanyasike kiasi hicho. Angalieni wenzenu wakenya na wasomali na wanigeria, na waghana wanafanya kweli, tunaona matunda ya kazi yao kwa nchi zao, ninyi poaaaaaaaaaaaaaaaa mnalala kibongo bongo bongo, mnisamehe kama nitakuwa nimegusa mioyo yenu
 

Bongo tunaijua bwana, si wageni wa nchi yetu hadi tufanye research ama sivyo wasomi wetu ambao wengi wangependa kufanya kazi Tanzania wasingekimbia kwenda nchi mbali mbali zikiwemo Namibia, RSA, Botswana, UK, US, Canada n.k.

Wewe uko Bongo lakini unajua kwamba Watanzania wanaopata mshahara kama huo si wengi!! Sijui hizo data ulizipata wapi. Kuna Watanzania wengi sana ambao hawana majigambo wala hawapigi kelele ya jinsi mambo yalivyowanyookea kutokana na elimu zao walizozipata Tanazania au nchi za nje. Kurudi Bongo inataka moyo wa hali ya juu na hizi karaha zisizokwisha kila siku mara maji hamna, mara umeme hakuna mara mafuriko, vyote hivi kama tungekuwa na Viongozi wazuri ni vitu ambavyo tunaweza kabisa kuvimaliza lakini wapi watapanda majukwaani na kupiga alinacha zao huku nchi ikirudi nyuma kila kukicha. Msiwachuuze wenezenu wakafungasha kurudi bongo halafu wakabaki wanajuta kilio cha kusaga meno. Viongozi wakikutana na Watanzania walio nje kila siku hudai kwamba serikali inaweka mazingira mazuri mbali mbali ikiwemo ajira ili mrudi nyumbani lakini miaka inakatika bado hayo mazingira mazuri yamebaki ni alinacha tu.
 

BAK

Hawa jamaa haina haja hata ya kuwajibu na hawa ndio wale unaowaona humu JF ambao angalau wanaweza kumiliki ama kutumia hizo iternet za makazini na wakirudi majumbani hadi umeme akadiriwe na Tanesco.Tatizo sisi huku hasa hizo habari za mafisadi ndio zinatuchefua kabisa hatujui kama tuwaonee huruma Watanzania ama tuwaache tu maana ni sawa na sikio la kufa.Hawa wenye mawazo haya ni wabinafsi wa hali ya juu na wanajifikiria wao tu na hawajali vizazi vingine,na hili ndio tatizo kubwa la Mwafrica.

SAHIBA
 

Thank you, Well said! hapa ndipo utakapoona jinsi wabongo walivyo na ntimanyongo...Wana wivu wa hali juu!!!! Na kutaka kusema vitu ambavyo hawajui lolote au kutumia mifano michache na kutaka kuifanya mifano hiyo michache ni 100% ya hali halisi za Watanzania wote!!!
 

Mods pls fanyeni kazi yenu tunayowaaminia.
 

Mkuu umeshasema thread imejaa ujuaji... halafu na wewe unaweka ujuaji!! sijui umegain nini!!???

To be honest, i work for the government so that money is impossible.. the motive was to highlight that even 50k is available in poor tanzania because 80% ya contribution humu ndani ni negative about our Tanzania

Yourname is Mine.. why does it hurt so much!!? your posts exposes a deep rooted slave who would say anything to disguise his/her home and family... naifananisha na mwana anayeshinda kwa mjomba kwasababu ya vitu na wanaangalia TV na yuko tayari kubadili ubini wake ili tu asifanane na kwao kwenye taa ya chmli

Halafu, Pumbaf mwenyewe kwa ujuaji
 


Yo Yo, at least you have taken a better approach to a very provocative post... its is true that the average pay in TZ is still below 500USD per month but it is wrong to say that everything bad is in Bongo and 50K are available and not uncommon... there are good things and more opportunities come our way everyday WE SEE THEM AND SOME SEIZE THEM PERIOD!!

Yes there re risks and we face them everyday and wont stop because its a route a nation has to follow to reach promised land, but this is everywhere and if all of us decide to abandon TZ like one YNIM [even using foul language for his/her motherland], sijui kama tutakuwa tunasaidia ndugu zetu

If all of us agree on everything... then JF would be very boring
 
Nadhani hii thread ingeitwa "TZ Immigrants come to the US with unrealistic expectations" ingekua accurate zaidi.
 
Huku Taifa linawahitajia kutowa mchango wao kwanini wasirudi hapa nyumbani ?mara kwa mara viongozi wetu wamekuwa wakiwashauri ndugu zetu walio nje ya nchi kurudi nyumbani na kulijenga taifa hili ambalo bado changa .Rais siku zote katika matembezi yake huko ulaya na marekani amekuwa na jitihada za kuwaeleza ndugu hao umuhimu wa kurudi nyumbani .
 
Niliondoka Tz kwa hiari yangu mwenyewe nitarudi kwa hiari yangu mwenyewe.
Rais hajui kilichotuleta vipi aingilie kati kututaka turudi?

Kama ni msoto, mbona upo kila mahali?

Hapa tunabeba mabox na kufagia vyoo lakini hatuadhiriki na kubomu kila mtu au hatuli kwa shangazi na mjomba.
Kizuri zaidi hizo coin wanazotupa mwisho wa mwezi zimeweza saidia wazee wetu waliostaafu na kulipwa pensheni mbuzi kule Malinyi.

Heri lawama kuliko fedheha.

WOTI IZI BAITINGI YU GAIZI?? WI A LEYING DAUNI HIA CHILLING BATI YU SIIM TU MAINDI.

HUAI A YU GETTING BANIDI WITH ZE PEPA WHICH IZI IN ZE FILDI???? EEH?

AZA PIPO BWANA!!!
 
1. Yaani mimi na mara ya kwanza kuona Mtanzania anakosa uzalendo na kusifu US au UK-a developed country kuliko home for whatever reasons!

Mkiona vinaelea basi vimeundwa!

Karibuni sana nyumbani ndugu zangu..bado ni nyumbani kwenu tu ni sehemu ya historia

yetu!

Karibuni Supu tam ya Kuku wa Kienyeji, Kongoro safi na mengine mengi tu mazuri tele!

2. Tz imebadilika sana na opportunities kibao tu! Wako wengi wameishi nje mda mrefu na kurudi Bongo na kuwa challenged na makubwa peers wao walioyafanya kwa mda mfupi bila hata kuiba!

3. Maendeleo ni popote tu duniani..sema uskae ukadharua nyumbani na wazee na mila

zetu! Wazee husema "Mpanda ngazi hushuka"!
 
kweli nyumbani ni nyumbani, lakini tanzania nako MH!!!!!! Ufisadi mwingi. USA na Ulaya kuna unafuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…