Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,378
Yap nami namkumbuka sana huyu mwandishi pamoja na akina Sam Kitogo, S.M.Bawji, faraj Katalambula, Agolo Andulu. kwani na hammie rajab yu wapi?
Baadhi ya vitabu nilivyosoma vya waandishi hawa ni hivi
>Roho mkononi
>Awe hai au amekufa namtaka
>Nimekoma ukuwadi na shogayo hasidi
>Njama, Kikomo, Kikosi cha kisasi & kufa na kupona
>Simu ya Kifo
>Joto la fedha
ha ha ha ilikuwa raha kwakweli wakati ule.
Yap nami namkumbuka sana huyu mwandishi pamoja na akina Sam Kitogo, S.M.Bawji, faraj Katalambula, Agolo Andulu. kwani na hammie rajab yu wapi?
Baadhi ya vitabu nilivyosoma vya waandishi hawa ni hivi
>Roho mkononi
>Awe hai au amekufa namtaka
>Nimekoma ukuwadi na shogayo hasidi
>Njama, Kikomo, Kikosi cha kisasi & kufa na kupona
>Simu ya Kifo
>Joto la fedha
ha ha ha ilikuwa raha kwakweli wakati ule.
Hasa huyu wa maggazeti flani ya udaku... simpendi!Mkuu inasikitisha sana, maana waandishi wa leo wote ni copy and paste tu, hakuna uandishi tena.
Kuna mtunzi anaitwa anaitwa Hussein Tuwa.........Jamaa ni mzuri sana kwenye utunzi,anatunga Riwaya/Vitabu vitamu sana...
Binafsi nimebahatika kusoma Riwaya zake kama Mdunguaji,Mtuhumiwa,Mkimbizi,Mfadhili, Bondia na Utata wa 9/12.......Jamaa anatisha hasa
Hussein Tuwa, Ahsante sana kwa kunikumbusha huyo mtu. Pia nimebahatika kusoma hizo Riwaya zake zote, Bondia sikuimalizia aisee... ila aliishia kutoa kitabu cha "MKIMBIZI" tu hivyo vingine nilisoma kwenye gazeti tu. Sijui kuna tatizo gani na kijana Tuwa sijui kapotelea wapi, nilijaribu sana kumtafuta, akafunguaga na website........... ila dooo sijui vipi kijana, alisema anandaa MTUHUMIWA.
Mageziti ya MIA kipindi kile yalikuwa na riwaya nzuri sana, kuna riwaya nilisoma kidogo inaitwa "hazina iliyofichika" sijiu aliandika nani ila ni mtu ambaye nilimkubali.
Pia kuna mtu anaitwa Ephraim Kezirahabi (kama sijakosea) ameandika, Gamba la Nyoka, Nagona, Dunia Uwanja wa fujo (kwa ninavyovifahamu).
Basi mkuu, hivyo vitabu vyako Heka heka na hicho cha Kashfa, watafute wataalam wakutengenezee script, ili utoe movies basi, au wewe unaonaje?Uandishi haulipi niliwahi kujidanganya after being inspired nikaandika HEKAHEKA ,kashifa .hadithi zikatoka msanii miaka ya tisini malipo yakawa kidogo na sikupata mtu wa kunisponser nikaghairi.baadae nikaona nitest novel.nikaandika HÖTSOUP in the beginning.ni cha kijasusi kinahusu gulfwarone irag .nilikua bush skupata spönser miaka hyo ya tisini na tano.
Mwisho nkaandika HOTSOUP the aftermath hicho miaka 2005 after gulfwar two nikaishia chapter six nikawa nimepata ajira nikabullshit.
Kwa hapa bongo fani hailipi labda upublish na kuuzia majuu
Basi mkuu, hivyo vitabu vyako Heka heka na hicho cha Kashfa, watafute wataalam wakutengenezee script, ili utoe movies basi, au wewe unaonaje?
Poa mkuu, mambo mazuri hayataki haraka.wazo zuri ntalifanyia kazi mkuu sema nko remote area and a little bit busy kiasi siwezi kusafiri kwa sasa
Poa mkuu, mambo mazuri hayataki haraka.
Sasa hivyo vitabu vyako bado vinapatika?
Hapo zamani nilikuwa nasoma katika magazeti hadithi za kusisimua za Eddie Ganel. Pia ameandika kitabu, Ndoto Ya Mwendawazimu. Kuna mtu ambaye ana habari za huyu mwandishi?
Kuna hivi vitabu nilivipenda sana, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, mtunzi alikuwa Muhammed Said Abdulla a.k.a Bwana Msa
mkuu mimi nimevisoma mzimu wa watu wa kale na duniani kuna watu bado ni navyo nimevihifadhi...ningependa kupata hivyo vingine vya bwa msa, ni wapi vinauzwa?
Kuna hivi vitabu nilivipenda sana, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, mtunzi alikuwa Muhammed Said Abdulla a.k.a Bwana Msa
Vitabu vingine ni Asali Chungu, Dunia Mti Mkavu, Utengano, Kiza katika Nuru, Tata za Asumini, Babu Alipofufuka mtunzi alikuwa Said Ahmed Mohamed
Wapo wachache waliobakia kama huyu Farouk M. Topan mtunzi wa kitabu cha Mfalme Juha, vile vile Mzee wetu Adam Shafi Adam bado pia yupo hai.
Vipi kuhusu Eric James Shigongo? Mbona anaandika sana hadithi, je yeye siyo gwiji kuzidi akina Hammie Rajab, Ben Mtobwa na Eddie Ganzel? Kuna watu wanadai kuwa anatafsiri riwaya za watu wengine je ni riwaya zipi?
Eddie Ganzel, A. E. Musiba, Ben Mtobwa na Hammie Rajabu wameshatutoka. Je baada yao ni mtanzania gani aliyeweza tena kuandika vitabu vinavyovutia kusoma kiasi cha kumfanya msomaji kusisimka, au tuseme fani ya uaadishi wa tamithilia ndio umekiwsha kabisa. Niliwahi kuosoma tamithilia moja iliyoandikwa na Eric SHigongo nikapata kichefuchefu kabisa.