Daah, kweli Supreme Ndala Kasheba:
-Nakumbuka wimbo wa "Marashi ya Pemba.".
-Pia nakumbuka, wimbo wa 'yellow card'..huyo mzee alikuwa anajua kupiga 'gitaa' si mchezo.
Ndiye pekee aliyekua anatumia Gita lenye nyuzi 12. Nyimbo zake Kokola na Dezo dezo ziliigwa na Tshela Muana, alipo fuatilia haki zake huko Kinshasa watu walimzushia amekufa, akawajibu kwa kibao Dunia Msongamana na alipozushiwa kafa kwa mara ya pili akaimba Yellow card. Kwa kweli alikua ni Mwanamuziki Mahiri ambaye pia alisaidia sana kwa ukuaji wa Muziki hapa Nchini.
Nakumbuka wakati fulani kulikuwa na mashindano ya Top Ten Show alipiga lile gita lake la nyuzi 12, mwishoni akalivunja kwa kunogesha show na mwisho wa siku akashinda yeye.
Nakumbuka wakati fulani kulikuwa na mashindano ya Top Ten Show alipiga lile gita lake la nyuzi 12, mwishoni akalivunja kwa kunogesha show na mwisho wa siku akashinda yeye.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.