nilinunua tshirt kutoka ebay,gharama yake ilikua tsh 23,000+free shipping,baada yakufanya malipo nilikuta nimekatwa 40000 kwenye bank account yangu,mbaya zaidi email nlioitumia haikua na jina langu kamili(fake name).baada ya kama wiki 3 niliwasiliana na seller akaniambia mzigo ushafika ila nlikua nimesafiri,nilivyorudi (baada ya mwezi mmoja baada ya mzigo kufika) nlienda posta na namba ya mzigo ambayo nilipewa baada tu kufanya malipo ya mzigo,varangati lilianza kwenye kutoa kitambulisho chenye jina ambalo linaendana na email niliotumia kununua mzigo ambapo nilitumia fake name,kidogo nifungwe, amna mtu aliyenielewa pale posta,nilionekana kama mwizi baada ya varangati kubwa nikapewa mzigo,kiufupi quality ya mzigo(tshirt) ilikua mbaya sanaa sijawai kuivaa mpaka leo ipo kabatini.kwaushauri, kwa upande wa mavazi ni bora unununue hapa bongo ambapo unaweza kuikagua kwa umakini zaidi bidhaa yako kabla haujainunua,nimeangalia youtube watu walionunua mavazi online wanavyolalamikia low quality ya mavazi walionunua kwa gharama kubwa.and that's my ebay testimony
Sent using
Jamii Forums mobile app