Uchaguzi 2020 EAC: Uchaguzi Mkuu umefuata taratibu, hongereni Watanzania

Sep 8, 2020
67
133
Jopo la waangalizi 89 waliobobea kwenye masuala ya demokrasia kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) likiongozwa na Mhe. Silvestre Ntibantunganya limesema uchaguzi wa Tanzania umefuata utaratibu, hivyo watanzania wanatakiwa kuendelea kuimarisha amani iliyopo.

Wabobezi hao, wenye weledi na uzoefu wa hali ya juu wa kusimamia chaguzi mbalimbali ulimwenguni, wamesema mzunguko wote wa uchaguzi umeenda kwa njia huru iliyogubikwa na haki.

Wataalamu hao wamesema vyama vyote vimefanya kampeni kwa uhuru, wasimamizi wa uchaguzi wamelinda haki za wapiga kura, na wapiga kura wamepata haki yao bila kubughudhiwa.

Aidha, manguli hao wamevitaka vyama vya siasa kufuata Sheria iwapo havitaridhishwa, sio kuhamasisha uvunjifu wa amani.

Pamoja na hayo, waangalizi wamesema kwamba uchaguzi wa mwaka huu umekua na amani ya hali ya juu.

Chanzo: BBC
 
Jopo la waangalizi 89 waliobobea kwenye masuala ya demokrasia kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) likiongozwa na Mhe. Silvestre Ntibantunganya limesema uchaguzi wa Tanzania umefuata utaratibu, hivyo watanzania wanatakiwa kuendelea kuimarisha amani iliyopo.
Huyo mrundi, silvestre ntibantunganya anatetea tu mwenzie jiWE, ila ukweli ni kinyume kabisa
 
Back
Top Bottom