Taswira ya Mwanamke katika Riwaya ya Kezilahabi (1971) Rosa Mistika
Mwandishi Kezilahabi katika riwaya yake ya Rosa Mistika anamtumia Rosa kama mhusika mkuu wa riwaya yake. Ukuu wake umezawadiwa kwa kubeba jina la riwaya husika. Rosa katika riwaya hiyo anaoneshwa kuwa alizaliwa na kukulia kwenye mazingira ya kunyanyaswa na baba yake, mzee Zakaria. Aidha, mwandishi anasawiri maisha ya Rosa alipokuwa anasomo shule ya sekondari na pia alipokuwa katika Chuo cha Ualimu. Mwandishi ametuonesha katika kazi yake hii, jinsi Rosa alivyobahatika kwa mafanikio makubwa kuhitimu mafunzo yake ya ualimu na kuajiriwa kama mwalimu. Mwisho mwandishi anamsawiri Rosa katika picha ya kusikitisha. Kwa ujumla, kwa kumpitia Kezilahabi, tunamwona mwanamke akisawiriwa katika taswira zifuatazo:
Watu mmekuwa mnachanganya miaka nenda miaka rudi. Kitabu kilichofungiwa na serikali ni Kaptula la Marx na wala sio Rosa Mistika. Japo vyote mwandishi wake ni Euphrase Kezilahabi.