DW: Tishio la baa la njaa Nchini Kenya, Twiga wafa kwa kukosa chakula, zaidi ya robo tatu ya mifugo imekufa kwa kukosa chakula

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,282

Shirika la Habari la Deutsche Welle (DW) Limetoa taarifa ya ukame na tishio la njaa linaloikumba nchi ya Kenya. Katika taarifa hiyo, imeonyesha idadi kubwa ya Twiga waliokufa kwa sababu ya ukame uliosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Taarifa hiyo imesema pia mifugo mingi haina chakula na maji na zaidi ya robo tatu ya mifugo hiyo imekufa kutokana na ukosefu wa chakula. Ukame huo pia umesababisha ongezeko la watoto wanaodumaa kwa kukosa virutubisho vya kutosha. Aidha DW wamesema mvua isiponyesha hivi karibuni kuna uwezekano wa idadi ya watu milioni 28 kukosa chakula cha kutosha.

====

Pia unaweza kusoma zaidi taarifa kutoka The East African:

Takriban Wakenya milioni 2.8 katika kaunti 23 wanahitaji chakula cha msaada kwa dharura, serikali imesema. Ingawa maafisa walisema hakuna mtu aliyekufa kwa njaa kufikia sasa, ukame unaendelea kukumba maeneo mengi ya nchi. Msemaji wa serikali Cyrus Oguna mnamo Alhamisi alisema hili ni ongezeko kutoka kwa watu milioni 2.1 ambao walikuwa na njaa Septemba iliyopita.

Hata hivyo, ripoti ya Shirika la Kimataifa la Oxfam iliyotolewa wiki jana ilionyesha kuwa idadi ya watu walioathiriwa inaweza kufikia milioni 3.1. Miongoni mwa kaunti zilizoathiriwa ni pamoja na Baringo, Isiolo, Mandera, Marsabit, Samburu, Turkana, Wajir, Kilifi, Lamu, Nyeri, Pokot Magharibi, Laikipia na Garissa, ambazo ziko katika hali mbaya ya ukame.

Hali inazidi kuwa mbaya katika maeneo ya Makueni, Taita Taveta na Tana River, huku kwa Embu, Kajiado na Narok, hali ni shwari. Meru na Tharaka Nithi wako katika hatua ya tahadhari, huku hali ikiimarika katika kaunti za Kitui na Kwale.

Chanzo: The East African
 
tuna wakaribisha ngorongoro mje mfuge ng'ombe... pia mjifunze jinsi ya kuishi na wanyama... >.<Ni utani ndg zangu

sehemu kubwa ya kenya ni jangwa au kame ina eleweka vyema, sehemu zilizo barikiwa ni huku wanapo pakana na tanzania kuanzia kisumu mpaka tsavo na mombasa...
 
Back
Top Bottom