DvD ya matukio ya kisiasa Arusha ipo mtaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DvD ya matukio ya kisiasa Arusha ipo mtaani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PakaJimmy, Mar 3, 2011.

 1. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wakuu,
  Leo nimefanikiwa kutazama kwa kifupi DVD ya matukio ya kisiasa na Mauaji ya Arusha, ikiwa imeandaliwa katika mfumo wa Documentary..

  Sijafanikiwa kuwajua walioandaa, lakini ni kwamba ilikuwa inagombaniwa sana na wanunuzi, mimi nimekosa nakala, nikalazimika kuazima kwa jamaa yangu ili niitazame kidogo...Inaleta hisia za aina yake.

  DVD hiyo inakwenda kwa jina UKIUKWAJI WA DEMOKRASIA, na imenakshiwa kwa bendera ya Taifa kwa juu, na inatembea kwa muda wa dakika 32.

  Sina uhakika kama ndiyo iliyoandaliwa na cdm, au ni wajasiriamali wa mitaani. Tulijaribu kuifanyia utundu tuiweke hapa, lakini imedhibitiwa, haikubali kukopiwa.

  DVD ndiyo hii


  na hii
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Paka Jimmy,
  Ulizia inauzwa kiasi gani. Tuko tayari kuinunua.
   
 3. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wapi huko inapopatikana?mz au ar au dar?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inauzwa tshs 6000/- tu...
  Ni ya ukweli mkuu!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inapatikana Arusha mkuu wetu.
  Naamini kuwa itasambaa kwa haraka sana kote mikoani!
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ukiitazama hakika utaona jinsi mapolisi wasivyoelewa uwepo wa chama zaid ya ccm!...Wamepofuka macho kabisa hawajui kuwa kuna kesho.

  Hapa Arusha kuna polisi aliuwawa 2 weeks ago, na baadhi ya watu wana'associate mauaji ya polisi huyo na matendo ya 5/1/2010...Inasemekana watu walii'note sura yake jinsi alivyokuwa anatoa kipigo kwa raia wakati wa maandamano.
   
 7. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hofu yangu ni 'silent' censorship...inaweza kuwa cencored kimya kimya sana wakuu kabla haijasambaa, walioitengeneza na kuisambaza sijui wamejipangaje kuhakikisha wanakwepa hilo...

  Mnakumbuka mwishoni mwa mwaka jana RAI waliandika stori fulani kuhusu namna Spika Sitta alivyokuwa karibu ahame CCM kwenda CHADEMA, lakini alipomfuata Rais Dkt. Slaa akamshauri haukuwa wakati mwafaka na isingesaidia pande zote, iwe kwake yeye hata CHADEMA...copies kibao sana zililinunuliwa mapeeeeeeeeema na 'wazee wa kazi wa mavazi meusi na miwani' ili zisisambae, KISA! Ilikuwa inampatia ujiko mkubwa Rais Dkt. Slaa na kuongeza ushawishi wa maamuzi yake ya busara mbele ya jamii.

  DvD hiyo bila shaka yoyote itakuwa kwa namna moja inaongeza ushawishi wa CDM na Rais Slaa kwa kiasi kikubwa, KAMA NAYO HAIJACHAKACHULIWA LKN, 4 ANY SELF INTEREST...just angalizo tu, maana...
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wapo wataalamu wa ICT humu jamvini nadhani watusaidie kukopi ili iwekwe humu na Youtube
   
 9. n

  nyantella JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ama kweli kufa kufaana! kama ni ukiukwaji wa demokrasia si ingetolewa bure?? sh. 6000/= ndugu wa marehemu wametoa kibali cha kutumia vifo vya ndugu zao au watapata mgao? If you ask me huyo aliyetengeneza hizo CD ni wa kufunga. Kumbe kuna agenda ya kibiashara katika hizi vurugu? That is what they call blood money !!!!!!!!!!!!! hazitamsaidia muuzaji Shame on you all. I hope uongozi wa CDM hauhusiki na hii biashara haramu!!!
   
 10. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini 6000 nadhani ni recovery cost ya media - DVD
   
 11. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Usiwe na wasiwasi mkuu. Ikipatikana copy moja tu itaenezwa dunia nzima within a minute. Subiri niipate.
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  wewe lazima sio mchaga, yaani unataka chama cha nyumbani kichakachuliwe mapato yake? tutaziuza hadi kopi ya mwisho mangi kama huna hela subiri kwanza turudishe pesa etu.
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unapenda sana bure..... EURO 3 zinakupa sana shida? Watu wametumia umeme, computer zao na camera kibao, muda wao na kutengeneza film na mwisho kuwa na ma-cover na picha ya cover juu. Bado wewe unaona ni hela nyingi na unataka WAKUPE BURE?

  Mkono mtupu haulambwi mkuu. Watu tunanunua CD original kwa Euro 15 au dola 20 kwa kuagiza kutoka nje na hapo weka na usafiri. Tujifunze kusaidia (ukiangalia bei) na si kufikiri jamaa watakuwa matajiri kwa hiyo bei.

  Hiyo bei ni bei ya kurudisha hela zao na si blood money. Wakiuza 100 wanapata laki 6 na kumbuka kuwa USALAMA WA TAIFA watakuwa nao sambamba na hivyo huwezi kuwa nazo nyingi. Na mwisho ni kwamba, hiyo ni bei ya kuuzia (muuzaji apate kifaida). Je watengenezaji kweli watatajirika kwa pesa hiyo kidogo inayopatikana? Tusiwe wepesi wa kushambulia kuwa fulani katajirika. Ungelikuwa wewe si ajabu ungelituuzia kwa bei ya 15,000.
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  dvd hiyo itakuwa ya uwongo
   
 15. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aminia mkuu.
   
 16. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  hawawezi kuizuia au wameshachelewa; kuna rafiki yangu yuko karagwe, about three days ago aliiona maeneo ya sokoni kayanga, laki aliyekuwa nayo ni mwoga. niliahidi nikiipata natengeneza 20 copies free na kuzisambaza.
   
 17. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ukweli unabaki palepale kwamba ni vigumu mno kukidanganya kizazi hiki cha .com Ukweli huu ndiyo unafafanua kwa nini CCM iliyobweteka kwa miango kadhaa bila ya kufanya mabadiliko ina wakati mgumu sasa kuliko wakati wowote tangu iasisiwe. Mimi sijaiona (Lakini nitaitafuta) ila naona uongo wa Saidi Mwema, Chagonja na Pinda unakaribia mwisho wake. Hongereni kizazi kipya!!!! Tanzania itakombolewa na ninyi.
   
 18. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kwa mtindo huo mbona ungefunga wote na wewe ukiwemo?
   
 19. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Acha unafiki. Na kina Mwema na Chagonja walipotoa ya kuwadhalilisha waliojeruhiwa na kuuwawa tuwashtaki wapi? Tena yao ilikuwa ya kupotosha kwelikweli. Sisi tinaitaka ili tupime ukweli uko wapi na nina uhakika wananchi wakiona jinsi mlivyopotosha hawatawaamini tena nyinyi na huyo mdudu wenu mnayemwita CCM.
   
 20. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mkuu hilo umelijua leo kwani? Ebu ona hii katuni,iko gazti la mtanzania la leo.Hilo halikwepeki mkuu,lazima watu wafaidike pale wenzao wanapoumia.
  [​IMG]
  [​IMG] kufa kufaana.jpg
   
Loading...