YoungCorporate
JF-Expert Member
- Apr 30, 2010
- 391
- 116
habari za leo wanajamii, mashabiki wa man u poleni kwa kipigo toka imarati...
Kwa wadau wanaofuatilia dv lottery 2012 matokeo yameshatoka leo May1, nilitaka kuuliza kuna yeyote humu amepenya jamani?? Au kuna ambaye amewahi kupata dv lottery (nazungimzia ile yenyewe inayotolewa na state department sio phishy agents) hii anisaidie maujanja pamoja na docs za kuwa nazo ikiwa umechaguliwa??
Sidhani kama kuna ujanja wowote ni bahati ya mtu tu. Na nawafahamu baadhi ya Wabongo waliobahatika kuchaguliwa katika bahati nasibu hii. Ila ni vizuri kukamilisha taratibu zote mapema badala ya kusubiri mpaka dakika za mwisho ambapo inakuwa ni kazi ngumu mno kutuma maombi. Unaweza ukapoteza masaa chungu nzima katika jitihada za kutuma maombi yako bila mafanikio yoyote.
mkuu nashukuru labda nifanunue kidogo, ile stage ya kutuma maombi online ilishapita sasa nimechaguliwa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa interview na masuala mengine sasa ndio nilitaka kujua kama kuna mzoefu aliepata miaka ya karibuni anipe details, ni kipi hasa wanahitaji?
Duuuu...siamini. Nimepata dv lottery!!!!!!
mkuu nashukuru labda nifanunue kidogo, ile stage ya kutuma maombi online ilishapita sasa nimechaguliwa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa interview na masuala mengine sasa ndio nilitaka kujua kama kuna mzoefu aliepata miaka ya karibuni anipe details, ni kipi hasa wanahitaji?
Kwanza utapata barua ya kukujulisha kuwa iko miongoni mwa waliochaguliwa kwenye DV loterry hiyo.
Kisha utatatakiwa kujaza form ambayo state dept watakutumia ili kudhibitisha kwamba unakubali au unaafiki ili hatua nyingine zifuate.
ukisha wajibu kuwa umekubali kisha watakutumia form za kujieleza wewe na familia yako yote yaani familia yako kama umeoa,wazazi wako wote.
utaeleza umewahi kuishi wapi miaka 10 iliyopita hiyo ni pamoja na shule,nchi ulizowahi kuishi.
Watahitaji nakala ya kila cheti ambacho utaelezea kuwa nacho,km.vyeti vya shule, kuzaliwa kama unavyo au affidavits zozote utakazo kuwa nazo.
Utatakiwa kupima afya yako kwa daktari watakaye kuelekeza wao na huyo akisha kamilisha vipimo atakupa majibu yako na bahasha ambayo iko sealed kwa ajili ya kuwatumia.Itakuchukua muda kias kwamba unaweza ukadhani hiyo kitu haipo watakuwa wanafuatilia taarifa ulizowapa.Endapo kuna kitu wanataka watawasiliana nawewe moja kwa moja.Kama kila kitu ulichowapa kiko kamili watakujulisha siku ya kwenda kwenye enterview na mahali. Kwa wale ambao wako USA unaweza kuadjust stutus yako au kuomba viza ya migrant.
Gharama ni kubwa kidogo kuliko viza ya kawaida hivyo jiandae kwa hilo.
Hayo ni maelezo kwa kifupi form zenyewe zinajieleza, na hawana usumbufu wowote.
kumbuka siku ya enterview kwenda na nakala halisi ya kila document uliyowatumia kwani watahitaji kuziona nakala halisi na watataka nakala hizo tena kwani zile za mwanzo zilikuwa kwa ajili ya state dept na hizo za sasa ni za uhamiaji(consular office).
mkuu shukrani sana kwa maelezo yaliyonyooka, hiyo barua ya kuniarifu nimeshinda nimeipata na wameandika niiretain, sasa sijui hizo form zinatumwa kwa posta au online? Na pia unakadiria itachukua muda gani toka kupata barua ya kuchaguliwa na kuitwa kwenye interview? Na pia wastani wa gharama ni kiasi gani mm nipo tanzania. Na je kwa uzoefu wako ni visa category gani ambayo ni nzuri kwa mm ambaye natarajia kwenda kuongeza nondo na kupiga boksi la uhalali? Natanguliza shukrani

Wakuu Heshima mbele kuuliza si ujinga , Ila ujinga wakati wa kwenda . Je na mimi naweza kujiunga online nikajaza Greencard ili na mimi nichaguliwe??? Au Mkuu unafanyaje hapo???
Naomba nikupe tahadhali hivi karibuni nilikuwa bongo na mtu mmoja akapata email ya kitapeli ikimujulisha kuwa amewin green card, sasa angalia kuna matapeli. Forms hizo zitatumwa kwako kutoka state dept zina (bar code).
Kumbuka hakuna malipo yoyote ambayo utatakiwa kuyafanya mpaka siku ya kuitwa ubalozini kwakuwa uko Tanzania.
Na hiyo itakuwa baada ya kukamilisha hatua zote hizo ambazo si chini ya miezi 6(napo sema miezi sita mara nyingi ni zaidi ya hiyo miezi) kwa maana taarifa zako zote na historia yako maafisa wa FBI na makachelo wengine wa kimarekani watazifanyia kazi wakisha kuclear kwamba siyo jambazi au huna matatizo yoyote ya kiafya n.k ndipo watakapo kujulisha tarehe na saa ya interview hapo ubalozini.
Siku ya interview huna maelezo mengi wanachotaka ni kukuona physically maana kumbuka muda wote utakuwa umekuwa unawasiliana nao kwa makaratasi na picha tu,hivyo wanachofanya siku hiyo nikukagua document's ulizowatumia na original copies ulizo nazo.Hivyo mpaka kufikia hatua hiyo huwa kuna miezi kadha. Jitahidi kuwa mkweli maana hawa jamaa watafika mpaka kijijini kwako(Kufanya Vetting).
Huchagui aina ya visa/viza kwani hiyo greencard or DV lottery Visa inajieleza, ni visa inayokupa status ya kuwa mkazi wa marekani(permanent residence),ambapo unakuwa na haki zote za raia wa Marekani isipokuwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa ngazi za kitaifa(federal).
Hivyo na sisitiza kama una barua hiyo na huna uhakika nayo nenda Ubalozi wa marekani uthibitishe kwani kuna utapeli umeenea hasa kwa kuzingatia kuwa watu wengi ni wageni kwenye swala hili, usimtumie mtu malipo yoyote malipo yanalipwa siku ya interview ambayo haifanyiwi mahala popote zaidi ya ubalozini.
Hiyo green card ni visa category na huwezi kubadilisha inaitwa DV visa na ukija wapewa green card inayokupa uwezo wa kufanya hayo yote uliyoyataje legally. Fomu utapata kwa posta kwa adress uliyopatia barua inweza kuja baada ya miezi 4 hivi zipo online pia unaweza kuzicheck uzifahamu but hushauriwi kuzijaza kwa vile wanavytuma wanakuwa wametoa na visa allocation namba. Ukijaza na kurudisa utasubiri tena kama miezi mi 4 mingine then itakuja barua nyingine kukupa visa interview appointment ubalozini hapa ndo utaenda na vyeti vyako original na copy, kwenye fomu hakuna vyeti unavyotuma bado kumbuka hapo watauliza level ya elimu yako na historia na familia dependants unaotegemea kuondoka nao au watakaokufuata kwa kutumia visa yako baadaye.
Gharama mwaka 2009 ilikuwa $750 kwa kila kichwa sidhani kama imeshuka zaidi itakuwa imepanda tu! Unaruhusiwa kuondoka na familia yako yote yaani mke watoto na dependants wako wote wanaokutegemea walio chini ya 18 yrs ambayo ni single. So jiandae wanapokea $ na madafu pia kwa thamani hiyo siku ya interview. Hamna maswali ya kusumbua ila ni kujustify tu vyeti na familia yako
Kwa ujumla itakuchukua kama mwaka hivi kumaliza process na kupata Visa ya kuingia US na pia utapewa 6 months uwe umesafiri. Kingine muhimu uwe na contact ya mtu anayekufahamu ambaye atatakiwa kusign affidavit form ya kukupokea na kukuguide usijekuwa public charge and anatakiwa aonyeshe uwezo wa kifedha kukuhudumia kwa miezi michache.
mkuu mbona naona kama maelekezo yanataka nijaze ile ya online tena wanasuggest mapema iwezekanavyo coz wanataka by sept 30 this yr iwe tayrai nimeitwa kwenye interview?? Au mm sijaelewa?? Hapo kwenye mwenyeji ndio nina tatizo sina mtu ninayemfahamu aliopo US, je nitumie skills gani?? Pia nina elimu ya chuo lakini mpaka sasa sijafuatalia cheti coz nilipata kazi baada ya kumaliza so sikufuatalia tena na ninajua itachukua muda, je naweza kusbmit zile result slips tu then vyeti halisi nikatumia vya 4 na 6, mm natumia category ya education kama eligibility?
Kwanza utapata barua ya kukujulisha kuwa iko miongoni mwa waliochaguliwa kwenye DV loterry hiyo.
Kisha utatatakiwa kujaza form ambayo state dept watakutumia ili kudhibitisha kwamba unakubali au unaafiki ili hatua nyingine zifuate.
ukisha wajibu kuwa umekubali kisha watakutumia form za kujieleza wewe na familia yako yote yaani familia yako kama umeoa,wazazi wako wote.
utaeleza umewahi kuishi wapi miaka 10 iliyopita hiyo ni pamoja na shule,nchi ulizowahi kuishi.
Watahitaji nakala ya kila cheti ambacho utaelezea kuwa nacho,km.vyeti vya shule, kuzaliwa kama unavyo au affidavits zozote utakazo kuwa nazo.
Utatakiwa kupima afya yako kwa daktari watakaye kuelekeza wao na huyo akisha kamilisha vipimo atakupa majibu yako na bahasha ambayo iko sealed kwa ajili ya kuwatumia.Itakuchukua muda kias kwamba unaweza ukadhani hiyo kitu haipo watakuwa wanafuatilia taarifa ulizowapa.Endapo kuna kitu wanataka watawasiliana nawewe moja kwa moja.Kama kila kitu ulichowapa kiko kamili watakujulisha siku ya kwenda kwenye enterview na mahali. Kwa wale ambao wako USA unaweza kuadjust stutus yako au kuomba viza ya migrant.
Gharama ni kubwa kidogo kuliko viza ya kawaida hivyo jiandae kwa hilo.
Hayo ni maelezo kwa kifupi form zenyewe zinajieleza, na hawana usumbufu wowote.
kumbuka siku ya enterview kwenda na nakala halisi ya kila document uliyowatumia kwani watahitaji kuziona nakala halisi na watataka nakala hizo tena kwani zile za mwanzo zilikuwa kwa ajili ya state dept na hizo za sasa ni za uhamiaji(consular office).
mkuu thanks again, hii ninyozungumzia ni dv halisi inayotolewa na state department katika website ya dvlottery.state.gov barua ina bar code na pia namna ya kuipata ni baada ya kujaza info za wakati wa kuapply kama umewahi kushiriki dv nadhani unaelewa. Nimeona kwenye ile barua maelezo zaidi yanapatikana dvselectee.state.gov ambapo pia zile form za kentuck zipo ambapo natakiwa kuzijaza na kuzituma, sasa kuna clause moja kwenye form yataka nijaze mwenyeji wangu US adress yake na simu lakini mm sina mtu wa karibu alie US hapo nafanyeje?
Kuhusu pesa ni kweli wamesema ni pesa ya viza kawaida nitalipia ubalozini ambapo kwa category ya dv ni kama usd 420 hilo sio tatizo kwangu, pia kwenye form wanahitaji nijaze mji ninanotarajia kwa perm residedc, sijawahi kufika us sina idea, je mkuu unakauzoefu na amerika unipe ideas?
Mambo mengine ni ya kawaida kama vyeti pasip
Ni kweli mara nyingi wanapenda uwe na mwenyeji wa kukupokea.Kwa sababu wanategemea kuwa mara unapoingia USA utahitaji mahali pa kuishi, na kuna hatua nyinginezo za kufanya kama kupata namba ya Social Security ambayo bila kuwa na namba hiyo ni vigumu kufanya jambo lolote hasa kupata kazi, kufungua account ya banki, kupata leseni ya udereva na mambo mengi. Kwa hiyo katika kipindi hicho unapokiwa kwenye hatua hiyo unahitaji mwenyeji.
Huyo mwenyeji ukimpata atakuandikia barua ambayo utakwenda nayo ubalozini siku ya interview ni kama mdhamini wako, nasema hivyo kwa kuwa nisha dhamini watu wawili ambao nao walipata green card zao wakiwa huko nyumbani, na nilijitahidi kuwaelezea kila hatua kwani na mimi nilibahatika kupata hiyo card.Labda ni kuambie kuwa ni gharama kidogo lakini utaona matunda yake ndugu yangu, kwa hiyo kazana na usichelewe kwani mko wengi na watachujwa kutoka watu 100,000 waliopewa barua kama yako hadi 55,000 tu.