Usimsaliti rafiki yako mkomeshe huyo shemeji yako kwa kumuita mchumba wako hapo nyumbani umtambulishe kuwa ni mke wa rafiki yako kapitia kuwasalimia so unataka wafahamiane naamini atakuaga tu hawezi kulala hapo na umlazimishe mchumba ako abaki mlale wote ataona sasa njama zake zimekufa
Ndugu yangu umesh,nashindwa kuamini kilichotokea kwa kweli,hata hivyo namshukuru Mungu wangu kwa kweli!!!Enheee! Enheee! Enheee! Enheee! Enheee! Enheee!
Bahati yako. Ungeisoma namba. unafikiri mchezo. Dunia hadaa, ulimwengu shujaa. Chezea HIV +++ wewe. Du!
Huu ushauri naunga mkono moja kwa mojaFanya kitendo ambacho kitamfanya rafiki yako awe proud na wewe wanawake wapo tunza heshima ya rafiki yako fanya maamuzi magumu ili hata siku za mbeleni ujiproud mwenyewe kwa maamuzi ya msingi na busara. Mwokoe rafiki yako
Ebwanaaaee kama shemeji yupo mwelekeze kwangu, mama watotot kasafiriMrejesho pls..maama isue ilikuwa ya jana hii
Lete mrejesho tumetoa ushauri wetu toka jana au ili kuwa hadithi?Haujajua tu situation ilivyokuwa,afu sikuwahi kufikiria kama angekuwa wa aina hii,that's why sikushtuka kabisa,kwanza nlijua anasafari nyingine na sio rasmi kuja kwangu,the way alivyo kwanza sikufikiria kabisa kama mwisho wa siku angekuwa mnyama namna hii!!!
I'll be the last to comment baada ya mrejesho
Nimeshaeleza kilichotokea ndugu yangu,soma page za nyuma hapo utajua kilichotokea,kwa sasa sina hata mood njema,mwili mzima unatetemeka!!!Lete mrejesho tumetoa ushauri wetu toka jana au ili kuwa hadithi?
(1)nini kilitokea baada ya wewe kwenda kulala hoteli?
(2)uliporudi asubuhi ulimkuta nyumbani?alijisikiaje?
(3)mpaka mda huu bado yuko nyumbani?au kaondoka?mwisho rafiki yako umemwambia?
Niishie hapo kwanza .
Unatetemeka nini,wewe kwanini usimkaushie alivyofika moro wakati alikua hapajui kwako na unajua alichokifata....Nimeshaeleza kilichotokea ndugu yangu,soma page za nyuma hapo utajua kilichotokea,kwa sasa sina hata mood njema,mwili mzima unatetemeka!!!
Hakika kwa hili wewe ni zaidi ya rafiki,umenisaidia sana!Karibu rafiki angu na pole na majanga pia namshkuru Mungu kwa ajili yako kwa namna ulivyookoka na mimi kua sehemu ya ushindi wako
fanya ku-capture hiyo text utuwekee hapa kama uthibitishoNdugu zanguni,namshukuru sana,lakini pia nawashukuruni ninyi wadau mbali mbali kwa kunishauri katika hili,kipekee nimshukuru rafiki yangu karena,alinitia moyo na kuniongezea ujasiri ktk kuikabili hali ambayo sikuitegemea.
Hakika asubuhi hii nimefika nyumbani,sijamkuta mchumba wa rafiki yangu.
Nimeshtuka kwa mambo mawili ambayo kwa kweli sijui namna ya kuyakabili.
1.Jamaa yangu amenipigia simu asubuhi sana,anaonekana kupoa sanaaaa,kitu ambacho sio kawaida yake kabisa,(sijui amepata habari gani juu ya hii issue).
Mbaya zaidi ni ujumbe alionitumia huyu shemeji yangu,umenifanya nichanganyikiwe zaidi,naomba ninukuu ujumbe wake,then mniambie nini nifanye jamani,naomba mnivumilie tu ndugu zangu,
"Bahati yako we mwanaume,kutoka moyoni nawachukia sana wanaume,mwambie na rafiki yako,kwa maisha yangu ya sasa nalipa kisasi kwa mtu yeyote anaitwa mwanaume,I'M HIV POSITIVE,umenusurika but your friend unknowingly is already positive,mshukuru Mungu wako mshenzi wewe"
Nimeishiwa pozi kwa kwelinashindwa kuamini shemeji yangu mpole na mkarimu kweli kweli awezakuwa mnyama kiasi hiki.
Kinachoniumiza ni juu ya rafiki yangu,je,anajua hali hii??,nimwambie kilichotokea??au nimnyamazie tu??
Hakika duniani tunayo dhiki juu,daaah!!!