Duuuh, kweli wanawake wengine!

Mkuu me cna cha kucomment ila nasubiri mrejesho tu kesho asubuhi..
 
Bora umenisaidia aisee,SITAKI KABISA KUMSALITI RAFIKI YANGU,naona muda unazidi kwenda,shemeji yangu amesinzia hapa kwenye kochi,na mimi sijapata kujua haswa nifanye nini,jamani nikienda kulala hotelini nikamuacha hapa,yaweza kuleta madhara hasi??
Vipi ukienda lala hotelini demu akaona anaumbuka akafanya kitu kibaya kwako kama vile kunywa sumu
 
 
Vipi ukienda lala hotelini demu akaona anaumbuka akafanya kitu kibaya kwako kama vile kunywa sumu
Kufa sio kazi rahisi aisee,naamini hawezi kujiua akiwa nyumbani kwangu,MUNGU NA AEPUSHIE MBALI,nipo zangu hotelini,nimemuacha nyumbani!!!
 
Haiwezekani ke mwenye mtu wake aende kwa shemeji yake bila sababu maalum tena bila mchumba wake kujua. Dalili zilishaonyesha hana lengo zuri ulitakiwa ukate mawasiliano mapema kabla hajafika kwako. Imagine huyo jamaa yake amfanyie suprise aende dom wewe utajielezaje??
Na huyo mchumba wako nae akija atakuelewa?? Mwambie asipoondoka unampigia jamaa yake na usifute hizo msg kama ushahidi
 
Fanya kitendo ambacho kitamfanya rafiki yako awe proud na wewe wanawake wapo tunza heshima ya rafiki yako fanya maamuzi magumu ili hata siku za mbeleni ujiproud mwenyewe kwa maamuzi ya msingi na busara. Mwokoe rafiki yako
Nimependa majibu yako. Safi sana
 
Lala tu kwako kwa Amani ila usimle maana ndo itakuwa anataka kila siku , na wala hataondoka na sijui utamjibu nini huyo rafiki yako endapo utajikuta umemla, just be a man and let no temptation come to your way....
 
Uliruhusu akuzoee sana na hayo ndo matunda yake.
 
Ndugu yangu kusema ukweli,nashindwa kumwambia jamaa coz anaweza asiamini ntakachomwambia,jamaa anamwamini sana msichana wake,awezafikiri kuwa nawagombanisha tu,nathamini urafiki wetu,sipendi kugombana naye kabisa!!!
Sms ulizochat nae ndo ushahidi wako, sasa kama na wewe ulikua unamchombeza huko kwenye msg ndo utaisoma number Lol
 
Mfukuze haraka sana tena mapema
Acha mazoea mabaya na shemeji yako
Yan apo miss chagga lazima tu kuna vijimazoea ambavyo walikuwa wamewekeana ivi kweli mtu afunge tu safar jaman mmh sijui kwakweli kwanza mimi nilivyo siwapendi mashemeji wanafiki sana hata ayo mazoea siwezi kujenga
 
Kila mtu amemsema mdada wa watu okey ana makosa ila kwangu wote wana makosa,,wewe shemeji itakuwa tu kuna mazingira ambayo mlijengeana hadi mkafikia apo kwa hali ya kawaida siyo rahisi kabsa akufungie safar iv iv tu tena bila woga wa kuwa unaweza kumwambia bf wake au yeye anaweza kumkuta gf wako, wanaume acheni tabia ya kupenda kuentertain watoto wa kike aya ndo mazara yake,
 
Ndugu zanguni,namshukuru sana,lakini pia nawashukuruni ninyi wadau mbali mbali kwa kunishauri katika hili,kipekee nimshukuru rafiki yangu karena,alinitia moyo na kuniongezea ujasiri ktk kuikabili hali ambayo sikuitegemea.
Hakika asubuhi hii nimefika nyumbani,sijamkuta mchumba wa rafiki yangu.
Nimeshtuka kwa mambo mawili ambayo kwa kweli sijui namna ya kuyakabili.
1.Jamaa yangu amenipigia simu asubuhi sana,anaonekana kupoa sanaaaa,kitu ambacho sio kawaida yake kabisa,(sijui amepata habari gani juu ya hii issue).
Mbaya zaidi ni ujumbe alionitumia huyu shemeji yangu,umenifanya nichanganyikiwe zaidi,naomba ninukuu ujumbe wake,then mniambie nini nifanye jamani,naomba mnivumilie tu ndugu zangu,
"Bahati yako we mwanaume,kutoka moyoni nawachukia sana wanaume,mwambie na rafiki yako,kwa maisha yangu ya sasa nalipa kisasi kwa mtu yeyote anaitwa mwanaume,I'M HIV POSITIVE,umenusurika but your friend unknowingly is already positive,mshukuru Mungu wako mshenzi wewe"
Nimeishiwa pozi kwa kwelinashindwa kuamini shemeji yangu mpole na mkarimu kweli kweli awezakuwa mnyama kiasi hiki.
Kinachoniumiza ni juu ya rafiki yangu,je,anajua hali hii??,nimwambie kilichotokea??au nimnyamazie tu??
Hakika duniani tunayo dhiki juu,daaah!!!
 
Mrejesho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…