Duu,wanawake wa mjini noooomaaaaaa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duu,wanawake wa mjini noooomaaaaaa!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mchajikobe, Jun 30, 2012.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Leo wakati natoka kwenye mihangaiko yangu,kama kawaida barabara za mjini zinauhusiano mzuri sana na foleni,wakati tupo kwenye foleni kuna gari kama latatu mbele yetu lilikuwa limezimika katikati ya barabara,aliyekuwa anaendesha gari hiyo ni binti mmoja mrembo,bila kuomba msaada alibaki ndani ya gari na kuanza kupiga simu,hata hivyo kulikuwa hamna usumbufu kwetu kwasababu hata hiyo foleni ilikuwa haisogei,mara wakatokea vijana wawili wakaja kuisukuma ile gari ili kuiweka pembezoni mwa barabara,yule dada hakutoa shukrani wala kuongea nao chochote,zaidi ya kuendelea kupiga simu tuu,wale vijana walipoondoka yule dada akashuka akiwa ametilia kimini cha hatari na kufungua boneti kisha kufunga bila kufanya chochote,akaingia tena ndani ya gari na kuendelea kupiga simu.Mara ikatokea AUDI nyeusi akashuka mwanaume mmoja mtanashati mkononi anagalon la mafuta la lita tano wakaweka yale mafuta kisha yule dada akaiwasha ile gari kama anataka kuondoka na yule jamaa ambaye alionekana kama ni mume au mpenzi wake akaondoka,lakini cha kushangaza nikwamba yule mwanamke alilizima gari nakuendeleaa kukaa pale pale,haukupita muda mrefu ikaja prado akashuka mwanaume mwingine huku akiwa amebeba galon kama yule wa mara ya kwanza,yule mwanamke akafanya vilevile,jamaa akaondoka mwanamke akazima gari na kuendelea kubaki hapo hapo,kitu ambacho kilinishangaza ni kwamba lilikuja Mercedes benzi na mbaba mmoja naye akashuka na galon ya mafuta akamuongezea kisha akampa yule mwanamke kitu mkononi bila shaka ni hela kisha jamaa akaondoka,na yule dada naye akaingia ndani ya gari na kuondoka,hii ni kitu iliyotokea jioni ya leo maeneo ya kinondoni karibu na Hugo Bar!!Sasa huyu mwanamke inaelekea muda wote aliokuwa anaongea na simu alikuwa anamdanganya mmoja mmoja kuwa ameishiwa mafuta mpaka mwisho ametoka na lita kumi na tano,duu wanawake wa mjini hawafai,na unaweza kukuta hapo alikuwa na appointment na mwanaume mwingine!!!!
   
 2. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  duh ipo siku watashuka wote wakati mmoja akicheza hiyo gemu ya kutojaza mafuta ya kutosha.
   
 3. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hapa ndio mjini....ukijifanya unajua kupenda watu wanakutizama tu...uyo mchuchu unakuta kuna mbishi wa town anatafuna free mandela.
   
 4. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Wanawake wangekuwa kama wanaume sijui ingekuaje ile tabia ya kutongoza mpaka miaka 60, uzuri wao hapo alipo na kimini chake atazila za hao majamaa ila baada ya miaka kama mitano mbele kama asipou-control mwili wake na thamani yake inashuka hata wa kumwekea lita 2 atakosekana.
   
 5. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,638
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu hapo anachukua mzigo kiulaini with no cost na viwanja vyote wanakwenda hana zaidi ya neno nakupenda na kumsaidia kubeba handbag na kumsifia hapa na pale bila kusahau kumpigia simu mara kwa mara wakati wengine wanazama kwenye ATM kila kukicha lakini ndio hivyo mifuko imetofautiana maana unaweza kukuta mtu amehonga nyumba ukamcheka kumbe mwenzako ametoa asilimia 3 ya kipato chake na yule aliyeonga laki moja ukaona ndogo kumbe ametoa 80% ya kipato chake cha siku 20 hapo kimahesabu alietoa nyingi ni wa laki moja maana ana kazi ya ziada kutafuta hela ya kufidia.
   
 6. g

  gpluse JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 80
  Kwani we bado wadanganyika na hao malaya? Pole!!!
   
 7. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Story ya kutunga! "..magari hayasogei,.. kuikaja Aud..ikaja prado..ikaja benz.." ungeniambia ulikua nje ya folen unashuhudia angalau kidogo ungeeleweka japo nayo ingetia shaka kwani kwa hali halisi ya folen ya dar, kuwaita watu 3 toka sehemu tofauti wakaja inachukua muda mrefu
   
 8. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hata kama ya kutunga....ni uongo mtamu sana...

  Na hizi tabia ni kweli kabisa wanawake wa dar town wanazo
   
 9. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,355
  Likes Received: 2,360
  Trophy Points: 280
  Wenye mioyo ya kupenda kweli mbona karne hii hatuponi.Daaa.... Hapa bongo usiombe demu wako awe mweupe alfu angalau awe mrefu hata kidogo uone waleta mafuta watavyokuwa wengi.
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Tutafika, nakubaliana na wewe! Sasa kupiga mzinga 5lts za petrol mtu anaendesha audi? Haiingii akilini aisee! Manake sms tu ya 'darling nimeishiwa, sijui hata kama mafuta yatanifikisha home' ingetosha kuhusisha mpesa (kwa yule mwenye suzuki) ama sms banking kwa wenye audi na prado,lol!

  Mnatafuta kutusakama tu! Hata sie tunahonga wapenzi wetu sana tu, lakini hatulalamiki! Mtoa mada wakaka hata wakichangishwa 11,000 tu kila mmoja wewe unalalamika! Kha!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  mjini shule kijiji kilimo
   
 12. kiLimIlire

  kiLimIlire Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mjini akili, nguvu kijijini
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha ha ha ha.
  WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
   
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  kwani tatizo ninini? kwanza sh almost ni kama 11200/= kweli inawatoa jasho na kuwafanya mpoteze muda kudiscuss.

  wewe unapiga mznga ama unahongwa sh ngapi na madem zako? mbona siye huwa tunahonga sana tu?mbona hatulalamik? naboreka sana pale tunaposakamwa kwa mtu kuhongwa sh 33600/=na wanaume 3 tofauti na pia naona kma ni kweli bint hajui technique manake just an sms moja ya " hny ma dearest love you so much., ma gas tank is drained and i dont have enough banks sweetie" yaani in afraction of a minute lazima mpesa oe crdb cardless ma nmb pesa fasta ingehusu.
   
 15. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  chezeiya daslam weye!!! mjini kuna wenyewe baba!
   
 16. babe S

  babe S JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 3,703
  Likes Received: 19,820
  Trophy Points: 280
  Na muda wote huo ulikua unamuangalia tu?
   
 17. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,003
  Trophy Points: 280
  Wanawake wanajua sana kuchuna pesa mbele wapo kimslahi zaid
   
 18. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Hilo ndilo lililokuja kwenye kichwa changu, ni bora angetuambia yeye ni muuza miwa alikuwa pembeni ya barabara!
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,679
  Trophy Points: 280
  Mi nashindwa kuzielewa akili za wanawake,badala ya kuzungumzia ujinga wa huyo mwanamke mwenzao wa kushindwa kuwa mwaminifu wao wanaletj excuse. . . . . . . .. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Hapa mtoa mada hajazungumzia kiasi cha bei ya mafuta wala hela alizolipiwa mafuta.Pia hajazungumzia kuhongwa,yeye amezungumzia namna huyo mwanamke alivyo wa hovyo kwa kuwapanga wanaume!
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa kikubwa sio facts za kesi,kikubwa ni kwamba je tumejifunza nini tokana na hii riwaya?
  Binafsi nimeshuhudia mara nyingi mwanamke ana collude na landlord na matokea yake wanaume wanne watano wanamlipia mwanamke kodi ya nyumba hiyo hiyo kisha hela wanagawana na mwenye nyumba,au mwanamke anauguliwa bili ya hospitali analipa bishanga Erickb52 na Asprin bila kujijua,mambo haya yapo aisee.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...