Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

WIKI HII KATIKA SIASA ZA US

TRUMP ZIARANI PHOENIX, ARIZONA

MASHAKA JUU YAKE ''UNFIT' YANAONGEZA

Rais Trump amemaliza hotuba yake katika mkutano wa mtindo wa Kampeni. Haikuwa ziara rasimu ya kiserikali
Baadhi ya viongozi wa Phoenix, AZ walimshauri aahirishe safari kwa kuzingatia suala la Charlottesville

Kwamba kulikuwa na uwezekano wa vurugu kutokana na jinsi alivyo handle tatizo hilo akionyesha moral failure
Mkutano wake wa leo uliojaza watu ndani na waandamaji nje, vurugu zimetokea kwa kiasi kidogo

Hotuba ya Rais Trump haielezeki ilikusudia nini kwa muda wa saa nzima na robo ikiacha maswali mengi kuhusu Rais wa Marekani na uwezo wa kuongoza taifa hilo hasa kuzingatia kile kinachosemwa 'unfit for office''

Trump alianza hotuba kwa kuzungumzia suala la Charlottesville. Hili ni suala ambao wengi wa wapiga debe wake hawakupenda aliongelee kutokana na utata wake. Jana alizungumzia akihutubia taifa kwa teleprompter

Leo alikuwa anatumia maneno yake mwenyewe na kuzua utata. Utata mkubwa ni pale alipoelezea hotuba zake zilizoleta matatizo akiondoa maneno mengi aliyoongea.

Kwa lugha nyingine akiongopa kati ya alichosema siku za awali na anachoeleza leo hii.
Hii ilikuwa low point kwa kujua media zina rekodi zote zilizo wazi

Katika suala hilo Trump alijichanganya akisema 'wanataka kufuta historia yetu' maneno ambayo white supremacists wameyatumia. Katika mlolongo wa hotuba kulikuwa na kujichanganya sana

Trump akageukia media akisema zinazotosha habari zake na kutaja media kama CNN na Washington post kama feki akizishambulia kikamilifu na akisifia Fox News ambayo mara nyingi ametengeneza nayo habari

Kundi jingine lilikuwa la senator McCain na Flake ambao ilikuwa kama anawaambia wapiga kura ni tatizo
Maseneta hao ni wa Republicans, McCain akipiga kura ya no kwa repeal and replace Obamacare, Flake akihoji uwezo na uimara wa Rais kutokana na 'moral failure aliyoonyesha Charlottesville''

Trump hakumuacha Obama kama kawaida yake na hilo lilitegemewa huku akimshambulia Hillary Clinton
Hakuna sababu zinazoweza kueleza kwa undani alifikaje kwa watu hao

Kama kawaida alisema katika miezi 8 ameweka rekodi ya ajira Milioni. Kipindi kama hicho mwaka jana Rais Obama alitengeneza ajira nyingi zaidi. Rais Trump anasema unemployment ni 17 yrs low.
Well, akichukua nchi tayari ilikuwa katika 4.9 kutoka 9 aliyoikuta Obama na sasa inasimama katika 4.3%

Jambo jingine alilozungumzia ni ujenzi wa ukuta akisema anaweza ku shut down the gov. kama haitapita

Trump hakuacha wajumbe wa baraza lake la CEO's anaosema wanamwita pembeni ili waongee naye
Hawa walijiuzulu kutokana na suala la Charlottesville

Kwa ufupi hotuba nzima haikuwa na mpangilio wala facts na hilo ndilo mjadala kwasasa. Alimshambulia kila aliyepingana naye bila mpangilio.

Kilichotokea leo ni Trump kuchochea kuni na kuwapa sababu ''wabaya'' wake. NYT inaripoti kuwa Senator majority McConnel ameeleza wasi wasi kama Trump anaweza ku salvage his presidency

Wawili hao hawajaongea kwa takribani wiki mbili
Jana Spika Ryan akimweleza Trump kama mtu aliye mess up katika suala la Charlottesville

Hotuba yake inachochea media na katika wiki mbili zijazo atakuwa na wakati mgumu sana kwa issue kadhaa

Itaendelea....
 
Hotuba yake inachochea media na katika wiki mbili zijazo atakuwa na wakati mgumu sana kwa issue kadhaa
Naona anakoleza moto...sera ya ubabe nje kwa hapa inaweza kumletea matatizo makubwa. Kitendo cha kusaliti maneno yake mwenyewe kuhusu Afghanistan ni kibaya sana. Military Industry Complex, sasa wako WH!! Korea Kaskazini kasema jana hata US iweke vikwazo gani, kamwe hata acha kutengeneza silaha zake za kujilinda. Silaha zake za nuklia anasema hazimo kwenye mjadala wa kutafuta suluhu ya usalama Korea peninsula!

Moscow 'preparing inevitable response' as US hits Russians with new sanctions over N. Korea
Neocons return
 
MKUTANO WA PHOENIX

Ilikuwa ni dhahiri Rais Trump alikusudia kushambulia vyombo asivyovipenda
Rais Trump ana mbinu za kubadili mijadala na kuielekeza anapotaka

Alitambua kushambulia media kwa Charlottesvile kutaelekeza mjadala upande huo

Hili litamsaidia kufunika habari za Russia. Hakuna ajuaye ''Russia''itatoa majibu gani
Ni wazi hapendelei uchunguzi huo kwani unaweza kueleza mengi asiyotaka yajulikane

Kosa ni kutotambua ufanyajikazi wa media za US. Waandishi wana majukumu maalum ya kufuatilia. Kubadili mjadala hakuwezi kuzima uandishi unaohusu jambo fulani

Wengi WH walitaka Charlottesvile ifike mwisho,anairudisha katika media mwenyewe
Magazeti na TV zinaoanisha alichosema siku za nyuma na 'omission' ya Arizona jana

Kwa mfano wakati ananukuu kauli zake za nyuma hakuzungumzia 'many sides, many sides' chimbuko la mjadala kwa wanaosema ilikuwa 'moral equivalency' kitu kisicho sahihi

Pili, wiki iliyopita alisema katika makundi yote walikuwepo watu wazuri 'good people'
Jana aliondoa katika nukuu kwasababu watu walihoji, mtu mwema anawezaje kuwa ndani ya makundi yaliyoimba 'Jews will not replace us, Blood and soil etc'

Na kubwa zaidi ni kushambulia maseneta McCain na Flake ambao Majority leader McConnel amewatetea. Katika kudhhirisha hilo maseneta wametuma matangazo ya kuwatetea na kumnanga yule anayepigiwa debe na Trump mid term elections

Hili litampa ugumu,ugomvi na senate utamkwamisha kamailivyokuwa Obamacare repeal

Trump anaitaka senate ibadili utaratibu wa kura. Badala ya 60 ziwe simple majority
Hili lilifanyika wakati wa kura ya kumthibitisha Jaji Gorsuch likifanywa na McConnel.
Ni unlikely enate itabadili utaratibu huo

Kwanza, Republicans wana hofu ikiwa watapoteza senate wakiwa wamebadili utaratibu watapata tabu kuwazuia Democrats 'Filibuster' katika hoja

Pili, tayari Trump ana ugomvi nao akiwemo McConnel anayepaswa kusimamia hilo

Ingawa ilionekana anaongea na political base yake inayopenda kumsikia akisema lolote, madhara ya kauli zake ni makubwa kuliko faida alizopata.

Mkutano wa jana ulilenga kujenga umaarufu baada ya poll kuonyesha anapoteza sehemu kubwa ya uungwaji mkono ikiwemo base yake

Ukimsikiliza kwa makini ni kama alitaka kuchanganya umma wa US lakini pia kama mtu aliyekata tamaa kwa hoja ya liwalo na liwe.

Trump ni survivor wa matukio mengi ya kuboronga kisiasa
Kwa mwendo wa jana jahazi linazidi kuingia maji

Tusemezane
 
SAGA LA RUSSIA LAREJEA TARATIBU

Ugomvi na media si jambo jema kwa Trump. Baada ya wiki ya Charlottesville ambalo kwa kila kiwango alibofoa na hata alipopata nafasi ya kurekebisha aliboronga zaidi, suala la Russia limerejea
Kama tulivyosema bandiko la awali kabla ya wiki Trump anajikuta katika mazingira yale yale

Rais Trump hakuwa na sababu za kulaani media tena akiazitaja kwa majina.
Media za US ni tofauti na zina mengi zinayoyafanyia kazi.

Trump hapendi media kama CNN kwasababu ya kueleza kilichopo na si kumsifia kama Fox News

Jana kuna habari za kupatikana kwa 'email' moja ikimuhusisha kiongozi wa juu wa kampeni na Russia
Haijasemwa nini kilichomo lakini inatosha kusema inafuatiliwa kwa ukaribu

Kuna uwezakano hakuna lolote la muhimu, lakini katika mazingira ya ado ado zinazoendelea ni wazi utawala hauna raha na kila mara ni katika kufikiri nini kitatokea au kitachumbuliwa hata kama hakihusiani na Russia

Wiki hii inaripotiwa kuwa na tifu kati ya McConnel, senate majority na Rais Trump
Moja ya sababu ni McConnel kushindwa kuzuia suala la vikwazo kwa Russia lililopitishwa kwa 98-2

Trump anamlaumu McConnel kwa kushindwa kuzuia suala la uchunguzi wa Russia ingawa haielezwi McConnel angewezaje, iwapo ni kuvunja kamati au kuzikataza zisiendelee na uchunguzi

Kukiwa na wingu linalohitaji majibu ya ushiriki wa Russia, ni wazi kuna tapatapa inayotia shaka
Si lazima ihusiane na Russia lakini pia inaweza kuibua mambo kama tax na investment za Trump

Tusemezane
 
Jana kuna habari za kupatikana kwa 'email' moja ikimuhusisha kiongozi wa juu wa kampeni na Russia
Haijasemwa nini kilichomo lakini inatosha kusema inafuatiliwa kwa ukaribu
Nadhani...Deep state inaelekea kuichukua WH mazima. Hii si hali ya kawaida vyombo vya usalama vya nchi husika kulazimisha kufanya uchunguzi kwenye majengo ya kidiplomasia ya nchi nyingine. Kwa mara nyingine US inaonyesha hegemony yake kwenye masuala ya hatari kwa usalama wa ulimwengu. Kwa hali ya sasa Trump, virtually, ameishapoteza usukani wa kuendesha mambo hapo WH.

Moscow hands in note of protest to US over plan to search trade mission in Washington
 
Ulionekana moshi katika jengo moja la ubalozi wa Russia lakini haukuwa moto wa jengo kuungua bali inadhaniwa ni documents muhimu zenye ushahidi dhidi ya Russia zilikuwa zinachomwa baada ya kuwepo habari kwamba vyombo vya dola vya Marekani vilikuwa tayari kuvamia jengo hilo kwa upekuzi wa kufa mtu.
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

ARAPIO, MAFURIKO TEXAS, RUSSIA N.K.

Katika wiki nzima habari kubwa ni ya mafuriko makubwa katika miaka zaidi ya 100 yaliyokumba jimbo la Texas has miji ya Houston na Beamont ambako mamilioni ya watu wameachwa bila makazi kukiwa na vifo 47 hadi sasa

Janga hilo kubwa imeupukwakwa sehemu kubwa kutokana na ushirikiano wa wananchi wenyewe
Funzo lililopatikana kwa majanga ya Katrina na namna Obama alivyo kabili Sandy yamesaidia katika organization

Rais Trump amerudi leo ikiwa mara ya pili, ingawa mara ya kwanza alitia doa kidogo hasa alipoongea na wahanga na kisha kuchomekea idadi ya watu waliojitokeza kumsikiliza wakati wa maafa hayo

Ingawa hali ya uokozi inaendelea vizuri kuna changamoto za kuurudisha mji wa Houston, wa nne kwa ukubwa katika hali ya kawaida. Huduma nyingi zimeathirika na majanga ya moto yakijotokeza hasa viwandani

Kwa mantiki, kunahitajika kiasi kikubwa cha fedha kuidhinishwa na Congress jambo linaloweza kuzua utata

Wakati wa Obama na tukio la Sandy fedha izliidhinishwa baada ya siku 60 kutokana na conservatives akiwemo Ted Cruz kuzuia tu kwa visingizio. Swali visingizio hivyo vitakuwepo tena kwa Republicans wale wale?

Sheriff Arapaio
Huyu ni askari kutoka Arizona ambaye ni mhafidhina na alitiwa hatiani kwa kosa la 'ubaguzi' wakati akitekeleza majukumu yake. Ni mtu maarufu Arizona ambaye kesi aliyokuwa nayo ilisababisha asigombe congress

Ni mshirika mkubwa wa Trump hasa katika suala la ujenzi wa ukuta 'wall' akilipigia chapuo kama Trump

Katika hali isiyokuwa ya kawaida ikihusisha tukio la kibaguzi ambalo linafuatiliwa na sakata la Charlestosville, Rais Obama alitangaza msamaha kwa Arapaio siku dhoruba ya Harvey ikirindima katika mji wa Texas

Alipoulizwa kwanini alitoa msamaha siku hiyo Rais Trump alisema alijua tukio la Texas ni kubwa na kwamba msamaha wake ungepata rating kubwa katika TV.

Ukweli ni kuwa hakutaka mjadala wa suala hilo linalowagusa Walatino zaidi urindime, makovu ya Charlestoville yakiwa mabichi na akijua Harvey itaua mjadala, na hilo alifanikiwa kwa muda mfupi na ni tatizo kwa muda mrefu

Inaendelea....
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US
MAFURIKO TEXAS, RUSSIA N.K.

Miongoni mwa mambo yaliyojiri bila kupewa uzito kutokana na mafuriko ni kazi za bwana Mueller na seneti zinazochunguza sakata la Russia. Senti imemwita Don Trump Jr katika mahojiano bila kamera wala kiapo

Mahojiano yatafanyika Sept. Trump Jr amekaririwa akisema suala zina ni 'phony' yaani uzushi tu , haijulikani kwanini hataki mahojiano ya wazi na kwanini hataki kiapo 'oath'
Kujichanganya kutokana na emails baada ya kuficha wahusika wa mkutano wake kunatia shaka

Anachokikwepa ni kubanwa kuhusu Rais Trump kuwa na taarifa za kikao hicho cha siri
Pia kukwepa hoja ya Rais Trump alishirikia kuandika statement ya awali iliyojulikana ni ya uongo.

Mueller: Amepewa taarifa ya awali iliyaondikwa na Rais Trump kuhusu kumfukuza Comey wa FBI.
Ikumbukwe Comey aliandikiwa barua na Rosenstein hata hivyo kuna 'draft' ya Trump
Haijulikani draft ilisema nini , yote ni katika uchunguzi wa sakata la Russia ukimhusisha Comey

Tarehe 1 sept aliyefikisha barua ya kumfukuza Comey FBI katika ofisi alitangaza kujiuzulu ushauri WH kwasababu za kiuchumi. Haieleweki ni sababu gani ikizingatiwa ni mshirika na swahiba mkubwa wa Trump kwa miaka dahari

Kujenga Ukuta: Aliahidi Rais Trump akisema gharama za ujenzi zitalipwa na Mexico.
Katika maongezi na Rais wa Mexico, Trump alisema si jambo muhimu ingawa kisiasa lina impact
Kwa pressure kutoka kwa ''base'' Rais Trump amerudi kuomba pesa za ujenzi wa ukuta 'wall'' congress

Swali linalomkabili ni kuhusu ni kwanini congress ilipe ikiwa aliahidi Mexico kulipia?
Wakati huo huo Rais wa Mexico alihutubia mabunge ya pamoja ya nchi hiyo amesisitiza Mexico haitalipa

Rais Trump anatishia kufunga shughuli za serikali kama congress haitaptisha pesa za ujenzi wa ukuta
Kauli imeamsha hisia na hasira miongoni mwa Republicans hasa conservatives na inabaki kuwa mwiba

DACA: Deffered action for childhood arrivals
Ni sera iliyoahirisha hatua dhidi ya vijana chini ya umri wa miaka 31 mwaka 2012 waliojiandikisha katika vyuo, mashule au majeshini kurudishwa makwao. Hawa kwa lugha nyingine wanaitwa Dreamers wakiishi ndoto ya US

DACA inatakiwa isainiwe tena mwezi huu au ifutwe na Trump anaonyesha dalili ya kutaka kuifuta.
Maamuzi atayatoa kabla ya jumanne tarehe 6 sept.
Miongoni mwa wanaotaka asiani tena ni Republicans wakionya nguvu ya vijana inayoweza kuwasumbua baadaye

North Korea: Imefanya jaribio la Hydrogen Bomu linalkadiriwa kuwa kubwa mara 6 ya lile la Hiroshima
Nkorea ni pasua kichwa kwa Marekani na washirika wake Japan na South Korea

Rais Trump ametishia kufuta mikataba ya biashara na taifa litakalofanya biashara na Nkorea kama sehemu ya kuimarisha vikwazo. Hapa amelenga China inayofanya biashara kwa takribani asilimia 90

Wakati huo huo ametishia kufuta mkataba na SouthKorea kama alivyoahidi. Suala hilo linaonekana kupingwa na viongozi wa ulinzi na usalama kwa kuzingatia umuhimu wa South Korea katika kumkabili Nkorea

Viongozi wa usalama wanasema Skorea ni strategic partner na shughuli za biashara zinaweza kuathiri sana mpango mzima wa kukabiliana na Nkorea

Kwa mtazamo wa Nkorea, ni wazi weledi wa Rais Trump kwa siasa za dunia ni wa kutilia shaka sana, matumaini yapo kwa wasaidizi wake wanaoielewa dunia. Hata hivyo kila uchao kukiwa na tweet bila mpangilio inatisha

Tusemezane
 
SIASA ZA DC NA YANAYOJIRI

DACA NA WIRETAP YA TRUMP TOWER

Sakata la DACA (Deffered action childhood arrivals) limechukua sura mpya. Rais Trump anatarajiwa kuweka msimamo juu ya suala hilo hapo kesho, hata hivyo habari zilizojiri zinasema Trump ameamua kusogeza mbele kwa miezi 6 program hiyo ili kutoa nafasi kwa Congress kuja na plan itakayohusu uhamiaji 'immigration'

DACA ni suala tata sana, Rais Trump amebadili misimamo mara nyingi sana. Utata unakuja katika ukweli wa suala hilo kuwagawa Republicans. Democrats hawana mjadala wanataka program iendelee kama alivyoanzisha Obama

Republicans wanaona tatizo kubwa kuingia katika mzozo na millennials walioonyesha kwa Obama na Sanders nguvu yao katika sanduku la kura. Wakati huo huo mashirika na makampuni 400 yamepingana na uamuzi wa Trump yakisema dreamers ni sehemu muhimu ya ukuaji wa makampuni na mashirika na uchumi kwa ujumla

Rais Trump kutoa miezi 6 na kusukuma jambo hilo congress ni kukwepa matatizo.
DACA ilianzishwa na Obama na kufanya kazi na Congress hadi ikapita.

Trump anapaswa kuonyesha leadership si kumtupia McConnel na Ryan mzigo kama ilivyokuwa Obamacare. Failure ya Obamacare inahusishwa na congress, Trump akiwa ameipigia upatu wa hafla kila hatua house iliyofikia. Anachukua credit anakwepa responsibilities!

DOJ na FBI wakana WIretap aliyosema Trump
Katika tukio jingine, mbele ya mahakama wizara ya sheria (DOJ) na FBI kupitia kitengo chao cha NSD(National security division) wamesema hawana ushahidi wa madai ya Rais Trump kuwa ali wiretap Trump Tower

Hayo wameyasema mbele ya mahakama kufuatia kesi iliyofungulia na kitengo kinachojihusisha na kuiangalia serikali 'watch dog' chini ya kifungu cha Freedom of information act.

Hili limemaliza kabisa kauli ya Trump ya wiretap inayosemwa ni ''utter nonsense'', kauli itakayomwinda kwa muda mrefu ujao katika anga za siasa. Bado madai ya illegal voters hajayathibitisha

Barua
Ile barua aliyoandika Obama na kuiacha WH oval office siku ya makabidhiano imewekwa wazi
Ni utamaduni wa Rais anayeondoka kumwandikia anayemfuata. Ni barua ndefu ya maneno 250 tofauti na watangulizi wake. Barua ilijaa nasaha zenye hekima ambazo wachunguzi wanazioanisha na hali inayojiri sasa

Tusemezane
 
DACA YAFIKIA UKOMO
MZIGO UPO CONGRESS, TRUMP APATA SHINIKIZO ABADILI BADILI MISIMAMO

DACA tuliyoeleza mabandiko yaliyotangulia imefikia ukomo Jumanne. Kwamba hakuna atakayeruhusiwa kuomba baada ya muda huo na wenye DACA inayokwisha ndani ya miezi 6 wataruhusiwa kuomba tena hadi March 2018.

Katika muda huo Congress imepewa jukumu la kuja na mpango wa uhamiaji 'immigration'.
Hili limemaliza muda wa amri ya Obama iliyoanzisha DACA na kupingwa na state nyingi zikiwa za Republicans

Kesi kuhusu Obama ''kukiuka katiba'' kwa amri ya DACA haikuwahi kusikilizwa

Kwa ufupi baada ya mswada wa immigration kushindwa wakati wa Obama, Rais huyo alichukua jukumu la executive order ya muda wa miaka 2 ili kutoa nafasi kwa congress kutafuta suluhu ya kudumu

Exec order hiyo ndiyo iliyopelekea baadhi ya state kusema amekiuka katiba kwa suala linalohusu congress

Hivi karibuni baada ya Trump kuingia madarakani state 10 ziliandika barua ya kusudio la kuishtaki serikali ikiwa haitafuta DACA tarehe 5 sept 2017. Idara ya sheria imesema serikali ingeshindwa kama wangeenda mahakamani

Ni kwa msingi huo ilibidi 'itafutwe' njia rahisi ya kufuta na kutoa muda kwa congress kuja na mpango kazi ili kukwepa mashaka na 'kusitiri' dreamers wanaoathirika na DACA

Hapa ni mchezo umechezwa ili ionekane Trump hakukusudia isipokuwa amelazimika kutokana na state 10
Halafu kwamba ameona huruma na kutoa miezi 6 akitupa mzigo kwa congress

Shinikizo limekuwa kubwa kutoa makampuni, mashirika na makundi ya jamii imemlazimu Trump ku tweet na kusema ikiwa congress haitafanya kazi katika miezi 6 atachukua uamuzi mpya 'revisiting' the decision

Hapa anataka kuaminisha watu anaweza kubadili msimamo ikiwa congress hawatafanya hivyo
Hoja ya uhamiaji ilishindikana wakati wa Obama kwasababu hizo hizo za DACA na haionekani kama zimeondoka

Ku-revisit decision ni kuchukua hatua alizochukua Obama ambazo Trump na state 10 walisema ni ''haramu''

Tump anacheza na congress , dreamers na political base yake akitaka kujivua lawama lakini akitaka credit
Wachanguzi wanahoji, Trump aligombea kama deal maker, iko wapi?
Mbona kila kitu anakwepa 'mzigo' na aliyojaribu ameshindwa?

Akiwa amevuruga wajumbe wa seneti, hana maelewano nahouse ni wakati mgumu kuweza kufanya deal lolote. Kauli zake za siku za nyuma dhidi ya wenzake zinamweka katika wakati mgumu

Kwa US, mgawanyo wa madaraka ni wazi, congress si sehemu ya exec branch

Tusemezane
 
Teh teh teh...naona kibao kimegeuka.

Kumbe all along waliokuwa wana collude na Russia ni Democrats na Hillary wao.

Hahahahahaaa daah! Siasa bana.
 
Teh teh teh...naona kibao kimegeuka.

Kumbe all along waliokuwa wana collude na Russia ni Democrats na Hillary wao.

Hahahahahaaa daah! Siasa bana.
Msukuma bwana...! Hata akiishi Ulaya miaka yake yote ulimbukeni na ushamba haumtoki hata kwa kusuguliwa na dodoki. Wasukuma wote ughaibuni huwaambii kitu...wote wako nyuma ya huyu dikteta wetu uchwara na si ajabu huko Marekani wengi wao wanamshabikia mwehu mwingine pacha wa Magufuli. Ila uzuri wa huko ni kwamba huko Trump kafungwa kamba tofauti na hapa ambapo vichaa wako huru, wanaranda nyikani wanavyotaka!
 
Msukuma bwana...! Hata akiishi Ulaya miaka yake yote ulimbukeni na ushamba haumtoki hata kwa kusuguliwa na dodoki. Wasukuma wote ughaibuni huwaambii kitu...wote wako nyuma ya huyu dikteta wetu uchwara na si ajabu huko Marekani wengi wao wanamshabikia mwehu mwingine pacha wa Magufuli. Ila uzuri wa huko ni kwamba huko Trump kafungwa kamba tofauti na hapa ambapo vichaa wako huru, wanaranda nyikani wanavyotaka!
Umetoroka daycare wewe eeh?
 
Last I heard, ikulu ya Marekani imegeuzwa daycare center. Pacha wa Sizonje aliyepanga humo anahitaji kweli huduma hiyo! Kwa Tanzania bahati mbaya hatuna providers waliobobea.
 
Imenukuliwa kutoka rt.com
====
headlines to you.



RT

LIVE

searchMenu mobile

HomeUS News

Why Flynn’s plea is a dead end for ‘Russiagate’ conspiracy

Published time: 1 Dec, 2017 23:33Edited time: 1 Dec, 2017 23:36



Former US National Security Adviser Michael Flynn in Washington, US, December 1, 2017 © Jonathan Ernst / Reuters

President Donald Trump’s short-lived national security adviser, Michael Flynn, pleaded guilty to lying to the FBI. Most US media jumped on the plea as proof of Trump’s collusion with Russia. Actual documents, however, tell a different story.

A court document signed by special counsel Robert Mueller, dated Thursday, specifies two instances of Flynn telling FBI investigators things that were not true. They relate to two conversations he had with Russian Ambassador Sergey Kislyak, in December 2016.

In the Statement of Offense signed by Flynn at his court appearance on Friday, he admitted to acting on instructions from a senior “Presidential Transition Team” (PTT) official, prompting breathless speculation if that was Trump himself, his son-in-law Jared Kushner, or someone else altogether. The one question nobody seems to be asking is, “So what?”

It is intuitively obvious to even the most casual observer that Flynn’s “crime” is a procedural one: he told FBI investigators he hadn’t done a thing that he actually did. But was the thing he did - namely, speak with the Russian ambassador to the US - against the law? Not really.

Read more

Former national security adviser Flynn pleads guilty to lying to FBI

Under the 1799 Logan Act, it is technically against the law for a private US citizen to engage in diplomacy. However, only two people have ever been indicted under that law, and no one has ever been prosecuted. Flynn was a member of the presidential transition team whose duties involved contacts with foreign diplomats. So why would the FBI even ask him about his contacts with Ambassador Kislyak?

“There was nothing wrong with the incoming national security adviser’s having meetings with foreign counterparts or discussing such matters as the sanctions in those meetings,” Andrew McCarthy of National Review wrote on Friday.

Because Flynn was “generally despised by Obama administration officials,” McCarthy added, “there has always been cynical suspicion that the decision to interview him was driven by the expectation that he would provide the FBI with an account inconsistent with the recorded conversation - i.e., that Flynn was being set up for prosecution on a process crime.”

Back in May, former deputy Attorney General Sally Yates testified before the Senate Judiciary subcommittee that she came to the White House on January 26 - two days after Flynn’s FBI interview - to say that he had lied about his conversations with Kislyak. How did she know? That, she said, was “based on classified information.”

Clearly, Yates knew Flynn was lying about the conversations because US intelligence had been listening in on them. An Obama administration official leaked that information to the Washington Post’s David Ignatius, who reported on the Flynn-Kislyak conversation on January 12, eight days before Trump’s inauguration.
 
Imenukuliwa kutoka rt.com
Naona wewe ni mfuatiliaji mzuri wa rt.com. Bila shaka hata hapa Tanzania hakuna media unayoiamini kama UHURU au TBC! Ndugu yangu mambo ya Marekani yaache yalivyo...Uchunguzi wa Nixon ulichukua miaka miwili; wa Trump ndio sasa una miezi na hata mwaka bado.

Hakuna mtu hata moja kwenye kambi ya Trump ambaye anajua ukweli ni kitu gani, vuta subira kwani ukweli hauzikwi hata siku moja...lock her up kwa sasa imeshageuka na kuwa lock him up na bado!


Katika hii picha waongo wanaonekana wakiongozwa na muongo-in-chief Donald Trump!
Siku zao zahesabika, vuta subira!
 
Naona wewe ni mfuatiliaji mzuri wa rt.com. Bila shaka hata hapa Tanzania hakuna media unayoiamini kama UHURU au TBC! Ndugu yangu mambo ya Marekani yaache yalivyo...Uchunguzi wa Nixon ulichukua miaka miwili; wa Trump ndio sasa una miezi na hata mwaka bado.

Hakuna mtu hata moja kwenye kambi ya Trump ambaye anajua ukweli ni kitu gani, vuta subira kwani ukweli hauzikwi hata siku moja...lock her up kwa sasa imeshageuka na kuwa lock him up na bado!


Katika hii picha waongo wanaonekana wakiongozwa na muongo-in-chief Donald Trump!
Siku zao zahesabika, vuta subira!
Asante kwa maoni yako. Lakini ,Mwalimu wangu mkuu saidizi hapa JF, kuna kitu unakikosea. Kitu hicho ni kudharau uwepo wa nguvu HALISI za kidunia. Katika zama hizi huwezi kupuuzia nguvu halisi ilizonazo Russia kiweledi, na huwezi kupuuza nguvu halisi ilizonazo CCM na serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kiweledi pia. Huwezi!! Kama kweli wewe ni mfuatiliaji wa trends za masuala ya kidunia na kitaifa kwa karibu. Nina imani kabisa unafuatilia trends hizi fairly. Imani hii ndiyo inanifanya kukushangaa kiasi chakuona unakosea mahali fulani.
 
Back
Top Bottom