Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

YANAYOJIRI SAKATA LA RUSSIA NA US

Wiki hii imejaa mazonge zonge ya sakata la uchunguzi kuhusu Russia kuingilia uchaguzi
Kwa hali ilivyo ni rahisi kuchanganya mambo kwasababu imefanya hivyo makusudi

Sakata la uchunguzi limekuwepo kwa muda mrefu.

Wiki 3 zilizopita Rais Trump akaingiza la Obama na wire tapping ambalo vyombo vya usalama vilikanusha kutokea.

Baada ya taarifa hiyo, WH ikaja na utetezi wa surveillance. Tumeeleza huko nyuma tofauti ya hayo mawili
Rais Trump akasema hataomba radhi kwasababu katika wiki mbili litatokea jambo kumthibitisha sahihi

Mwenyekiti wa kamati ya bunge Nunes akasema kuna information anazifuatilia kuhusu hilo

Wiki hii alikwenda WH, na kisha kuongea na vyombo vya habari.

Alisema, hakuna ushahidi wa wiretap lakini kuna nyaraka zinazohusu surveillance(incidentally)

Taarifa hiyo hakuwa ameifikisha kamati ya intel, jambo lililozua mtafaruku
Imethibitika, kazi ya kupata nyaraka za surveillance alipewa WH

Hoja ikaja, kwanini hakujadili na kamati kabla ya kwenda Ikulu? Nani alimkaribisha Ikulu?
Na kwanini hakusema alikwenda siku mbili ? Kwanini alikwenda kwenye eneo linalochunguzwa?
Kwanini taarifa yake imefuatilia kauli ya 'wiki mbili' na ile ya jambo linakuja yake mwenyewe?
Nunes alijitetea hata hivyo kuna shinikizo ajiuzulu, kwamba, kamati haitakuwa huru

Shinikizo hilo linatoka Dem na GOP wanataka kwenda kwa kina katika suala la Russia
Katika hali isiyotarajiwa Nunes anasema lazima suala la leak lifanyiwe kazi na kalifanya agenda

Nunes alikuwa mshauri wakati wa mpito 'Transition' kuelekea WH
Anachofanya ni kupoteza la Russia, kusafisha ''wire ta'' na kufanya leak kama tatizo

Kufuatilia hayo, Seneti inafanya uchunguzi kuhusu Russia na si menginenyo

Hapo ndipo tunapata kamati mbili, ya Nunes (House) ambayo imepoteza credibility
Kamati ya seneti inayofanya uchunguzi kwa utaratibu wake.
Halafu kuna FBI na Intel community

Nunes amesaidia hoja ya kamati huru au proscutor kuwa na mashiko kwani yake haina credibility

Watu waanza kuhaha, wengine wapo tayari kutosa jahazi kama tunavyoona kwa Flynn

Inaendelea....
 
WAANZA 'KUTOSA' JAHAZI

Aliyekuwa AG wakati Trump anaingia ambaye alifukuzwa, Sally Yates alijtolea kwenda mbele ya kamati
Mwenyekiti Nunes akaahirisha kikao bila sababu akitaka mahojiano yafanyike nyuma ya Camera

Yates aanasemwa kumshauri Trump kuhusu uteuzi wa Flynn na mazonge zonge aliyo nayo, alipuuzwa

Inaonekana ana habari zitakazo embarrass WH. Nunes kajitahidi kuhakikisha hasikiki

Wakati huo huo, kuna kuungaanishwa kwa vigogo wa kampeni ya Trump na sakata
Mahusiano ya kampeni meneja wake, Flyyn na mkwewe Jared yanacgunguzwa kwa undani

Jared na wenzake wamejitolea kufika mbele ya kamati ili kuhojiwa.
Wachunguzi wanasema hii ni katika mchoro na Nunes ili kuwasafisha na kufifisha suala la Russia

Katika hali isiyotaeajiwa, Gen Flynn ameomba kupewa hifadhi (immunity),ana habari anazotaka kushea na vyombo husika. Immunity ina maana atakachosema kisijechukuliwa kama ushahidi wa kumshtaki

Haieleweki ana habari gani za kuongea alizoombea hifadhi (immunity) hadi sasa

Gen Flynn ni mshiriki mkubwa wa kampeni ya Trump hadi anakuwa mshauri wa ulinzi na usalama
Mahusiano yake na Turkey na Russia yana utata, inaonekana ni key figure katika uchunguzi

Inawezakana amehisi kuwepo kwa taarifa zaidi zinazomhusu.
Kutafuta immunity kupitia lawyer ni kujihifadhi na matatizo mbeleni.

Muhimu, hakuna ajauye nini anataka kusema, lakini mazingira yanatia shaka
WH ilikuwa na vikao usiku mzima kuangalia suala zima

Sakata la Russia linaweza kutokuwa na ushiriki, tatizo ni kuwepo na jitihadakulizima kutoka kwa baadhi ya Republicans walio karibu na WH. Hilo linapaplilia curiosity

Limefika mahali kuna hoja ya kutaka Rais ataoe tax return kutokana na complicated financial transactions zinazofanywa na washirika wake wa karibu sana

Mbinu ya kuhamisha mjadala inaonekana kukwama. Jana ali tweet kuhusu vita yake na wenzake wa Republicans wanaojiita freedom cuacus. Media hazikutilia maanani zikijua huo ni mchezo wake

Kwa hali ilivyo kama mtakumbuka,, tulisema media za US zilianza kuzunguka mitaani zakaingia Trump tower lakini safari yote mwisho wake ni WH na hapo panaonekana kuwa karibu sana sasa hivi

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, kuna huu msemo wa kuweka akiba ya maneno, haya sasa kunakucha...hebu mcheki Michael Flynn mwaka jana mwezi wa Julai...



Kwa sasa anaomba immunity lakini je alisemaje kuhusu immunity?



Na je Trump mwenyewe ambaye leo anadai Flynn apewe immunity aliwahi kusemaje kwa Clinton?



Kwa kweli dunia ni mviringo...kama wasemavyo wahenga...the chickens have finally come home to roost!
 
Kizungumkuti kiko njiani...tik tak tik tak tik tak tik tak...
 
Kizungumkuti kiko njiani...tik tak tik tak tik tak tik tak...

Hivi kumbe bado kuna watu wanaamini Trump na campaign team yake wanahusika na 'Russia Meddling kwenye uchaguzi wa US'!! Hii 'issue' ya Russia inawapotezea mda serikali ya US, Congress, media kubwa duniani na wananchi wa US na wasio wa US.

Kungekuwa na anything tangible Rais Obama angeweka wazi kabla hajaondoka ikizingatiwa alikuwa hampendi Trump na Trump asingekuwa Rais. Anyway endeleeni kufuatilia hizo conjectures ila msiwe serious sana na hivi vitu.
 
Hivi kumbe bado kuna watu wanaamini Trump na campaign team yake wanahusika na 'Russia Meddling kwenye uchaguzi wa US'!! Hii 'issue' ya Russia inawapotezea mda serikali ya US, Congress, media kubwa duniani na wananchi wa US na wasio wa US.

Kungekuwa na anything tangible Rais Obama angeweka wazi kabla hajaondoka ikizingatiwa alikuwa hampendi Trump na Trump asingekuwa Rais. Anyway endeleeni kufuatilia hizo conjectures ila msiwe serious sana na hivi vitu.
Kalaghabaho...
 
Kuna mtu alitupiwa kamba na yeye kwa kudhani anajihami kajikuta kitanzi kinazidi kukaza...kwa sasa ni muda tu na kila siku huo muda unazidi kusogea kwa kasi ambayo haikutegemewa kabisa. Chezea Marekani...
 
Kuku taratibu ananyonyolewa manyoya...Sessions, Flynn, Bashite (Bannon), Nunes and the list goes on. Muda si mrefu kuna mtu atabaki kama alivyozaliwa na hapo ndipo patachimbika. Marekani watu hawakurupuki...naona mfa maji anatafuta boya la kujiokoa lakini kwa Susan Rice watazidi kuzama tu. Washukuru sana habari za North Korea na Syria kwani zimewapa tu breathing space ya muda mfupi.
 
Kuku taratibu ananyonyolewa manyoya...Sessions, Flynn, Bashite (Bannon), Nunes and the list goes on. Muda si mrefu kuna mtu atabaki kama alivyozaliwa na hapo ndipo patachimbika. Marekani watu hawakurupuki...naona mfa maji anatafuta boya la kujiokoa lakini kwa Susan Rice watazidi kuzama tu. Washukuru sana habari za North Korea na Syria kwani zimewapa tu breathing space ya muda mfupi.
Suala la Susan Rice kama national security adviser linapotoshwa.

Wakurugenzi wote wa zamani kutoka Dems and GOP wanasema ili umasiking itokee siyo security adviser anaomba.
Inatokea pale Intel inapoona kuna umuhimu wa taarifa hizo kumfikia.

Kama atahitaji kujua ni nani, ataomba Intel community na zitapima kama uzito wa suala hilo unaruhusu unmasking.Ni jambo la routine na si geni linafanyika kila mara

Kilichotokea si kuomba majina kama WH na surrogates wanavyosema.

Katika kutafuta foreign intelligence inatokea kuna washirika wa US ambao ''incidentally'' wanajikuta wameingia katika suala zima la surveillance

Wachunguzi wa mambo wanasema ikiwa kuna taarifa zaidi Trump ana uwezo wa kufanya mambo mawili

Moja, ku declassify information ili zipatikane
Pili, kutumia Intel organs kufanya uchuguzi

Hayo hajafanya anakuja na allegations za 'crime' ambazo hazina ushahidi

Hili linakwenda ambapo Rice akiitwa kutoa ushahidi itabidi amwage kila alichosikia.

Hivyo ni ngumu sana kinachoendelea ni porojo.
Mtego huo ameingia Nunes kwasababu Yates anataka ku testify under oath

Huyu alikuwa AG na alimshauri Trump kuhusu Flynn na madudu yanayomzunguka

Kwa maneno mengine habari za Yates zina ushirika na za Rice kwa nature ya kazi zao. Anachojua Yates ndicho alichosikia kutoka kwa Susan Rice

Nunes ameona maji yanazidi unga kaamua kukaa pembeni kwa muda kama Sessions

Mwanamkakati Bannon ameondolewa katika baraza la usalama kama demotion.

Hii ni baada ya kushindwa kuelewana na Matis na kushindwa kuzuia 'tatizo'

Kuna republican wanajaribu sana kuzuia tuhuma zisizo na uthibitisho.
Wanatambua mwisho wake ni kuitwa kwa wahusika na huenda makubwa yakajulikana

Tayari kuna uhusiano wa backwater founder Eric Prince, dada yake ni waziri wa elimu. Eric aliongoza vikao vya siri kati ya wasiri wa Putin, UAE huko Seychelles siku nane kabla ya Trump hajatawazwa

Huyu naye ana mahusiano na watu wengine walioko kwenye radar ya Russia invest

Ukitazama kwa undani kitendo cha Rais Trump kuficha ficha habari za Russia investigations kinaonyesha kuna moshi unafuka.

Hicho kinawapa wapinzani wake nguvu ya kuendelea kufuatilia.
Hata kama hakuna collusion mwisho wa siku mengi yatajulikana

Jared Kushner kaingia, na suala la Bank ya Russia limeingia.

Hapo kunakuzungukwa,wapo wanaodai Trump aonyeshe tax return at least 10 years

Hili suala litafunikwa na habari za juu juu lakini lipo na litamtesa sana

Ni afadhali angeharakisha lifike mwisho, swali, anaogopa kitu gani?

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, hizi habari za Syria na North Korea zimewapa ahueni wa muda kwani kwa siku ya jana zilifunika mengi yaliyokuwa yachukue front page. Yuko jasusi wa Kirusi akiyekuwa amekamatwa na kukabiliwa na kesi lakini cha ajabu akaja kuachiwa kinyemela na haraka haraka tayari karudishwa kwao Urusi.

Hata hivyo pamoja na nuclear option ndani ya Senate ambayo nayo ilipangwa kuwa gumzo na kufunika breaking news za the Investigator kuwa the investigated haijafanikiwa. Mwenyekiti wa kamati ya usalama kwenye House, Nunes, mambo yamemgeuka na sasa amekuwa mtuhumiwa anayechunguzwa!

Mambo si mambo na bado sana...Susan akiitwa kwenye kamati kujieleza, ka pandora box kanaweza kufunguliwa na hapo huyo aliyemtuhumu anaweza kujikuta pagumu. Ni mtego mbaya sana na kuna hatari ya kuwanasa wengine wengi tu kama itakavyokuwa siku Yates naye akimwaga ya kwake.

Huyu jamaa ana roho ngumu lakini sasa ni wazi kuna woga unaonekana unaanza kumuandama na akiendelea kuropoka hovyo kama anavyofanya atajikuta kikaangoni...ni swala la muda tu na huko muda wanao. Hii inanikumbusha utunzi wa Jamea Hadley Chase wa The vulture is a patient bird...!
 
Mkuu Mag3

Jasusi unayezungumzia amechiwa miezi 6 kabla ya kumaliza kifungo chake akisindikizwa kinyemela na maafisa wa US kurudi Moscow

Suala la Syria nalo linaonyesha mapungufu ingawa linasaidia kuziba habari
Media za US zinajua timing, ghafla utaona news zitakapotokea na kufunika mengine

Kama unakumbuka Trump alianza kwa hoja ya 'job' akitembelea makampuni n.k
Hoja ilikufa taratibu kwasababu ya Russia investigation

Nunes alikuwa mshauri wa Tranisition team!

Mikutano yote ya nyuma ya Trump Tower ya akina Jared na Eric inajulikana

Ipo siku hoja itarudi kwa mzee, je, alijua nini kinaendelea? Na alifanya nini?

Hoja kubwa inayomhusu kwa sasa ni ukweli kuwa transition team ilikuwa na mawasiliano na nchi za nje bila kupitia state department inayoratibu shughuli hizo. Kwanini? Ni swali

Mikutano ya Eric na matajiri wa Russia huko Seychelles inaanza kujitokeza taratibu

Tayari tuliyosema media zinatafuta mlango wa Trump Tower, sasa zimeshaingia zinatafuta mlango wa kutokea ili kuelekea 1600 Pen.

Hata kama hakuna kitu, hili suala litaibua mengi sana tuliyokuwa hatuyajui, na ndipo uoga unapomwingia mzee.

Tusemezane
 
SAKATA LA 'RUSSIA'
SYRIA YATUMIKA KUPUNGUZA KASI, SI KUZIMA HOJA

Kwa wanajamvi, uzi huu tulisema siasa za Marekani za nje hazibadiliki bila kujali nani yupo madarakani. Tulisema kutokana na kauli za Trump,wengi waliziamini bila tafakuri

Trump aliingia na sera ya kujitenga na kutanguliza masilahi ya US kwanza.
Alilaani uwepo wa majeshi nchi za nje na kwamba rasilimali zitumike US si kwingineko

Mgeni wa kwanza alikuwa Waziri mkuu wa Japan Trump akiahidi kuongeza majeshi
Waliofuata ni Teresa May Trump akiahidi kuimarisha NATO tofauti na kuifuta

Mtakumbuka tulisema majeshi ya US hayapo nje kama hisani bali masilahi yake
Tukaeleza kuhusu mashariki ya kati na jinsi ilivyo hasa uwepo wa Iran, Russia na China

Mzozo wa Syria umeshadidia vema hoja tulizowahi kuzungumzia. Leo Marekani ambayo hata Wakimbizi walionekana balaa Trump anaingilia katika suala la Syria

Suala la Syria si rahisi kama alivyowaza.
Katika wiki takribani mbili misimamo yake na maafisa wake imebadilika kila uchao.

Miaka ya nyuma, na wakati wa kampeni Trump alimuonya Obama kutoingilia mzozo wa Syria na kusema tatizo hilo litamalizwa na wa Syria wenyewe.

Wiki chache zilizopita alimalaumu Obama kwa kutolimaliza tatizo.
Ghafla silaha za sumu zikatumika huku akipewa shinikizo la kufanya jambo

Kabla hatujaendelea hebu tuangalie kwanini Obama hakuchukua hatua Syria?

Sehemu ya II inaendelea
 
Sehemu ya II

Syria ililipuka kutoka na Arab Spring.

Tofauti na sehemu nyingine, kulikuwa na makundi yakimpinga Rais Bashir Al Assad.

Walikuwepo wapinzani wa serikali, makundi ya maeneo na kundi la ISIS

Haikuwa rahisi kubaini nani alikuwa mpinzani wa kweli wa Assad

Obama aliambiwa awape silaha wapinzani, akachelea yasijetokea ya Osama ambaye kimantiki alijengwa na US.

Alikuwa na shaka silaha kufika mikononi mwa ISIS na likawa tatizo siku za mbeleni

Kubwa zaidi ni kuwa Syria ilikuwa inapigana na ISIS na hivyo kuishambulia ilikuwa ni kudhoofisha jitihada za kupambana na ISIS.

Wakati huo huo US ilikuwa na mazungumzo kuhusu silaha na Iran, washirika wakiwa ni Russia na nchi nyingine. Kuondoa focus kwa Iran kusingewezesha mazungumzo

Siasa za mashariki ya kati zina mafunzo. Obama aliona kilichotokea baada ya Saddam Kuondolewa na Gaddafi kuangushwa. Hakuna aliyejua nini kitafuata Assad akiondoka

Obama alikuwa katika jitihada za kumaliza vita ya Iraq, huku akiimarisha utawala wa Afghanistani na kurudisha askari takribani 150,000 kutoka maeneo hayo

Ikumbukwe alipoomba congress iidhinishe halikujadiliwa Republican wakiwa na House

Ni kutokana na hali hiyo, Obama alisita kuingilia kati akichelea madhara zaidi katika utawala wale kwa funzo alililolipata kutoka kwa mtangulizi wake

Je, ilikuwa vema kwa Trump kumlaumu wakati alizungumza kutoingilia kati mzozo?

Trump ameshambulia Syria, ingawa shambulizi halionekani kuleta madhara.
Hadi sasa eneo lililoshambuliwa linatumika na majeshi ya Syria kama kawaida

Habari iliyopo ni kuhusu lengo la shambulizi. Kushambulia hakutoshi bila kuwa na plan ya muda mrefu. Trump haonekani kuwa na Plan yoyote, Sec Tillerson akisema hili, Sec Sean akisema lile, balozi Nikki Hailey akisema hili. Hakuna anayejua nini kinafuata

Pamoja na hayo, Syria imepunguza habari kuhusu sakata la Russia.

Na katika kueneleza habari hizo, US imesogeza meli zake Korea Kaskazini.

Tatizo linajitokeza ni mahusiano na 'wadau' wenye masilahi Syria, yaani Iran na Russia

Inaendelea...
 
Sehemu ya II

Mzozo wa Syria unaleta sintofahamu kati ya Russia ,Iran na US.
Hilo limepeleka mvutano 'strain' katika mahusiano ya Trump na 'Swahiba' Putin

Trump asilaumiwe kwa kauli zake za nyuma, hakuwa na ufahamu na siasa za US hasa za nje. Kwamba, kuna masilahi ya US ambayo ni ngumu sana kuyaepuka

Tatizo linalomkabili ni kutoafikiana na Russia. Kwasasa wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu mahusiano ya kampeni au washirika wake na Russia, kuna uwezekano Russia wakatumia karata hiyo kumbana

Ndivyo ambavyo Russia walitaka kufanya 'blackmail' kwa mshauri wa ulinzi wa Trump aliyefukuzwa Gen Flynn. Kwa sasa ni ngumu kidogo kwa Trump kuikabili Russia

Russia watatumia suala la uchaguzi kuhakikisha wanaondoa focus yake maeneo kama Syria. Tunaweza kusikia takwimu zaidi zikihusisha kampeni yake katika kufanikisha hilo

Kwasasa Trump anakabiliwa na hali nzito. Kwanza, kumaliza suala la Syria kwasababu hana sababu za kumlaumu Obama ingawa alikuwa upande wake siku za nyuma

Pili, suala la Korea ambalo China inatumia kuibana US kuhusu ushirika wake na Taiwan
Na tatu suala la Russia hacking ambalo Trump hapendi liendelee kusikika

Kwa wenzetu wa US, kelele za Syria zitakuwa na muda tu, suala la uchunguzi linaendelea kama kawaida na baada ya muda litaibuka tena

Tutaendelea kusikia Trump akianzisha utata wa masuala ya nje ili kufunika habari za ndani. Ujanja wa ku tweet sasa umefikia kikomo kwani inaeleweka ni mbinu ya 'distraction'. Hata hivyo, mzozo wowote hauwezi kumaliza au kuzika suala la Russia

Hakuna ajuaye ukweli wa kipi kilitokea, hata hivyo jitihada za Trump kulifunika ikiwa ni pamoja na kusema uongo au kuzusha habari zinatoa shaka kwa wanaofuatilia

Kujiuzulu ka Nune, mwenyekiti wa Intel kunaeleza jinsi ambavyo 'wanaweza kuziba ndoo kwa kutoboa matundu' tutafafanua
 
Sehemu ya IV

Nunes ajitoa suala la Russia

Mwenyekiti wa Intel comm bw Nunes amejitoa katika kamati ili kupisha uchunguzi

Nunes alikuwa katika kuchunguzwa na kamati ya maadili kutoka na kitendo cha kwenda WH kwa siku mbili, kufanya press conference katika eneo linalotuhumiwa

Kujitoa kwa Nunes si kwasababu anachunguzwa.
Ukweli ni kuwa uchunguzi ungeweza kuendelea wakati akiendelea na kamati yake

Nunes amekuwa kizingiti akizuia mashahidi kama Yates kwenda mbele ya kamati. Akiahirisha vikao na wakuu wa ulinzi na usalama na kila aina ya vitimbwi

Nunes alikuwa mshauri 'transition' hakuna shaka alifanya kudhoofisha uchunguzi.
Kwa mfano, aligeuza uchunguzi kuwa surveillance wakati hoja ilikuwa Obama na wire tapping

Kitendo cha kwenda WH kilidhaniwa ni cha ''heri'' kwa Trump.
Kwa bahati mbaya kimezua tatizo na kumlazimisha ajitoe.

Baada ya kubainika alikuwa WH, Dems na GOP walionyesha kukosa imani na kamati

Wote wakataka uchunguzi wa kamati maalumu ya congress au Special prosecutor.
Haya ni mambo ambayo Trump na timu yake ndani ya GOP hawapendi yatokeo

Ili kuepusha balaa wakamtaka Nunes akae pembeni kwani aliyemrithi naye pia ni mshirika wa Trump lakini at least itaonyesha kamati inafanya kazi kwa uhuru

Hizo ndizo tricks zilizotumika kuepuka kamati maalumu au special prosecutor

Hata hivyo, suala la hacking litarudi, media zinafanya yao, intel community yao, house yao na Seneti yao. Mchanganyiko huo unapelekea kiwewe ndani ya WH

Nani ataweza kufanya ''mazingaombwe'' ikiwa kuna la kusema au kutosema?

Tusemezane
 
SIKU 100 ZA UTAWALA

Wanajamvi,

Tulikuwa safari na majukumu mengine hatukuwa na muda wa kutosha. Tumerejea nyumbani sasa

Tunarejea jamvini kuendelea na mijadala inayohusu siasa za US kwa wakati tulio nao
Tunaelekea siku 100 za mwanzo za utawala wa Trump.

Siku hizo si za lazima ni utamaduni ulioanza mwaka 1933 na Rais FDR ingawa hakumaanisha siku hizo bali za bunge katika kipindi fulani

Tukiwa na siku 2 kabla ya kumalizika siku 100 hatutajadili kwani katika siasa siku 1 ni nyingi, na itakuwa ni unfair kama Rais Trump atapimwa kwa siku 98. Tutasubiri siku 100 zitime

Katika mfuulizo wa mabandiko,tulieleza mengi huku baadhi ya wachanga au wasiotaka kujifunza au kwa wanaojifunza ushabiki waliingia na hoja bila kuwa na ufahamu, ilimradi tu.

Hakuna tulichojadili ambacho hakitokio sasa, nje ya mjadala wetu.''Wanasema maandiko yapo ubaoni''

Katika mfufulizo wa mabandiko yajayo kuanzia Jumamosi tutajadili kwa kina haya

-Kampeni si sawa na kutawala

- Sera za Rais Trump za America first na protectionism

- China kama currency Manipulator

-Ujenzi wa ukuta kuzuia immigrants

-Travel Ban

- Healthcare

-Infrastucture spending

- National debt

-Tax cut

-NAFTA

-NATO

-US Military na kusambaa duniani

-Vita ya ISIS na Iraq

-Syria, Russia ,Iran na Korea

-Siasa za Mashariki ya kati ,Israel na Palestina

-Sakata la Russia na linavyozidi kusogea mtaa wa Pen wenye jengo namba 1600

Tutapitia kila kimoja kuyaona mabadiliko kama yapo ya sera za siku 100 zilizopita na zama za leo

Tusemezane
 
Sehemu ya I kati ya V

SIKU 100 ZA UTAWALA

Tumeeleza ni utamaduni tu tangu FDR 1933 kupima hatua alizochukua Rais nyuma ya Oval office
Hatua hizo ni za kueleza nini kimefanyika. Katika siku 100 FDR alipitisha miswada 15 mingi ya uchumi

Rais Trump katika siku za karibuni amekuwa na mahojiano na vyombo vya habari kama AP, Reuters, Fox n.k. katika kufafanua mambo kadhaa. Hili ni tofauti na kukutana na wanahabari, si kawaida yake

Hatua za dakika za mwisho ni katika kuhakikisha ana la kusema ndani ya siku 100
Kwa kawaida Rais huzungumza na wananchi, katika hali tofauti, Trump anaonekana kujali base yake

Kura za maoni ambazo kwake hutegemea matokeo anayotaraji zinaonyesha katika siku 100 approval rate yake ipo katika 40% kiwango cha chini sana kwa Marais wa US wa siku za karibuni

Hata hivyo, 96% ya 'base' yake inaamini anafanya kazi vizuri. Kama matkumbuka tuliwahi kusema katika kampeni, ana 30-40% inayosimama naye no matter what. Ni base loyal kwake

Katika mahojiano ya leo, Rais amekiri kuwa hakujua kazi ya Urais ni ngumu kiasi hicho na anapenda maisha yake ya awali. Hili limeshangaza watu , kwamba, Rais wao hakujua uzito wa majukumu

Wiki iliyokwisha Trump alikiri kutawala si sawa na kampeni. Katika uzi huu tulisema hilo siku nyingi.

Kabla ya hapo alikiri kuwa kufuta Affordable ACT (Obamacare) ni complicated kiasi hicho

Na siku za karibuni alikiri kuwa kutawala si sawa na real estate, kunahitaji mbinu na mambo mengi

Alieleza kuhusu mahusiano ya kikazi na House na Senate yalivyo magumu na yanavyohitaji maarifa

Katika sehemu hii ya I tuna summarized haya, Trump anakiri
Kazi ya kutawala ni ngumu kuliko alivyofikiri
Obamacare ni complicated kuliko alivyodhani
Kutawala si sawa na kazi ya biashara aliyofanya

Wanaofuatilia uzi huu kwa umakini , utulivu na kujifunza au kujadiliana haya si mageni tumeyajadili. Kwa wasiotaka kuelewa au waliogoma . Wajifunze

Inaendelea sehemu ya II
 
Asante sana, Mwalimu wangu. Na mimi nipo hapa kujifunza kwa kuchangia katika mjadala huu katika kulinganisha utawala wa US na utawala wetu ( wa Tanzania). Katika mjadala nitajikita kwenye vipengele ulivyovianisha kwenye posts zako hapo juu. Bado ninahoja za kiuanafunzi hivyo msisite kuniweka sawa.

Kwa kuanza ni guse kidogo juu ya kauli ya Trump kuwa "hakujua kazi ya Urais ni ngumu kiasi hicho na anapenda maisha yake ya awali". Kwa kauli hii inadhibitisaha imani yangu kuwa wanasiasa wa Marekani hawatofautiani sana na wanasiasa wetu. Rais wetu Dr. Magufuli aliwahi kusikika kutoa kauli inayofanana na hiyo. Baadhi ya watanzania walimdhiaki tena hapa JF. Leo tunaambiwa Trump mwanasiasa na rais wa Marekani analalamika hivyo hivyo nasubiri kejeli kwa watanzania hawa kwake. Kwa sasa nina hisi kwa asilimia nyingi kuwa rais wetu anaipenda kazi yake ya sasa (siamini hata kidogo kama anaichukia kazi zake za awali) mbali na changamaoto za kazi hiyo; kwa sababu ni kwa kazi hii ile Tanzania anayoitaka ya Viwanda, ya watanzania wanaojiamini, watanzania wanaojitegemea kiuchumi na kijamii naweza kwa kiasi kikubwa kuipata. Mimi namuombea kwa Mungu afanikiwe kwenye hilo (kuipata Tanzania anayoitaka na mimi naitaka pia) huku akizingatia haki kwa wote kama anavyofanya sasa.

Hata hivyo kama Trump ni mzalendo wa kweli kwa nchi yake, ataimudu kazi ya urais kama Rais wetu Dr. Magufuli (mzalendo na anayewapenda watanzania wote wanaotii taratibu na sheria za nchi) anavyoonyesha dalili zote kwa asilimia 100 kumudu kazi hiyo. Bahati mbaya sana Trump sidhani kama anawapenda wamarekani wote wanaotii sheria za nchi hiyo ingawa anaonyesha dalili za uzalendo kwa silimia 99.9999! Na hiki ndicho kimojawapo ya sababu kadhaa zinazonifanya nifikirie kuwa ataidhoofisha Marekani taratibu.
====
Updates:
----------
Donald Trump’s election strategy relied to a degree on the image of an anti-establishment billionaire who could fix a broken DC. Instead, his actions in office have been aligned with the policies of the same special interests he used to speak out against.
'Broken by US power machine': Trump’s 100 days prove his maverick image was fake
 
Nikikumbuka zile kelele za recount kule Wisconsin, Michigan, Pennsylvania nacheeeeeeeeeeka sana.

Hoja kuu iikuwa 'ni kwa nini Trump hataki warudie kuzihesabu kura kwenye hayo majimbo?'.

Baadaye yakaja mambo ya kuwashawishi electors wasimpigie kura Trump.

Hahahaaa....well...mwishowe walinyooka tu wenyewe.

Na yule bibi Jill Stein naye kapotelea wapi?

:D:D:D:D:D
 
Back
Top Bottom