Duru za siasa: Uchaguzi ni juu ya ilani/sera na hatma ya nchi



HATUJASIKIASERA ZINAZOONGOZA TAIFA


TUNASIKIAUTENDAJI, HATUJUI NI KWA ‘RAMANI IPI'


Ahadi zitolewazona wagombea ni majukumu ya kila siku ya serikali za dunia.


Kwa jichopana, tatizo si ahadi, tatizo ni namna gan/njia zipi ahadi zinaweza kufikiwa.


Kila mmojawetu anaweza kuorodhesha ahadi za ujenzi wa shule, barabara, madaraja n.k.kwavile atakuwa na mamlaka, pesa hazina,anaweza kuongea na wafadhili n.k.


Kwa mantikihiyo, wagombea zaidi ya 50 walijitokeza kuchukua fomu kutoka pande zote Kuna kituhatukijui au hatukiulizi. ni lini tumekaa tukaweka utaratibu wa kujiongoza kamataifa?


Utaratibu wakujiongoza una maana moja kubwa. Kwamba, vyama vinaweza kuingia na kutoka madarakaniwakati wowote, taifa linabaki na thamanizake (core values)


Utaratibu kwa maana ya katiba haukidhii haja ya wakati.Tulipiga kelele tuandike upya katiba kwa miaka mingi ijayo


Katiba inatupa dira ya namna gani tunataka kulijengataifa letu


Hatukujifunzamiaka 10 iliyopita mabilioni yalipotolewa kwa mtakwa tu ya watu na si sera zanchi. Hatuwezi kueleza yameleta tija gani kwasababu hatukuwa na mwongozo zaidiya ushabiki


Suala lakatiba tumelipa kisogo. Tunataka nyumbabila ramani. Wagombea hawatuambii nini misimamo juu ya nyaraka muhimuwatakayotumia kupata mamlaka ya kutuongoza


CCMwamekimbia hoja ya katiba. Tunakumbuka ubabe katika katiba. Wameandika na ipo kiporo. Hoja kubwa siku za mbeleni ni ‘hilo halikuwa tatizo la wananchi'' Wameweka kiporo wakisubiri muda.


Yes, watakuwana mamlaka na uwezo wakipewa madaraka.Wanatumaini kutumia ubabe kunyang'anya haki kama walivyofanya


UKAWA wamekaakimya kana kwamba hilo si taifa. Wameacha hoja iliyozizima vema masikioni mwawananchi. Hoja iliyowapa umaarufu na Imani mbele ya umma


Tuwaulize Watanzania,kwanini Magufuli/CCM hawaongelei katiba? Hivi siku wakileta katiba kiporowataulizwa nini?


Je, hilohatulioni kama tatizo la siku za mbeleni? Wanatuongoza kwa kutumia utaratibugani? Ule wa 1977 au huu walioandika wenyewe pale Dodoma?


Tuendelee kuwashangiliawakipiga push ups, tusije, tunarudia tusije lia tena kuhusu katiba. Wana yao nawala hatukuwauliza. Hawakutueleza nahatukutaka kuwauliza


Tusemezane



 
MM "tusiharakishe katiba,tukae chini" tukajitia upofu. Tunaposema Maendeleo ni Hesabu wanasema ni Kubadilisha vyama!!!
 
TUNACHOTAKA KUPATA na TUNACHOPASWA KUPATA, hatujui tapaswacho, tunalilia HULKA zetu! Maendeleo si mchezo bahati nasibu.
 
Back
Top Bottom