Duru za siasa: Uchaguzi ni juu ya ilani/sera na hatma ya nchi

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,410
31,395
UTANGULIZI

Uchaguzi ni tukio la kidemokarasia la kuchagua au kuchaguliwa kupata watakaokupewa madaraka


Si tukio la kupata ''watawala'' bali viongozi watakaotumikia wananchi

Ni muhimu kuwajua wenye madaraka kwa hulka na tabia ,maono, na wanachosimamia kupitia vyama vyao tu

Ni haki kwa wananchi kuwajua wagombea nafasi mbali mbali kwa hulka, tabia,na wasifu .

Ni muhimu kujua ilani/sera walizopewa si kwa maandishi bali wanavyozitafsiri na kuzijengea hoja. Tutalitolea mfano mbele

Nchi masikini zinazokumbatia demokrasia ya kujfiunza tunachagua viongozi kama watu, kwa muonekano na ubabaishaji wao

Tawala za kiasili za machifu zilizingatia mrithi wa kiti kwa tabia, maono , unyenyekevu na sifa za uongozi.

Aghalabu, mrithi mtaraJiwa angeweza kuachwa kwasababu tu hakidhi vigezo na si kuwa ndiye mrithi anayefuata


Na wala si kwa Afrika tu, Uingereza ilishatokea mfalme ‘akaachia ngazi' (King Edward VIII 1936-Abdication)

Kwa Waafrika limekuwa tatizo. Tunaangalia mambo yasiyo na umuhimu kuliko tunayopaswa kuyatolea uamuzi kweye kura

Nchini, mijadala imetawaliwa na hisia, fitna, majungu n.k.

Tumeusahau ilani/sera zitakazotumika ‘kutusaidia au kutuhukumu' Mwisho tunavuta viti na majamvi tukilalamika.

Tuliowapa madaraka kwa upuuzi wetu wa ‘homeboy' au kabila,kanda na dini wanajilimbikizia

Mwishowe kutuporomoshea mitusi wanapo mnadi mlinzi wa malimbikizo anayefuata. Si wao ni sisi wajinga, hatukuangalia


Ni kwa msingi huo, tunaona umuhimu wa majadiliano kuhusu wagombea na ilanisera.

Bila kufanya hivyo tutarudi kujiuliza inakuwaje tuliwachagua wakiwa hawajui kwanini sisi ni masikini.

Tutajiuliza kwanini umasikini unatopea badala ya kupungua.


Tutabaki taifa mahiri la walalamikaji, na la wazembe wa kufikiri

Tunaangalia kwa fikra katika mabandiko yajayo

Inaendelea….
 
Sehemu ya I

ILANI/SERA

Kwanini tuantakiwa tuangalie ilani/sera?

Kwanza tufahamu sera(Policy) na Ilani (manifesto ) ni vitu gani

Ilani ya uchaguzi ni tamko mbele ya umma juu ya sera na chama husika.

Hivyo, Ilani imebeba sera, na sera ni sehemu ya ilani katika eneo fulani

Kwa mfano, ukisema ilani ya uchaguzi ya chama X kuhusu mambo kadhaa hiyo ni Ilani. Sera itafafanua mambo hayo

Katiba 1977 inampa Rais madaraka makubwa hata ya kubadili au kuanzisha sera kinyume na ilani ya uchaguzi

Kwavile hatuzingatia ilani za uchaguzi,tunalishwa ahadi hata kama hazina ukweli na si misimamo ya vyama

Mfano, Ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 haizungumziikatiba.Jambo kama muungano ni sera ya serikali 2

Mwaka 2012, Mwenyekiti/Rais akatangaza mchakato wa katiba mpya, kinyume na ilani na sera za CCM.

Rais hakufanya makosa kwa mujibu wa katiba yetu,anaweza kutenda jambo hilo katika misingi halali

Swali la kujiuliza, je ndicho alichowaambia wananchi wakati wa kampeni?

Je, ndilo wananchi walilomtuma wakati wa kampeni au kupitia wawakilishi wao? Jibu ni hapana

Je, alifanya kinyume cha sheria? Jibu ni hapana. Kilichotokea ni kukiuka ilani ya CCM

Kwa weledi, hakuna kosa lililotendwa, bali wananchi bila itikadi zao walipaswa ‘kuiadhibu'ccm kwa udanganyifu

Madhara zaidi ni ya mchakato kumilikiwa kwa taratibu halali, ukipoka haki za wananchi kuhusu hatma yao.

Mchakato ukaendeshwa kisiasa badala ya wananchi kushiriki kama wadau wakubwa

Katiba imeshindikana, hatuwezi kuilaumu CCM kwani haikuwa sera yao.

Tunawaulaumu kwa kudandia sera isiyokuwepo katika ilani yao na kuleta yaliyotokea.

Hatuwezi kumlaumu mwenyekiti wa CCM aliyeanzisha mchakato, katiba inamruhusu.

Tujilaumu, hatukumuuliza wakati wa kampeni, wala hatukuhoji kwanini CCM waliteka jambo nje ya ilani yao

Wananchi hawakuangalia mambo muhimu ya mgombea , Ilani au sera . Wlisukumwa na hoja hafifu, 'anafaa'

Makosa yanaendelea, kuongelea nani anakipara nani ana suti nzuri badala ya sifa za uongozi

Inaendelea
 
Sehemu ya II

ILANI/SERA ZINAFAFANULIWA NA WAGOMBEA?

Baada ya ''kusomewa'' Ilani yenye sera tunapaswa kuangalia kuziangalia katika uhalisia wake

Kwa mfano, kama sera ni ya elimu, sera hiyo inasemaje, inajibu vipi hoja za jamii,inatekelezwa vipi,na rasilimali zipi

Hojakubwa si elimu ya bure, ni je elimu inayotolewa inakidhi haja ya wakati tulio nao na ujao?

Matatizo ya elimu ni ya yapi, na nini kifanyike. Hizi habari za elimu ya bure bila kuonyesha undani wake hazina mashiko

Kwa dunia ya sasa , elimu ni sehemu ya uchumi. Si kuwa uchumi unawezesha elimu bali vinategemeana

Elimu si laptop za bure,ni suala linalohusisha sera, mipango, utekelezaji. Haya tunayosikia sasa ni hayaelezi kwa kina.

Hivi unawezaje kutoa laptop kwa shule chini ya mbuyu, na mwalimu anayeishi nyumba ya nyasi?

Laptop inamsaidia vipi mwalimu anayetumia mkaa kuandika katika ubao? Je, tumewaluliza haya wahusika!

Wagombea wanatambua sisi ni wavivu,wanaorodhesha matatizo, si kueleza sera na jinsi gani zitatatua matatizo husika

Kwa mfano, mgombea anaposema ataimarisha huduma za afya,aeleze huduma zipi, na kwa njia zipi na rasilimali zipi

Kama ni suala la kuorodhesha matatizo, kila mmoja anawezakuwa mgombea Uraisi

Akitokea mtu na kusema atatua matizo ya maji, atakuwa amegusa sehemu ya jamii kwasababu tatizo la maji ni la kitaifa?

Je, anafaa kuwa mgombea wa Urais kwa vile tu anaweza kurodhesha matatizo?

Watanzani ni watu wa aina ya pekee. Takribani mwezi, hoja zinazoongelewa ni wingi wa watu katika mikutano

Hoja za mgombea gani kavaa suti nzuri na yupi kapiga chafya bila leso. Hatuangalii mambo yanayogusa maisha yetu

Wanasiasa wanajua udhaifu wetu na wanautumia

Lengo ni kupata madaraka kwanza, mengine yatatafutiwa ufumbuzi wakiwa katika viti vya enzi

Mfano, ukiangalia CCM na‘'UKAWA'' suala la muungano halijazungumzwa, kuogopa kuudhi makundi ya jamii

Tujiulize ,hawa wanaotaka madaraka, wanakusudia nini kuhusu suala hili nyeti kama hawaliongelei leo?

Je, huu si udanganyifu kama ule ukimya, baada ya kupata ‘ukuu' wanaanzisha mchakato kwa nia zao na si zetu!

Rais ajaye akiwa wa Lumumba au Ufipa, akaamua kuandika katiba na kusaini, tutambana vipi kupitia ilani ya uchaguzi?

Yatajirudia ya CCM, katiba si sera ya chama. Tutawajibu nini, ikiwa walipita na hatukuwauliza

Inaendelea....
 
Sehemu ya III

Uchaguzi ni mradi (project) kama mingine ingawa tofauti za maana halisi zinaweza kutoshabihiana.

Kwa vile ni ''mradi'' tunawajibu wa kuwangalia watakaoongoza kwa sifa njema/mbovu na wasifu (Resume au CV zao)

Tutathmini kile kinachoitwa SWOT matrix nguvu,udhaifu, fursa na tishio(strength/weakness/opportunities and threat)

Tuangalie maono yao kama wao (vision) na jinsi wanavyotetea sera za ilani zavyama vyao (manifesto/ policy)

Katika mjadala tuhoji ''specifics au details'' kwa uyakinifu na kina cha hoja .

Mfano, moja ya sera za CCM ni ‘kilimo kwanza' kwanini inahitajika, italenga nini, kupata nini na kutumia rasiimali gani.

Je, kilimo kwanza ya awali imefanikiwa kiasi gani na imeshindwa kutokana na nini

Sera za ‘UKAWA' moja ni elimu. Je, imelenga nini, kwa nani, italeta nini naitafanikishwa kwa njia zipi

Vyama vyote vimewalenga vijana na ajira. Vijana wapi wamelengwa, takwimu gani zitatumika kutuonyesha matokeo

Vyama vyote vinaongelea suala la kufufua viwanda

Tuangalie,ni viwanda gani? Vya toothpick na toilet paper! Vya kusindika, vya kuunganisha au vya kutengeneza?

Vimawelenga akina nani, vijana wote au makundi fulani?

Kwanini viwanda vilivyokuwepo vimekufa, nini kitakuwa tofauti safari hii ili miaka 5 visife tena

Elimu: Tuhoji,wanasema elimu ni bure hadi chuo kikukuu. Kwasasa, wanafunzi hawapati mikopo kwa uhaba wa fedha.

Hiyo ya bure kwa kila mmoja itawezekana kwa kutumia vyanzo gani vya mapato?

Na inakuwaje haikuwezekana sasa , itawezekana miaka 5 ijayo?

Inaendelea..
 

Wagombe wote wa CCM/UKAWAwametumika serikali za sasa, ni kipya kipi watakifanya kufikia malengo?

Nini andhani hakikuwa sawa ambacho wanategemea kubadili

Moja ya matatizo tuliyo nayo ni mfumo mbaya wa uendeshaji washughuli zetu.

Kwamba,mfumo unaruhusu uhalifu na haujali kuwajibika kwa kila mmoja wetu.

Mfumo hautengenezi maridhiano katika masuala kama ya kitaifa.

Yotehayo yanaweza kubadilika tukibadilisha utaratibu unaotuongoza kisheria na taratibu

Tuwaulize, wanasimamia wapi katika masuala ya katiba,muungano, miundo ya serikali za miji, vijiji n ahata kata?

Hoja zipo chini ya mwamvuli wa uchumi.

Tuwaulize,nini watafanya ili kuweza ku-balance bajeti yetu. Kuacha utegemezi, kuongeza wigio wa mapato .

Nini watafanya kukuza sekta zinazochangia mapato

Sera zao kuhusu madini, mali asili, utalii na biashara zimelenga kufikia nini na zitalisaidiaje taifa

Haya ni kwa uchache na muongozo tu tunategemea yataongezekakadri tutakavyochangia hoja

Ni muhimu kukumbuka, ahadi za mtu au watu si sehemu ya sheria za nchi.

Mwaka 2010 kila kijiji kiliahidiwa jambo kadhaa.

Leo hakuna ahadi iliyotimizwa na wahusika wanakwenda kupumzika.

Wametudanganya sasa ni wakati wao wa mapumziko.

Bado tunarudia makosa yale yale, hatuwaulizi tunashangilia suti, na vipara vyao, vitambi n.k.

Lazima tuwabane. Habari za laptop zinazotumia mafuta ya taa ni hila na udanganyifu tunaopaswa kuukomesha.

Kama hatuanzi leo, tujiandae November 1 kusikia tusiyotarajia, nasi kubakl tukialalamika

Wametufanya wajinga, tukikubali tutakuwa wajinga zaidi

Kabla ya kuendelea, tuweke kituo ili kusikiliza jamvi linasema nini kisha tutachangia

Wanajamvi karibuni

Tusemezane
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-kuhusu-kufikiria-kwetu-kuhusu-watawala.html

Picha kwa hisani ya MzeeMwanakijiji

Hapa kuna maswali

1 Tuanze kujenga shule upya?

2 Tutoe elimu bure kwa waliomo ndani ya jego?

3 Tutoe laptop kwa kila mwalimu?

Kuna fikra kidogo,kwanini imetokea hivi? Ni ubovu wa sera au wa wasimamizi huko Darisalama?

Kwanini hawasemi watafanya nini kuhusu jengo kama hilo , wanatushawishi upo uwezekano wa kusomesha bure waliomo ndani ya mjengo wakifaulu kwua hai

Kwanini hatuwaulizi katika kampeni, hali kama hiyo ipo miaka zaidi ya 20! Nini watafanya ndani ya miaka 5 kuibadili hali hiyo, kwa rasilimali gani !
 
Asante sana Nguruvi3 kwa bandiko lako.. TNaomba muda wa kumlilia kijana wetu na nafikiri nina haki ya kulia maana ndio dawa ya kuondoa uchungu nilio nao...
Kwakweli kuna machungu!
Niligoma kuamini hadi walipofikia watu 4000 wakichangia ndipo nilipoamini .

JokaKuu kamwelezea kwa ufupi sehemu fulani,nikabubujikwa na machozi.

Mwenyezi munguampunzishe kwa amani

 
Last edited by a moderator:
Ndugu Nguruvi3,

Naomba niwe wa kwanza kutoa hoja.

Sisi kama wananchi na Jamhuri, nadhani tumepotea katika nyika yenye miiba, majabali na vichaka vinavyotufanya tupoteze ufahamu na kushindwa kabisa kujitambua.

Tunalalamika kunaswa huku ndani ya nyika kukiwa na jua la mchana, ilhali tunakosa mwamko wa maana kutuliza akili zetu na miili yetu, tujipange sawa kuondoka kwenye nyika kabla ya usiku wa kiza tororo kuingia.

Kijamii, tumejijenga sana kutegema mtu, watu au kikundi fulani kushika hatamu na kutuongoza. Nguvu za kujituma tuwe washiriki kamili kulifyeka pori au kuitafuta njia thabiti yenye kutuepusha miiba, vichaka, visiki na majabali hatutaki kuzitumia kwa umoja au wingi kwa pamoja, bali tunayajaza mapafu yetu na hewa ya kulalamika, kipiga vijembe, madongo, udaku, mipasho na kusengenyana. Mwisho wa siku hubakia kulalamika kuwa giza linaingia tumekwama nyikani na tunazama msituni!

Haki hii ya sisi kuwa washiriki wa dhati tumeitupa na kuwakabidhi wengine jukumu hilo na kila miaka mitano tunafanya "renewal" ya hiyo delegation of authority.

Vyama vinapojiunda, hutokana na mtazamo na utashi/msukumo wa nia ya kufanya jambo fulani kwa niaba ya jamii nzima. Ndio maana tuna viongozi.

Tunatoa imani yetu kwa watu tunaoamini kwa dhati kuwa wanatufaa kuwa viongozi, tunajisalimisha haki zetu za upeo wa mawazo na fikra na kuwapa mamlaka kamili watuundie falsafa za kisiasa na kiutendaji katika azma yao ya kuongoza nchi.

Cha kwanza cha msingi ni Vision (maono ya mbali), Goals and Objectives (malengo na makusudio) kinafuatiwa na Ideology (itikadi-Imani), kisha Manifesto (ilani-katiba) inayokwenda sambamba na Policy (sera-mipango) tukitoka hapo tunatunga Bill/Laws (Miswaada/Sheria) na kujenga Governing Principles (kanuni), Planning (mipango), Communication (upashanaji wa habari) na kazi ya kwanza huanza implementation/Production (utekelezaji/uzalishaji).

Katika maisha ya Vision (life cycle) kuna checks and balances (ukaguzi, ufuatiliaji), kuna mambo ambayo tunayaweka kama vigezo (criteria) za kuhakikisha kazi inafanyika vizuri :Vitendea Kazi (resources)Majukumu (responsibilities) Umakini (thoroughness), Ufanisi (efficiency), Uimara (Sustainability) Uwajibikaji (accountability), Uadilifu (integrity), Usimamizi/Ufuatiliaji (supervision and follow up), Ukaguzi (quality check), Juhudi na Tija (efforts) Maarifa (expertise/knowledge) kupima (measuring) Maoni (feed back) na matokeo (results-end product).

Nimechukulia mkondo wa kisayansi na falsafa kuanza kujenga hoja yangu kwa kuwa pamoja na kuwa tunaangalia uchaguzi tulionao hapa mbele yetu, lakini kuishibisha hoja yako na madhumuni makubwa ya kutuletea hoja hii na masawli uliyoyaweka, ni vyema tujipime tulipo nyikani tufanyeje kuweza kuondoka nyikani kwa salama.

Siasa na uongozi zinapaswa kuwa ni mfumo na wenye mtiririko kama huu ambapo ama jamii kwa ushiriki wa kila siku au kwa dhamana ya mtu, watu au chama wanapaswa kuyaweka na kuyapa kipaumbele ili kufikia lengo maalum.

UKiangalia kwa makini, ni kweli uchaguzi huu kwa mara nyingine pamoja na kuwa na utashi mkubwa sana wa "kisomi", bado kama nafsi mojamoja na Taifa kwa ujumla tumejikita katika vihoja na matukio yanayobebwa na hisia, ushabiki na uvivu wa kuhoji na kushindwa kuuliza maswali ya msingi kupima tulikotoka, tunakotaka kwenda, tunachoambiwa kuwa ni sahihi au ndio njia muafaka, malengo na matokeo yake ya muda mfupi na muda mrefu.

TUnajifahamu kuwa ni masikini, wanyonge na ni ombaomba. Kwenye self assesment tunatambua tuna matatizo ya elimu duni, mfumo dhaifu wa uzalishaji wa kilimo na viwanda, mapato hafifu, kutapeliwa ama kwa hiari kupitia mikataba ya kiuchumi na mashirika ya nje na nchi za nje au hujuma za ndani ya nchi zinazotukosesha mapato ya kutuhudumia kwa kila tunachokitaka.

Je pamoja na ufahamu huu, tunafanya nini kurekebisha kasoro (fix and correct the deficiencies and inefficiency/ineffectiveness) ambazo tumezilea miaka nenda rudi kwa kutoa imani na dhamana kwa watu ambao uwezo wao na maono yao hayawezi kututoa nyikani na usiku unaingia tukiwa hatujielewi tunakwenda wapi.

NItaendelea baadae.....
 
Wananchi na Jamhuri, nadhani tumepotea katika nyika yenye miiba, majabali navichaka vinavyotufanya tupoteze ufahamu na kushindwa kujitambua.Tunalalamika ilhalitunakosa mwamko wa maana kutuliza akili zetu

Kijamii, tumejijenga sana kutegema mtu, watu au kikundi fulani kushika hatamuna kutuongoza.
Nguvu za kujituma,mwisho hubakia tumekwama nyikani na tunazama msituni

Cha kwanza cha msingi ni Vision (maono ya mbali), Goals and Objectives (malengona makusudio) kinafuatiwa na Ideology (itikadi-Imani), kisha Manifesto(ilani-katiba) inayokwenda sambamba na Policy (sera-mipango) tukitoka hapotunatunga Bill/Laws (Miswaada/Sheria) na kujenga Governing Principles (kanuni),Planning (mipango), Communication (upashanaji wa habari) na kazi ya kwanzahuanza implementation/Production (utekelezaji/uzalishaji).

Katika maisha ya Vision (life cycle) kuna checks and balances (ukaguzi,ufuatiliaji), kuna mambo ambayo tunayaweka kama vigezo (criteria) zakuhakikisha kazi inafanyika vizuri :Vitendea Kazi (resources)Majukumu(responsibilities) Umakini (thoroughness), Ufanisi (efficiency), Uimara(Sustainability) Uwajibikaji (accountability), Uadilifu (integrity), Usimamizi/Ufuatiliaji(supervision and follow up), Ukaguzi (quality check), Juhudi na Tija (efforts)Maarifa (expertise/knowledge) kupima (measuring) Maoni (feed back) na matokeo(results-end product).


Taifa kwa ujumla tumejikita katika vihoja na matukio yanayobebwa na hisia,ushabiki na uvivu wa kuhoji na kushindwa kuuliza maswali ya msingi kupimatulikotoka, tunakotaka kwenda, tunachoambiwa kuwa ni sahihi au ndio njiamuafaka, malengo na matokeo yake ya muda mfupi na muda mrefu.

TUnajifahamu kuwa ni masikini, wanyonge na ni ombaomba, tunatambua tunamatatizo ya elimu duni, mfumo dhaifu wa uzalishaji wa kilimo na viwanda, mapatohafifu, kutapeliwa ama kwa hiari kupitia mikataba ya kiuchumi na mashirika yanje na nchi za nje au hujuma za ndani ya nchi zinazotukosesha mapato yakutuhudumia kwa kila tunachokitaka.

Je pamoja na ufahamu huu, tunafanya nini kurekebisha kasoro (fix and correctthe deficiencies and inefficiency/ineffectiveness) ambazo tumezilea miaka nendarudi kwa kutoa imani na dhamana kwa watu ambao uwezo wao na maono yao hayawezikututoa nyikani na usiku unaingia tukiwa hatujielewi tunakwenda wapi...
Mkuu naomba nichangie wakati tunasubiri umalizie hoja zako. Niwie radhi kuingilia mtiririko, hoja zako zimenikuna kupita kiasi

Kwa maoni yetu maneno nukuu hapo juu ndiyo mabadiliko. Kwamba, yubadilike katikakufikiri na kuamua

Miaka 50 inatosha kutambua tupo njia sahihi au la. Inatosha kujitathmini si kwa kujiangalia wenyewe na kushusha viwango vyetu vya ufaulu, bali kuangalia wenzetu tuliokuwa nao kama Singapore wapo wapi

Singapore ilijitenga kutoka Malaysia mwaka 1965 chini ya Lee Kuwan Yew (LKY) waziri mkuu wa kwanza.
Singapore haikuwa na rasilimali zozote na ilikuwa third word kama sisi

Miaka 50 baadaye, Singapore ni nchi ya dunia ya kwanza. LKY amebadili nchi kwa miaka10 na kuanzia hapo wanapaa

Vision ya LKY,ilikuwa kujenga taifa lisilo na rushwa na la wanaowajibika (Corruption free society and accountability)kwa falsafa ya Meriitocratic .

Falsafa hiyo ina tafasiri nyingi, moja ya hizo ni serikali kuendeshwa kwa utilitarian and pragmatic.

Utilitarian ni aina ya mlolongo(consequentialism) unaosema kipimo cha jambo ni matokeo ya kutenda kwa usahihi au makosa

Na pragmatism inatafsiriwa kama chombo cha maono, utatuzi na vitendo. Hizo mbilin dizo zinaunda meritocratic ya LKY

Hadi hapo tunaona LKY alikuwa na vision, philosophy and Ideology. Kupitia hayo matatu ndani ya meritocratic, LKY akatengeneza manifesto, policy, criteria,accountability na mwisho kapata results, i.e Asian Tiger then first world Singapore

Miaka25 ya mwanzo tulikuwa tunajenga uwezo, vyanzo vya nishati, elimu, huduma za msingi za afya na elimu.
Tuliweza kujenga viwanda vya toothpick, nyembe, ndala na khanga kuelekea katika ujenzi wa viwanda zaidi
Vision ya Nyerere wakatyi huo ilikuwa kuejnga uwezo, na kuona mbali tatizo la ajira kwa vijana ndani ya miaka 50 tuliyopo

Miaka 25 tumesomewa ilani na sera zile zile za CCM zilizotumika miaka 50.
Tena kuna upungufu maana mgombea wa CCM anapozungumzia kufua viwanda, huko ni kuvia kwa akili ni uzezeta mzuri tu

Viwanda vimeuawa na CCM na hao walioua leo wanataka kuvifufua. Kana kwamba, hatuna watu wanaoweza kufikiri tofauti

Miaka10 iliyopita haina kipimo, leo wanakuja na habari ya kututoa msituni.

Kama hawakuweza miaka 10 au 25 watawezaje miaka 5?

LKY aliweza kwa miaka 20 tu leo Singapore ni nchi ya dunia ya kwanza.

Sisi tuliopata Uhuru miaka 4 kabla ya Singapore tupo katika kundi la nchi 25 masikini sana duniani.

Kwamba, hata uchumi wa kati hatupo. Lazima kuna tatizo na tujiulize kama hatuchukui hatua leo tunasubiri lini na kwanini?

Hatuwaulizi hao CCM kwanini sisi ni masikini sana duniani na tumefikaje hapo.
Tunawashangilia tukiwa na njaa na kaniki kufunika sehemu zetu nyeti. Hatufikiri zaidi! Hatuwaulizi kwanini tupo hapa

Hatuhoji kwanini hawakuweza elimu na afya, tudhani wanaweza leo.

Hatuwaulizi kwanini wanashusha viwango vya ufaulu , tunasngilia elimu bure hata bila ya namba.
Kana kwamba, elimu ni fungu la nazi tutakaloletewa kutoka Mkuranga.

Hatuulizi kabisa yanayotuhusu ya kila siku. Kwanini kuna academy, kwanini wanafunzi wanafeli, kwanini wanakosa mikopo.
Kwanini wazazi waende kujifungua kwa kununua nyembe, lakini tuaminishwe elimu ya bure. Hatuulizi

Tunashangilia ahadi za kuletewa mwezi na nyota katika sebule zetu

Hatuwaulizi wagombea nini falsafa zao kama tulivyoona hapo kwa LKY.

Tunabaki na vihoja na viroja, tukiwachekea, shamba la mahindi likimalizwa


Wanajua sisi ni matutusa, hawana aibu. Wana photocopy ilani na kuziweka katika karatasi za rangi wakisema wanaleta mabadiliko

Hatuwaulizi, mabadiliko yapi? Na wala hatuwaulizi kabisa, tunapiga vigegele, vifijo na nderemo.
 
Sera na Ilani hutangaza na kubainisha kusudio la mtu katika wajibu wake kama kiongozi, na huundwa kwa makubaliano ya kichama.

Kwa Tanzania, tumegeuza Sera na Ilani kuwa mapitio ya wajibu wa kila siku, bila kuweka wazi ni vitu gani vitapewa vipaumbele katika kipindi fulani.

Ni kutokana na mapungufu ya umakini, madhaifu ya mipango na papara za kufanya kila kitu kwa wakati mmoja na kukipa kipaumbele, uzorotaji wa maendeleo umeongezeka, kero na masumbufu kwa jamii yameongezeka na Sera na Ilani zinajaa madudu mengi yasiyoeleweka.

Mfano, tuchukulie Chama tawala ambacho ndicho pekee Sera an Ilani zake zimeweza kufanyiwa kazi kutokana na kuwa madarakani kwa maiaka yote tangu tupate uhuru. Je ni mafanikio gani tumeyapata ya kudumu katika sera yake ya elimu?

Ilani ya CCM itasema tumejenga au tutajenga nyumba za waalimu 10 kila mwaka, fedha zitatengwa kisha nyumba zitajengwa. Je mfumo wa elimu umenufaika vipi kwa walimu kujengewa mahali pa kujisitiri? Je kero masumbufu yanayowapata waalimu na wanafunzi yatatatuliwa na ujenzi wa nyumba 10?

Kama nyumba hizi 10 zingekuwa kwenye mpango wa maendeleo ya kujenga nyumba bora na bila kujali ni Polisi, Wauguzi au Madaktari, basi kusudio la kujenga nyumba lingeeleweka.

Lakini swali linakuja je mwalimu huyu akiachishwa kazi au kuhamishwa, hii nyumba si anahama? hivyo lengo la kumjengea nyumba linageuka kuwa mwananchi huyu, alipewa nyumba hii kama "mkopo" au kuazimwa.

Sasa kwa sisi wengine wenye ujamaa wa mrengo wa kibepari tutauliza, kwa nini mwalimu hakuwezeshwa kupitia mkopo nafuuu kujenga nyumba yake bila kujali nafasi yake? Kwa nini suala la kila mtu kuwa na nyumba bora lisiwe ni msukumo wa kutoa mikopo na kuwawezesha watu wawe na nyumba zao wanazozimiliki na kurudisha mikopo (hata usio na riba) kwa serikali na kuondoa dhana potofu ya utegemezi?

Hapo nimeonyesha ni jinsi gani sera moja inaweza ingilianan na ingine lakini kutokana na ukosefu wa umakini, tunaweza kusema Sera ya elimu imeendelea kwa Mwalimu kujengewa nyumba.

Sasa utakuta kuwa sekta hii ya elimu ina matatizo mengine: ukosefu wa vyoo, madawati, lishe, vitendea kazi vya waalimu na wanafunzi, maji na chanjo za kinga. Hapo hatujazungumzia mitaala, ukubwa wa darasa, idadi ya waalimu, uwezo wa kitaaluma wa waalimu, ushiriki wa wazazi katika mfumo wa elimu na masomo ya mwanafunzi.

Kwa haraka haraka, utaona kwa kuangalia suala la elimu pekee, kuna masuala ya afya, lishe, nyumba, maji, fedha (mikopo) na mengine mengi yanayoingiliana ili tupate kuwa na mfumo mzuri wa elimu utakao zalisha wahitimu (si kufaulu mitihani pekee) wenye uwezo wa kuinia katika uzalishaji ama kwa kujiajiri au kuajiriwa.

Tulipopata uhuru, tuliweka umuhimu katika Sera ya elimu katika kujua kusoma, kuandika na kuhesabu. Hivi vitatu vilikuwa ni vitu vya msingi, tukapanua wigo kwa kutaifisha shule ziwe mali ya umma kutoa nafasi sawa kwa wananchi, tukatoa elimu ya UPE na Elimu ya watu wazima.

Tukafungua shule za ufundi, vyuo vya waganga, mabwana shamba, mifugo, uvuvi, ualimu na fani nyingine ili kupanua uwezo wa kielimu na kutoa nafasi/fursa kwa wananchi kujichagulia fani wanazozitaka ili kushiriki uzalishaji mali.

Lakini katika utekelezaji wa sera, tukasahau vitu vingi na badala ya kurudi kwenye ubao na kuandika upya na kuhoji kila kifungu cha sera hizo za elimu, tukaanzisha sera mpyampya zenye malengo ya kutoa matunda ya haraka haraka, kukawa na compound effects kama nyumba za waalimu, ada na karo, vitabu na utitiri wa mambo mengi ambayo yamefanya mfumo wetu wa elimu kuzorota.

Hivyo kwa kushindwa kuwa na umakini, kushindwa kukaa chini na kuangalia mfumo wa elimu kwa mapana, tuliona kuwa tukiongeza majengo na kutoa fursa za kila mtoto kuvaa sare ya shule, kwenda akiwa na kidaftari kimoja, kalamu, dumu la maji na ufagio wa chelewa kusafisha mazingira, basi kuwepo kwake shuleni tutakuwa tumetoa elimu kwa Taifa.

Mtoto huyu, anatoka kwenye nyumba ambayo lishe ina shida, maji hakuna, kipato cha ndani hakitoshelezi kustawisha familia. Anafika shuleni analazimika kwenda tafuta kuni, kuteka maji mtoni ili waalimu wapate kuni na maji ya nyumbani kwao, ili chakula cha shuleni kipikwe, anabanwa na haja, choo hakionekani, anakimbilia msituni au choo kimefurika, hana dawati, mwalimu ana matatizo mengi nyumbani, mshahara kacheleweshewa, hivyo kiwango na ubora wake kufundisha wanafunzi ni hafifu.

Kifupi wote (Mwalimu na Mwanafunzi) wanakutana Darasani na Shuleni wakiwa na matatizo lukuki yanayofanya kubadilisha kabisa malengo halisi ya kuelimisha, na huishia kuwa na masomo yanayolenga ufaulu, bila kujenga uelewa, nadhari ainayokosa vitendo, lugha na vitendea kazi vugumu visivyosaidia kuelimisha mwanafunzi.

Leo tunapokutana na wale ambao walibahatika kusomabila adha (watoto wa jamii ya kipato cha kati na cha juu) au wageni wa nje (wakenya, makaburu, wazungu) kisha kwa uchache wao wnapewa nafasi za kuajiriwa na kuaminika kufanya kazi na kupewa majukumu, tunashindwa kujielewa hata kuangalia tatizo liko wapi.

Aidha tunashindwa kuainisha kwa umakini kuwa sera ya elimu si fanisi, ina mapungufu ambayo kwa msingi yanatukwamisha kuwa na maendeleo tunayoyataka.

Tunapoangalia uchaguzi huu na hata tukishapata Rais, Wabunge na Madiwani, kazi ya kuhakiki na kupitia Sera ya elimu haiishi mpaka miaka mitano ijayo.

Ni kazi endelevu na hivi viraka vya division 5 au kubadilisha mfumo wa mitihani si jibu.
 


Mkuu Rev. Kishoka
Nianzie hapoulipoanzia. Umesema ‘watanzania tumegeuza sera/Ilani kama mapitio ya wajibu wakila siku''

Inashangaza wagombea wanaposema watahakikisha wafanyakazi wanapata mishahara kwa wakati.Hii haiwezi kuwa sera/Ilani bali wajibu wa kila siku

Umeongeleasuala la elimu. Kwamba, wagombea wanatoa ahadi za ujenzi wa nyumba za walimu.Kwao nyumba za walimu ndilo tatizo la elimu nchini

Kwa uhalisia, sera/Ilani inatakiwa itambue tatizo la elimu, ilieleze na kuonyeshaufumbuzi wake utakuwa nini kwa mujibu wa chama husika

Tatizo laelimu linaweza kuwa pana kuliko linavyooneka. Inaweza kuwa ni walimu wasiofuzu, mitaala mibovu, sera mbovu, masilahi duni, mazingira mabovu, kukosekana vitendea kazi bora, kukosa mwamko kwa wazazi n.k.

Hayo ndiyo yanayoangaliwa katika sera/Ilani kwa undani na kutolewa majibu kama tatizo la elimu na si kuahidi mishahara kwa wakati

Mfano waPili, nani anajua sera/ilani ya vyama kuhusu katiba na suala la muungano.
Matokeo ya kutouliza haya ni hasara kama ya bunge la katiba.
Vurugu zotezilitokana na kutojua sera/ilani za vyama zikoje na zinaweza kuonanishwa vipi



Haya ni mambo yanayotakiwa kuwekwa mezani. Si ya mapitio kama ujenzi wa barabara.
Ujenzi wa barabara si sera/ilani ni jukumu la kila serikali ya dunia.


Sera/Ilani inaweza kuwa mawasiliano, na katika hilo mkazo unaweza kuwekwa katika eneo fulani kama ujenzi wa barabara au reli.

Kama ulivyosema, huwezi kuwa na ilani/sera zinazozungumzia barabara, reli, boti nameli kwa wakati mmoja.
Lazima kuwe na kipaumbele ambacho ni sera/ilani. Kipaumbele hicho kijibu hali ya wakati na matarajio ya siku za mbeleni


Kwa mfano,ukisema reli katika std, hapa ielezwe, reli hiyo imelenga nini kwanini na kwa matokeo gani.
Kuiongelea reli tu bila kueleza hayo, ni sawa na kuongelea majukumu na wajibu wa serikali wa kila siku kama sera/ilani, Kosa!
 



Sera/Ilani inaweza kuwa mawasiliano, na katika hilo mkazo unaweza kuwekwa katika eneo fulani kama ujenzi wa barabara au reli.

Kama ulivyosema, huwezi kuwa na ilani/sera zinazozungumzia barabara, reli, boti nameli kwa wakati mmoja.
Lazima kuwe na kipaumbele ambacho ni sera/ilani. Kipaumbele hicho kijibu hali ya wakati na matarajio ya siku za mbeleni


Kwa mfano,ukisema reli katika std, hapa ielezwe, reli hiyo imelenga nini kwanini na kwa matokeo gani.
Kuiongelea reli tu bila kueleza hayo, ni sawa na kuongelea majukumu na wajibu wa serikali wa kila siku kama sera/ilani, Kosa!

Sasa ndugu Nguruvi3 naona unaingilia mtiririko wa mawazo yangu in advance, na sidhani kama nina electrons kichwani zinazotuma mawazo yangu kwenye cyberspace!

Jioni hiii nilidhamiria kuja na kuongelea suala la Barabara kama sera, lakini si shida nitaendelea na kulipambanua na kuonyesha mafupi ya kuonyeshwa wajibu kuwa Sera au ishara ya ushindi kuleta maendeleo.

Hakuna sera ya barabara, madaraja au reli. Sera inayoweza kuelezeka ni ya miundombinu na mawasiliano.

Ujenzi wa barabara ni sehemu ya uimarishaji wa miundo mbinu, ni sehemu ya bajeti ya serikali katika kuboresha miundombinu.

Lakini si kweli na si ustaarabu kulaghai Taifa kusema mafanikio ya Serikali ni kujenga barabara au kudai ni Serikali ya Chama fulani au Chama fulani ndio imeleta barabara. Huko ni kuwadharau wananchi na kuwatusi na si sera hata kidogo.

Wananchi wametoa zabuni ya kutaka mtu atakayefanya kazi kwa niaba yao kutekeleza matakwa yao, zabuni hii hupitisha kwa mfumo wa uchaguzi mkuu na kura.

Matakwa ya wananchi ni mengi : shughuli za maendeleo na uzalishaji, huduma za jamii (afya, elimu, maji, ajira), kusimamia na kukusanya mapato, kulinda Taifa na kusimamia haki na sheria, na la mwisho ni kuthamini utu na dhamana ya Uzabuni kupitia Katiba na mgawanyo wa kikazi wa Serikali.

Kutokana na matakwa au mahitaji haya, ambayo yanaweza kushabihiana na vision, Vyama vya siasa hupaswa kuunda sera na ilani ili kuweza kufanya kazi kutokana na uzabuni walioshinda.

Sasa wananchi wanataka miundombinu iliyo imara ambayo itaruhusu wao, bidhaa na mazao kuweza kupita kutoka kona moja hadi nyingine.

Sera ya miundo mbinu ingekuwa ni kuangalia ni jinsi gani nchi inaweza kufikika kwa ufanisi kila kona ili kusambaza maendeleo, kupeleka huduma na kuruhusu movement ya watu na bidhaa.

Tulipopata uhuru, tulirithi miundo mbinu iliyojengwa na wakoloni. TUkaendeleza kwa kadiri ya mahitaji yalivyoongezeka na hata kuambatana na kukua kwa idadi ya watu.

Lakini kama tutajisifu leo kwa kujenga barabara (ukweli tumepanua tuu barabara na kuweka lami) lakini hatuoanishi na mahitaji wala kuonyesha ni vipi usimamizi wake haukuwa wa makini.

Mfano, jiji la Dar na njia zinazoingia Dar ni zile zile tangu ukoloni. Magufuli katika hotuba yake moja Bungeni aliongelea vipimo vya upana wa barabara uliofanya na Wakoloni miaka ya 1940s.

Lakini, kushindikana kwa Dar kuwa na mfumo bora wa barabara kwa zaidi ya miaka 30 pamoja na mfumuko wa idadi ya watu kuongezeka, kuongezeka kwa magari na msongamano ambao sasa umeishia kufanya watu watumie takriban masaa 3-5 kutoka nyumbani kwenda kazini na kurudi, haiwezekani tukasifia ma-flyover, DART au lami mpya na kusema tumeleta maendeleo. Tulichofanya ni kuweka viraka katika mfumo ule ule uliozeeka na ni dhahiri ni ukosefu wa Sera.

Nikiendelea tena kuiangalia barabara ya MOrogoro, inashangaza kuwa mpaka leo hii, njia kuu ya kuingia Dar inategemea Daraja la Ruvu, siku daraja likianguka kwa uzee au kusombwa maji ya mafuriko, Dari haitawezekana kuingilika au kutoka, huduma zitasimama na kero zitakuwa nyingi.

Reli, bandari, usafiri wa ndege na maji, mifereji, madaraja nayo inafanywa kama ni sera, lakini ni wajibu wa Serikali kuhakikisha miundo mbinu inafanya kazi na kama ni sera, ni heri Sera ya miundo mbinu ingelenga hatua za kuhakikisha huduma za usafirishaji na uchukuzi zinafanyika kwa ufanisi mkubwa, kubunguza misongamano na ucheleweshaji wa usafirishaji, kutumia mbinu bora na zenye gharama bora na nafuu kusafirisha mizigo (reli ya kati, Tanga na Tazara zimeachwa zioze na tunakimbilia malori kwa kuwa ni miradi ya watu binafsi na hata viongozi), bomba la mafuta la Tazama liko chali na hatukuona umuhimu kujenga bomba la kutoka Dar mpaka Mwanza (Elisante Muro alikuja na wazo na kupeleka Serikalini akanyang'anywa na kupewa yule Mu-Omani mwenye Nat Oil na leo ni mwaka wa 25 hatujajenga bomba la mafuta kutoka Dar hadi Mwanza kitu ambacho kingepunguza uagizaji wa malori ya mafuta na kuharibu barabara kutokana na udhaifu na uimara wa hati hati wa barabara).

Tukija kwenye ndege an vivuko vya majini, kwa miaka 25 tumekuwa tunafanya majaribio ya kuendesha shirika la ndege, meli na hata pantoni.

Sera inayoeleweka ingekuwa ni serikali kuweka mazingira mazuri na kuachia sekta binafsi imiliki na kuendesha shughuli za usafirishaji, serikali ibakie kuwa mmiliki wa Mataruma ya reli, viwanja vya ndege, bandari na kusimamia sheria na kanuni za mfumo wa uchukuzi huku yenyewe ikikusanya kodi (road toll na fuel taxes to be added) ya mauzo na matumizi ya barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari.

Kwa kuwa viongozi na vyama havina vision kubwa na pana ya Uchukuzi na Miundombinu, tunaishia kurukaruka kama panzi kutoka project moja moaka nyingine, tunataka kumwaga lami kila kona na kukwepa kuchonga njia mpya ili kupanua mfumo wa barabara na kusambaza huduma mbali zaidi.

Kumalizia suala la Sera ya Uchukuzi, miaka 20 iliyopita niliuliza ni kwa nini Chalinze haikufikiriak kuwa inland port na kufanywa kuwa loading and unloading dry dock ya mizigo kwenda bandarini KUrasini?

Wazo lilinijia kuona kwa wenzetu kuwa pale Chalinze kuwa kwa kuwa ni njia panda ya kwenda kusini, kati na kaskazini, mizigo yote ingefika Chalinze, ikawa processed kutokana na kanuniza freighting na forwading ikapandishwa kwenye makontena (pia ujenzi wa Container warehouse) na kuwekwa kwenye treni kwenda bandarini. Hapo Chalinze TRA na Customs wangeweka kituo kikubwa cha ukaguzi wa mizigo inayoondoka Tanzania na hata ile ambayo si ya kuja Dar bali kwenda mikoani na nchi majirani, zingeshushwa kutoka kwenye meli na kuwekwa kwenye treni mpaka Chalinze.

Sasa tafakari ni jinsi gani uchukuzi huu na kufikiria hivyo ambako kungesambaza maendeleo pale Chalinze kuwa mji mkubwa wa kibiashara na hata viwanda, kupunguza msongamano wa watu na magari Dar na kupanua maendeleo mbali na Dar pekee.

Kwangu sera inayoeleweka ya uchukuzi ingesema kuwa kuna lengo la kuhakikisha kuwa muda wa usafiri kati ya Dar na Mwanza kwa gari unakuwa masaa 8 au 10, kwa treni unakuwa masaa 9 au 12, kwamba barabara zinahifadhiwa na kufanyiwa marekebisho kila mwaka, madaraja kupimwa uwezo wake wa kuhimili kila baada ya miaka mitano, kuwa badala ya kujenga daraja la kutoka Bahari beach mpaka KIvukoni, tungeweka feri za mwendo kasi za kutosha miaka 15 iliyopita kutoka Bagamoyo, Bahari beach, Kawe na Ferry, kupunguza msongamano, kivuko cha kigamboni kisingekuwa kitendawili tangu enzi za Nalaila Kiula.

Ni faraja kuona barabara za lami kila kona, lakini pia proper maintenance inahitajika kuhakikisha mifereji ya kando ni imara na imefunikwa na haigeuki kuwa dampo la takataka. Ama enforcement ya safety driving iwe ya hali ya juu kudhibiti madereva wanaoendesha reckless bila kufuata kanuni na wala kusiwe an haja ya kuweka matuta ya viazi barabarani kupunguza kasi.

La zaidi pamoja na major roadways ni kuwepo kwa barabara za watu wa miguu, baiskeli na hata madaraja ya juu kuvuka barabara (kama la Manzese) na service roads sambamba na barabara kuu.

Lengo liwe kurahisisha uchukuzi, ili kukuza uchumi, kuongeza ufanisi na kusambaza maendeleo. Naam hapo ndipo sera inaweza eleweka, wananchi watafurahia matunda ya Mzabuni kwa mapana na si kusomewa urefu wa barabara.
 
Nguruvi3,

Umegusia hapo juu suala la Sera kuhusu katiba na muungano. Nitaliongelea haraka haraka.

Leo CCM wanadai wao wanataka Serikali mbili na Katiba ya 1977 na marekebisho kadhaa hadi 2005 yanafaa.

Lakini Sera hii ya CCM kuhsiana na Muungano na Katiba hauendani na matakwa ya wananchi wake, walioipa zabuni ya kuongoza nchi.

Ama CCM imekuwa na unafiki kueleza kinagaubaga kwa nini inasimaima Seriakli mbili, kwa nini inapuuzia kero za muungano na sababu wanayotoa ni eti "tunawaenzi waasisi wa Tanzania Mwalimu Nyerere na Karume"

Nusu ya wapiga kura wamemsikia Karume, hawakuwahu kumuona, hawaelewi Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwaje, zaidi ya kulazimishwa kuamini Mapinduzi na Muungano vilikuwa ni sahihi.

Badala ya kujenga hoja inayoeleweka kueleza kwa nini CCM wanaona Sera ya Serikali mbili inafaa, wanakimbilia kusema Katiba inasema hivyo.

Lakini ni katiba hii hii ambayo ina utata, na ukungu mwingi ambao watu wanaupigia kelele kama kero na masumbufu kwao: iwe ni kero za muungano, madaraka makubwa ya Urais, udhaifuwa mihimili ya Bunge na Mahakama au muundo wa Tawala za mikoa na kulazimisha mgombea wa udiwani, ubunge na urais lazima atokane na chama.

Wananchi wanaambiwa, ni kufuru kuongelea suala la muungano au kuhoji uhalali na umakini ya katiba kutokana na mazingira ya leo.

Kwa hadaa na unafiki, Rais akaruhusu mchakato wa Rasimu ya Katiba, akajiundia Bunge la Katiba, akaidhinisha fedha ambazo hazikupangwa kibajeti kushughulikia mchakato na pale CCM walipokataa mapendekezo, UKAWA ukazaliwa, CCM wakaandika katiba yao, ikatangazwa kijeshijeshi, ikalazimishwa kuchapishwa na karibu ipigiwe kura ya maoni kibabe ili ipite.

Leo suala la Katiba na hatima ya Muungano ni bado kitendawili kwa kuwa katika vyama hasa CCM, bado kuna unafiki na mgawanyiko wa Watanganyika na Wazanzibari ndani ya Chama na hatima ya Muungano huo.
 
MAGUFULI ANATUPA MFANO 'MZURI' WA MJADLA HUU

Tumeongelea kuhusu sera/Ilani kwamba ni mtazamo wa jumla wa eneo na si wajibu wa kila siku wa serikali husika

Katika kampeni zinazoendelea, Mgombea wa CCM mh Magufuli ameyasema haya kule Bukoba kama sera/Ilani ya CCM

Elimu: Anafahamu matatizo ya wanafunzi na atayafanyia kazi. Hakueleza matatizo hayo ni yapi.

Huko nyuma alizungumzia matatizo ya Walimu, kwa kitu kinaitwa 'customize' kwamba kila mmoja anapimiwa 'nguo' kwa urefu na kimo

Hiyo siyo sera, sera ni kuzungumzia tatizo la elimu kwa ujumla, kulieleza na kutoa ufumbuzi

Katika kufanya hivyo, unaweza kuona pengine tatizo si la wanafunzi ni la mfumo unaoplelekea matatizo kwa wanafunzi

Kodi: Magufuli anasema ataangalia kodi ya wafanyakazi wanaoumia. Kwamba, atapunguza kutoka asilimia 11 hadi anayoijua yeye. Hiyo si sera, ni sehemu ya policy zitakazotokana na Ilani ya uchaguzi kuhusu suala la kodi

Ni wazi kuna maeneo yataongezewa kodi kama atapunguza kwa wafanyakazi. Hilo si baya, lakini aainishe ni eneo gani lenye matatizo litakalofidia kodi anayosema. Katika kufanya hivyo, sera/Ilani yake ingezungumzia mfumo wa kodi anaotaka kuubadilisha kwa jumla.

Haiwezekani akapunguza kodi 'sera' yake bila kuangalia mfumo mzima wa kodi, makusanyo, mapato , tozo, misamaha, ukwepaji n.k.

Angeeleweka kama angesema, sera/Ilani yake ni kufuta misamaha ya kodi, kuongeza corporate tax ili kupunguza tax kwa mfanyakazi

Si suala la kuchagua kitu kutokana na watu walioko katika mkutano. Viongozi hawajui tofauti, tutegemee nini wakiwa katika uongozi?

Hawajui kwasababu hawawezi kutenganisha sera/ilani na majukumu ya kila siku, vision yake ipo wapi?

Ndiyo yale ya kusema CCM itajenga daraja la Wami.Kujenga madaraja ni majukumu ya kila siku ya serikali, si sera.

Kuimarisha miundo mbinu kwa ujenzi wa madaraja katika muda fulani ukilenga abcd hiyo inaweza kuwa sera ya miundo mbinu

Rev Kishoka, hili la katiba ni muhimu Haiwezekani kiongozi hatuambi muundo wa nchi. Na hapa hatakwepa suala la muungano

Kutokana na kutokuwa na sera/Ilani matatizo mengi yamejitokeza katika suala la katiba na muungano

Katiba, tumeona mihimili 3 ikisigishana katika baadhi ya masuala.Ni jambo linalogusa utendaji,masilahi mapana ya nchi na wananchi

Leo tunaona katiba ya JMT 1977 isivyoweza kufanya kazi Zanzibar tukiwa na Rais wa JMT.

Hili ni tatizo la linalotakiwa kushughulikiwa kama agenda ya uchaguzi.

Tume zinaundwa kubadilisha katiba bila ridhaa ya wananchi,zinafanya kazi kufurahisha makundi na si masilahi ya taifa

Hapa tutoe mfano. Katika kutaka kuungwa mkono na wazanzibar, Rais na tume za kero zimejadili gesi na mafuta nje ya utaratibu.

Sheria zimepitishwa kwa hila na nguvu bungeni zikieleza hilo Kilichofanyika ni kufurahisha wazanzibar

Kwa undani hilo ni tatizo kubwa sana.Nchi zenye matatizo ya rasilimali kama Nigeria zimeishia katika machafuko

Ipo siku wananchi watataka kujua uhalali wa tume za kero na kwanini suala la rasilimali halikujadiliwa kitaifa

Mfumo mzima wa muungano utaingia katika misuko suko na kila aina ya madhara yatakuwa sehemu ya mjadala.

Kwamba, gesi na mafuta tu inakuwa precursor na catalyst ya matatio mengine.

Tunarudi kule kule kuunda tume za kuipuuzi zisizo na majibu kama zile 10 zilizoshindwa kutoa majibu ya muungano

Katika hili, CCM na Wapinzani hawawezi kujificha. watueleze sera zao ni zipi ili wananchi tuweze kuchagua na wengi watapewa.

CCM kukaa kimya ni janja ya kukwepa ukweli ulio wazi. Muungano ni tatizo, lazima lijadiliwe kwa mizania ya sera/ Ilani.

Hili si sawa sawa na ujenzi wa flyover na daraja la Wami

Tunachouliza, Magufuli na CCM kwanini wamekaa kimya kuhusu jambo zito kama hili. Wanakwepa nini wanaogopa nini

Ni lazima wananchi tuwabane watueleze, kama hawana la kusema, hawana njia na vision na hawatufai.

Muda wa kuongoza taifa hili kwa ramli kama ilivyokuwa miaka 10 au 20 ndicho chanzo cha matatizo tuliyo nayo

Elezeni wazi ili wananchi waamue kama wapo tayari kuendelea nanyi au mnahitaji muda wa kujipanga

CCM wamekimbia hoja na kurukia vihoja na viroja ,mipasho n.k. ni ushahidi miaka 50 haijawasiadia kutambua nini wananchi wanataka.

Wananchi nanyi mna sehemu yenu, kuona jinsi CCM wanavyodanganya maana wao ni chama tawala.

Hawana lolote la kueleza kuhusu sera/ilani juu ya katiba na muundo wa nchi.

Hatuwezi kutegemea tena hisani kama ya JK iliyopelekea taifa hili hasara ya tume na bunge la katiba.
 
Nguruvi3,

Leo numekutana na Economist la wiki hii na hiki kipande hapa kilinisisimua kisha kikaniletea masikitiko nikiangalia jinsi mfumo wetu wa elimu unavyokosa uwekezaji mahiri. Cha kujiuliza ni kuwa nii lini ambapo tunaweza kuwa na malengo ya uhakika ya kuliinua Taifa letu kiasi kwamba Dola Bilioni 15 kutumika kwa elimu, maji au afya ikawa ni kitu cha kawaida?

SHORTLY before 10pm, BMWs and school buses line the streets of Daechi-dong, a neighbourhood in the stylish district of Gangnam in Seoul. Soon, secondary-school pupils will spill out of its hagwon, or private crammers; around 1,000 of these night schools are packed into the area, including the most prestigious in the city. After five hours of tuition, in English, maths or science, following a full day at school, the teens will be whisked home-to more study, past midnight.
Such is the ordeal of education in South Korea. From a tender age all pupils (and their parents) are fixated on the eight-hour multiple-choice entrance exam for university, to which three-quarters of school-leavers go. Because competition is fierce, parents plough money into private tuition-over 18 trillion won ($15 billion) last year, or more than a tenth of household spending-to improve their children's chances of getting into the best secondary schools (see chart).

The crème de la cram | The Economist
 
Leo nitaomba nipitia "Sera" moja ambayo ililetwa na JK inayojulikana kama "Kilimo Kwanza".

Tofauti na kauli mbiu ya Ari, Kasi na Nguvu Mpya, naamini Kilimo Kwanza ilikuwa ni sera yenye nia na malengo mazuri. Lakini, sera hii ilikuwa na mapungufu makubwa ambayo mpaka leo, Kilimo Kwanza kimeshindwa kuleta mafanikio ya kuboresha ustawi wa mkulima, kuoongeza uzalishaji wa chakula, kupunguza uagizaji wa vyakula, kuleta viwanda vya kusindika vyakula.

Sera ilikuja na mwamko mkubwa sana na kupokelewa vizuri na wananchi. Wito ulipokewa kwa shangwe nchi nzima. Lakini kuna matatizo mengi ambayo yalikuwa yanaikabili sekta ya kilimo, yaliendelea kuwa kero na matatizo mpaka leo hii.

Matatizo haya ambayo Sera hii haikuyaangalia kwa umakini ni yafuatayo:


  • Umiliki halali wa ardhi, pamoja na hati za ardhi/mashamba
  • Mitaji na mikopo kwa wakulima, wafugaji, wavuvi
  • Pembejeo; mbegu, zana za kilimo, mbolea
  • Maghala
  • Soko
  • Maji
  • Majosho ya mifugo
  • Dawa za mifugo
  • Nyavu na chambo za uvuvi
  • Uchukuzi/Usafiri

Na mengine mengi ambayo ungeweza kuorodhesha kuwa ndio mahitaji ya msingi katika kuhakikisha sekta hizijinakuwa na maisha yanaboreka.

Si lazima kuorodhesha mapungufu ya sera hii, ni rahisi sana kwetu kuona ni vipi sera ilishindwa kuleta manufaa kwa wananchi, bali ikaishia kuleta unyang'anyaji wa ardhi, kuletwa matreka kupitia Jeshi kwa zabuni za mashaka, kuongezeka kwa bai za chakula na uhaba wa chakula n.k.

Ndio baada ya kuchechemea, Kilimo Kwanza ikaundiwa idara ya uhamasishaji: Big Result Now.

Mpaka leo hii wakati Kikwete anaondoka madarakani, hali ya mkulima bado ipo pale pale, hatuna viwanda vya kuengezeza vyakula au kusindika, bado tunaagiza chakula kwa wingi, na mengineyo mengi.

HIvyo pamoja na kuwa na sera, mapungufu ya kimipango na kiufuatiliaji (breakdown kwenye bandiko la9 hapo juu) yameendelea na sasa si ajabu Magufuli au Lowassa nao watakuja na sera mpya kabisa na si kuendeleza pale ambapo Kilimo Kwanza kimefika na kukwama.
 
Nguruvi3,

Leo numekutana na Economist la wiki hii na hiki kipande hapa kilinisisimua kisha kikaniletea masikitiko nikiangalia jinsi mfumo wetu wa elimu unavyokosa uwekezaji mahiri. Cha kujiuliza ni kuwa nii lini ambapo tunaweza kuwa na malengo ya uhakika ya kuliinua Taifa letu kiasi kwamba Dola Bilioni 15 kutumika kwa elimu, maji au afya ikawa ni kitu cha kawaida?



The crème de la cram | The Economist
Rev , hapo juu tumeelezea namna Lee Kuan Yew alivyoibadili Singapore kwa miaka 10.Ukisoma habari kuhusu Singapore utaona jinsi elimu inavyotiliwa mkazo.

Imeandikwa, gharama za tuition kwa walimu binafsi ni kubwa kuliko wanaofanya kazi.
Maana yake ni kuwa, wenzetu wanainvest katika elimu

Jana nimesoma gazeti moja lililoandika sekondari mbili, wanafunzi wanalala chini.
Hawa ndio tunategemea washindane na hao wa Seol Korea katika karne hii.

Sikwamba hatuwezi kuwekeza katika elimu, tatizo ni kutokuwa na maarifa na pili vipaumbele.
Hela za kuimarisha elimu hakuna, pesa za kuchezea za bunge maalumu zipo

Denila nchi hadi sasa ni Trilioni 40, na imeandikwa gazeti la Nipashe,wastani wa kukopa ni 1.2 Trilioni kwa mwezi kwa takwimu za miezi michache.

Kiasi hicho ukikichunguza kinakwenda katika 10 % za mabaehewa, wakandarasi n.k.
Hakuna inayoingia katika elimu

Hapa ndipo tunakuwa bias kwa kusema CCM wametufikisha pa bovu.

Katika kampeni hizi walitakiwa walinde rekodi ya miaka 50 katika mambo kama elimu.
Tunachosikia ni Magufuli kujua shida za wanafunzi.

Shida gani za wanafunzi zaidi ya shida kubwa ya elimu? Tatizo la elimu ni nini mheshimiwa Magufuli?
Tuelezwe kwa namba na mantiki, si kupitia mabonanza ya akina Diamond.

Hayo tuyaache Bilcana,katika siasa za uongozi tuzungumzie issue kama za elimu, afya, katiba, deni lataifa, mapato , matumizi,kilimo, vyanzo vya mapato zaidi ya bia na sigara n.k.

Ukiwasikiliza CCM huwezi kujua tofauti yao na wapinzani.
Hakuna cha maana wanachotetea au kusimamia wakiwa na rekodi ya miaka 50!

Wananchi tunawachekea hatuoni madhara. Trilioni 40 ni deni letu hata kama chanzo ni akina Magufuli na CCM.
Elimu mbovu ni tatizo letu hata kama chanzo ni CCM
Mkumbuke,mwaka 2005 tuliuziwa mbuzi wa gunia. Baada ya uchaguzi tu, tukasikia hawajui kwanini sisi ni masikini

Walihubiri maziwa na asali kama hawa tunaowaona. Leo wanaenda kupumzika wakituacha na umasikini. Hatujifunzi, Watanzania ni watu wa aina ya pekee. Hawajifunzi hata kama somo lipo katika damu au jasho lao! hawajifunzi


 
KILIMO KWANZA

Kilimo kwanza imeshindwa. Tatizo si kilimo kwanza au nia ya kilimo kwanza.

Tatizo ni lile lile la kwamba hakuna sera/Ilani. Mambo yanafanyika kutokana na utashi wa watu.

Nitoke nje kidogo, suala la katiba ilikuwa utashi wa mtu kutokana na shinikizo la kisiasa. Haikuwa sera/Ilani ya CCM.
Hakukuwa na maandalizi wala usimamizi. BMLK likawa hasara kwa walipa kodi

Ndivyo ilivyokuwa kwa elimu. Lowassa na JK walipoingia madarakani kulikuwa na mitazamo tofauti.

Lowassa akisisitiza kuhusu elimu , Jk akiwa hana uhakika nini kifanyike.

Zikajengwa shule za kata haraka haraka bila maandalizi ya kutosha. Shule hazina walimu wala vifaa. Haikuwa sera/Ilani ya CCM
Hakukuwa na maandalizi wala mipango kwasababu ni fikra za mtu au watu na si sera zilizotathminiwa

Lowassa alipoondoka , Pinda akaja na kilimo kwanza. Haikuwa sera wala ilani ya CCM.

Kilimo kwanza ilitangazwa bungeni kwanza, wataalamu wa kuunga unga wakapewa kazi kwa maagizo ya kuzingatia kilimo kwanza, na si planning. Kwamba wahakikishe wanafuata maagizo ya wanasiasa na si ya utaalamu wao. Utashi wa mtu au watu na si sera/Ilani

Usambazaji wa pembejeo , uingizaji wa mtrekta, usimamizi vyote vikatawaliwa na rushwa.

Na kwavile uongozi hufanya kazi kwa ajili ya uchaguzi na si maono, kila jambo likaachwa kama lilivyo.

Viongozi wakarukia elimu wakitaka kubadilisha lugha ya kufundishia kama ni tatizo.

Ghafla BRN badala ya kutoa results za kilimo kwanza ikaja na kupunguza viwango vya ufaulu, watoto wafaulu kuelekea uchaguzi.

Hadi hapo hatuwezi kusema kilimo kwanza ilikuwa na mipango.

Ndivyo ilivyo sasa wakati Magufuli anazungumzia Kilimo kwanza bila kueleza hata sentensi, kilimo kwanza ya kwanza ilikwama wapi na anataraji kufanya nini tofauti. Huyu alikuwa sehemu ya maamuzi ya kilimo kwanza, hivyo tuna mengi ya kumdai.

Ndio maana tunasema, kama hatuwaulizi, wataorodhesha mambo 10000 mengine yakiwa ya wajibu na kutuaminisha wanataka kutuvusha. Hapana! tuwaulize, kama hawana majibu tuwaombe wakae pembeni.

Magufuli/CCM, nini kilikwamisha kilimo kwanza na hii ya Magufuli itakuwa tofauti kwa namna gani?

Magufuli/CCM tuambieni, nini kiliua viwanda vya kahawa ya Tanzania, wakati ya Ethiopia inatamba duniani. Magufuli/CCM mnafufua viwanda kwa utaratibu gani ikiwa Magufuli/CCM mligeuza Mang'ula ghala la chumvi na hakumuweza hata kurudisha jengo!

Magufuli/CCM mnataka kujenga viwanda gani zaidi ya Mwatex, Mutex, Moproco, Magunia , Tanneries, Tanganyika packers n.k. mlivifanyia mnada wa bure miaka michache iliyopita na Magufuli ulishiriki, leo unataka kujenga viwanda gani zaidi ya vile ulivyoshiriki kuvigawa na kuwa maghala ya chumvi?

Tuwaulize hawa, wanatufanya ndondocha! Trilioni 40 deni ni letu tukiwaacha watatubebesha mzigo! Tuwaulize
 
Back
Top Bottom