Mkuu Mchambuzi ahasante na salaam zao huko nyumbani.Mkuu Nguruvi3,Asante sana kwa hoja nzuri juu ya yanayojiri katika suala zima la mchakato wa katiba; Nimekuwa nikikufuatilia kwa muda mrefu sana kuhusiana na mada husika;
siku nyingi ulishasema upinzani ulishakosea na taifa halitapata katiba itakayotokana na wananchi;je, unadhani safari ya pili ya upinzani kwenda ikulu kuonana na Rais (JK) inaweza zaa matunda ambayo yatabadilisha mtazamo wako wa awali?
Na je, hivi tunaweza thibitisha kwamba Rais alishatia 'sign' muswada husika kuwa sheria na kuelekeza urudi bungeni kwa marekebisho? Marekebisho yepi hasa? Kilichoenea mitaani ni uvumi lakini ni vigumu kuhakikisha juu ukweli uliopo; pengine una taarifa sahihi zaidi, nipo kijijini kwahiyo mengi yamenipita;
JingalaFalsafa Ni masikitiko kwa vizazi vyetu na sisi wenyewe huko mbeleni. Tunashindwa kusimamia utajiri, uchumi na sasa tumeshindwa kuweka sheria za kukosoa makosa ya nyuma.Duh! Hatuna budi kujipa pole wanaTz! Lakini kwa aina ya siasa ambazo tumekubali kuwa nazo, HAKUNA JIPYA!
Werevu na wenye busara mlishatahadharisha, tukawasikia, sadly tulishakubali kushikishwa makali na wanasiasa! Hapa ndipo napoikubali na kuililia sana BOTTOM-UP APROACH, alikwisha isemea Mkuu Mchambuzi.
Mkuu wangu Nguruvi3, tujipe pole tu, maana tunashuhudia namna sisi wenyewe tunavyowachimbia kaburi wajukuu wetu. INAUMA SANA
JingalaFalsafa Ni masikitiko kwa vizazi vyetu na sisi wenyewe huko mbeleni. Tunashindwa kusimamia utajiri, uchumi na sasa tumeshindwa kuweka sheria za kukosoa makosa ya nyuma.
Naukumbuka sana mjadala na Mchambuzi kuhusu Bottom up approach au top to bottom. Moja kati ya mambo tuliyokinzana ilikuwa ni bottom up. Mimi nilisema bottom up ndiko tunatakiwa tuelekeze nguvu. Mchambuzi akasema je tuna civil society za kutosha na zenye uwezo wa kuifanya hiyo bottom up?
Approach yangu ndio hiyo unayoisema na hadi leo nabaki kusema tunahitaji bottom up approach. Pamoja na hayo hoja ya mchambuzi kuwa je tuna civil society za kutosha kuibea bottom up approach imejidhihirisha mapema zaidi kuliko alivyosema. Ukweli ni kuwa thamani ya hoja yake tunaiona less than a year tangu aitoe! Nitafafanua
Endapo tungekuwa na civil society za nguvu mchakato huu pamoja na kutekwa bado ungeweza kurudi mikononi mwa wananchi. Tunachokiona ni kuvutana kwa vyama vya kisiasa kwa jambo ambalo hakika si la kisiasa.
Hili ni la societies, approach yake ingekuwa na nguvu sana kuliko ilivyo sasa.
Kitu ninachotaka kuumuliza Mchambuzi ni je, tumechelewa kuwa na hizo civil societies!
Na pili how do we build them tukijua ni civil na uwepo wake unatakiwa kuwa natural tunachohitaji ni ku nuture!
cc Mchambuzi
Excellent ! nasubiri umalizie!Afrika na ICC: Ubeberu wa Mataifa Makubwa na Uharamia wa Viongozi wetu[/B]
Na Ben Saanane[/B]
Mwishoni mwa wiki iliyopita Viongozi wa Nchi za Africa walikua Makao Makuu ya Umoja huo Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili mpango wa kujiondoa katika mkataba wa Roma unaoongoza Mahakama ya kupambana na uhalifu wa kivita na makosa makubwa ya Jinai dhidi ya Ubinadamu duniani, ICC (International Criminal Court).
Hoja kuu ni kuwa mahakama hii inawalenga Viongozi kutoka Mataifa ya Afrika tu. Hii ni hoja yenye ukweli kwa kiasi Fulani, maana asilimia kubwa ya kesi zilizoko kwenye Mahakama hii kwa sasa ni kutoka Afrika huku rekodi zikionyesha hata Kesi nyingi za nyuma zilizowahi kushughulikiwa na Mahakama hiyo zinahusu Watuhuniwa kutoka Afrika zaidi.
Ukiacha sababu hizo lakini pia Viongozi wa Afrika nao wana ajenda yao juu hili azimio lao la kutaka kujitoa ICC, azimio ambalo halikupata uungwaji mkono wa kutosha katika Kikao hicho cha juzi japo kuliibuliwa azimio jipya mwishoni mwa kikao la kumtaka Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kutohudhuria Mahakamani wakati wa Kesi yake inayopangwa kusikilizwa mwezi ujao.
Nchi 34 kati ya 54 za Umoja wa Afrika zimesaini Mkataba wa Roma wa kukubali kuanzishwa kwa Mahakama hii. Wakati Viongozi wa Nchi hizo waliposaini haraka haraka mkataba wa ICC na kuziingiza nchi zao walidhani wanazuia mapinduzi dhidi yao kutoka kwa waasi, na walikwenda hatua mbele zaidi ya kujifanya kuwa hawatatambua matumizi ya mtutu katika kubadilisha utawala kwa njia ya kupindua serikali.
Hawakufikiria wala kutilia maanani kuwa ili kukomesha ‘mapinduzi ya kijeshi' ni lazima kuimarisha utawala bora wa sheria bila kuminya demokrasia ili sauti huru zisikike na pia kujali zaidi maslahi ya wananchi wan chi hizo. Mapinduzi ya kijeshi Afrika yanachochewa kwa kiwango kikubwa na tawala kandamizi zilizominya uhuru wa maoni na kuzuia sauti za wananchi wenye mawazo kinzani pamoja na wanaharakati.
Jambo la kufurahisha ni kuwa wapo Viongozi zaidi ya 12 wa Nchi za Afrika waliopo Madarakani na ambao ni wanachama wa AU ambao waliingia madarakani kwa mtutu wa Bunduki na wengine wakisalia madarakani kwa kupora chaguzi. Kipindi wanapitisha azimio la kutotambua mapinduzi ya kijeshi idadi hii ilikua kubwa zaidi na hao hao walioingia madarakani kijeshi au kwa wizi wa kura ndiyo waliotangaza kutotambua mapinduzi hayo ya kijeshi.
Kwa mujibu wa Maandishi ya Vitabu vya Kitafiti kuhusu Mapinduzi ya Kijeshi katika Mchi za Kiafrika kama 'Coup D'Etat' cha Mwandishi Edward Luttwak na 'Political Order In Changing' kilichoandikwa na Samuel P.Huntngton, ilionekana kuwa pamoja na ushawishi kutoka mataifa ya nje lakini Upendeleo,Ufisadi na hali ngumu ya kiuchumi na kijamii ni mojawapo ya vichocheo vikubwa kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyoikumba Afrika.
Kwa kipindi cha karibia miaka 60 tangu Nchi za Kiafrika zipate Uhuru, Afrika Imeshudia Mapinduzi ya Kijeshi zaidi ya 40 huku Nchi ya Nigeria ikiongoza kwa kukumbwa na Mapinduzi 10 ya kijeshi Kati ya mwaka 1966-1999 ikifuatiwa na Ghana iliyokumbwa na zaidi ya Mapinduzi 9 ya Kijeshi.
Kwa hiyo badala ya kufikiria namna ya kuondoa sababu na vichocheo vinavyochochea uwezekano wa Mapinduzi ya Kijeshi huko baadae, Viongozi wetu hawa wa Afrika waliamua kufumba macho na kuchagua njia waliyoiona ni rahisi zaidi kwa wakati huo bila kutazama athari zake kwao pia, yaani Mkataba wa Roma wenye kuasisi Mahakama ya ICC.
Kwa mfano suala la Uchaguzi kwa nchi za Afrika ni kichocheo kikubwa cha uvunjifu wa amani na mapinduzi kwa njia ya mtutu. Viongozi wa Afrika wanaogopana kuambiana ukweli au hawaheshimiani kwa kuwa tabia zao za ukiukaji wa sheria na kutowajali raia wao zinafanana. Labda tuangazie kwa kifupi tu nchini Kenya ambako ndipo chanzo cha hatua hizi za AU.
Wakati Mwai Kibaki, Uhuru Kenyatta na wanasiasa wengine wa kilichokuwa Chama Tawala cha Kenya cha PNU walipofanya udanganyifu kwenye uchaguzi wa Rais na wabunge nchini Kenya Mwaka 2007, hali iliyosababisha wapinzani kutoka chama cha ODM wakiongozwa na Willium Ruto na Raila Odinga kwa upande mwingine kuingia barabarani kupinga kuporwa uchaguzi huo na kusababisha mauaji ya watu zaidi ya 1000 na wengine zaidi ya 600,000 ya wasiokuwa na hatia kukosa makazi, Umoja wa Afrika, AU haukutangaza moja kwa moja kumchukulia hatua Mwai Kibaki na Watawala wengine.
Umoja huu haukutangaza kumtenga Mwai Kibaki na serikali yake na hata Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Dk. Koffi Annan walipopelekwa kusuluhisha mgogoro huo walipata wakati mgumu kwa kuwa Kibaki alikuwa akiwadharau wote wawili kwa sababu ya rekodi zao za Ufisadi wakati wakiongoza Tanzania na Umoja wa Mataifa. Mkapa akituhumiwa kwa kufisadi mgodi wa Kiwira na Annan akitajwa kwa kashfa ya ‘Mafuta kwa chakula' ya Iraq.
Wakati wote huo wa vurugu za Kenya waliokuwa wanapoteza maisha ni raia wanyonge tu kutoka maeneo mbalimbali wan chi hiyo. Sasa' swali la kujiulia ni kuwa kuna haja gani ya kufanya uchaguzi ikiwa aliyeshinda uchaguzi anaporwa ushindi? Kuna tofauti gani kati ya Mapinduzi ya kijeshi (Coup d'tat) na wizi wa kura? Unapopora haki ya raia kuchagua,unapopora haki ya raia kutoa sauti. Hayo ni mapinduzi ya matakwa ya umma (coup D'Civillien). Hayo ni mapinduzi mapya baada ya Coup d'tat. Viongozi wa Afrika wamelibariki hilo.Unafiki ulioje?
Mara zote mapinduzi ya aina hii yasipofanikiwa kwa asilimia kubwa husababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.Tulishuhudia jaribio hili kule Cot de'Ivore. Laurent Gbagbo alishindwa uchaguzi na Mpinzani wake Allasaine Outtara, akaamua kufanya ‘Coup de' civillien'.Afrika haikufua dafu,walitoa sauti za kinafiki kukemea na hali ilizidi kuwa mbaya na kuhatarisha amani kiasi kilichopelekea uwezekano wa kuzuka vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi jumuiya ya kimataifa ikiongozwa na Mkoloni wa zamani wa nchi hiyo, Ufaransa walipoingilia kati na hatimaye Gbagbo akakamatwa akiwa amejificha kwa aibu. Leo anashtakiwa mbele ya mahakama ya ICC, Mahakama hii ndiyo ambayo Viongozi hawa wanataka kujitoa ili kujiepusha na haya yanayomkuta Gbagbo.
Kwa hiyo tunaona kwamba mjadala wa Viongozi wa AU na nia yao ya kujadili suala la kujiondoa ICC linalenga pia kuwalinda viongozi hawa ambao wengi wao wamekiuka haki za binadamu na pia kuua na kutesa wapinzani wao. Ni azimio la kikatili.
Mbona hawajitoi kwenye Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO)? Inatambulika kuwa Benki ya Dunia na Shirika la fedha Duniani ni nyenzo kuu za mabeberu zinazotumika kuzinyonya nchi zinazoendelea na hasa zile nchi zenye viongozi wasiofikiria mbele. Heri yao wananchi wa Venezuela waliojiondoa kutokana na ushupavu wa Rais wao Kamaradi Hugo Chavez.Vyombo hivi vya mabeberu (IMF, WB na WTO) ni hatari kwa Afrika na Ustawi wa wananchi wa Afrika kuliko Al-Qaeda na Al-Shaabab ambayo ni makundi hatari kwa Mabeberu, Vibaraka na maslahi yao popote pale duniani. Jambo kubwa la kinafiki kutoka kwa viongozi wetu hawa ni kuwa Viongozi wengi wa Afrika walioshitakiwa ICC walipelekwa huko na serikali za nchi zao ambazo viongozi wake walikusanyika huko mjini Addis Ababa kulalama kuwa ICC inawashtaki wao tu.
Serikali zilizopeleka kesi na watuhumiwa wenye asili ya kiafrika huko ‘The Hague' ni pamoja Serikali za nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda. Kesi nyingine mbili za Darfur na ile ya Libya zilipelekwa mbele ya mahakama hiyo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mamlaka yake zikiwa na sapoti ya wanachama wa baraza hilo kutoka barani Afrika.
Nilishawahi kusema baadhi ya viongozi wa Afrika ni ‘mambumbumbu'. Hata Makao Makuu mapya ya AU walipokaa kujadili hili la kujitoa ICC yamejengwa kwa Msaada wa ‘Beberu Mpya' wa dunia, UCHINA, ambaye rekodi yake juu ya ukiukwaji wa haki za binaadam inajulikana namna ilivyo mbaya, zaidi sasa Nchi hiyo imekuwa bingwa wa kuzuia Demokrasia Duniani. Viongozi wa Afrika ni wabinafsi na hawawezi kuona mbele hadi hatari iwaguse wao binafsi. Hawajali maslahi ya nchi zao. Si wale Viongozi wa kaliba ya kina Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Nelson Mandela, Ahmed Sekou Toure, Thomas Sankara, Gamal Abdel Nasser, Patrice Lumumba. Viongozi tunaowaheshimu katika ujengaji wa hoja kwa maslahi ya nchi na bara la Afrika kwa vitendo tofauti na hawa madikteta waoga.
Viongozi wa sasa wa Afrika walipotia saini mkataba wa Roma walikuwa na akili zao timamu, waliona namna Marekani, China na Urusi ambao ni Wajumbe watatu muhimu wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa aidha walipokacha kusaini mkataba wote au hata kujiwekea sharia zao za ndani za kuzuia matumizi ya Mkataba huo wa Roma kwa raia wao. Leo wanalalamika na kuhoji uhalali wa wajumbe hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wasioikubali ICC kisheria kupitisha kukamatwa kwa Rais Omar Hassa Al-bashir wa Sudan kwa kadhia ya Darfur.
Makala hii inaendelea.....
Excellent ! nasubiri umalizie!