Duru za siasa - Matukio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za siasa - Matukio

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Oct 24, 2011.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280

  YALIYOJADILIWA

  CCM na waraka wa rasimu ya katiba #2 86Uzao wa mtoto familia ya Malkia #26

  Lipumba akutana na rais JK #255
  Uvamizi nyumbani kwa Mbowe #241

  Kilichomsibu Morsi na somo kwa Tanzania #2 29 Sakata la Tahariri square #2 24
  Ziara ya Obama Afrika #2 20

  Kikao cha baadhi ya wakuu wa EAC #2 13
  Snowden na sakata la uvujishaji wa sri za Marekani #212

  Nadharia ya tatu kuhusu mabomu Arusha yajadiliwa na Makwaia wa Kuhenga #210

  Milipuko ya mabomu Arusha(Kanisani na mkutano wa CDM) #176 , #180 , #181 , #2 05

  Chadema na mzozo wa Bavicha #133 , #134 , #139 , #160

  Rasimu ya katiba ya Tanzania #184 , #188 , #190 , #191 , #192 , #193 , #194 , #197 , #198

  Kuvuja kwa siri za usalama wa Marekani #199

  Mgogoro wa Congo na M23 #137 , #139 , #160

  Mgogoro wa Video ya Lwakatare #161

  Mlipuko wa bomu Boston #167 , #168 , #173

  Mgogoro bungeni Dodoma #171

  Matokeo ya mtihani na zogo linalotokea #175

  Ziara ya rais wa China #164

  Profesa Lipumba na kauli tata za kisiasa #182

  Tatizo la gesi Mtwara #178

  Mwandishi Kibanda/Mwangosi #69 , #150 , #152

  Hali ya mashariki ya kati (Turkey na Syria) #200

  Uchaguzi Iran #200

  Uchaguzi wa Vatican #142 , #147 , #150

  Uchaguzi wa CCM #10 , #66 , #79 , #124

  Kauli ya mnadhimu mkuu wa jeshi #

  Uchaguzi wa Marekani #8 , #9 , #11 , #52 #61 , #65 , #80 , #84 , #85 , #86 , #88 , #91 , #92 , #94 , #96 , #106 , #107 , #117 , #123 , #124 , #141

  Uchaguzi wa Misri na siasa za Brotherhood #5 , #10 , #14 , #30 , #44 , #52 ,

  Siasa za Mashariki ya kati #2 , #73 , #127 , #131 , #132 , #161 , #169 , #178 , #131

  Vifo cha Margereth Thatcher,Hugo Chavez na Meles Zenawi #60 , #166

  Waziri mkuu Pinda kuzomewa #75

  Matukio duniani #74

  duru za siasa #302


  Other link

  https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/167157-duru-za-siasa-mgongano-wa-mawazo-17.html

  https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/625029-mtazamo-kuhusu-hotuba-ya-jk-kuzindua-bunge-maalum-la-katiba.html


  https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/614493-duru-za-siasa-bunge-la-katiba-upotoshaji-na-kiwewe-cha-kuzinduka-tanganyika.html
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  WASI WASI WA MAGEUZI MASHARIKI YA KATI

  Hapo nyuma nilieleza wasi wasi wa nchi za magahribi kutokana na hali ya mashariki ya kati. Wasi wasi huo haushii hapo unakwenda zaidi na kuwagusa waisrael ambao wamezungukwa kila kona na waleta mageuzi. Jasmeen revolution ilipopamba moto Tunisi na kuhamia Misiri, nchi za magharibi zilijaribu sana kuzuia kwa sababu kuu mbili. 1. Kwamba yangeambukiza nchi zingine 2. Yangeleta ugumu katika kudhibiti hali ya usalama mashariki ya kati. Na ukweli hayo ndiyo yanayotokea hata kama hayajawa wazi.

  Maambukizi tumeyaona na yamegusa hata falme kuu ya Saudi Arabia.
  Ugumu umeanza kuonekana pale askari wa misri bila kibali kukubali kuachia misaada ifike gaza kwa mpaka wa Rafah.
  Ubalozi wa Israel kushambuliwa na Misri kuchukua jukumu la usuluhishi wa mgogoro kati ya Hamas na Fatah.

  Ugumu unaonekana pale Tunisia walipochagua chama chenye msimamo wa dini ya kiislam na hivi karibuni Libya kusema itafuata sharia katika katiba yake ya nchi. Ikifika hapo nchi za magharibi zinakuwa katika wakati mgumu sana.

  Lakini ugumu zaidi ni kwa marekani ambayo miaka yote imekuwa na 'double standard' kuhusu suala la Palestine. Nchi za ulaya zinaonekana dhahiri kuchoka na Israel ingawa ni vigumu kutamka dhahiri. Wananchi wa nchi hizo wanaonyesha chuki ya chini chini kuhusu suala hilo.

  Marekani ambayo ni mfadhili mkubwa wa Israel kijeshi sasa inatafakari kuhusu nguvu ya spring revolution. Wanapoona nguvu ya umma inavyojidhihiri kule Syria na Yemeni chaguo lao linakuwa ni dogo sana. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi Waisrael wameomba wenzao wa Palestine warejee mezani kwa mashauriano. Huko nyuma walikuwa na msimamo kuwa lazima wapalestina wawatambue kwanza kabla ya kukaa mezani. Hii inaonyesha hofu kubwa inayowazonga.

  Uchaguzi wa misri unakaribia na duru za siasa zinatanabahisha kuwa chama cha kidini cha Brotherhood kinazidi kupata umaarufu na huenda kikawa na wawakilishi wengi katika bunge lijalo. Brotherhood wamekataa kumsimamisha mgombea wao katika kiti cha urais. Hii isifanye mtu adhani wao ni dhaifu, la hasha. Brotherhood inaundwa na wasomi waliobobea sana katika nyanja za sheria, udaktari na injinia. Ni chama chenye wasomi walioenea dunia nzima na wengi wao wamesomea hapo hapo na baadaye kwenda nchi za magaharibi.

  Wahitimu wengi wametoka katika kile chuo kikuu cha Al Azhar. Ikumbukwe tu kuwa kiongozi wa Alqaeeda kwa sasa Imam Dr Ayaman Alzawahiri alikuwa ni mwanachama wa brotherhood,lakini baadaye walikorofishana na yeye kwenda kumuunga mkono Osama.

  Wachunguzi wa duru za kisiasa wanasema misimamo ya jinsi gani ya kuendesha mambo ndiyo iliyozaa mgogoro wa Zawahiri na Brotherhood.

  Itaendelea..
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Inaendelea..

  Misimamo yao inatofautina kwa mambo mengi lakini inaelezwa kuwa ni kutokana na itikadi zao juu ya kukabiliana na nchi za magaribi.
  Ikumbukwe kuwa Zawahir ni msomi katika fani ya udakatri wa binadamu kama walivyo muslim brotherhood na hakuna shaka alitokea huko.
  Yeye anaamini kuwa njia bora ni kutumia nguvu dhidi ya adui, na wasomi wa brotherhood wanasema ni kutumia fikra zaidi. Ilipofika hapo akaamua kujiondosha brotherhood na kujiunga na Alqaeeda.

  Huko kwa kutumia usomi wake na CV yake ya kufungwa na mubarka katika kuuetetea usilam alikubaliwa haraka sana. Alzawahir alifungwa na Mubarak kwasababu ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha Anwar Saadat. Kisa kikubwa kikiwa ni makubaliano ya camp David kati ya Saadat na Menahim Beigin, jambo lililoonekana kama usaliti.

  Yeye ndiye alikuwa msemaji mkuu wa Alqaeeda na hakika ukisikiliza kanda za video anazotoa hutokuwa na shaka kuwa yeye ni msomi haswa.
  Tukirudi nyuma kidogo, hawa brotherhood ni wasomi sana na wanatumia sana akili katika kukabiliana na siasa za ulimwengu. Ikumbukwe kuwa matatizo kama ya cartoon yalianza na brotherhood. Baada ya picha kuchorwa brotherhood walizipata na kwa kutumia usomi wao waliweza kuzua tunayoyajua leo hii. Huwa hawapendi kuwa katikakati ya jukwaa 'central stage' lakini ni wachezaji wazuri nyuma ya pazia 'behind the scene'.

  Mubarak alipoondolewa madarkani wengi walitaraji kusikia mgombea wa brotherhood, wao kwa usomi wao wakasema hawatasimamisha mgombea. Hili sijambo la kipuuzi kwani wanajua uungwaji mkono upo kwa wananchi na si dola.

  Kuna mfano mzuri wa maudhui yao. Hamas walikuwa wanajinasibu kuwa wao ni wababe wa kukabiliana na mwisrael lakini kila uchaguzi wakawa wanashindwa. Wakajipanga wakijua kuwa nguvu ya kweli ipo katika umma na si dola. Wakaanza kutoa huduma za afya na elimu kwa wananchi. Wakafikia mahali wanakwenda nyumba kwa nyumba kujua matatizo ya raia na kuyatolea ufumbuzi. Wana nidhamu ya hali ya juu ya matumizi yao ya fedha pengine ni kwasababu ncha ya upanga haipo mbali na fisadi yoyote. Uchaguzi ulipofanyika wakashinda katika sanaduku la kura na kuwatupa nje Fatah ambao walikuwa na tuhuma nyingi za ubadhirifu na kutowajali wananchi.

  Mageuzi ya mashariki ya kati ukweli ni kuwa hayakuwapendeza wamagharibi ila wafanyeje na hali imekuwa hivyo?Hofu kubwa ni kuwa huenda ukanda wa gaza na ule wa magahribi siku moja vinaweza kutawaliwa na Hamas ambao wameonyesha wazi kuwa wanaweza kushinda kwa kutumia sanduku la kura.

  Kwa upande mwingine Misri ikiwa na ushawishi wa Muslimbrotherhood inaweza kuwa kikwazo. Libya ndiyo inaonekana kuwa tete upande wa kusini na hali ya mambo Tunisia ni ya dola ya sharia. Usisahau kuwa kuna beiruti kusini iliyopo chini ya Imam Hassan Nasrala.
  Jirani ya Israel kuna Turkey ambaye amekataliwa na EU kwasababu ya uislam naye kasema basi anatafuta mahali pa kujibanza ambako ni dola za kiislam. Kwa mtazamo huo Israel inakabailiwa na hali tete sana kwasababu haijulikani 'spring revolution' inaanzia wapi na inishia wapi.

  Kwa mtazamo wa harka haraka inaweza kuonekana mambo ni shwari mashriki ya kati, lakini ukweli ni kuwa hali bado ni tete sana.
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  HALI YA MASHARIKI YA KATI BADO TATA

  Wiki imegubikwa na Tahariri square, ile ile iliyomuondoa Mubarak sasa inataka kumuondoa General Tantawi.
  Uchaguzi wa awali katika ngazi za serikali za mitaa ulikuwa uanze wiki hii lakini hali imebadilika.
  Kinyume na matarajio ya wengi hata Arabu league walikuwa wawe na kikao Cairo kujadili hali ya Syria. Nadhani hii ni kama nilivyowahi kusema ilikuwa ni hali iliyowahadaa wengi wakidhani kuwa mambo ni shwari.

  Ugumu wa suala upo katika nchi ya masir ambayo inajulikana kuwa Africa lakini yenye ushwaishi wa hali ya juu sana kwa siasa za mashariki ya kati. Wenyewe wanaiita umul dunia (yaani mama wa dunia kama sitakosea maana hiyo au maandishi).
  Masir inajulikana sana katika historia ya mashariki ya kati, lakini pia tofauti na nchi jirani Masir ina wasomi wengi na hakika wamewekeza sana katika elimu. Kile chuo kikuu cha Alazah ni moja ya vyuo vikongwe sana duniani.

  Wanachodai wamasir ni kasi ndogo ya mabadiliko ya kuondoa utawala wa kijeshi na kurudisha mamlaka kwa raia. Kwa hali yoyote ile nchi iliyokuwa haina taasisi mbadala haikuwa rahisi kufanya mageuzi kwa muda mfupi. Hicho kinafahamika kwa wananchi wengi.
  Kinachobadili mawazo ya wananchi ni matarajio ya haraka lakini pia kuna kitu cha msingi sana ambacho ni Muslim Brotherhood.

  Brotherhood kama nilivyoeleza awali ni watu wenye mbinu sana na ndio maana ushawishi wa masir ni mkubwa miongoni mwa majirani. Brothehood wamen'gamua kuwa kuna njama za kuunda taasisi ambayo haitakidhi mahitaji yao na huenda ikawa kikwazo. Inasemwa kuwa General Tantawi amekuwa akishawishiwa na nchi za magharibi kuhakikisha kuwa atakayekuja ni mtu wao.

  Bortherhood wakatumia mbinu zao ingawa wao hawaonekani. Yale mahema ya kutibu majeruhi ni kazi ya brotherhood, huduma zote na organization ni kazi yao lakini kama walivyo na mbinu kamwe huwezi kuwaona au kuwasikia.

  Ingawa wapo wanaoamini ni mabdiliko ya wananchi tu ukweli unabaki kuwa brotherhood sasa wapo katika nafasi nzuri kuliko wakati mwingine. Hii si nzuri kwa nchi za magharibi na uwezekano wa kuwa na political tension ni mkubwa sana. Kama hali haitatengemaa masir, basi eneo lote la mashariki ya kati linabaki kuwa tete.
  Umuhimu wa habari za masir unazigubika zile za Syria si kwa upendeleo bali kwa umhimu wake katika eneo la mashariki ya kati.

  Kasi ya mabadiliko aliyotamka leo Tantawi inaweza ikatuliza mambo kwasababu jambo lolote litakalofanyika haraka ndiyo baraka ya brotherhood. Wao ni taasisi iliyojihimu na kujizatiti kwa muda mrefu sana na kuwepo kwa vyama au taasisi changa kunawapa wao nafasi zaidi. Haja yao si kuwa na kiongozi wa juu bali kumiliki sehemu kuu za serikali kama bunge ili rais ajaye atimize matakwa yao.

  Hali mashariki ya kati bado ni tete sana.
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Muslim Brotherhood sure of election victory as Tahrir unrest lingers
  The army and the interim government continue to prepare for Monday's first round of parliamentary elections, which threaten to split the opposition.
  By Anshel Pfeffer

  Meanwhile, the army and the interim government continued to prepare for Monday's first round of parliamentary elections. The elections threaten to split the opposition: While some members of the protest movement are calling for this week's elections to be deferred until power is transferred to civilian hands, and several parties have announced that they would boycott the balloting, the Muslim Brotherhood is determined to win a large number of seats in parliament. In an effort to ensure orderly elections, the Islamic group has said it does not support the current wave of protests.

  But a large number of Muslim Brotherhood members turned up in a show of support for the demonstrators nonetheless, and some of the movement's members announced they were breaking with the organization. One female university student declared that, although she was an Islamist, the Muslim Brotherhood had shown it was only out for its own interests and she would not vote for the group.

  Convinced of their upcoming success in the vote, some Muslim Brotherhood supporters had concerns beyond Egypt's borders - over Israel's intentions to dismantle the temporary Mughrabi bridge leading to the Temple Mount in Jerusalem. At Al-Azhar University, a stronghold of the movement, giant posters called for the defense of the Al-Aqsa Mosque on the mount, and Palestinian flags mingled with Egyptian ones. Guests of honor at prayers at the university were members of a Hamas delegation that was in Cairo for talks with Palestinian Authority officials.

  One Muslim Brotherhood activist, Bayuma Tayara, said his group did not need to campaign at this point. The movement has been doing grassroots work for years, he said, and every Egyptian knows who the Muslim Brotherhood is. He denied that the group was busying itself with the Palestinian issue to distract attention from ongoing demonstrations in Cairo and said the group was sure of victory.

  Sermon after sermon before and after the prayers at the university accused Israel of harming Muslim holy places and claimed that the Jews were defiling Palestine. One speaker said that all of Palestine would be liberated via Cairo's Tahrir Square - where demonstrations earlier this year brought down President Hosni Mubarak's regime.

  Among the crowd was Abed Khaled, an accountant, who said the Jews would be fought until the fighters' last drop of blood. Acknowledging that such a step was not currently feasible, he said that after an election victory the army would be prepared for war against Israel.
  For his part, however, another Muslim Brotherhood activist said that if Israel respects Palestinian rights, the peace treaty with Israel could be maintained, saying that he and his colleagues wanted to live in peace with Israel.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Wiki mbili zilizopita tuliangalia hali ya mambo mashariki ya kati hasa Misri ambako nilieleza mapema kuwa Tahariri square ilikuwa na mkono wa Muslim brotherhood. Kuna rafiki yangu alinipinga na kusema zilikuwa hisia zangu na si ukweli wa mambo. Tunaona zaidi waandishi wengi wakiliongelea jambo hili katika mizania ile ile.

  Brotherhood ni werevu na uchaguzi wa leo wanaonekana watazoa viti na huo ndio mwanzo wa kuingia madarakani ingawa ni kimya kimya. Tusubiri matokeo ya uchaguzi wa leo yatatupa nini.

  Nikumbushe kuwa Morocco kulikuwa na uchaguzi uliochagizwa na spring revolution ingawa si kwa kasi ya misiri, Libya au Tunisia. Katika uchaguzi huo chama chenye msimamo wa kati (moderate islamists) kimechukua ushindi wa sehemu kubwa.
  Inaweza kuwa haina maana ukiangalia kwa mtazamo wa haraka, lakini kama upo Tel avivu, Jeruslame au Washington hili lazima lisimbue watu na vichwa vyao.

  Swali kubwa linaloumiza kichwa ni kuwa haya mageuzi mwisho wake ni nini na nani anafuata baada ya! Je, ndiyo ule usemi wa kiswahili umetimia 'jini limetoka ndani ya chupa'!
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  MASHARIKI YA KATI NA HALI TETE YA KISIASA
  Baada ya mageuzi ya jasmine ambayo pia yanajulikana kama 'spring revolution', wengi walidhani mambo yatatulia usiku mmoja. La hasha, bado hali ni tete kule kwa umul dunia au mama wa duni Masri kama inavyojulikana kwa waarabu. Brother hood wameshinda chaguzi za serikali za mitaa na sasa wanajiandaa na uchaguzi mkuu.
  Huko libya tawi la Borthehood inajitokeza wazi wazi kuwania uongozi wa nchi. Tunisia ni wazi nguvu ya Bortherhood inashamiri ingawa wanajulikana kama waislam wenye mtazamo wa kati.

  Hali mashariki ya kati imebadilika ghafla mara baada ya kuwepo tishio la kuipiga Iran kwasababu ya ukaidi wa kutosimamisha utengenezaji wa nishati ya nuklia inayoaminika kuwa huenda ikatengeneza bomu la nyuklia.
  Ugumu ni pale bomu hilo linapofikiriwa kutumiwa kuiondoa Israel. Hapa Waisrael matumbo joto.
  Wanachotaka kufanya ni kama kile cha kulipua viwanda vya Iraq

  Utetezi wa wale wasiotaka kuona Iran inakuwa na teknolojia hiyo ni kuwa silaha hizo si vema zikamilikiwa na nchi zisizo imara 'unstable countries' hasa katika ukanda wa moto 'volatile region' wa mashariki yake.
  Wanadai kuwa huenda silaha hizo zikatumika kuimaliza Israel kama alivyoahidi Ahmadinajade.
  Ukweli ni kuwa hakuna sababu yenye mashiko bali hofu za nchi za magaharibi kutokana na upinzani unaoweza kutokea na kubadili nguvu ' balance of power'.

  Sababu hizo hazina mashiko kwasababu hakuna taifa lililowahi kuomba kibali cha kumiliki nishati hiyo.
  Hapo mashariki ya kati na mbali utaona Pakistan inamiliki nyuklia, India inamiliki lakini pia Israel inazo.
  Swali ni kuwa hawa walipewa kibali na nani ambako Iran ingeweza kuchukua kama wao?
  Na kwanini Israel ione hatari na si Lebanon, Syria au Misiri zote zenye mpaka nayo?

  Kwa upande wa pili wa shilingi, umilikaji wa silaha za maangamizi unahitaji sehemu imara' stable'.
  Rais wa marekani alipoulizwa nini kitafanyika baada ya kuanguka umoja wa kisovieti, alijibu kwa mkato kana kwamba hakuna tatizo kubwa.

  Tatizo limekuwa kubwa kuliko ilivyodhaniwa kwasababu si silaha zilizouzwa bali utaalamu na wataalamu wa kutengeneza ambao wengi wamehamia mashariki ya kati na ndiyo wanazisumbua nchi za magharibi. Hili wasingependa kuliona linatokea.

  Lakini pia Iran ina mashia wengi kuliko Saudia na hivyo kutakuwa na mashindano ya silaha kama ikifanikiwa.
  Hivyo chagizo la kuizuia Iran si Israel tu hata Saudia na wadogo zake wangependa kuliona hilo linatokea.

  TATIZO
  Obama angependa kutumika njia za kidiplomasia kuimaliza Iran. Hivyo ndivyo alivyoahidi kuyashughulikia matatizo ya Marekani katia siasa za nje. Asingependa kuona analiingiza taifa katika vita kwasababu wamarekani wamechoshwa na vita visivyoisha. Hili litamletea taabu katika mwaka huu wa uchaguzi.

  Obama anakabiliwa na upinzani wa wahafidhina wa Republican wanaotafuta kura za Waisrael. Ingawa Waisrael ni wachache nchini marekani lakini wana ushawishi mkubwa hasa katika umiliki wa vyombo vya habari na biashara.
  Hili linamweka Obama katika shinikizo kubwa .

  Israel wanataka kuishambulia mapema Iran (pre-emptive strategy). Sehemu kubwa ya nguvu yao kijeshi inatoka Marekani. Ingawa nimesema hapo awali kuwa jamii za masuni kama Saudia Arabia zingependa kuona Iran ya mashia inashambuliwa, hali itakuwa tofauti Israel ikifanya hivyo 'unilateral decision'.
  Hii itaonekana kama vita ya Wayahudi dhidi ya Waislam, na wote wataweka tofauti zao dhidi ya adui yao Israel.

  Marekani inayotegemea sana nchi za mashariki ya kati kama Qatar, Saudia na Jordan itajikuta na wakati mgumu ima kukuabliana na Israel au kuwasaliti washirika. Ni kwa msingi huo marekani ingependa kuwe na ushirika 'broad colition' itayowajumuisha waarabu kabla ya kushambulia ili kujenga uhalali kama ule wa Libya.
  Kwa upande mwingine Israel inaona tishio linaongezeka.
  Hapo ndipo hali mashariki ya kati inakuwa tete sana na inahitaji uongozi ulio na fikra.
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  UCHAGUZI WA MAREKANI (REPUBLICAN)

  Mbio za kumpata mpinzani wa Rais Obama zinaendelea na sasa wagombea wa kihafidhina(conservative) wamebaki 3. Anayeogoza ni Mitt Romney, akifuatiwa na Rick Santorum.
  Wengine waliopoteza matumaini ni spika wa zamani Gingrich na mbunge Ron Paul.

  Mbio hizo ni za kupata idadi ya wajumbe 1144 ili mgombea atangazwe kuwa mshindi.
  Hata kama haitafika hapo itategemea nani ana wajumbe wa kutosha.
  Inaweza kuwa wajumbe wakakaribiana sana na kulazimu mkutano mkuu wa wajumbe kuamua kwa kura nani abebe bendera ya chama.

  Kwa hali ilivyo ni ngumu sana kumzidi Mitt Romney akiwa na wajumbe zaidi ya 500 na anayemfuata zaidi ya 200.
  Kuna mambo mawili yanayojitokeza kwa sasa
  1. Kuwataka wapinzani wa Romney wajitoe ili kumpa nafasi ya kujiandaa kwa kukabiliana na Obama
  2. Inaonekana mnyukano unazidi kukimomonyoa chama badala ya kukijenga.

  Kwanini mchuano bado unaendelea?
  1. Mitt Romney, tajiri mkubwa ametumia pesa nyingi sana kuzidi wenzake.
  Matangazo na kampeni yake imelenga kuwachafua wenzake hasa Gingrich.
  Hili limepandisha hasira wapinzani wake ambao kwa kuficha hisia zao wanadai Romney si mhafidhina wa kutosha na hivyo uwezekano wa kumshinda Obama ni mdogo ndiyo maana bado wapo mbioni.

  2. Rick Santorum bado ana imani kuwa majimbo yaliyobaki yanaweza kumpatia wajumbe wa kumwezesha kutengeneza kesi mbele ya mkutano mkuu ili uamue nani anafaa kuwa mgombea

  3. Ili kuweza kupata wajumbe wa kutosha Santorum anamtaka Gingrich ajitoe. Wakati huo huo lengo 'target' ya Gingrich ni kumtesa Romney kama kulipa kisasi cha uharibifu wa kampeni yake kutokana na matangazo.

  Hali hailsi ni kuwa Romney anataka wenzake wajitoe ili apate nafasi ya kujiandaa.
  Santorum anataka Gingrich ajitoe ili kuweza kupata wajumbe zaidi akabiliane na Romney.
  Gingrich anataka kulipa kisasi cha kumtesa Romney.

  Uchaguzi wa awali (primaries) unategemea utaratibu wa jimbo( state). Kuna state ambazo mshindi anapewa wajumbe wote, zipo state mgombea anapewa kutokana na asilimia ya wapiga kura(percentage), kuna state mgombea anapewa kutokana na popular vote(kura ya umaarufu), zipo state wanaopiga kura ni wajumbe wa chama( caucus) na zipo state wajumbe wanapatikana kutokana na ushindi wa eneo na idadi yake. Kwakweli ni mchakato unaochanganya kama hujauzoea.

  Kampeni za uchaguzi zinafanyika kwa njia za kisayansi sana. Sio suala la kupanda gari na kuanza kuzunguka tu.
  Kwa kuanzia tu nidokeze kuwa timu za kampeni zinaundwa na watu waliobobea katika fani mbali mbali ni waajiriwa wa kampeni. Timu hizo zinahusisha watu wa fani za jamii (Socialogists), wanasaikolojia( Psychologist), watu wanaoshghulikia mgawanyo na idadi ya (Demographic), wabiga debe(Pundits), Wanamikakati( Strategists) n.k.

  Sehemu inayofuata tutaangalia kampeni zinafanyika vipi kuhusisha nini na kwa mkakati gani.
  Tutaoanisha na hali halisi ya nchi yetu kwa kuzingatia mazingira yetu na kuona kama tunaweza kujifunza lolote.

  Itaendelea.....
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Inaendelea....
  Hatua ya kwanza ni kwa mgombea kuunda kikosi kazi ili kubaini jinsi gani anakubali ndani ya chama na jamii yake(exploration team) na kuleta usuli (feedback). Baada ya hapo timu inaajiri wafanyakazi wenye sifa katika nafasi mbali mbali. Maafisa mawasiliano(communication officer), wabiga debe( pundits), wanamkikati(strategist),wataalumu wa siasa ya jamii 'political analyst) n.k. Hawa wanakuwa waajiriwa kulingana na nafasi zo na kazi ya campaign team ni kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa upande wake

  Imekuwa ni kawaida kusikia wakuu wa vitengo vya kampeni wakijiuzulu kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na matamshi yasiyolingana na maudhui ya kampeni. Imetokea kwa Obama,Mcain, Carter, Clinton n.k.
  Hili linampa unafuu mgombea kwasababu anakuwa na wafanyakazi sio viongozi wenzake na linampa unafuu wa kutawala na kumwajibisha asiyefanya vema.

  Mtandao huo ni kuanzia ngazi ya taifa hadi katika wilaya. Hivyo ndivyo wagombea wanauwezo wa 'ku-organize' kampeni katika nchi kubwa kama Marekani au India na Brazili kwa viwango tofauti katika madaraja ya dunia.

  Ni tofauti na sisi ambapo viongozi wa chama ndio hao hao wakuu wa kampeni na kila kitu. Suala la uwajibikaji linakuwa halipo kabisa. Fikiria kidogo, hivi Kikwete anawezaje kumwajibisha Malecela au Dr Slaa kumwajibisha Zitto. Kutokana na hali hiyo majungu na kutetana kunakuwa kama sehemu ya utendaji na sio kampeni.

  Kibaya zaidi watu wanaojishughulisha na kampeni, kwanza hawana utaalamu au uzooefu wa kufanya kampeni za kisiasa, na matokeo yake ni yale tunayoyaona kila siku matusi, kashfa na kauli za kuudhi na kukera wala siyo sera au mipango.

  Ukifuatilia kampeni za mwaka 2008 utaona Obama aliweza kuwashinda manguli wa Democrat kama akina Hilary, Joe Biden, Richardson n.k. Siri kubwa ni jinsi kampeni yake ilivyokuwa inaliangalia suala la uchaguzi kwa mtizamo tofauti.
  Wakati wengi waliamini vijana hawapigi kura Obama alielekeza nguvu zake huko. Wakati wengine walikuwa wanaangalia majimbo yenye wajumbe wengi yeye alielekeza nguvu zake hata kwenye wajumbe 10.

  Hii maana yake ni kuwa wataalamu wake wa 'demograph' ambao ni mgawanyo wa watu walijua wapi waelekeze nguvu na pesa na wapi wasitilie maanani. Hili tunaliona pia kwa Mitt Romney na Santorum ambapo Santorum amejikitika kwa evangelical na Mitt Romney kwenye miji mikubwa. Inategmea mtu ataliangaliaje lakini ni wazi kuwa kuwagawa wapiga kura kwa makundi ni tatizo kubwa sana kisiasa.

  Kuna kundi la wapiga kura linaitwa independent ambalo hata Tanzania lipo. Hili ndilo huamua nani ashinde panapotokea mvutano na mchuano mkali kama wa CCM na Chadema. Unapojaribu kuchomeka chembe ya kugawa makundi, uwezekano wa kushinda unakuwa mdogo sana kwasababu hutawapata independent.

  Kosa hili limefanywa na chama cha CUF kwa kudhani kuwa kujifunganisha na imani kulitosha kukisaidia chama kutwaa dola. Huu ni ujinga unatokana na kuwa na wanasiasa wa kubumba na si wataalamu.

  Makosa hayo yanaonekana katika vyama vyote. Ndiyo maana CCM huchomeka chembe za udini na ukabila wakijua kuwa hiyo itawasadia kupata independent kutokana na ukongwe wao. Wao ndiyo walizua udini wa Chadema baada ya ukabila kushindwa.

  Lakini pia timu ya kampeni ina kazi ya kufanya tathmini ya chaguzi zilizopita na zinazoendelea. Ni nadra sana kuona vyama vya siasa vikifanya hivyo hapa nchini. Hii ni ushahidi kuwa kampeni zinaendeshwa bila utaalamu wala wataalamu bali wachumia matumbo.

  Ni makosa chama cha siasa kufanya siasa za msimu. Siasa ni suala endelevu na kila mara linataka tathmini,mrejeo na mkakati. Wenzetu kama wa Marekani mtandao wao ni mnene kiasi cha kujua nani anakubalika wapi na kwanini.
  Sisi hujikuta tukishtukizwa bila kujua nani anakubalika wapi.
  Matokeo ya hayo ni kukurupuka bila kuwa na mtandao sehemu husika, kuwachukua viongozi kutoka makuu makuu tukidhani kuwa ushawaishi wao redioni unaweza wavuta wapiga kura

  Hakika mtu anayejua sehemu flani ni rai wa sehemu hiyo. Hivi kwanini kusiwe na waajiriwa wa kampeni waliobobea wanaoweza kuendesha kampeni kisayasi? Kwani kampeni meneja lazima awe mbunge au mtu wa makao makuu na si kiongozi wa mkoa au kanda akisadiwa na wale wa chini yake?

  Utashangaa vyama havijui hata kutumia teknolojia kuwafikia wapiga kura. Ni mara ngapi umesikia tangazo la kunadi au kunanga chama kingine katika redio? Kwanini wategemee TBC na wasizitumie FM station.

  Majibu yake ni rahisi hakuna mkakati wa kampeni na watu wanadhani kampeni ni mikusanyiko ya watu tu.

  Ujumbe wangu wa leo ni kuwa pamoja na uchanga wa vyama na demokrasia yetu, kuna ukweli kuwa bado hatujaweza kutumia njia za kisayansi kushinda uchaguzi. Tumekuwa tukilalamika kuibiwa kura kama kisingizio bila kujua kuwa wizi una kikomo hasa pale ushindi unapokuwa dhahiri.

  Ni wakati vyama vikae chini na kuangalia mbinu na mikakati ya ushindi na si kutegemea personalities ndani ya vyama.
  Kuna kitu kinakosekana katika kuunganisha dot, tumefanya siasa kama kazi ya kila mtu hata asiyejua na kusahau kuwa ni kazi ya kitaalamu.

  Hadi tutakapobadilika na kwenda na wakati kama wenzetu bado tunamiaka mingi sana ya kujikomboa kidemkrasia.

  Itaendelea....
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  YA MUSLIM BROTHERHOOD YAMEANZA KUJITOKEZA, CCM TUMBO JOTO

  Katika mabandiko #29,30,31,32,33,34 tumejadili kuhusu hali ya kisiasa ilivyotete mashariki ya kati. Nilisema bado hali ni tete sana na spring rvolution pengine ndiyo kwanza ilkuwa inaanza. Kuondoka kwa Gaddafi na Mubarak ni sehemu tu ya mabadiliko lakini si mabadiliko kamili kwasababu bado yapo yaliyokuwa yamejificha.

  Kwa hakika Marekani haikufurahia mageuzi hayo kwa kasi yake na yalivyojitokeza bila kutarajiwa.
  Jaribio la kuahirisha muda wa Mubarak kujiuzulu ili apatikane 'mtu wao' lilishimdikana kutokana na wimbi la mageuzi.

  Wasi wasi wa marekani ni kuwa nani atakayekuja baada ya Mubarak ikizingatiwa kuwa chama cha Muslim brotherhood kimekuwa nyuma ya kila badiliko mashariki ya kati hata ghasia tunazoziona. Moja ya mambo yaliyochochewa na brotherhood ni katuni pamoja na uchomaji wa vitabu viyakatifu.
  Kama nilivyosema awali Bortherhood ni wasomi sana na ni ngumu kujua wanapanga au wanafikiria nini.

  Baada tu ya Jasmine revolution wao wakajiita 'freedom and justice party' ili kuficha ile identity yao. Wakati huo huo wakikanusha kuwa hawatamsimamisha mgombea hasa kwenye nafasi ya Urais. Mara walipobaini serikali ya kijeshi ilikuwa ina mkakati wa kupitisha muda ili kujenga mazingira ya kuandaa mgombea wao, Brotherhood wakachochea Tahariri square ya pili. Hayo yakiendelea uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa ukiendelea na hakika Brotherhood wakapata viti.
  Hivi karibuni kumekuwepo na uchaguzi wa bunge na Brotherhood wamevuna viti vya kutosha

  Majuzi wametangaza kuwa wanamsimamisha mgombea katika nafasi ya Urais. Huu ni mtihani kwa nchi za magharibi kwani Brotherhood wamefuata taratibu zote za kidemokrasia na wanazidi kupanda ngazi.
  Kuwanyima furasa ya kusimamamisha mgombea ni kuwanyima fursa halali kabisa ya kidemokrasia.
  Lakini pia Brotherhood wanaweza kujitoa katika kinyang'anyiro cha urasi. Swali ni kuwa Rais ajae ataendesha vipi serikali ili hali brotherhood wana umiliki mzuri tu wa Bunge?
  Hakika hiki ni kisu kianchokata pande zote!

  Mfano huu wa Brotherhood ni somo zuri ambalo CCM wamelielewa vema sana. Ni kama coincidence kuwa model ya brotherhood kule Misri inafanana sana na hali ya mambo ilivyo hapa kwetu kisiasa na wala simaanishi kiitikadi za dini

  CCM imeshinda chaguzi za vyama vingi na kila mara ikijinasibu kwa kishindo. Ni kishindo kinachotokana na mbinu nyingi na si sanduku la kura tu, lakini tukubali kuwa mwenye kisu kikali ndiye mla nyama na hicho kisu wanacho CCM.
  Kadri muda unavyosonga mbele ni wazi kuwa zile mbio za Urais zilizokuwa zinatafuta mshindi wa pili sasa ni ushindani wa mshindi wa kwanza.

  Kinachotatiza CCM ni ukweli kuwa kila mara wapinzani wamekuwa wanaongeza idadi ya wabunge.
  Na wala si idadi tu ni ubora wa wabunge. Hakuna shaka kuwa wabunge wengi wa upinzani wana mtazamo na fikra huru zaidi kuliko wenzao wa CCM. Ni rahisi kukutana na kijana akakuambia anamjua Tundu Lisu, Halima Mdee, Mnyika achilia mbali akina Zitto n.k.
  Kijana huyo anaweza kutojua Wabunge wa chama tawala kwasababu ni nadra wao kupata fursa za kuchangia mambo ya kitaifa hasa yanayogusa maisha ya kawaida ya wananchi.

  Zaidi ya hapo ngome kubwa za CCM zimeshavunjwa. Dar es salaam ambayo 'traditionally' ni CCM sasa ina wabunge wawili wa uinzani, na hakika majimbo 2 ya CCM ni kwasababu ya ubabe tu vinginevyo tungesikia mengine.

  Arusha imeshaangukia mikononi mwa wapinzani, Kilimanjaro zimebaki wilaya za Mwanga na Same ambazo taarifa nilizo nazo utiifu kwa CCM sasa unatoweka

  Mwanza tayari, Mbeya ndiko mahali chachu ilipoanzia kwa kanda za nyanda za juu na imeshaambukiza Iringa. Ninachotaka kusema ni kuwa 'key constituents' zinamegwa kila uchao

  Rika la vijana limetokea kuwa na chuki na CCM kiasi kisichoelezeka. Hili ni pamoja na lile la wasomi wa vyuo n.k.
  CCM inafahamu hilo, na mbinu waliyotumia uchaguzi uliopita ya kufunga vyuo ili kutawanya kura imekiumiza chama kuliko kukisadia. Wanavyuo hao waliorudishwa makwao kupisha uchaguzi kwasababu za kisiasa na si kitaaluma ndiyo walioongoza mabadiliko huko wilayani. Kufunga vyuo ili majimbo ya mijini hasa Dar yasichukiwe na wapinzani ni mkakati mbovu na wa kijinga sana CCM iliwahi kufanya

  CCM imakabiliwa na changamoto nyingi sana
  1. Haikubaliki miongoni mwa jamii ya wasomi
  2.Imechokwa na daraja la kati 'middle class'
  3.Inaandamwa na kashfa na hivyo kuwa 'on defensive' badala ya kuwa offensive. Matokeo yake ni sera za akina Lusinde
  4. Mvutano kati ya wenye chama halisi na kundi la wafanyabiashara ambao wanajua fika ustawi wao unategemea uwepo ndani ya chama
  5. Makundi ndani ya chama yanayopigana vita kuwania uongozi
  6.Inazidi kupoteza umaarufu kwa kukosa hoja ya kuonyesha uhalali wa kupewa uongozi wa nchi zaidi baa da ya miaka 50

  Mambo hayo yanakiweka CCM katika wakati mgumu sana na wala hayawezi kutatuliwa katika muda mfupi wenye mvutano'tension' kuelekea 2015.

  CCM inajinasibu kuwa kwa kutumia ukubwa wa nchi na hasa vijijini kuliko na watu wasioweza kupambanua inaweza kushinda nafasi kama ya urais. Hili pia litategemea msaada wa mbinu na usaidizi wa vyombo kama tume ya uchaguzi.

  Kwa hali ilivyo sasa uchaguzi ukifanyika leo CCM itapoteza zaidi ya wabunge 50. Idadi hiyo itaongezeka kadri muda unavyokwenda.

  Kinachowatatiza sana CCM ni yale ya Brotherhood kuwa wanaweza kuwa na Rais lakini bunge likawa la wapinzani au basi CCM ikakosa 2/3 majority. Ikifika hapo hakuna anayetamani Urais tena isipokuwa wale wanaokwenda Ikulu kibiashara.
  Ikifika hapo CCM wanaingiwa na kiwewe kwasababu umiliki wa nchi kwa asilimia zaidi ya 50 katika bunge na serikali sasa inaanza kuwa ndoto. CCM inajiandaa kwa kipigo kikali kama cha KANU,UNIP n.k. Vyama hivyo vilianza kudorora kwa mtindo wa CCM na sasa vimefutika au kubaki kwenye makabrasha ya historia. Anayedhani CCM ni tofauti basi atafutiwe matibabu haraka kwani muda si mshiriki mzuri kwake

  Endapo vyama vya upinzani vitakwepa fitna za udini na ukabila, kutumiwa kwa baadhi ya watu(mamluki) na kuacha malumbano yasiyo na tija basi nafasi ipo wazi kuchukua au kushiriki uongozi wa nchi kikamilifu

  Changamoto inayovikabili vyama vya upinzani ni migogoro ndani yake na uendeshaji wa vyama kama taasisi za kisiasa.
  Hatari kubwa ni ile itakayotokana na wimbi la wanaCCM wanaojiandaa kuondoka. Hawa wapokelewe kama wanachama na si viongozi kwasababu kuhama kwao si kwa kufuata itikadi au kuongoza mabadiliko ni kuchumia tumbo na wengine wakiwa mamluki.

  Tusemezane
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  UCHAGUZI MAREKANI NA MISRI

  Baada ya wiki za malumbano ya siasa za ndani sasa tuzirejee siasa za nje kwa kuangalia nchi mbili zenye ushawishi katika siasa za dunia, Marekani kwa Obama na Misri.

  Tumeona katika mabadiko yaliopita jinsi siasa za Misri zinavyosumbua jumuiya ya nchi za magaharibi na Uarabuni kwa ujumla. Baada ya kuondoka mubaraka kwa shinikizo la wananchi hasa vijana, wana harakati hao hawakuunda umoja wowote wa kisiasa. Ndiyo ikawa nafasi za vyama vya kimakundi kama Muslim Brotherhood, Sufi wa madhehebu ya sufiani kunyatia uongozi.

  Kama nilivyowahi kuandika, Brotherhood ni werevu na wasomi sana. Ingawa hawakujitokeza Tahariri square, uratibu wote wa shughuli ulifanywa nao. Hii ilikuwa ni kuzuia hujuma zozote kuwa mageuzi yalikuwa na mkono wa Muslim Brothehood ambao wangehusishwa na siasa kali au za kigaidi. Walitangaza kuwa hawana nia ya kugombea urais. Tunaowajua tulijua ni changa la macho, wao waligombea nafasi za bunge na sasa wanalitawala kwa kiasi flani.

  Uchaguzi huu walisimamisha mgombea wao ambaye aliwekewa pingamizi kuwa mama yake amechukua urai wa marekani.
  Kwa sheria za Misri mgombea ni lazima awe raia ikiwa ni pamoja na wanafamilia kama baba na mama.
  Hata hivyo wameweka mgombea mwingine ambaye sasa anaingia duru la pili kupambana na waziri mkuu aliyeteuliwa na Mubarak wakati machafuko yakiendelea.

  Kinachoshangaza ni kuwa wale waliotarajiwa wamebwagwa ikiwa ni pamoja na Amr Moussa aliyekuwa katibu mkuu wa jumuiya ya waarabu(Arab League). Matokeo yanashangaza na haijulikani hatima ya duru la pili itatoa nani kama Rais.

  Ikiwa Rais atatoka brotherhood basi nchi za magharibi na Israel watakuwa na wakati mgumu sana. Endapo atakuwa aliyekuwa waziri mkuu bado vurugu zitaendelea. Watu hawataki mabaki ya Mubarak na wengine wanawasi wasi na Brotherhood kwa historia yake. Jibu litapatikana katika wiki mbili zijazo.

  Huko Marekani mtifuano unaendelea kati ya Obama wa Democrat na Mitt Romney wa Republican.
  Vita vipo katika majimbo yanayobadilika (swing states) kama Carolina Ohio n.k.

  Obama amefaulu kuwadhibiti Republican katika eneo lao la kujidai la ulinzi na usalama(Nationa security) kwa kuwakamata na kuua wanamtandao wengi sana wa Alqaeeda akiwemo Osama Bin Laden. Kifo cha Osam aliyewashinda marais wawili waliotangulia ni big plus kwa Obama. Ameweza kudhibiti matukio mengi ya ugaidi na hivi karibuni waliweza kupenyeza mtu wao(double agent) ambaye alifanikiwa kuichukua teknoloji ya bomu lisiloweza kung'amuliwa na vifaa na kulifikisha marekani salama kabisa. CIA wanafanya uchunguzi wa jinsi ya kuzuia mbinu hizo kama zilivyoanza kutekelezwa na Abdulla Mutalab(under wear ) bomu ambaye yupo magereza za marekani.

  Obama ameweza kumaliza vita vya Iraq alivyovipinga na kuahidi kuvimaliza kwa utulivu(with responsibility). Juzi amewaita washirika wake wa NATO kupanga namna ya kumaliza vita ya Afghan. Haya yanampa nafasi kwa ukweli kuwa wamarekani wamechoshwa na vita. Hili limewafunga mdomo Republican wanaoamini mabomu zaidi ya majadiliano. Umma umechoka

  Obama pia anasifiwa kwa kuingilia mgogoro wa Libya bila askari na kwa ushirika na NATO. Utaona kuwa hata ndege za marekani ziliposhambulia Libya, marekani ilisema imeombwa na nchi za NATO kwakuwa ilikuwa na teknolojia maalumu(Unique technology) ambayo leo tunaijua ni ile ya stealth kama ilivyotumiwa na askari waliomuua Osam Bin Laden.

  Tatizo la Obama ni uchumi. Licha ya ukweli kuwa ametengeneza ajira milioni 4 ukilinganisha na milioni 6 zilizopotea kabla ya kuingia madarakani, bado kuna mamilioni ya wamarekani wasio na kazi na hawa hawaamini kuwa sera za uchumi za Obama ni nzuri. Hata hivyo ukiangalia kwa takwimu utaona nchi inatengeneza ajira kuliko zilizokuwa zinapotea.
  Utengeeza(manufacturing) umekua na kuchangia ongezeko la ajira pengine kuliko wakati wowote wa miaka 10 iliyopita

  Bei za mafuta zimeteteresha sana uchumi na ilifikia mahali pipa moja lilikuwa ni dollar 107 ingawa sas ni kati ya dola 92-95. Hili lilitoa nafasi kwa republican kumshambulia Obama hata kama suluhisho la haraka haliwezekani.

  Mgombea wa Republican Mitt Romney anaonekana kumshambulia Obama katika eneo hilo la uchumi. Anaweka historia yake kama mfanyabiashara mwenye uwezo wa kujua hali ya uchumi na kutengeneza ajira.

  Hili analifanya ili kupata kura za wenye hasira na hali ya uchumi. Ni mpango wa hatari sana kwa mgombea(Risk strategy) kwasababu uchumi ukiimarika au kuonyesha kuimarika hatakuwa na hoja. Inabashiriwa kuwa kabla ya November uchumi unaweza kukua na kuongeza ajira.
  Ikifika hapo wapo wanaoona kuwa kwanini Mitt Romney aombe kazi kwa mapungufu ya Obama na si kile atakachokifanya?

  Republican wana wasi wasi endapo mkakati huo ni madhubuti na endelevu(sustainable). Ikizingatiwa kuwa Romney ana matatizo na base ya Republican(evangelical) na kutokubalika miongoni mwa washirika,safari yake inakuwa ngumu kidogo

  Tukiangalia mgawanyo wa makundi (ethenics) vita ya kura za Walatino ni 60 kwa 27 asilimia upande wa Obama(in favor of). Kwahiyo karata aliyo nayo Romney ni uchumi, ni karata nzuri lakini si sahihi kuilalia na kuitegemea. Labda tu aombe uchumi wa ulaya (Euro zone) uendelee kutetereka na tatizo la Greece lizirudishe juhudi za kuimarisha uchumi dunia nyuma.

  Hata hivyo miezi 5 ni mingi sana, na yupo mwanasiasa wa uingereza aliyewahi kusema katika maisha ya siasa siku moja ni nyingi sana na inaweza kubadili mwelelekeo na mwenendo wa kisiasa.

  Tusemezane
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3, kauli ya Obama ya kuunga mkono ndoa za jinsia moja ni mojawapo ya karata zake kwa ajili ya uchaguzi ujao??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Katavi, hilo lina ukweli kabisa.

  Chama cha Republican (GOP) ni cha kihafidhina na kinaamini katika mambo fulani (fundamenta principles). Wao hawapendi mabadiliko katika jamii yao. Wanaitaka Marekani ile ya George Washington kama ubepari, imani za dini hasa evangelism, serikali ndogo, serikali ndogo na soko huria. Soko huria halina maana bidhaa bali ''survival for the fittest'' kama nitaeleweka.
  Katika imani hawaamini katika ndoa za jinsia zinazofanana wala ushoga kwasababu 'base ya republican ni evangelism'

  Democrat wanajulikana kama Liberal au [left wing]. Wao ni progressive na wanapenda mabadiliko. Wanaamini kuna umuhimu wa kubadilika kutokana na nyakati. Kwahiyo political base yao ipo kwa waliberali (wanaopenda mabadiliko)
  Hawa ni pamoja na wanandoa za jinsia moja.

  Wanandoa wa jinsia moja hawaundi kubwa sana linaloweza kubadili matokeo kwa urahisi lakini katika uchaguzi mkali na wenye kukaribiana kimatokeo (too close to call) wana umuhimu sana. Umuhimu wao zaidi ni ushawaishi wao katika jamii.
  Kuna sehemu kubwa sana ya watu maarufu 'celebrity' katika kundi hili. Kuliteka kundi hili ni kuteka ushawishi.

  Obama alipozitambua ndoa za jinsia moja siku iliyofuata alikuwa na 'fund raising' ambayo ilifanikiwa sana. Inasemekana kundi hili lilifurahia sana tamko lake. Hata ukiangalia muda alipotoa tamko na matukio yaliyofuata ni dhahiri ilikuwa ni 'calculated move'.

  Tatizo linalomkabili Mitt Romney ni kuwa, kwanza anaonekana 'Rude' yaani mkatili mwenye dharau hata miongoni mwa wahafidhina wenzake. Pili yeye ni muumini wa kanisa la Mormon, imani inayopingwa na evangelists. Hili linafanya ile republican base isiwe na munkari 'excited'. Hili linawatia sana hofu republican kwasababu huenda evangelists wakapiga kura tu kumkataa Obama na si kwasababu wanampenda Romney. Kuna uwezekano wengine wasione umuhimu wa kupiga kura na hilo litapunguza nguvu katika 'base' ya republican.

  Safu inayofuata tutajaribu kuziangalia ' political bases' za vyama vyetu nchini, CCM, CHADEMA, CUF na NCCR

  Tusemezane
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  YA BROTHERHOOD YAMETIMIA, TULISEMA NA SASA NI KWELI

  Tutaendelea na hoja ya bandiko namba# 103. Kutokana na habari zilizojiri Misiri hebu tuangalie kwa uchache ni nini kimejiri.

  MUSLIM BROTHERHOOD WASHINDA UCHAGUZI

  Mgombea wa chama chenye cha Muslim Brotherhood ametangazwa kuwa Rais wa Misri. Hii ni baada ya duru la pili. Duru la kwanza liliwaenguea watarajiwa 'front runners' kama katika mkuu wa Arab League Amour Mousa na aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la Atomic dunia Al Baradei.
  Mwenguo wa awamu ya kwanza ulimuondoa pia mgombea halisi wa chama cha Muslim brotherhood kwa hoja ya uraia wa wazazi wake kule Marekani.

  Duru la pili likawa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha anga mwanajeshi Ahmed Shafik ambaye aliteuliwa na Mubarak sikuza za mwisho wa utawala wake kuwa Waziri mkuu. Shafiki ana fungamano kubwa sana na jeshi na hakika alipigiwa upatu na jeshi ili awe rasi ajaye.

  Brotherhood walimsimamisha mgombea baada ya wa awali kuenguliwa.
  Huyu ni bwana Mohame Mursi ambaye sasa ni rais Mteule wa Misri.
  Bwana Mursi ni Engineer mwenye shahada ya PhD na alikuwa profesa katika chuo kikuu cha California.

  Huko nyuma katika safu hii nimewahi kueleza kuwa Muslim Brotherhood ni kundi linaloundwa na wasomi waliobobea sana na wanafanya mambo yao kisomi sana. Mmoja wa wanachama wake alikuwa ni Ayaman AlZawahir ambaye ni kamanda wa kikundi cha Alqaeeda. Al Zawahi ni Daktari (Surgeon) kitaaluma.
  Kutokana na kujawa na jazba na kutokuwa na subra alishindwa kuishi na wasomi wa Brotherhood kama nilivyowahi kueleza huko nyuma akahamia Alqaeeda.

  Mageuzi ya Tahariri yalikuwa na mkono wa Brotherhood ingawa hawakujitokeza. Ni wao waliokuwa wanatoa huduma zote kwa waandamanaji, majeruhi na wahanga wa Tahariri.
  Hawakuwa na haraka ya kuutaka urais ikiwa ni mbinu ya kuwapumbaza wale wasiopenda neno hilo Muslim brotherhood kama Israel, Marekani na nchi za kiarabu zenye msimamo wa kati.

  Walishinda uchaguzi wa mitaa na kisha kumiliki bunge. Wiki iliyopita katika harakati za kuzuia brotherhood utawala wa kijeshi ulivunja bunge ili kuleta sintofahamu miongoni mwa Brotherhood. Wasomi hawa hawakuhamaki na walibaki na mtazamo wa kumnadi kiongozi wao (Never distracted by political manourver from their opponents)
  Sasa walichokitaka wamekipata. Hakika sisi wengine tuliona hili siku nyingi sana na ushindi wa leo unakamilisha tu maoni yetu ya siku za nyuma.

  NINI MUSTAKABALI WA MISRI NA SIASA ZA KIMATAIFA!

  Hakika Wamisri hawakuwa na chaguo katika uchaguzi huu. Ahmed Shafik alikuwa ni mabaki ya Mubarak na Mohamed Mursi ambaye ni watu wa msimamo mkali. T
  uliwahi kusema Wamisri ni progressive na hawapendi sharia. Walikuwa njia panda ndiyo maana kuna mgawanyiko wa 50/50.

  MOHAMED MURSI
  Anakabiliwa na mambo makubwa yafuatayo
  1. Kikundi cha waislam cha Sufi chenye falsa ya Sufism. Kikundi hiki ni sehemu ya waislam na moja ya sifa zao ni Dhikr.
  Neno Sufi lina maana nyingi na tafsiri nyingi na tutazingalia tafsiri hizo na misimamo yao siku zijazo.
  Hawa Sufi watamsumbua bwana Mursi kwasababu ni watu wanaotaka utawala wa zama zile za mahalifa.
  Hawana subra kama Brotherhood na wala hawana wasomi katika fani nyingine ukiachilia dini.

  2. Vyombo vyote vya usalama wa nchi vipo chini ya jeshi lililokuwa linamuunga mkono aliyeshindwa Shafik.
  Itamuiwa ngumu sana bw Mursi kuvunja nguvu hii na atakakbiliana na upinzani mkubwa hata kama si wa vita.

  3. Waislam wenye msimamo mkali dhidi ya Israel sasa watatoa makucha yao kwa vile brotherhood kimekuwa kikiamini kuwa kuna upendeleo na uonevu mkubwa katika eneo la mashariki ya kati hasa Israel na Palestina.

  Bw Mursi atakuwa na wakati mgumu wa kuweka mizania kati ya taswira yake kimataifa na masilahi ya chama chake na wale wanaokiona kama ukombozi dhidi ya ukandamizaji.

  MAREKANI NA ISRAEL ZINA MSIMAMO GANI!
  Hofu kubwa imetanda Israel hasa kuhusu makubaliano ya Camp David yaliyotiwa saini na Anwar Saadat na Menahim Beigin. Ni makubaliano hayo yaliyopelekea Saadat kuuwawa na hakika waliokuwa nyuma ya mauaji huo ni Brotherhood.
  Mmoja wa watuhumiwa ni kiongozi wa Alqaeeda kwa sasa Al Zawhir.
  Swali ni je, ''kichaa kapewa rungu'' na je mkataba utaendelea kama ulivyo?

  Kwa upande wa marekani hasa kuelekea uchaguzi matokeo haya si mazuri kwa Obama hata kidogo. Moja ya sera za Marekani ni kuhakikisha usalama wa Israel. Kitendo cha Muslim Bortherhood kushika madaraka ni tishio kwa usalama wa Israel na hilo litaonekana kama uzembe wa Obama kutotumia maguvu ya marekani katika ushawishi.
  Republican watawachochea Waisrael wanaomiliki vyombo vya uchumi na habari Marekani na hili litamgharimu sana Rais Obama.

  Kadri tunavyosonga mbele tutaendelea kuchambua hali ya mambo mashariki ya kati ambayo tulisema bado shwari siku za nyuma na ndivyo ilivyo hadi leo

  Tusemezane
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Duru za siasa.
  Nguruvi3,
  Tujadili siasa za Mashariki ya Kati tumeona chama cha (Muslims Brotherhood) kimepewa nafasi ya kuwaongoza Wamisri, Rais Mohamed Morsi atafanikiwa kwenye siasa zake, tumeona upande mwingine wa Baraza la Kijeshi limevunja Bunge na kutanganza kujiongezea mamlaka zaidi na pia limeunda kamati maalumu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya katiba kwa lengo la kupunguza madaraka ya rais na kujipa lenyewe mamlaka makubwa.

  Marekani na Israel walikuwa wanapenda Ahmad Shafiq ashinde kwani walitegemea ni masalia ya utawala wa Mubarak, kwao hana athari mbaya kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati.

  Inasemekana wafuasi wa Muslim Brotherhood wanapanga kufanya maandamano makubwa Taharir kupiga hatua ya baraza la kijeshi la nchi hiyo kujilmbikizia madaraka makubwa. Hofu ingine kwa Marekani na Israel na mafungamano ya Brotherhood na chama cha Hamas.

  Hofu ingine ni kutumia ukanda wa Misri kupitisha meli kubwa za kijeshi za Kimarekani kuelekea Asia na Mashariki ya Kati kupitia Suez Canal, kwani mtazamo wa Muslims Brotherhood ni kuwa Marekani ndio adui yao wa kwanza kwa maslahi yao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ritz,
  Tatizo la Misri ni kwamba tangu mapinduzi ya 1952 ambapo Gamal Abdel Nasser aliingia mamlakani Misri mimekuwa inaendeshwa kijeshi. Alipofariki Nasser, makamu wake Sadat akashika mikoba, na Sadat alipouawa ni Mubarak, mwanajeshi mwingine, aliyeshika uongozi. Kwa hiyo kwa miaka 60 sasa uongozi wa Misri umetoka jeshini. Nadhani inawawia vigumu wanajeshi kukubali utawala wa kiraia na ndiyo sababu walifuta bunge na kupunguza mamlaka ya rais mpya. Rais hawezi kumwondoa mamlakani au kumhamisha mkuu wa majeshi. Lakini swali tunalopaswa kujiuliza ni je wataendelea mpaka lini kuzuia matakwa ya umma. Lakini kuhusu utawala, nafikiri Morsi atakuwa moderate. Hana njia katika uhusiano wake na Israel na kadhalika Misri imekuwa mtegemeaji mkubwa wa misaada ya kifedha na kijeshi kwa Marekani. Kwa hiyo in the short run huo uhusiano utaendelea na nafikiri, kama watawala sasa, Moslem Brotherhood watalazimika kuangalia upya uhusiano wao na Hamas.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Ritz,
  Katika kipindi cha miaka 60 kama alivyosema Jasusi Misri imekuwa katika utawala wa kijeshi na kati ya hiyo 30 ni Hosni Mubarak peke yake. Wanajeshi wameshaona kuwa kutawala ni haki yao. Unajua, kutawala sijui niseme ni 'addiction''! Hakuna mtu anayepewa madaraka akayaachia kirahisi hasa vinchi masikini kama vyetu.

  Baada ya anguko la Mubarak jeshi liliendeleza madaraka kwa kumweka Gen Tantawi. Wakaitisha uchaguzi wa haraka wa serikali za mitaa wakijua kuwa Muslim Brotherhood watasusia. Hawakujua kuwa Brotherhood walishajipanga. Matokeo yake wakachukua viti na kisha uchaguzi wa wabunge wakamiliki Bunge.

  Brotherhood ni wasomi sana, walifanya hivyo kwasababu kuu mbili.
  1. Kuanza kujijenga katika ngazi ya chini (grassroot level).
  2. Kumiliki bunge ili Rais ajaye kama hatatoka kwao waweze kumdhibiti kwa njia ya bunge

  Wanajeshi wakamweka Shafiq ambaye ni chaguo la Marekani na kumwekea vikwazo mgombea halisi wa Brotherhood.
  Aliyetoa siri ya mgombea wa Brotherhood kuwa na wazazi walichokua uraia wa Marekani ni Marekani
  Brotherhood walikuwa na plan A na B na wakachukua Plan B ambayo ni Morsi

  Wanajeshi wakaamua kuvunja bunge wiki moja kabla ya uchaguzi kwasababu:
  1. Kujihadhari baada ya kuona brotherhood wanaongoza kura za maoni na wakajua ushindi ni kitendawili.
  2. Kuwachanganya Brotherhood ili waache kampeni na kuanza malalamiko.

  Brotherhood kama ninavyosema ni wajanja, wakaa kimya wakashinda uchaguzi.
  Sasa Jeshi linataka kupunguza madaraka ya Rais. Kwanza limesema Rais hawezi kutangaza vita bila kukukbaliwa na jeshi.
  Hapo inaonyesha wanataka kuwa juu ya Rais.

  Wananchi wanataka wanajeshi warudi kambini na hili litazua mvutano tena.

  Morsi hadi sasa ameonyesha kuwa ni moderate kwa kusema ataheshimu mikataba yote na hapa anaongelea Camp David.
  Make no mistake, hawa ni Brotherhood wana subra na wanaona mbali sana. May be 2 years down the raod wanaweza kuja ni kitu kingine kinacholeta maana wanayoitaka wao.

  Mtihani wa Morsi na Brotherhood ni kuhusu Hamas. Na kama unavyojua Hamas wana uhusiano na Hizboullah ya Imam Hussein Nasrallah. Na Hizboullah wana connection na Syria. Hapo unaona equation ilivyo complicated!
  Ingawa Morsi anasema atawaleta pamoja Fatah na Hamas, historia inaonyesha kuwa Brotherhood hawaipendi Fatah.

  Kwa upande wa Marekani mtihani upo sehemu mbili
  1. Kuilinda Israel
  2. Suez canal kwa usafiri wa majeshi na vifaa.

  Ni mapema mno kusema nini kitatokea siku za karibuni ni wazi kuwa CIA wanafanya kazi usiku na mchana.
  Hili la Misri limetia doa sera za Obama kuhusu mambo ya nje. Republican wameanza kulitumia kama sehemu ya nyundo hasa baada ya Obama kufanikiwa sana kurudisha heshima ya Marekani kimataifa na pia kumuondoa OBL.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3,

  ..kwa kweli US inahitaji Raisi atakayekataa kuwa "msukule" wa wa-Israel.

  ..nilisikiliza debate ya Republican contenders[romney,gigrich,santorum] walipoulizwa swali na Palestinian-American. Majibu waliyompa yalikuwa yakushangaza,kusikitisha,na kukatisha tamaa, kwa wakati mmoja.

  ..Wakati umefika kwa Wapalestina kupewa haki yao. Haki yenyewe ni kuheshimiwa kwa mipaka iliyoelekezwa na UN, pamoja na "kifuta machozi" kuhusu right to return. Yakifanyika hayo mawili naamini Mashariki ya Kati itatulia.

  ..Mgogoro wa mashariki ya kati ukitatuliwa, vyama kama Hizbollah,Hamas,na Muslim Brotherhood, itabidi vibadilike na kuanza kuyashughulikia matatizo ya kiuchumi na kijamii ya nchi wanazoziongoza. Actually that might be a death spell kwa vyama hivyo kama ilivyokuwa kwa vyama vya ukombozi vya Afrika vilivyoshindwa ku-keep up na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii ktk nchi zao.
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Nguruvi3.

  Ni kweli unachosema, kisiasa kwa mtazamo wa wengi siasa za Misri kwa sasa zinachukuwa mkondo mpya wa kimapinduzi ya fikra za Brotherhood ambapo toka kuasisiwa kwake na Hassan Albanah na fikra hizo kusambaa katika nchi za kiarabu kama Palestina baadaye nchi za kiafrika ambapo Sudan ilikuwa ya kwanza kufanikisha hilo pale wafuasi wa Muslim Brotherhood maafisa wa kijeshi Hassan Al-Turab na General Omar Al-Basher walipofanikisha mapinduzi na kuitawala Sudan kwa mtazamo na fikra za Muslims Brotherhood.

  Lakini Muslims Brothrehood wameonekana na uhusiano mzuri na wafuasi wa Kikristo nchini Misri, madhebu ya Coptic Kanisa la kale kabisa la mashariki liligawaika toka Kanisa kuu la mashariki la Uyunani la Othodox, walikuwa bega kwa bega kwenye maandamano viwanja vya taharir, Rais Mohamed Morsl kasema hatawajumuisha kwenye serikali yake mpya.

  Ni suala la muda ngoja tusubiri tuone hali itakuwaje Misri na siasa mpya za Rais Mohammed Morsl.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Rais atakayekuwa kinyume na Israel hawezi kuachwa hai kama akishinda.
   
Loading...